Janga la pombe kali na anguko la kizazi: Kilio cha wazazi na hatari kwa Taifa

Janga la pombe kali na anguko la kizazi: Kilio cha wazazi na hatari kwa Taifa

Wengine mnaishi Tanzania gani jamani, hao vijana wanaongamia na pombe hatuwaoni wengine, mnakuza tatzo tu, achen watu waburidike, pombe ipo miaka nenda miaka Rudi,
 
Pombe ni tatizo kweli kweli,hata juice nyingi. Za viwandani na energy si salama sana.ninafikiria ni wakati muafaka wa serikali kuweka sheria kuhusu utengenezaji wa vyakula na hata hizo pombe za kienyeji.fikiria Kuna mkoa watu wakisindika pombe za kienyeji wanaweka sabuni ya unga kama catalyst,na hizo zinamadhara kiafya.
 
Pombe ni tatizo kweli kweli,hata juice nyingi. Za viwandani na energy si salama sana.ninafikiria ni wakati muafaka wa serikali kuweka sheria kuhusu utengenezaji wa vyakula na hata hizo pombe za kienyeji.fikiria Kuna mkoa watu wakisindika pombe za kienyeji wanaweka sabuni ya unga kama catalyst,na hizo zinamadhara kiafya.
Catalyst is any chemical substance used to alter the chemical reactions and remains unchanged.

Kwaresma Njema
 
Mkuu hata energy drinks na soda zinaua mafigo ila ni uchaguzi wa mtu.

Ngono inapukutisha watu, ndoa zinaua watu ila ndio hivyo acha watu wawe huruu.

Serikali imepima pombe kadhaa imeona ziko sawa na imeziruhusu, sasa kinachobaki ni wewe kuamua utumie au usitumie ila sio serikali ikuamlie ilhali wewe ni mtu huru.

Note. Everything too much is harmful.
Mimi nilikuwa mnywaji mkubwa wa pombe kali kwa miaka mingi hivyo najua ninachokiongea ni kitu gani.

Marafiki wanaendelea kuteseka kwa figo kuathiriwa na pombe, majuzi tumemzika mwingine. Alikuwa mlevi kupindukia.

Pombe ina sukari na sukari inaharibu ubongo, yapo madhara mengine mengi tu.
 
Katika kila kijiji, mitaa na miji ya Tanzania, kuna kilio kinachoumiza mioyo ya wengi, lakini hakuna anayekisikia. Ni kilio cha wazazi waliokatishwa tamaa, wakiona vijana wao wakiteketea katika wimbi la pombe kali zinazouzwa kiholela. Vijana waliopaswa kuwa nguvu kazi ya taifa, faraja ya wazazi wao na walinzi wa kesho, sasa ni mizigo ya familia zao na jamii kwa ujumla.

Ni hali ya kutisha kuona mzazi akilia machozi ya uchungu kwa sababu ya mwanae aliyekuwa na ndoto, akili timamu na nguvu za kufanya kazi, sasa akiwa tegemezi, mlevi kupindukia, asiye na malengo wala heshima kwa maisha. Wazazi waliokuwa na matumaini ya kusaidiwa na watoto wao wakati wa uzee, sasa wanajikuta wakihangaika kutafuta chakula kwa ajili ya watoto waliovuka umri wa kutegemea wazazi wao. Wanajuta kwa nini walihangaika kuwalea, kwa nini walitumia nguvu zao kuwapeleka shule, ilhali sasa watoto hao wamekuwa mateka wa pombe kali.

Pombe Kali Imechukua Nguvu Kazi ya Taifa

Usalama wa taifa siyo tu bunduki na askari wa kulinda mipaka. Taifa lisilo na vijana wenye akili timamu na nguvu za kufanya kazi ni taifa lililoangamia. Taifa lenye vijana wengi waliopoteza mwelekeo kwa sababu ya unywaji holela wa pombe kali ni taifa lililo hatarini kupoteza maendeleo yake. Vijana hawa walipaswa kuwa wahandisi, madaktari, walimu, wakulima, wafanyabiashara, lakini sasa ni watu waliokosa dira, wakitangatanga mitaani na kufanya vitendo vya aibu vinavyothibitisha kuwa akili zao zimeharibika na pombe kali.

