Jana nimepiga picha na Diamond ila watu wanakataa siyo yeye

Jana nimepiga picha na Diamond ila watu wanakataa siyo yeye

Daktari wa Meno

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2019
Posts
509
Reaction score
1,610
Kwanza nimejikuta nachukia sana barakoa baada ya watu kukataa kuwa mtu niliyepiga naye picha siyo Diamond. Jana nilikuwa namsikiliza redioni asubuhi na akasema anaenda kuonesha watu hotel yake aliyonunua nikajiandaa kufika maeneo yale aliyokuwa anaenda ili nikapige naye picha kwani mimi ni shabiki wake.

Nilifika mapema eneo lile na kusubiri aje ili niombe picha na yeye. Kweli akafika na kutembeza watu kwenye ile hotel yake nikiwa nje namsubiri atoke. Baada ya nusu saa akatoka nikamkimbilia na kuomba picha na yeye akakubali na nikampa jamaa mmoja simu atupige picha kama mbili.

Baada ya kupiga picha nikamtumia rafiki yangu yuko kijijini na kumwambia awaambie watu wa nyumbani kuwa nimepiga picha na Diamond. Akawaonesha ila baada ya muda wa nusu saa nikaanza kupigiwa simu na watu wa kijijini mbona huyo siyo Diamond, hata sura yake haionekani vizuri. Niliwaelesha sana ila hawauamini nikajikuta napata hata hasira.

Walikataa kuwa siyo yeye eti sura yake haionekani vizuri, wanadai siwezi kupiga picha na yeye, nilimwambia mama awaambie kweli yule ni Diamond japo wamekataa kisa alikuwa kavaa barakoa na haonekani vizuri uso. Sasa nimekosa la kufanya anayejua ukweli kuwa ni Diamond ni mimi na Diamond mwenyewe wengine kama hawaamini sina namna ya kuwaambia wakaamini.

Yule ni Diamond ila tu amevaa barakoa hajaonekana sura yote.
 
Leo umeng'aza mkuu..mwenzio kiduku lilo alisoma mchezo akaona ajikatae kwa muda akae karantini ili akirudi aje na kasi mpya...Na wewe fanya hivyo ukiendelea utazidi poteza mvuto.
 
Mtanesco ungebaki kijijini kwenu katika kipindi hiki. Dar kunatisha.
 
Back
Top Bottom