Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumpa nafasi ya kuhudumu katika baraza la mawaziri, akisema kuwa ni heshima kubwa isiyofutika katika maisha yake.
Akizungumza leo Jumatatu, Februari 24, 2025, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Lushoto, Tanga, Makamba amesema kuwa amejifunza mambo mengi kupitia uongozi wa Rais Samia tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, na baadaye kuwa Waziri wa Nishati, kisha Waziri wa Mambo ya Nje.
"Mheshimiwa Rais shukrani kutoka sakafu ya moyo wangu kwa kuniamini na kuniteua kuwa waziri wako. Katika kipindi nilichofanya kazi na wewe, nimejifunza sana na nimeelimika mno. Wewe ndiye ulinifundisha uongozi wa uwaziri, na ikiwa nina weledi wowote katika utumishi ni kwa mkono wako na hii nitaenda nayo kaburini," amesema Makamba.
Makamba alihudumu kama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Muungano na Mazingira) katika serikali ya awamu ya tano, kabla ya kuteuliwa na Rais Samia kushika wizara za nishati na baadaye mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Samia alikerwa na Makamba baada ya kutafuta umaarufu kupitia suala la sekta ya anga. Aliongea kwamba yeye na waziri mwenzake wameshaongea na kulimaliza suala hilo.
Ukweli ni kwamba lile suala lilimhusu mkurugenzi wa mamlaka ya anga kabla hata halijamfikia waziri wa mambo ya nje.
Samia kaongea kidiplomasia na pia Makamba ni mdau muhimu wa CCM haswa katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.