Pombe kali sasa inapatikana kwa bei rahisi, hata kwa mia tano tu. Vijana wengi masikini, wasioweza kumudu maisha, wanapata unafuu wa muda mfupi kwa kunywa pombe hizo ili kusahau shida zao, pasipo kujua wanaharibu maisha yao milele. Hakuna udhibiti wa uzalishaji wala usambazaji wake. Baa zipo kila mtaa, vibanda vya kuuza pombe vimeenea vijijini na mijini, na hakuna anayejali athari zake.

Wapi Serikali? Wapi Wawakilishi wa Wananchi?

Wawakilishi wa wananchi na viongozi wa serikali wamekaa kimya, wakiangalia taifa likiangamia polepole. Wanajikita kwenye mijadala isiyo na msingi, wakisahau kuwa kizazi cha leo ndicho msingi wa kesho. Sheria kali hazipo kudhibiti pombe hizi zinazotengeneza taifa la waraibu, wasioweza kufanya kazi, wanaoishia kuwa mzigo kwa jamii. Ni wapi sheria zinazoweka udhibiti wa uzalishaji, usambazaji na matumizi ya pombe kali? Ni wapi mipango ya kuokoa vijana kutoka kwenye mtego huu wa pombe za bei rahisi zinazouzwa kila kona?

Ikiwa hatua hazitachukuliwa sasa, basi taifa lijipange kwa mzigo mkubwa wa hospitali zilizojaa wagonjwa wa figo, kansa, magonjwa ya ini na matatizo ya akili. Vijana waliodhoofika kutokana na pombe kali hawatakuwa na mchango wowote kwa taifa, zaidi ya kuwa mzigo wa matibabu na ulinzi wa jamii.

Kilio cha Wazazi: Taifa Linapoteza Kizazi

Fikiria mama aliyemlea mtoto wake kwa shida, akimhangaikia kwa miaka yote, akimpeleka shule kwa matumaini ya kupata msaada siku za baadaye. Leo, mtoto huyo hana tena akili timamu. Amegeuka mlevi wa kutupwa, asiyetambua majukumu yake, aliyeharibu afya yake, aliyeharibu maisha yake. Mzazi anabaki na maumivu makali, akikosa mtu wa kumfariji, akijutia miaka yote ya juhudi zake.

Baba aliyekuwa na matumaini ya kuona mwanae akichukua nafasi yake kama kichwa cha familia, sasa analia kwa uchungu. Anaona kijana wake akidhoofika kila siku, akikosa heshima kwa jamii, akiacha kufanya kazi, akiishia kuwa mlemavu wa akili kwa sababu ya pombe kali. Anauliza, “Serikali iko wapi?”

Ni kilio kisicho na majibu. Ni kilio cha wazazi waliojaa majonzi, waliokata tamaa, waliopoteza matumaini yao kwa watoto wao.

Serikali Lazima Ichukue Hatua Mara Moja

Haiwezekani taifa likaendelea kwa mwendo huu. Serikali lazima itunge sheria kali kudhibiti uzalishaji na uuzaji wa pombe kali. Zifuatazo ni hatua muhimu zinazopaswa kuchukuliwa mara moja:

1. Kupiga marufuku uuzaji wa pombe kali kwa rejareja – Pombe zisizodhibitiwa zinauzwa hata kwa watoto wa shule, hali inayoathiri kizazi kijacho. Vile vile imekuwa ni jambo la kawaida pombe kuuzwa kila mahali hata kwenye maduka ya dawa, pembembejeo, mama ntilie, nyumbani kwa mtu na hivyo upatikanaji wake kuwa rahisi kuliko.


2. Kuweka umri wa unywaji wa pombe kali na kufuatilia utekelezaji wake – Vijana wadogo wanaathirika kwa sababu hakuna udhibiti wa umri wa wanywaji wa pombe kali.


