Januari tuwekee ushahidi wa video ya Kamati ya Bunge au Mbunge aliyekuita 'Mshenzi'

Januari tuwekee ushahidi wa video ya Kamati ya Bunge au Mbunge aliyekuita 'Mshenzi'

Mtumishiwetu

Senior Member
Joined
Jul 13, 2022
Posts
196
Reaction score
346
Nimeona Video inayosambaa kwa kasi sana mitandaoni ya Waziri wa Nishati, Januari Makamba akiwaita wabunge na watanzania wapuuzi na kama hawamtaki wamuue.

Kwenye hotuba yake ametumia neno MSHENZI huyo akimaanisha wabunge na Kamati ya Bunge ya Nishati iliyohoji bungeni kuhusu kuchelewa kwa Mradi wa JNHPP na kukatika kwa umeme kuwa wamekuwa wakimtuka na kumuita MSHENZI.

Sasa tunaomba Makamba na vijana wake mlioko humu mtuwekee clip ya Mbunge au Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge alipotamka Makamba Mshenzi bungeni ili tutumie kama rejea muhimu. kama ambavyo sisi tuna clip yake anayowaita watanzania wapuuzi na wamuue.

Hata mawe yatasema..kipara hana nia ya dhati kumaliza mradi wa jnhpp..ndio mana kutwa kuchwa kiguu njia na mitungi ya gesi kichwani.

#MaendeleoHayanaChama
 
....
Kwenye hotuba yake ametumia neno MSHENZI huyo akimaanisha wabunge na Kamati ya Bunge ya Nishati iliyohoji bungeni kuhusu kuchelewa kwa Mradi wa JNHPP na kukatika kwa umeme kuwa wamekuwa wakimtuka na kumuita MSHENZI.

Sasa tunaomba Makamba na vijana wake mlioko humu mtuwekee clip ya Mbunge au Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge alipotamka Makamba Mshenzi bungeni ili tutumie kama rejea muhimu. kama ambavyo sisi tuna clip yake anayowaita watanzania wapuuzi na wamuue.

... pamoja na speech kukaa kimipashomipasho, hakuna mahali aliposema Kamati ya Bunge imemuita MSHENZI. Acha kumlisha maneno hata kama humpendi tena maneno ya hatari.
 
... pamoja na speech kukaa kimipashomipasho, hakuna mahali aliposema Kamati ya Bunge imemuita MSHENZI. Acha kumlisha maneno hata kama humpendi tena maneno ya hatari.
Sasa hata kama hakutaja waliohoji suala hilo ni Kamati ya Bunge ya Nishati sasa wewe ndio utuambie alikuwa anamjibu nani na kama jambo hulijui ni vizuri ukaliacha lilivyo kuliko kulishabikia hili jambo ni kubwa tofauti na unavyofikiria wewe Makamba ni kiongozi Mkubwa wa Kitaifa
 
Malipo ni hapa hapa duniani acha utukanwe na bado.

Wakati clip zenu zinavuja mkimtukana Magufuli mliona raha eee
 
WALIOHOJI KUHUSU SUALA LA KUKATIKA KWA UMEME NA KUCHELEWA KWA MRADI WA JNHPP NI HAWA HAPA SOMA SEHEMU YA TAARIFA YAO ALAFU NDIO MRUDI HAPA KUBISHA

TAARIFA YA MWAKA YA SHUGHULI ZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI KWA KIPINDI CHA JANUARI, 2021 HADI FEBRUARI, 2022

[Imetolewa chini ya Kanuni ya 136 (15) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni, 2020]

Mheshimiwa Spika,
Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ni mradi muhimu sana hasa ikizingatiwa kuwa ni Mradi wa Kimkakati.

Ni matamanio ya Kamati kuona kuwa Mradi huu unakamilika kwa wakati ili kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, Kamati hairidhishwi na kasi ya utekelezaji wa mradi huu kwani maeneo mengi yapo chini ya wastani wa utekelezaji kimkataba.

iv. Kukatika Umeme mara kwa mara

Mheshimiwa Spika,
Kamati ilipokea Taarifa ya Wizara kuhusu changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini. Katika Taarifa hiyo ilielezwa kuwa, kukatika kwa umeme kuna sababu zifuatazo:

i. Kutokuwa na matengenezo ya kutosha kwenye miundombinu ya ufuaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme;

ii. Uchakavu wa miundombinu ya kufua, kusafirisha na kusambaza umeme; na iii. Kuzidiwa kwa vituo vya kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na kuongezeka kwa watumiaji ukilinganisha na miundombinu iliyopo.

Mheshimiwa Spika, Kamati Ilielezwa kuwa ili kukabiliana na changamoto hizi, tayari TANESCO imeandaa mikakati mbalimbali ikiwemo ya muda mfupi, wa kati na mrefu; na ili iweze kutekelezwa kikamilifu zinahitajika takribani Shilingi Trilioni 2.

Mheshimiwa Spika, Kamati inasikitishwa na sababu zilizotolewa kuhusu kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini kwani Kamati inaona kuwa kukatika umeme mara kwa mara ni jambo ambalo lingeweza kuzuilika endapo Serikali ingechukua hatua madhubuti kwa kutekeleza mpango wa ukarabati wa miundombinu ya TANESCO na kuipatia fedha za kutosha kwa ajili ya ukarabati.

Hii ni sehemu ya TAARIFA YA KAMATI YA NISHATI

Acha uchonganishi hakuna tatizo lolote kwenye hii clip ya Mh. Anaasa kuepukana na uongo. Watanzania tunahitaji watu wanaosema ukweli
Umesikiliza aliposema wanasema mshenzi huyo.... sasa hakuna Mbunge aliyesema mshenzi bali waliweka mezani hoja za wananchi. soma taarifa ya kamati ya nishati ndio utaelewa

Katiba mpya itasimamia maadili ya VIONGOZI wa umma na kutotukanana hovyo hapa NCHINI!

Pia itaondoa viongozi wabovu na wa wavivu kusimamia miradi ya SERIKALI na WANANCHI!

Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA!
 
Umesikiliza aliposema wanasema mshenzi huyo.... sasa hakuna Mbunge aliyesema mshenzi bali waliweka mezani hoja za wananchi. soma taarifa ya kamati ya nishati ndio utaelewa
Kwani yeye ametaja mbunge yoyote?
 
Acha uchonganishi hakuna tatizo lolote kwenye hii clip ya Mh. Anaasa kuepukana na uongo. Watanzania tunahitaji watu wanaosema ukweli
Mnafungua akaunti mpya kumtetea, acha mwezi wa kwanza apite kwenye tanuri na hapo ni waziri tu kazi nzito je akiwa Rais?

Ukikutana na Makamba sehemu yoyote mwambie JPM alikuwa mwanaume hajawahi kulalamika popote zaidi ya kuomba kuombewa maana kazi ni ngumu
 
Back
Top Bottom