nahavache
JF-Expert Member
- Apr 3, 2009
- 871
- 247
Mwaka 2005 nikiwa Zanzibar wakati wa uchaguzi, CCM ilikuwa inaaminika kwa kuchukua vijana mtaani kuwafundisha kuvuruga mikutano ya CUF. In fact wanachama wengi wa CUF waliumizwa sana wakati wanatoka mikutanoni. Kwa sababu vikundi kama hivi vilikuwa ni maarufu kule Dafur kipindi kile kwa jina la Janjaweed, hawa vijana nao kule Zanzibar wakajulikana kwa jina maarufu Janjaweed. Baada ya uchaguzi, na CCM kushinda, vijana hawa walibaki mtaani bila kazi na vipesa vichache walivyopewa viliisha na sasa wengi wao wameishia kuwa wavuta madawa. Njia hii ndiyo inatumiwa sana na CCM sasa huku bara baada ya kukosa ukubali wa wananchi. Janjaweed wanatumiwa kwa njia nyingi sana, mara nyingine mpaka kupiga kura mara zaidi ya tano kama ilivyotokea Zanzibar. CUF wangekuwa hawako badarakani, wangesema uzoefu wao na Janjaweed. In fact, greengard ni Janjaweed