3. Udhibiti wa uzalishaji wa pombe kali – Serikali ihakikishe kwamba pombe kali zinazozalishwa zinafuata viwango vya afya na siyo kemikali zinazoua vijana wa taifa. Pia, upatikanaji wake uwe wa gharama na sio rahisi kuepusha matumizi yasio na tija. Kijana anaamka asubuhi kutafuta elfu mbili tu ili akalewe na kutimiza malengo yake kwa siku. Ni lini tutakuwa na vijana wabunifu? Ni lini watu watakuwa na uchungu wa maendeleo kama malengo ni kutafuta elfu mbili peke yake?


4. Kuongeza elimu kwa jamii kuhusu athari za pombe kali – Watu waelimishwe kuhusu hatari zinazotokana na matumizi mabaya ya pombe, ili kuwaepusha vijana wasiingie katika mtego huu.


5. Kuanzisha vituo vya kusaidia waathirika wa pombe kali – Vijana wengi waliopotea kwa pombe kali wanahitaji msaada wa kurejeshwa katika hali yao ya kawaida. Serikali inapaswa kuwekeza katika vituo vya kuwasaidia waraibu wa pombe kali.



Hitimisho

Janga la pombe kali ni bomu linalosubiri kulipuka. Ikiwa hatua hazitachukuliwa sasa, taifa litakosa kizazi chenye afya na akili timamu, na badala yake tutakuwa na taifa la watu wasioweza kuchangia maendeleo, wagonjwa wa kudumu na tegemezi wa jamii.

Serikali, wawakilishi wa wananchi, na jamii kwa ujumla lazima wachukue hatua sasa kuokoa kizazi cha leo kwa ajili ya taifa la kesho. Ikiwa hakuna hatua itakayochukuliwa, basi historia itawahukumu wote waliokaa kimya wakati taifa likiangamia mikononi mwa pombe kali.

Wazazi wanalilia watoto wao. Ni wakati wa serikali kusikia kilio hicho.
Na wengi wakilewa wanashikishwa ukuta so pombe na ushoga huwezi vitenganisha
 
Serikali, wawakilishi wa wananchi, na jamii kwa ujumla lazima wachukue hatua sasa kuokoa kizazi cha leo kwa ajili ya taifa la kesho. Ikiwa hakuna hatua itakayochukuliwa, basi historia itawahukumu wote waliokaa kimya wakati taifa likiangamia mikononi mwa pombe kali.👌🏿📌
mkuu leo umezungumza ukweli juu ya madhara ya pombe na huu ndio uwalisia wako kongole kwa hilo, nguvu hii itumike pia kufutilia mbali ile mada ya walevi na wanywa pombe kwani kwa namna moja au nyingine inawapa mshawasha vijana kuingia kwenye ulivi leo wa bia kesho visungura hadi gongo wakifikiri hayo ndio maisha. kwa sasa naona mada zako zimejikita katika ubunifu jambo ambalo ni zuri tofauti na ulozi na pombe hapo kabla hapo kwakweli umekaza buti meku...,ni kweli hatuwezi kuwanasua wote basi tuwabunguze kwani walevi(wapumbavu) hawawezi kuisha
 
Hali ni mbaya sana,muda mwingi tunalinda viongozi badala ya vizazi vijavyo,namshukuru mleta mada.Pombe kali zinaua vijana na kuwazeesha haraka,nguvu kazi imepungua mno.Ukikosea ukampa kibarua sh 5000 akatoka kidogo tu anarudi amelewa chakari.Usalama usiwe mambo ya Siasa na uongozi tu,hiki kizazi kinaangamia kwa ulevi nani ataoa watoto wenu na wato wetu!!?
 
"Usalama wa Taifa sio bunduki tu na askari wa kulinda mipaka"..

Hapo ndio matatizo yetu yanapoanzia na kuishi kizamani bila kujua mifumo sasa inahitaji watu wenye akili nyingi na maarifa mengi na kukiweka kila kitu under control.
 
