KIVUMBI NA JASHO: DJUMA, BANGALA
.
Djuma Shaban, Lomalisa Mutambala na kiraka Yannick Bangala juzi kwa nyakati tofauti wamegonga mlango wa kutaka kuondoka na kwenye vikao vyao kulihusisha majibizano makali.
.
Djuma na Bangala ndio walianza ambapo waliwasilisha ombi la kusitisha mwaka mmoja wa mkataba baada ya kutumikia mmoja kwa mafanikio Jangwani. Mikataba yao inaisha mwakani.
.
Habari za uhakika ni kuwa wawili hao awali walipewa nusu ya ada ya usajili na katika miezi ya karibuni wamekuwa wakifosi kumaliziwa bila mafanikio, hivyo Katika hoja zao ni kwamba kile kiasi walichopewa awali ni cha muda waliofanya kazi kwa hiyo wanachodai kitumike kusitisha mkataba sehemu iliyobaki jambo ambalo limeibua mjadala mzito ndani ya uongozi na hata kikao cha jana hakikufikia muafaka.
.
Mabosi wa Yanga wamepata uhakika kwamba wakishafanya uamuzi huo tu ndani ya siku mbili watani wao Simba na wapinzani wao Azam watashtua kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kwamba “mgeni tumempata”. Simba na Azam zinashindana kimyakimya kusaka saini ya Bangala ambaye msimu mmoja uliopita alikuwa mchezaji bora wa ligi kwenda kuimarisha eneo la kiungo wa chini.
View attachment 2660502