Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Bumbuli, January Makamba leo Jumatatu ya Septemba 08, 2025 amepokelewa kwa shangwe na wananchi wa jimbo hilo baada ya kuwasili katika uzinduzi wa kampeni za udiwani kwenye Kata ya Mponde.
Makamba ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa amealikwa kama mgeni rasmi katika uzinduzi huo unaofanyika kijiji cha Kweminyasa, ambapo ametumia nafasi hiyo kumnadi mgombea Urais wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge wa Bumbuli(CCM), Mhandisi Ramadhan Singano, pamoja na mgombea Diwani wa Kata ya Mponde, Mbaraka Ramadhani Utanda maarufu kama Manyaunyau.