Januari Makamba: Wanaozuia bomba la mafuta lisijengwe ni wanafiki. EWURA yatoa kibali cha kuanza Ujenzi

Mbona kama nawe huna tofauti kubwa nae, ulitaka Magufuli asitajwe? why asitajwe kama yeye alikuwa mwanzilishi wa huu mradi?

Kwanini unaingiza habari za chuki kwa Makamba kwa jambo lililo wazi kama hilo? huyo Makamba mwenyewe unayemtetea ameshaonesha chuki kwa Magufuli mara nyingi tu, tena mpaka baba yake.

Mimi naona wote hamchekani, ni mashabiki wa watu tu.
Mimi sio shabiki wa mtu, bali haki, utu na uzalendo.
 
Total energy.....
Chainizi
Conservators
Communities
Ubabelism
Wadaka Fursa
 
Mbona kama nawe huna tofauti kubwa nae, ulitaka Magufuli asitajwe? why asitajwe kama yeye alikuwa mwanzilishi wa huu mradi?

Kwanini unaingiza habari za chuki kwa Makamba kwa jambo lililo wazi kama hilo? huyo Makamba mwenyewe unayemtetea ameshaonesha chuki kwa Magufuli mara nyingi tu, tena mpaka baba yake...

Haya mambo kuweni makini nayo, huu ulimbukeni wa kutengeneza timu sioni kama una maana yoyote.
Hapana yaani mtu analalamika mikutano mingi ya miradi Sasa nikadhani hoja yake ndio hiyo kumbe ghafla alitaka kusikia JPM anapewa credit yaani kama JPM angepewa credit mkutano usingekua na kasoro!! Kama sio chuki ni nini haswaa?

Kipindi JPM akiwa Rais alikua anamkosoa sana JK kuwa hakufanya kitu na alikua fisadi na Hawa Hawa walishangilia eti Cha kushangaza Leo ndio wanatambua umuhimu wa kumsifia mtangulizi wako!!

Double standards haiwezi tusaidia kitu
 
Kwani kuna ubaya gani si miaka michache tu Uganda walikuwa back and forth wakijiuma uma ilo bomba lipite Tanzania au Kenya; na nchi zote mbili zikipeleka arguments kwanini lipite kwao.

Ata Museveni mwenyewe alipokuwa Chato aliweka wazi, Magufuli ndio aliemshawishi zaidi kuamua lipitie Tanzania. Sasa kuna shida gani akisema mtu alietumia nguvu hilo bomba kupitishwa Tanzania.

Yaani ata kwenye mradi wa bwawa la Nyerere bila ya soni uso mkavu anataka kuondoa credit za mtu alieasisi mradi.
Kumbe shida Yako ni kusikia JPM atajwe Sasa kelele zote kwamba mikutano ya EACOP imekua mingi sana Ina faida gani? Ungesema tu kuwa tatizo sio mikutano mingi ila ni jina la JPM!!

Acheni chuki zisizokuwa na sababu, mbona juzi kampongeza JPM kwa kukataa lockdown ila sijaona ukipongeza hilo
 
Wewe januari ndio mnafiki namba moja na upara wako huo. Mtalipia tu. Mnahujumu maslahi ya taifa kwa tamaa zenu
 
Kumbe shida Yako ni kusikia JPM atajwe Sasa kelele zote kwamba mikutano ya EACOP imekua mingi sana Ina faida gani? Ungesema tu kuwa tatizo sio mikutano mingi ila ni jina la JPM!!

Acheni chuki zisizokuwa na sababu, mbona juzi kampongeza JPM kwa kukataa lockdown ila sijaona ukipongeza hilo
Binafsi kipindi cha Magufuli alipokuwa anachukua credit za wenzake cheaply nilikuwa na sema haya haya ninayosema leo.

Mifano ni kwa uchache Terminal 2, Hospitali ya Mloganzila, mission aliyoanza nayo kimya kimya marehemu Mahiga kuzunguka jela zote nchini na kuangalia kesi zisizo na kichwa wala miguu na kutaka wafungwa wa aina hiyo kuachiwa, jitihada za Makamba kwenye kuzuia viroba na mifuko ya plastic; sehemu zote hizo Magufuli alipokuwa credit kwa wahusika nilisema haya haya.

Na sio kila maamuzi ya Magufuli pia nilikuwa nashangalia mfano ununuzi wa ndege, kuzuia covid vaccination, baraza la mawaziri lililoja watu wa kanda ya ziwa; to name a few.

Support yangu ya Magufuli ni kutokana na misimamo yangu niliyoeleza na yeye hayo mambo ilikuwa ni sehemu kubwa ya uongozi wake kutaka haki, utu na uzalendo. Zitto mwenyewe anakiri kulikuwa na discipline serikalini.

Sehemu zingine ninapo support Magufuli ni kwenye jitihada zake za ujenzi wa miundombinu mbinu, uwezi kuendelea bila ya easy access ya kuingia na kutoka sehemu za uzalishaji na support nyingine ni kwenye kuwabadili watanzania tabia maendeleo yanataka attitude sahihi pia.

