Janga la njaa linakodolea Wakenya macho kufuatia uvamizi wa nzige ambao wanaendelea kusababisha uharibifu

Janga la njaa linakodolea Wakenya macho kufuatia uvamizi wa nzige ambao wanaendelea kusababisha uharibifu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
JANGA la njaa linakodolea Wakenya macho kufuatia uvamizi wa nzige ambao wanaendelea kusababisha uharibifu mkubwa wa mimea nchini.

Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo duniani (FAO) ambalo husimamiwa na Umoja wa Mataifa (UN), nzige waliokomaa na wengine wachanga walikuwa wameonekana katika kaunti 13 kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kufikia Jumatano, wadudu hao waharibifu waliendelea kuenea maeneo mengi nchini. Serikali sasa imekiri hali hii itasababisha ugumu wa hali ya maisha mwaka 2020 kutokana na athari mbaya kwa kilimo na uchumi.

Kwenye taarifa ya sera ya bajeti ya mwaka wa 2020/2021, Waziri wa Fedha Ukur Yatani alisema, athari ya nzige kwa kilimo itasababisha gharama ya maisha kupanda na hivyo kuathiri ukuaji wa uchumi.

“Uvamizi wa nzige nchini mwishoni mwa 2019 hadi mapema 2020 ni hatari kwa kilimo na uzalishaji wa chakula cha kutosheleza mahitaji ya wananchi. Serikali itaendelea kufuatilia hali hiyo na kuweka mikakati ya kifedha na sera za kuimarisha uchumi,” akasema.

Janga la nzige kama la sasa halijashuhudiwa nchini kwa miaka 70.

Wakulima katika maeneo yanayosifika kwa uzalishaji wa chakula ya Rift Valley na magharibi mwa nchi wana matumaini kwamba ushauri wa wataalamu wanaosema upepo hautawaruhusu nzige kuelekea huko utakuwa wa kweli.

Sehemu nyingi za nchi ambazo zimevamiwa kufikia sasa ni maeneo ambapo wananchi hutegemea ufugaji kujipatia. Hali hii inaibua hofu ya vita vya kijamii kwa wafugaji watakaokosa malisho ya mifugo wao siku zijazo.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Bw QU Dongyu, alisisitiza ni sharti hatua zote zinazochukuliwa zijumuishe juhudi za kuwezesha wakazi kukidhi mahitaji yao ili kuzuia athari zaidi.

“Jamii za Afrika Mashariki tayari hukabiliwa na ukame wa muda mrefu ambao umeathiri uwezo wao wa kilimo na riziki. Tunahitaji kuwasaidia kurudia hali yao ya kawaida pundenzige watakapoondoka,” akasema.

Kwa mujibu wa mwongozo wa UN kuhusu mbinu za kupambana na ghasia za kupigania rasilimali, uhaba au ukosefu wa mali asili zinazotegemewa na binadamu kama vile lishe ya mifugo na maji huwa ni mojawapo ya sababu kuu za vita vya kijamii.

Takwimu zinaonyesha kuwa, wingu moja la nzige huweza kutafuna takriban kilo milioni 192 ya mimea kwa siku. Uzani huu ni sawa na takriban magunia milioni mbili ya mahindi ya kilo tisini kila moja.

Imebainika kwamba, wakati nzige wanavamia eneo, masomo huathirika kwa kuwa watoto hutolewa madarasani kwenda kuwashtua watoroke.

Mnamo Jumanne, hali hii ilishuhudiwa katika eneo la Masaku, Kaunti ya Machakos ambapo mamia ya wanafunzi wa shule za msingi na upili waliungana na walimu na wazazi kwa takriban saa 15 kufukuza nzige.

Mbinu ya kunyunyiza dawa kutoka angani kuua nzige pia inaibua hofu ya uharibifu wa mazingira na athari za kiafya.

