#COVID19 Janet Museveni: Walimu wasiochanjwa wazuiwe kuingia darasani shule zitakapoofunguliwa tena

#COVID19 Janet Museveni: Walimu wasiochanjwa wazuiwe kuingia darasani shule zitakapoofunguliwa tena

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Waziri wa elimu wa Uganda ameamuru walimu nchini kote kupata chanjo ya Covid-19 vinginevyo wazuiwe kuingia madarasani shule zitakapofunguliwa.

Janet Museveni, ambaye ni mke wa Rais Museveni, ameonya kuwa mwalimu yeyote atakayekwenda kazini akiwa na cheti cha kughushi kuthibitisha kuwa amechanjwa atakuwa hatarini kupoteza kazi yake.

Amesema kuchanjwa kwa walimu kutasaidia kuwalinda wanafunzi dhidi ya virusi na kuongeza kuwa vituo vya chanjo vitawekwa kwenye shule na vyuo vikuu vitakapofunguliwa.

Bibi Museveni amekuwa kwenye shinikizo wiki za hivi karibuni la kutakiwa kufugua tena shule, ambazo zilifungwa tarehe 6 mwezi Juni ili kudhibiti maambukizi ya wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona.
 
Tanzania tuna shida sana ya waalimu wa sayansi na lugha ya kiingereza. Hawa wenzetu Alhadullilaah!.... Serikali Yetu ya JMT iwaajiri hao watakaotupwa nje hata kwa mkataba.
 
Hao ndiyo wenye kujua nini maana ya kuwa na dhamana juu ya maisha ya watu.

#COVID19 - Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

Hongereni Uganda hongereni Rwanda.

IMG_20210823_163723_810.jpg


No wonder mnapotengeneza magari sisi tunatengeneza ya kukokotwa na ng'ombe.

IMG_20210823_164414_378.jpg


What a contrast?
 
Kulazimishana chanjo afrika mashariki imekua fasheni
 
Back
Top Bottom