Sasa kuna mijitu serikalini na ndani ya CCM wao wanataka kufanya mambo with impunity kama walivyozoea miaka yote ya business as usual. Mfano unakuta jitu linaenda kukopa bank kwa sababu ya kuanzisha biashara ya kutoa huduma mahususi kwa serikali tu. Serikali ikisema tunaenda na utaratibu mwingine wa kufanya mambo huduma zako aziitajiki linaanza matusi, kuna watu vitega uchumi vya serikali na CCM mapato yanayokusanywa hapo wanadhani kuchukua percentage ni haki yao, kuna watu kuna watu huko kwenye services level wenye mishahara ya laki tano washajiwekea kwa mwezi inabidi apate zaidi ya million moja ya ziada kupitia rushwa ikibidi asumbue wateja; yaani ni ovyo ovyo ovyo. Kutokana na mazuri yake na kwa mitazamo yangu tunaona ‘eye to eye’ semehu nyingi ndio maana na support mambo yake mengi mpaka leo.

Hayo mengine ya chuki binafsi na viongozi wengine ni hisia zako tu na wepesi wa kudhani kila wakati mtu anapokosolewa basi ni personal.

Hivi unaanzaje kumchukia mtu ambae humjui at personal level mie huwa naona hizo ni mental issues kwa sababu ata sijui hasira nae nazitoa wapi. Halikadhalika siwezi acha kukosoa mapungufu yake hasa akiwa mwanasiasa maana maamuzi yake au tabia zake zina influence jamii.
 
Duh kama makamba ameanza kutema cheche za kiume hivi basi he is fit to be the next president

Big up makamba

Title ya thread ilipaswa iwe,"makamba atema cheche,ayaparua mabeberu"
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa kibali cha Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Mtukula hadi Tanga lenye urefu wa km 1147.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), James A. Mwainyekule amesema EWURA imetoa kibali cha Ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi kwa EACOP.

Kibali hicho ni cha kujenga Bomba la mafuta ghafi kuanzia Mtukula Mkoni Kagera hadi Chongoleani Mkaoni Tanga.

James A. Mwainyekule, amesema Bomba hilo litapita katika Mikoa nane ambayo ni Kagera, Tanga, Manyara, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga na Geita.

Naye Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema Wanaozuia bomba la mafuta gafi lisijengwe ni Wanafiki. Kayasema hayo wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (#EWURA) ikitoa kibali cha ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Mtukula Mkoani Kagera hadi Chongoleani, Tanga lenye urefu wa KM 1147.

amesema “Kuna maneno mengi kuhusu bomba, wenzetu Ulaya wakidai halistahili kujengwa, hata Bunge la Ulaya limetoa Azimio ambalo ni maneno tu, wenzetu Nchi za Afrika na zinazoendelea kuna unafiki tena mkubwa sana, msingi wa maendeleo yao ilikuwa ni uvunaji wa rasilimali kama hizi mfano makaa ya mawe na gesi.”

Makamba amesema tahadhali zote za kimazingira zimechukuliwa kwani baada ya bomba kujengwa, juu yake tutapanda miti kiasi kwamba hutajua kama bomba limepita.

Bomba hilo litapita Mikoa 8 ambayo ni Kagera, Tanga, Manyara, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga na Geita.

Naye Omary Mgumba, Mkuu wa Mkoa wa Tanga akiongea kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa nane ambayo bomba limepita amesema hali ya Usalama ni nzuri. Wanaendela kufundisha wanavijiji ambapo bomba linapita ili walinde miundombinu kabla, wakati na baada ya mradi kumalizika.

Pia ameomba Serikali kuongeza Vituo vya Polisi kwenye Vituo sehemu bomba linapita.

Makamba: Juu ya bomba la mafuta kutapandwa miti

Kuna maneno kuwa linapita kwenye mbuga za Wanyama, vyanzo vya maji, watu wataathirika, hizo ni propaganda.

Kuna kazi kubwa imefanyika kulinda mazingira, bomba litakapopita patapandwa miti juu yake kiasi kwamba itakuwa ngumu kujua kama kuna bomba limepita.

Watu 9,898 wataguswa na mradi na kati yao watu 390 tu ndio ambao ardhi yao itachukuliwa na wamepewa fursa kama wanataka kujengewa nyumba nyingine au kulipwa, hakuna vurugu wala nguvu iliyotumika.

85 wameamua kujengewa nyumba, tumelipa fidia Tsh. Bilioni 29 kwa wale ambao bomba litapita katika maeneo yao, kazi ya kulipa inaendelea.

Kuhusu haki za binadamu zimezingatiwa, NEMC walitoa maelekezo ya nini cha kufanya, mradi pia utatoa ajira na manufaa ya kiuchumi.

Makamba: Kazi kubwa imefanyika kulinda mazingira na Haki za Bnadamu

Akizungumzia ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Kagera hadi Tanga amesema kuna kazi kubwa imefanyika kulinda mazingira sehemu ambapo litapita.

Amesema “Watu 9,898 wataguswa na mradi, kati yao Watu 390 ndio ambao ardhi yao itachukuliwa na wakapewa fursa kuchagua kujengewa nyumba nyingine au kulipwa, 85% wameamua kujengewa, pia tumelipa fidia Tsh. Bilioni 29 kwa ambao bomba litapita katika maeneo yao na zoezi la kulipa linaendelea.”

Aidha, amesema Haki za Binadamu zimezingatiwa kwa kuzingatia muongozo wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Hizi vibali huwa wanatoa mara ngapingapi au wanazi-update nakumbuka kipindi cha mwendazake ilitolewa
 
hayo mafuta ya M7 yakishindikana tuendelee na ujenzi wa bomba letu ila isambaze maji toka ziwa victoria kwenda kwenye hayo mikoa na vijiji vya jirani tuendelee na kilimo cha umwagiliaji
 
Back
Top Bottom