Elections 2010 January Makamba atumia ofisi ya rais kujitangaza jimboni Bumbuli kwa ubunge 2010

Barua feki...Iweje mhusika ashindwe kuandika jina lake kwa usahihi mara mbili kama katika hii barua hii.....Jina hapa ni "Jaruary" badala ya "January".....

Authenticity ya kipeperushi huwa inakuwa verified namna gani? How will you know kwamba hiki ni kipeperushi fake ama ni genuine? Kwanini watu tusiamini kwamba kukosea kuandika jina inaweza kuwa imewekwa purposely ili kujenga hoja kwamba kimeandaliwa na wapinzani wake?

Kama Jeshi la Polisi lingekuwa linaaminika, wangeanzia kwenye hiyo namba iliyowekwa hapo ili watu wakapate kadi za bure and from there wangejua nani anaendesha hizo kampeni. Lakini Jeshi letu la Polisi na TAKUKURU, hawana ujasiri wa kuchunguza na wakifanikiwa kuchunguza na wakagundua kwamba ni mtoto wa Makamba kweli, wataishia kusema stori nyingine za ajabu ajabu ili kufunika ukweli.
 

Kwani Januari mwenyewe ameshakanusha kuwa hahusiki na barua hiyo?

Tatizo linalokuja hapa ni pale anapotumia neno "Ikulu" chini ya jina lake, hata kama hakuwa na maana kuwa hilo ni agizo la Ikulu, wananchi wa kawaida watajua kuwa hiyo ni barua iliyotoka Ikulu. Matumizi ya neno "Ikulu" yanaweza kusababisha balaa kama mpinzani wake ataamua kuweka mwanashiria machachari ili kumtengua huyo Januari.
 
tatizo watu hawafikilii na nakuona nini impact ya vitu kama hivi, leo January ameachiwa afanye kampeni kabla ya wakati na wanaomfanyia kampeni ni viongozi wa chama ikiwa ni kinyume kabisa cha kanuni za chama hichohicho.

Je hapa usawa utakuwepo kweli? au uchaguzi utakuwa wa haki na sawa kweli?

zipo taarifa na ushahidi wa kutosha hata Mzee Makamba anafanya kampeni za kushinikiza kijana wake achukue nafasi tena si kwa kuomba ni kama lazima. Je hii ni demokrasia?

lakni pia lakini sheria mpya ya uchaguzi inampa nafasi kubwa katibu mkuu wa chama katika kuteua mgombea, je hapo itakuwaje?
 
Hivi mnamjua huyu mnayemsifia au mnamsikia tu? Kabla ya kusema yupi anafaa au hafai, mchunguzeni kwanza undani wake.

Watafuteni watu walio karibu naye, si lazima wawe marafiki wake. Binafsi, namfahamu Januari (ndio jina halisi, sio lile lenye Y), na kwa kumfahamu kwangu, nasema kazi ya SIASA hataiweza. Bora abaki kuwa msomi tu!
 
Ndugu zangu Watanzania ninaomba tufunguke macho,

Hawa wazee amabao wapo madarakani wanawaandaa watoto wao,kuchukua nafasi zao,Lakini Mwalimu Nyerere hakufanya hivyo,Tanzania ni kweli sio nchi ya Kifalme ya kurisishana uongozi,

Tuwe makini sana kwa jambo hili,mbegu hii ni wala rushwa tu,nina washauri hao wananchi wa Bumbuli wawe makini katika kufanya maamuzi yao

Chema chajiuza kibovu chajitembeza

Elisante Yona
 
Mie nshawaambia
Mwaka huu watanihonge VogueSiwapigii kura yangu, siwezi kufanya ujinga wa kuwatengenezea ugali hawa jamaa.

Waliniweza 2005 tu waliponipa T-shirt zao nigawe pale Mlimani kisha wao haooooo wakaishia, nikaambulia laki tano tu.

Nasema NIMEKOMA, na wala msinifuate tena.

Niacheni nikalime mapeasi na nyanya kule Lushoto na kaka Beee Mkaa hapaa

Shemdodo
 

........................ sema usiogope, sema !...................:cheer2:
 
Hii desturi ya kurithishana madaraka itatufikisha pabaya sana katika Taifa letu. Sisemi ni vibaya kwa mtoto kufuata nyayo za baba yake, bali ni vibaya mtoto huyo kubebwa kwenye njia hiyo hata kama hana uwezo na utashi.

Janauari Makamba kwa kiwango chochote siyo mtu wa jimbo la Bumbuli kwa hiyo hana uwezo kuwaongoza watu usiyo na uchungu nao.Huyu siyo mzawa wa Bumbuli wala hajahi kuishi katika jimbo hili hivyo hiyo pekee inamnyima sifa ya msingi ya kuweza kugombea uongozi.