Inawezekana unaishi maisha ya kipweke sana,ungeishi maisha ya kujichanganya ungegundua jinsi tatizo lilivyokubwa kongole kwa mtoa mada ameliona hili.
Katika mihangaikoyangu kwa hapa Tanzania nimelishuhudia hili tatizo kila nilikofika na kila niendako wanapombeyao kali iliyo maarufu kuna pombe kali za maziwa radha ya tangawizi,pipi kifua kahawa nk,kunasehemu nilifika watu wanaagiza cocktails za hizo radha kwa sh 2000!
e mnaishi Tanzania gani jamani, hao vijana wanaongamia na pombe hatuwaoni wengine, mnakuza tatzo tu, achen watu waburidike, pombe ipo miaka nenda miaka Rudi,
 
Nakumbuka double kick ilimuua bro angu mmoja hivi mtaani. Hivi visungura sijui vismat jin sio poa kabisa
 
Yaani mtu mzima na akili zake timamu anashindwa kulinda afya yake kwa kuepuka huo ulevi wa izo pombe kali mpka serikdli ingilie kati inasikitisha sana.

Kama umeshindwa kujione huruma mwenyewe unasubiri serekali zetu izi za kiafrica ikuhurumie niseme tu labda usubirie mauti tu hakuna jengine.
 
Mwaka 2015 kuelekea uchaguzi mkuu kulikuwa na tatizo kubwa la VIROBA serikali ya awamu ya 5 ilianza na katazo la viroba..vilikwisha wakati huo, kumbe watengenezaji walihodhi akiba kubwa baada ya katazo..wakabadilisha vifungashio vya Pombe hii na kuleta majina mapya..ikawa si viroba tena bali chupa ndogo za plastiki na hizi chupa hazina tofauti na viroba sababu ujazo ni ule ule..HUWEZI KUUZA POMBE KALI KWENYE CHUPA YA PLASTIKI YENYE UJAZO ML 100 au 200 hata 500!!!
Tuna taifa lenye hulka ya KUTOJALI kuanzia kwenye familia zetu..na mbaya kabisa tunachagua VIONGOZI wasiojali pia..! Rais Magufuli alikuwa tofauti hakuwa na tabia ya kutojali! Tulio nao sasa tabia ya kutojali waliyo nayo ni mara 5 zaidi ya kawaida!
Ni ujinga na uwenda wazimu kudhani nchi itajengwa kwa kodi ya Pombe haramu isiyozingatia viwango kwenye utengenezaji na uuzaji! labda kwa vile mapato ya Pombe hii yanagharimia ANASA za watawala ndio maana hawajali..na iwe dhambi hii iwanzingile wao na vizazi vyao!
Kitoko, smart gin, Simba rock, ambiance
 
Mimi nilikuwa mnywaji mkubwa wa pombe kali kwa miaka mingi hivyo najua ninachokiongea ni kitu gani.

Marafiki wanaendelea kuteseka kwa figo kuathiriwa na pombe, majuzi tumemzika mwingine. Alikuwa mlevi kupindukia.

Pombe ina sukari na sukari inaharibu ubongo, yapo madhara mengine mengi tu.
Sasa mkuu, bado ni uchaguzi wa mtu.

Na pombe hainywewi bila pesa, acha wachangie pato la taifa.

Hao wanaokata moto ni kua wanazidisha, na kama pombe imeruhusiwa nchini sio rahisi kumpangia mtu anywe kiasi gani.

Na hizi pombe za plastic ni matokeo ya kuzipiga marufuku zile pombe za karatasi.
 
Sasa mkuu, bado ni uchaguzi wa mtu.

Na pombe hainywewi bila pesa, acha wachangie pato la taifa.

Hao wanaokata moto ni kua wanazidisha, na kama pombe imeruhusiwa nchini sio rahisi kumpangia mtu anywe kiasi gani.

Na hizi pombe za plastic ni matokeo ya kuzipiga marufuku zile pombe za karatasi.
Starehe ya muda mfupi, utafika wakati wa mateso ya afya kwa mnywaji.
 
Vijana wanapotea na kuangamia kabisa, pombe kali zipigwe marufuku.
 
Back
Top Bottom