Ingawa serikali na asasi nyingine zinazohusika katika shughuli hiyo zilihakikishia umma kuhusu usalama wa kemikali zinazotumiwa, ripoti zinasema si rahisi kuepuka athari kwa afya na mazingira hasa nzige wanapoongezeka na kufanya dawa nyingi zaidi kumiminwa.

“Ni kweli, dawa zinazotumiwa kudhibiti nzige zinaweza kuathiri binadamu na wanyama zikitumiwa vibaya lakini hazisababishi kansa. Watu wana kila sababu ya kuingiwa hofu na kujitahadhari, lakini athari za dawa zinazotumiwa zinaweza kudhibitiwa kwa hivyo jamii isiwe na hofu,” FAO iliambia ‘Taifa Leo’ kupitia kwa taarifa.

Shirika hilo hupendekeza mataifa yaepushe uvamizi ndiposa huwa inatoa ilani mapema kabla nzige wavamie mahali.

FAO ilitoa tahadhari kwamba nzige watakuwepo kwa miezi sita na wasipodhibitiwa, wataongezeka mara 500 kwa idadi.

Kwa mujibu wa shirika hilo la UN, wingu moja la nzige huwa na mamia ya mamilioni ya wadudu hao waharibifu ambao huweza kusafiri kilomita 150 kwa siku. Umbali huo ni kama kutoka Nairobi hadi Narok mjini.

Kwa mujibu wa shirika la kuangazia wanyama la National Geographic, nzige waliweka historia mnamo 1954 wakati wingu moja liliposafiri kutoka kaskazini mashariki mwa Afrika hadi Uingereza.
 
sio jambo la kufurahia , kwani wakimaliza Kenya wataamia Tanzania.

Ni jambo la kimkakati kulimaliza. pia ni jambo la kumuomba Mungu, kwa hawa wadudu wakiingia katika nchi ndani ya siku chache wanakula mpaka mashina ya mimea.

Viwavi tu vinatutoaga jasho, sembuse nzige?
 
Inasikitisha sana, ndugu zetu wataangamia.
Imagine Hata bila nzige wakenya huangamia kwa Njaa, si ndio watamaliza ndugu zetu?
Sasa kama bila nzige wakenya huwa wanakufa kwa njaa vip sasa na hawa nzige hali itakuwa ngumu zaidi [emoji848][emoji848][emoji22][emoji22]
Sent using Jamii Forums mobile app
Mmeishiwa na hoja siku hizi. Naona kilichosalia ni kuiponda Kenya kwasababu ya majanga 'natural' kama kiangazi na uvamizi wa nzige. Hivi mnajua kwamba Kenya ni jangwa kwa 83% na wakati hamna kiangazi, kama mwaka huu, sehemu chache ambazo huwa ni jangwa kupindukia kama Turkana mambo huwa ni shwari? Nzige walitoka Eritrea, Djibouti, Ethiopia wakaingia hadi Somalia alafu Kenya na sasa hivi wamefika hadi gatuzi la Machakos. Yaani hapo ni gatuzi moja tu limesalia, Kajiado, kisha waingie Longido, Tz. Mnajimwambafy utadhani nzige wanaitambua CCM.
 
Mmeishiwa na hoja siku hizi. Naona kilichosalia ni kuiponda Kenya kwasababu ya majanga kama kiangazi na uvamizi wa nzige. Hivi mnajua kwamba Kenya ni jangwa kwa 83% na wakati hamna kiangazi, kama mwaka huu, sehemu chache ambazo huwa ni jangwa kupindukia kama Turkana mambo huwa ni shwari? Nzige walitoka Eritrea, Djibouti, Ethiopia wakaingia hadi Somalia alafu Kenya na sasa hivi wamefika hadi gatuzi la Machakos. Yaani hapo ni gatuzi moja tu limesalia, Kajiado, alafu waingie Longido, Tz.

