Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumpa nafasi ya kuhudumu katika baraza la mawaziri, akisema kuwa ni heshima kubwa isiyofutika katika maisha yake.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumza leo Jumatatu, Februari 24, 2025, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Lushoto, Tanga, Makamba amesema kuwa amejifunza mambo mengi kupitia uongozi wa Rais Samia tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, na baadaye kuwa Waziri wa Nishati, kisha Waziri wa Mambo ya Nje.
"Mheshimiwa Rais shukrani kutoka sakafu ya moyo wangu kwa kuniamini na kuniteua kuwa waziri wako. Katika kipindi nilichofanya kazi na wewe, nimejifunza sana na nimeelimika mno. Wewe ndiye ulinifundisha uongozi wa uwaziri, na ikiwa nina weledi wowote katika utumishi ni kwa mkono wako na hii nitaenda nayo kaburini," amesema Makamba.
Makamba alihudumu kama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Muungano na Mazingira) katika serikali ya awamu ya tano, kabla ya kuteuliwa na Rais Samia kushika wizara za nishati na baadaye mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.