GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kwa wasichana ni unyago, na kwa wavulana ni jando! Katika huu uzi, ,neno "jando" limetumika kama neno la jumla kwa wavulana na wasichana! Haya, twende sasa!
Kama umeshafika kwa Wakurya, Wamasai, Wamakonde, na makabila mengine yenye utaratibu wa kuwaingiza watoto wao ukubwani kwa njia ya tohara ambayo mara nyingi hufanyika bila ganzi, utakuwa unaelewa maana ya jando.
Mvulana akishaingia jando, huhesabiwa ni mtu mzima hata kama ni mdogo kiumri! Cha kufurahisha, hutarajiwa pia kubadilika kitabia kwa sababu sasa naye ni "mtu" mzima aliyefunzwa mambo ya utu uzima kwa mujibu wa jamii yao. Na kwa hakika, wengi wameonekana kuwa waaminifu sana kwa yale waliyofunzwa, na wengi walimudu kuyaishi hayo kabla ya Elimu waliyopewa jandoni haijafifishwa na Elimu nyingine toka vyanzo vingine!
Nasikia hata Israeli nayo ina utaratibu unaoweza kufanana na huo, ingawa sijui kama bado unaendelea kutekelezwa. Inasemekana, watoto wanapofikia umri wa miaka kumi na tatu, hupelekwa kwenye makambi ya pamoja na kuanza kufunzwa rasmi itikadi za Kiyahudi zitakazowafanya wajitambue Kiyahudi mahali popote watakakokuwa. Wengi ni mashahidi kuwa Wayahudi wengi, bila kujali uraia walio nao na nchi wanazoishi, wameendelea kuwa wazalendo kwa nchi yao ya asili nyakati za shida na raha, kwa uwaziri na kwa uficho.
Inawezekana ni mafunzo waliyopewa ndiyo yanayowasaidia kuwa hivyo?
Labda, na sisi tukiamua kuanzisha mfumo wa JANDO YA KITAIFA, ambapo watoto wamalizapo darasa la saba wanapelekwa kwenye makambi na kujengewa itikadi itakayowafanya kuwa wazalendo kwa nchi yao, hakutatusaidia kuibua kizazi cha kizalendo?
Ikiwa tutaweza kuwafunza watoto wajifunze kuliweka taifa mbele katika mazingira yoyote, hata kama itawafanya wakosane na wazazi wao, hatutaweza kuondoa tatizo la ufisadi huko mbeleni?
Ikiwa tutaweza kuwajengea watoto misimamo mikali katika kuipenda nchi yao, kama vile makundi ya kigaidi yanavyofanya kwa wafuasi wao kiasi cha kuwa tayari kuifia imani yao, hatutaifanya nchi yetu kuacha kuchezewa na wachache?
Kama mbinu tulizozizoea hazijafanikiwa kuinua kiwango cha uzalendo nchini, kwa nini tusijaribu mbinu ya jando ya kitaifa kwa maslahi mapana ya vizazi vijavyo?