Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Ilikuwa ni Nissan Civilian number C inayopiga ruti za Mbezi Mlandizi... Jana asubuhi mitaa ya Kibada ndio ilihitimisha safari yake hapa duniani kwa ajali ya moto.. Ilikufa kwa maumivu na upweke mkubwa bila msaada wowote
Wananchi walikuwepo.. Askari waliwepo.. Lakini wote walikuwa wamesimama mbali bila msaada.. Kwao ilikuwa ni ajali ya gari kuungua moto kwangu kilikuwa kifo cha gari
Nimeshakutana na vifo vingi sana.. Nimeshashuhudia watu wengi wakifa.. Wengine nimewasaidia kufa kwa mikono yangu mwenyewe.. Kitu nilichogundua.. Kifo hakizoeleki
Kifo cha gari jana kilikuwa kimojawapo.. Nikawaza namna walivyoanza safari yao pale Mlandizi.. Pengine konda na dereva hawakujua mwenzao anaumwa.. Wakamlazimisha hivyo hivyo
Kuna magari mengine yana roho mbaya sana, yakiumwa kisha yalazimishwe kufanya kazi huamua kujilipua na kufa na abiria.. Lilie la jana ni mbinguni moja kwa moja .. Liliamua kufa peke yake
Tajiri alitarajia kupokea kibunda cha wiki ama cha siku.. Hakupokea
Dereva naye alikuwa na matarajio yake na mipango yake kwa siku ya jana.. Yote iliyeyuka
Hivi konda anaweza kuwa mwaminifu akapeleka pess yote aliyokuwa keshakusanya? Ama atasingizia upotevu wakati wa taharuki?
Kuna abiria nauli yao ilikuwa ya kuungaunga.. Hao walikuwa na siku mbaya
Kuna ambao bado walikuwa hawajarudishiwa chenchi.. Hawa ilikula kkwao
Kuna ambao walikuwa hawajalipa nauli.. Hawa zali liliwaangukia.. Kufa kufaana
Pale ilipofia
Barabara pia iliumia
Kuna mimea iliungua
Kuna wadudu waliungua
Traffic walikosa bakshish na faini
Jiji limekosa mapato
Fundi gereji keshapoteza mteja
List ni ndefu.. Itoshe tu kusema kifo cha lile daladala kimeniuma sana maana kimeleta athari kwa wengi