Jimbo la Bumbuli halina ukame wa wazawa wenye moyo wa kizalendo kuweza kuliongoza Jimbo hili. Nitawashangaa saaaaana watu wa Bumbuli wakichagua mamluki mwenye nia ya kuwatumia kaka daraja la kupatia uwaziri ambao kwa serikali ya JK hutolewa kishikaji.

Kwa taarifa yenu huyu ni mtoto wa kufikia wa Makamba, na mama yake siyo mzawa wa jimbo hili yeye ni mwenyeji wa Kagera.
 
Upuuzi wa serikali ya jk na ikulu takatifu, ikulu haikuwahi kuchezewa namna hii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Inaonyesha ndugu yetu nawe umo, enzi hizo laki tano sio haba !!!!! Unaweza kuwarudishia ili kuonyesha hasira ulizonazo juu yao !
 
Jiulize

Ina maana Kampeni zimeanza ama?.........sasa jiulize

1.Tume ya Uchaguzi ipo wapi?
2. Maafisa Usalama wa Taifa wapo
3. Police wa eneo husika wapo?


Hawa watu wanafikiri WaTZ bado tu Wajinga.........
 
Tatizo la viongozi wa Kiafrika wengi wao huwa wanaboronga wakiwa madarakani sasa pindi wanapohisi muda wao umefika huwa wanajiandaa kwa mambo makuu mawili, moja ni kuhakikisha kuwa wanaacha watu wao madarakani ili kuwa na uhakika wa kulindwa kwa maovu yao waliyoyafanya wakiwa madarakani, pili hupenda kuongoza hata nje ya mfumo rasmi na ili kufanikisha hilo ndio huamua kuweka watu wao ili wawe kama puppet ( mwanasesere) wamchezee wanavyotaka kwa maslahi yao!
 
kinachonisikitisha ni upendeleo wa waziwazi anopewa January na kuacha huru akilivuruga jimbo na chama;

1. Anafanya kampeni za wazi
2. anatembea na viongozi wa chama kujinadi kinyume na kanuni
3. anatoa hongo waziwaz kwa wananchi ikiwa ni pesa,khanga na pikpiki...

4. malalamiko yot dhidi yake hayafanyiwi kazi na viongozi wa chama....
 

You could be absolutely right. Tatizo ni kwamba siasa za madaraka (power politics) za Tanzania hivi sasa zinaendeshwa kwa kujuana na kwa kutumia nyenzo za dola kuhakikisha ushindi unapatikana kwa "mteule".

Ndio maana wengine bado tunatafakari kauli ya muungwana kutozijali kura za wafanyakazi kama ujumbe hasa haukuwa kura si hoja katika ushindi wake na wa "wenzake". Hivyo, ugombea wa bwana Januari hauwezi kuepuka kutiliwa mashaka kama si mwendelezo wa mwelekeo wa ujenzi wa falme za baadhi ya wakulu nchini.
 
barua husika haionyeshi mhuri inavyoonekana rafu za kisiasa zimepiga hodi jf! mi simo!
 
Mimi hushindwa kuelewa, kwani kama January au Ridhwani anataka kuwa mbunge sasa ndo azuiliwe tu kwa kuwa baba yake ni Mtawala? Kesho tutasikia na watoto wa Lipumba au Mbowe nao wanataka kuiongoza CUF au VEMA, napo tutalalamika? au kwa kuwa watu mna chuki tu na CCM?

Mbona watoto wa MaDr wengi ninaowafahamu walisoma Udaktari na wakawa madaktari? Napo tutalalamika? Mbona Bush Jr naye alikuwa President wa Marekani au Karume Jr naye alikuwa wa Zenji...nao si ni binadamu na wana ndoto na malengo yao, kama ilivyokuwa kwa Baba zao! Kama wewe unayelalamika hapa unataka Uongozi au hutaki January au yeyote yule awe Kiongozi basi kapambane naye tu Ki-demokrasia, kwani unakatazwa?

Kumnyima mtu haki au hata kuhoji dhamira yake ya kutaka uongozi ni kuishambulia demokrasia na si sahihi hata kidogo! Hivi siku mwanao akitaka kuwa na nafasi kama ya kwako utamkataza? au kwa kuwa ya kwako ni ndogo tu na haijulikani sana kwa watu?

Tuweni na mitazamo CHANYA walau, mabadiliko ya nchi yetu hayatoletwa na kulalamikia kila kitu, tufanye kazi kwa kujipanga bwana
 
kinacholalamikiwa sio mtoto wa makamba kugombea ubunge,kinacholalamikiwa ni mtoto wa makamba kutumia wadhifa wa baba yake kujinadi,hiyo siyo demokrasia tena,yeye agombee yeye kama yeye sio kutumia cheo cha baba yake.

kwa mfano ingekuwa sio mtoto wa makamba takukuru wangekuwa wameshamuhoji kwa kuanza kampeni mapema lakini hawawezi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…