DOKEZO JANGA linalokuja Kawe round about na barabara ya Mwai Kibaki

DOKEZO JANGA linalokuja Kawe round about na barabara ya Mwai Kibaki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Kwa mnaotumia barabara hii asubuhi, tumeona msongamano mkubwa wa magari kila siku.
Magari mengi yamehama toka kutumia barabara ya Bagamoyo na sasa watu wengi waendao makazini mjini CBD wanaitumia Round About ya Kawe na hii barabara ya Mwai KIbaki.
Na msongamano huo si wa kitoto.
Siku askari wa Traffic wakichelewa kufika huwa ni balaa!

JANGA LINALO KUJA
Tumeona mablock NANE ya ghorofa nafikiri8 au9, Kawe Beach yanajengwa.
Vile vile kuna mablock nafikiri 8 au 9 hapo Tanganyika Packers yana maliziwa sasa hivi.
Hapo ina maana tumeongeza karibia wati 4,000 wenye magari yanayoweza fika hata 3,000 kila asubuhi .

Mziki wake utauona asubuhi kila mmoja akianza kwenda kazini.
Hii Round About ya Kawe na barabara ya Mwai Kibaki itakuwa haitoshi kubeba mzigo huu wa magari kwa wakati mmoja.

Hivyo basi katika muda huu , haraka sana barabara ya Kawe kwenda baramoyo road, barabara ya Mwai Kibaki, njia hizi zipanuliwe ili ziwe njia nne.
Huu ni ushauri tu.
 
Back
Top Bottom