#COVID19 Janet Museveni: Walimu wasiochanjwa wazuiwe kuingia darasani shule zitakapoofunguliwa tena

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Waziri wa elimu wa Uganda ameamuru walimu nchini kote kupata chanjo ya Covid-19 vinginevyo wazuiwe kuingia madarasani shule zitakapofunguliwa.

Janet Museveni, ambaye ni mke wa Rais Museveni, ameonya kuwa mwalimu yeyote atakayekwenda kazini akiwa na cheti cha kughushi kuthibitisha kuwa amechanjwa atakuwa hatarini kupoteza kazi yake.

Amesema kuchanjwa kwa walimu kutasaidia kuwalinda wanafunzi dhidi ya virusi na kuongeza kuwa vituo vya chanjo vitawekwa kwenye shule na vyuo vikuu vitakapofunguliwa.

Bibi Museveni amekuwa kwenye shinikizo wiki za hivi karibuni la kutakiwa kufugua tena shule, ambazo zilifungwa tarehe 6 mwezi Juni ili kudhibiti maambukizi ya wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona.
 
Tanzania tuna shida sana ya waalimu wa sayansi na lugha ya kiingereza. Hawa wenzetu Alhadullilaah!.... Serikali Yetu ya JMT iwaajiri hao watakaotupwa nje hata kwa mkataba.
 
Kulazimishana chanjo afrika mashariki imekua fasheni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…