SoC02 Janga la kupuuzia fursa mbalimbali katika jamii

SoC02 Janga la kupuuzia fursa mbalimbali katika jamii

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 15, 2022
Posts
5
Reaction score
0
FURSA ni kitendo Cha kuepo au kupatikana kwa nafasi au kazi au jambo lolote ambalo linaweza kumuingizia MTU kipato. Jambo hili linaweza kuwa ni jambo kubwa au dogo, vilevile FURSA inaweza kuhusisha kazi za ofisini au kazi za mitaani, zote hizi ni FURSA kwasababu zina uwezo wa kutuingizia kipato kitakacho tuwezesha Kama vijana au watanzania Kuendesha maisha yako ya Kila siku.

Katika maisha yetu tunayoishi Kuna FURSA MBALIMBALI ambazo hujitokeza siku Hadi siku, miongoni mwa FURSA hizi ni kilimo Cha bustani, uuzaji wa matunda, ajira za muda mfupi za sensa na FURSA nyingine nyingi ikiwemo ushindani wa kimichezo na kielimu Kama vile uandishi wa stori Kama hizi za jamiiforum. Hizo zote kwa ujumla wake zinaitwa FURSA kwa SABABU zinalengo la kutupatia kipato ambacho kinaweza kutumika Kama MTAJI au kipato hicho kinaweza kutumika Katika harakati zingine za kifamilia.

Miongoni mwa majanga sugu kwa vijana wakitanzania tulio wengi ni kuupuzia baadhi ya FURSA zinazojitokeza katika jamii zetu, kwa mfano vijana wengi wakitanzania hawashirika katika utumiaji wa FURSA za uandishi wa vitu Kama insha au stori mbalimbali zinazoweza kuleta tija. Hili ni tatizo kubwa ambalo linaweza kusababishwa na vitu mbalimbali ikiwemo kuto kujiamini katika kutumia FURSA hizo au kuto kujiamini kwamba na yeye Kama kijana anaposhiriki katika mashindano Kama Haya upo uwezekano na yeye akashinda.

Hali Kama hii ya KUPUUZIA FURSA zinazojitokeza katika jamii zetu ndio Inayopelekea ongezeko kubwa la vijana wasio na ajira, hii ni kutokana na wengi katika vijana kutopenda kujishughulisha katika shughuli mbalimbali ambazo zingeweza kuwaingizia kipato. Kwa mfano baada ya kumaliza chuo, vijana wengi hulalamikia ukosefu wa ajira, ni sawa lakini kwanini Kama kijana usifungue kilimo Cha mbogamboga au bustani ambayo ITAKUSAIDIA kukidhi mahitaji yako ya Kila siku, kwasababu mbogamboga ni miongoni mwa vitu ambavyo vinahitajika kwa kiwango kikubwa Kila siku.

Hali hii ya vijana wengi wa kitanzania KUPUUZIA FURSA MBALIMBALI katika jamii huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibika kwa sura ya kijana katika jamii zetu. Hii ni kwasababu ya kuto kuzitumia FURSA hizi ambako kunapelekea vijana wengi kubakia mitaani wakilalamika kwa kusema ajira hakuna, kitu kibaya zaidi ni kwamba vijana hao huamua kujiingiza katika makundi mabaya Kama vile makundi ya kubugi unga au kuuza madawa ya kulevya, uporaji na ujambazi, lakini Haya yote yamesababishwa na kutokutumia FURSA ambazo hujitokeza katika jamii zao ili ziwapatie japo MTAJI mdogo wa kuanzisha biashara mbalimbali japo ile ya kuuza matunda.

JANGA hili la kupuuzia FURSA katika jamii zetu vilevile linaweza kusabashwa na kutokuwa tayari kushindana na watu wengi, kwa mfano uandishi wa stori Kama hizi za mitandaoni, vijana wengi Huwa hatushiriki kwa kutokuwa tayari kushindana na watu wengi katika masuala mbalimbali, hivyo vijana wengi hurudi nyuma katika kutumia FURSA Kama hizi, hivyo basi vijana lazima tukumbuke kwamba ili tuweze kufanikiwa ni lazima tujaribu kutumia FURSA MBALIMBALI ambazo zinazojitokeza katika jamii zetu.

Katika Hali mbalimbali kwenye jamii zetu, Kama vijana inaweza kuwa vigumu kutumia FURSA hizi ndogondogo zinazojitokeza katika jamii, lakini tunaweza kuungana na kutengeneza vikundi vidogo vidogo ambavyo tunaweza kutumia vikundi hivyo kuendesha harakati zetu ndogondogo ambazo zinaweza kutupatia kipato Cha kuendesha maisha yetu ya Kila siku. Umoja,USHIRIKIANO na kuchapakazi kwa bidii kunaweza kutupa tija kubwa katika vikundi vyetu hivi katika jamii.

Kwa mfano vijana wanaweza kuungana ili waanzishe mradi wa kufuga kuku kwa SABABU uuzaji wa kuku ni biashara inayoendelea vizuri Sana kwa hivi Sasa, hivyo hii inaweza kuwa ni FURSA kubwa kwa vijana katika jamii kuitumia na kujitengenezea kipato Chao.

Vilevile Kwa upande wa wasichana au wadada wanaweza kuungana wakafungua sehemu ya kuuzia chakula japo mara moja kwa siku kwa kuanzia, kwa mfano wanaweza kua wanauza chai na vitafunwa Kila siku Asubuhi, shughuli hii inaweza kuwasaidia kupata kipato Cha kuwaendeshea maisha Yao ya Kila siku, lakini pia kufanya kazi kwa bidii na ustadi mkubwa kunaweza kuleta tija kubwa katika biashara Yao.

Kama kijana mpambanaji lazima uwe mtafutaji na mtumiaji mzuri wa Kila FURSA inayojitokeza mbele yako au katika jamii yako. Kufanya hivyo kutakusaidia kuepukana na uvivu na Tabia mbaya Kama vile wizi na Tabia nyingine zisizofaa.

Suala la kukaa bila kazi katika jamii hasa kwa vijana sio suala la sawa, kwasababu Kuna watu wana elimu kubwa lakini bado wanajishughulisha na kulima mbogamboga wakati wakisubiria ajira, kwahiyo sisi Kama vijana lazima tupambane ili kuhakikisha tunapata sehemu za kujishikiza na kutuingizia kipato,hasa kwa wale ambao ni wahitimu wa vyuo, hivyo basi vijana Haina budi tupige kazi ili mradi tu ni kazi za halali zinazo ruhusiwa na mambo mengine yanaweza kuwa sawa.

Kama inavyojulikana kwamba Asiye fanya kazi na asile hivyo ni muhimu Kama WATANZANIA tufanye kazi, nimalizie kwa kusema NDUGU ZANGU WATANZANIA, Usithubutu kuacha kazi wakati hujui kazi nyingine utaipata wapi, watu wenye hekima na weledi wanatushauri tuwe tunaendelea na kazi inayoumiza au yenye malipo madogo mpaka tunapopata kazi nyingine ndio tuachane nayo kazi hiyo inayoumiza, DAIMA USIISHI BILA KAZI KATIKA JAMII.
BY: MKAKA WA CHUO.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom