Januari Makamba: Wanaozuia bomba la mafuta lisijengwe ni wanafiki. EWURA yatoa kibali cha kuanza Ujenzi

Mimi sio shabiki wa mtu, bali haki, utu na uzalendo.
 
Total energy.....
Chainizi
Conservators
Communities
Ubabelism
Wadaka Fursa
 
Hapana yaani mtu analalamika mikutano mingi ya miradi Sasa nikadhani hoja yake ndio hiyo kumbe ghafla alitaka kusikia JPM anapewa credit yaani kama JPM angepewa credit mkutano usingekua na kasoro!! Kama sio chuki ni nini haswaa?

Kipindi JPM akiwa Rais alikua anamkosoa sana JK kuwa hakufanya kitu na alikua fisadi na Hawa Hawa walishangilia eti Cha kushangaza Leo ndio wanatambua umuhimu wa kumsifia mtangulizi wako!!

Double standards haiwezi tusaidia kitu
 
Kumbe shida Yako ni kusikia JPM atajwe Sasa kelele zote kwamba mikutano ya EACOP imekua mingi sana Ina faida gani? Ungesema tu kuwa tatizo sio mikutano mingi ila ni jina la JPM!!

Acheni chuki zisizokuwa na sababu, mbona juzi kampongeza JPM kwa kukataa lockdown ila sijaona ukipongeza hilo
 
Wewe januari ndio mnafiki namba moja na upara wako huo. Mtalipia tu. Mnahujumu maslahi ya taifa kwa tamaa zenu
 
Binafsi kipindi cha Magufuli alipokuwa anachukua credit za wenzake cheaply nilikuwa na sema haya haya ninayosema leo.

Mifano ni kwa uchache Terminal 2, Hospitali ya Mloganzila, mission aliyoanza nayo kimya kimya marehemu Mahiga kuzunguka jela zote nchini na kuangalia kesi zisizo na kichwa wala miguu na kutaka wafungwa wa aina hiyo kuachiwa, jitihada za Makamba kwenye kuzuia viroba na mifuko ya plastic; sehemu zote hizo Magufuli alipokuwa credit kwa wahusika nilisema haya haya.

Na sio kila maamuzi ya Magufuli pia nilikuwa nashangalia mfano ununuzi wa ndege, kuzuia covid vaccination, baraza la mawaziri lililoja watu wa kanda ya ziwa; to name a few.

Support yangu ya Magufuli ni kutokana na misimamo yangu niliyoeleza na yeye hayo mambo ilikuwa ni sehemu kubwa ya uongozi wake kutaka haki, utu na uzalendo. Zitto mwenyewe anakiri kulikuwa na discipline serikalini.

Sehemu zingine ninapo support Magufuli ni kwenye jitihada zake za ujenzi wa miundombinu mbinu, uwezi kuendelea bila ya easy access ya kuingia na kutoka sehemu za uzalishaji na support nyingine ni kwenye kuwabadili watanzania tabia maendeleo yanataka attitude sahihi pia.

Sasa kuna mijitu serikalini na ndani ya CCM wao wanataka kufanya mambo with impunity kama walivyozoea miaka yote ya business as usual. Mfano unakuta jitu linaenda kukopa bank kwa sababu ya kuanzisha biashara ya kutoa huduma mahususi kwa serikali tu. Serikali ikisema tunaenda na utaratibu mwingine wa kufanya mambo huduma zako aziitajiki linaanza matusi, kuna watu vitega uchumi vya serikali na CCM mapato yanayokusanywa hapo wanadhani kuchukua percentage ni haki yao, kuna watu kuna watu huko kwenye services level wenye mishahara ya laki tano washajiwekea kwa mwezi inabidi apate zaidi ya million moja ya ziada kupitia rushwa ikibidi asumbue wateja; yaani ni ovyo ovyo ovyo. Kutokana na mazuri yake na kwa mitazamo yangu tunaona ‘eye to eye’ semehu nyingi ndio maana na support mambo yake mengi mpaka leo.

Hayo mengine ya chuki binafsi na viongozi wengine ni hisia zako tu na wepesi wa kudhani kila wakati mtu anapokosolewa basi ni personal.

Hivi unaanzaje kumchukia mtu ambae humjui at personal level mie huwa naona hizo ni mental issues kwa sababu ata sijui hasira nae nazitoa wapi. Halikadhalika siwezi acha kukosoa mapungufu yake hasa akiwa mwanasiasa maana maamuzi yake au tabia zake zina influence jamii.
 
Kuna jina moja hapo la "fisadi mzalendo" likitajwa nachukia kweli.
 
Duh kama makamba ameanza kutema cheche za kiume hivi basi he is fit to be the next president

Big up makamba

Title ya thread ilipaswa iwe,"makamba atema cheche,ayaparua mabeberu"
 
Hizi vibali huwa wanatoa mara ngapingapi au wanazi-update nakumbuka kipindi cha mwendazake ilitolewa
 
hayo mafuta ya M7 yakishindikana tuendelee na ujenzi wa bomba letu ila isambaze maji toka ziwa victoria kwenda kwenye hayo mikoa na vijiji vya jirani tuendelee na kilimo cha umwagiliaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…