Janejelly Ntate aibukia jukwaa la uchumi la wanawake

Janejelly Ntate aibukia jukwaa la uchumi la wanawake

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MHE. JANEJELLY NTATE AIBUKIA JUKWAA LA UCHUMI LA WANAWAKE

Mbunge wa Wafanyakazi Taifa anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Janejelly James Ntate aibukia Jukwaa la Uchumi la Wanawake Mwanamtoti, Kata ya kijichi Dar es Salaam kuwaelezea umuhimu wa kumpongeza Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kufikia miaka miwili madarakani. Shughuli hiyo itafanyika tarehe 19.03.2019 Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

Mhe. Ntate amesema kuwa hata alipoachiwa na mtangulizi wake, hakuna kilichosimama kwa sababu Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) linaendelea kujengwa, Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Daraja la Busisi linaendelea, Madaraja ya juu ya Flyover zinaendelea, Miradi ya Barabara za mwendokasi (BRT) inaendelea.

Mhe. Ntate amewaomba wanawake wote kutoka katika Kata zote za Mkoa wa Dra es Salaam kuhudhuria sherehe za kumpongeza Rais Samia ili kumpongeza mama yetu ambapo sherehe hizo zitafanyika kitaifa katika Mkoa wa Dar es Salaam viwanja vya Mnazi mmoja na mgeni rasmi atakuwa ni yeye mwenyewe Rais Samia.

Mhe. Ntate amewaomba pia wababa kujitokeza kumpongeza Rais Samia kwa miaka miwili ya madarakani.​

WhatsApp Image 2023-03-01 at 20.49.55(1).jpeg




WhatsApp Image 2023-03-01 at 20.49.55.jpeg
 
Miaka miwili imepita sikujua kama Kuna mbunge anaitwa kwa jina hilo, ajitahidi kuchangia mada Bungeni
 
Back
Top Bottom