Ndo walivyokwambia wakitoka Kunyaland wanakuja[emoji1241] Baba Lao[emoji16]
 
Gharama ya Mkutano 1 wa ujinga wa BBI unaweza kumaliza nzige wote, sema hao Wanasiasa hawajali .
 
Ndo walivyokwambia wakitoka Kunyaland wanakuja[emoji1241] Baba Lao[emoji16]
Akili za kibongolala hizi, ushamba ushamba kama kawa. Mienendo ya nzige hao ilitabiriwa kisayansi kutoka Saudi Arabia, Oman, Yemen hadi walipoingia Afrika. Kule Saudia na Yemen bado wanateswa na nzige hao na bado wanaendelea kuingia Afrika kwa wingi. Alafu kila sehemu ambayo wanapita wanaacha mayai yao, mwezi wa pili ndio watakuwa wengi zaidi. Kama una uwezo wa kusoma ramani ndio hii hapa.
images
 
Nzige wenyewe wanasonga na rate ya kilomita 150 kwa siku, speed ya 16km/hr wakifagia kila kitu njiani. Alafu badala ya kufahamishana mmekomalia kuisema na kuiandama Kenya. Nangoja kuona mkijenga ukuta kama ule wa Mirerani, washenzi sana nyinyi viumbe.
 
Mmeishiwa na hoja siku hizi. Naona kilichosalia ni kuiponda Kenya kwasababu ya majanga 'natural' kama kiangazi na uvamizi wa nzige. Hivi mnajua kwamba Kenya ni jangwa kwa 83% na wakati hamna kiangazi, kama mwaka huu, sehemu chache ambazo huwa ni jangwa kupindukia kama Turkana mambo huwa ni shwari? Nzige walitoka Eritrea, Djibouti, Ethiopia wakaingia hadi Somalia alafu Kenya na sasa hivi wamefika hadi gatuzi la Machakos. Yaani hapo ni gatuzi moja tu limesalia, Kajiado, kisha waingie Longido, Tz. Mnajimwambafy utadhani nzige wanaitambua CCM.
Njaa Kenya husababishwa na uzembe wenu usijaribu kusingizia ukame, mbona uzalishaji wa chai na maua haukumbwi na ukame?

Ardhi yote nzuri yenye rutuba ni Mali ya wazungu na mabwenyenye, hawaoni umuhimu wowote wa kulima mahindi badala yake wanalima chai na maua.

Hata Galana Kulalu project ambayo ingewapunguzia njaa umewashinda kwa sababu ya uzembe na rushwa, eti unasingizia ukame, ubepari ndio sababu kubwa ya njaa na uzembe wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nzige wenyewe wanasonga na rate ya kilomita 150 kwa siku, speed ya 16km/hr wakifagia kila kitu njiani. Alafu badala ya kufahamishana mmekomalia kuisema na kuiandama Kenya. Nangoja kuona mkijenga ukuta kama wa Mirerani, washenzi sana nyinyi viumbe.
Subiri waingie Tanzania ndio mtajua tofauti ya Kenya na Tanzania, hata Alshabaab mlisema wangefika Tanzania, kila wakijaribu kupandikiza watu wao tunawazima haraka sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njaa Kenya husababishwa na uzembe wenu usijaribu kusingizia ukame, mbona uzalishaji wa chai na maua haukumbwi na ukame?

Ardhi yote nzuri yenye rutuba ni Mali ya wazungu na mabwenyenye, hawaoni umuhimu wowote wa kulima mahindi badala yake wanalima chai na maua.

Hata Galana Kulalu project ambayo ingewapunguzia njaa umewashinda kwa sababu ya uzembe na rushwa, eti unasingizia ukame, ubepari ndio sababu kubwa ya njaa na uzembe wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kawaida ya hawa wajinga kusingizia ukame kila mwaka wakati walifisadi miradi ya umwagiliaji.
 
Inasikitisha sana, ndugu zetu wataangamia.
Imagine Hata bila nzige wakenya huangamia kwa Njaa, hawa nzige si ndio watamaliza ndugu zetu?
Mwenyewe imenibidi nicheke japo sio Mazuri
Yaani bila Nzige Wananchi full Ukurutu
Sasa Hao Nzige nao wameingilia
Uchumi wa Kati kazi wanayo
 
Njaa Kenya husababishwa na uzembe wenu usijaribu kusingizia ukame, mbona uzalishaji wa chai na maua haukumbwi na ukame?

Ardhi yote nzuri yenye rutuba ni Mali ya wazungu na mabwenyenye, hawaoni umuhimu wowote wa kulima mahindi badala yake wanalima chai na maua.

Hata Galana Kulalu project ambayo ingewapunguzia njaa umewashinda kwa sababu ya uzembe na rushwa, eti unasingizia ukame, ubepari ndio sababu kubwa ya njaa na uzembe wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Muulize Huo Ukame
Hao Nzige wamefuata Jangwa!!
 
Akili za kibongolala hizi, ushamba ushamba kama kawa. Mienendo ya nzige hao ilitabiriwa kisayansi kutoka Saudi Arabia, Oman, Yemen hadi walipoingia Afrika. Kule Saudia na Yemen bado wanateswa na nzige hao na bado wanaendelea kuingia Afrika kwa wingi. Alafu kila sehemu ambayo wanapita wanaacha mayai yao, mwezi wa pili ndio watakuwa wengi zaidi. Kama una uwezo wa kusoma ramani ndio hii hapa.
images
Hao Saudia hawaombi Chakula
Nyie bila Nzige Full Njaa
 
Mmeishiwa na hoja siku hizi. Naona kilichosalia ni kuiponda Kenya kwasababu ya majanga 'natural' kama kiangazi na uvamizi wa nzige. Hivi mnajua kwamba Kenya ni jangwa kwa 83% na wakati hamna kiangazi, kama mwaka huu, sehemu chache ambazo huwa ni jangwa kupindukia kama Turkana mambo huwa ni shwari? Nzige walitoka Eritrea, Djibouti, Ethiopia wakaingia hadi Somalia alafu Kenya na sasa hivi wamefika hadi gatuzi la Machakos. Yaani hapo ni gatuzi moja tu limesalia, Kajiado, kisha waingie Longido, Tz. Mnajimwambafy utadhani nzige wanaitambua CCM.
Na hii ardhi ni % ngapi
tapatalk_1578844814230.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njaa Kenya husababishwa na uzembe wenu usijaribu kusingizia ukame, mbona uzalishaji wa chai na maua haukumbwi na ukame?

Ardhi yote nzuri yenye rutuba ni Mali ya wazungu na mabwenyenye, hawaoni umuhimu wowote wa kulima mahindi badala yake wanalima chai na maua.

Hata Galana Kulalu project ambayo ingewapunguzia njaa umewashinda kwa sababu ya uzembe na rushwa, eti unasingizia ukame, ubepari ndio sababu kubwa ya njaa na uzembe wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Aridhi yote ni hii hapa
tapatalk_1578844814230.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmeishiwa na hoja siku hizi. Naona kilichosalia ni kuiponda Kenya kwasababu ya majanga 'natural' kama kiangazi na uvamizi wa nzige. Hivi mnajua kwamba Kenya ni jangwa kwa 83% na wakati hamna kiangazi, kama mwaka huu, sehemu chache ambazo huwa ni jangwa kupindukia kama Turkana mambo huwa ni shwari? Nzige walitoka Eritrea, Djibouti, Ethiopia wakaingia hadi Somalia alafu Kenya na sasa hivi wamefika hadi gatuzi la Machakos. Yaani hapo ni gatuzi moja tu limesalia, Kajiado, kisha waingie Longido, Tz. Mnajimwambafy utadhani nzige wanaitambua CCM.
Asilimia 17% zinazobaki mmezifanyia nini?

IMG_7295.JPG
 
Back
Top Bottom