Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Haya
😂😂😂1. Rais ana wabunge wake.
2.Chambo kwa upinzani.
Huyu ni mtu muhimu mno kwa CCM. Kumuachia kirahisi hivyo kunatia shaka.
Amandla...
Makamba ni mtu ni kama vile MtakaHuyu jamaa amejua kujizuia hisia zake
Nafikiri ile exposure ya kufanya kazi na Viongozi tofauti tofauti vimeweza kumjenga
Kila la heri kwenye maisha mengine nje ya Ubunge!
Ni kweli MkuuMakamba ni mtu ni kama vile Mtaka
Hawezi kufa njaa. Bado kijana na kuna vyeo vingi serikalini ( ubalozi, Mkuu wa Taasisi n.k.) na kwenye Chama.Ananyenyekea Ili huku mbeleni ateuliwe kwenye cheo Fulani asife njaa, huo ndo ukweli
January hana akili anatumia mbinu za Lowassa ambazo zilikuwa sahihi wakati ule sio sasa. Yaani kwamba waandishi wameshtukiza ofisini kwake🤣🤣🤣 kwamba wamepigiana simu kwamba twendeni ofisini kwake na yeye hakuwa na taarifa! Tapeli mtupu.Mbunge wa Jimbo la Bumbuli anayemaliza muda wake, January Yusuph Makamba, amesema amepokea kwa moyo mkunjufu na utulivu maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kumuengua kwenye orodha ya wanachama wanaowania kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Makamba amezungumza hayo siku ya Jumatano wakati akizungumza na waandishi wa habari wa walioshtukiza na kufika ofisini kwake kwa lengo la kupata kauli yake kuhusu hatua hiyo ya chama.
“Ninaipokea na kuitii kwa moyo mmoja uamuzi wa Kamati Kuu. Mimi ni mwanachama na kiongozi mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi. Chama kina taratibu zake, na wajibu wangu ni kutii maamuzi ya vikao vyake,” amesema Makamba.
Ameeleza kuwa ameshawasiliana rasmi na uongozi wa CCM ngazi ya wilaya na kuwaarifu utayari wake wa kushirikiana nao pamoja na wanachama wengine kuhakikisha chama kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi huo.
Akizungumzia taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba sababu ya yeye kukatwa ni kutokana na madai kuwa anadaiwa kuwa na nia ya kugombea urais wa Tanzania, Makamba amekanusha vikali madai hayo, akisisitiza kuwa hana nia hiyo kwa sasa na kwamba hajawahi kuonesha dhamira hiyo.
“Mimi si mgombea wa urais, wala sijawahi kutangaza nia hiyo. Hayo ni maneno yanayozunguka kwenye medani za siasa. Kwenye siasa changamoto kama hizi ni za kawaida, na mimi niko tayari kuzipokea kwa heshima na utulivu,” amesema.
Kuhusu tetesi zinazodai kuwa huenda akahama chama kutokana na kukatwa katika mchakato huo, Makamba amekanusha uvumi huo akisema bado yupo ndani ya CCM na kwamba chama hicho bado kinabeba imani na maono yake ya kisiasa.
“Niko CCM, na niko sana. Chama hiki ndicho kilichonilea, kimenipa nafasi za kuwatumikia wananchi na bado naamini katika misingi yake. Sio kila changamoto ni sababu ya mtu kuhamahama,” amesisitiza.
Makamba aliwahi kuwa mbunge wa Bumbuli kwa vipindi vitatu na kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Nishati
Source Jambo TV
Wewe hiyo mimba aliyokuachia dhalim Magufuli imekufanya kuwa taahira kabisaLaana ya kushangilia kifo cha Magufuli inawatafuna
Qmmmae zake. Anatakiwa awe ndani kwa ufisadi pale Tanesco akiwa waziri wa nishati. Ahame chama aone kama hawajamtapisha fedha zote alizofisadi. Ccm ni mafisadi wakubwa qmmmae zao.Mbunge wa Jimbo la Bumbuli anayemaliza muda wake, January Yusuph Makamba, amesema amepokea kwa moyo mkunjufu na utulivu maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kumuengua kwenye orodha ya wanachama wanaowania kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Makamba amezungumza hayo siku ya Jumatano wakati akizungumza na waandishi wa habari wa walioshtukiza na kufika ofisini kwake kwa lengo la kupata kauli yake kuhusu hatua hiyo ya chama.
“Ninaipokea na kuitii kwa moyo mmoja uamuzi wa Kamati Kuu. Mimi ni mwanachama na kiongozi mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi. Chama kina taratibu zake, na wajibu wangu ni kutii maamuzi ya vikao vyake,” amesema Makamba.
Ameeleza kuwa ameshawasiliana rasmi na uongozi wa CCM ngazi ya wilaya na kuwaarifu utayari wake wa kushirikiana nao pamoja na wanachama wengine kuhakikisha chama kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi huo.
Akizungumzia taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba sababu ya yeye kukatwa ni kutokana na madai kuwa anadaiwa kuwa na nia ya kugombea urais wa Tanzania, Makamba amekanusha vikali madai hayo, akisisitiza kuwa hana nia hiyo kwa sasa na kwamba hajawahi kuonesha dhamira hiyo.
“Mimi si mgombea wa urais, wala sijawahi kutangaza nia hiyo. Hayo ni maneno yanayozunguka kwenye medani za siasa. Kwenye siasa changamoto kama hizi ni za kawaida, na mimi niko tayari kuzipokea kwa heshima na utulivu,” amesema.
Kuhusu tetesi zinazodai kuwa huenda akahama chama kutokana na kukatwa katika mchakato huo, Makamba amekanusha uvumi huo akisema bado yupo ndani ya CCM na kwamba chama hicho bado kinabeba imani na maono yake ya kisiasa.
“Niko CCM, na niko sana. Chama hiki ndicho kilichonilea, kimenipa nafasi za kuwatumikia wananchi na bado naamini katika misingi yake. Sio kila changamoto ni sababu ya mtu kuhamahama,” amesisitiza.
Makamba aliwahi kuwa mbunge wa Bumbuli kwa vipindi vitatu na kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Nishati
Source Jambo TV
Anaogopa ufisadi wake unaweza mtupa gerezani.Ananyenyekea Ili huku mbeleni ateuliwe kwenye cheo Fulani asife njaa, huo ndo ukweli
Hivi mtu wa 28 January, 1974 ana miaka 51 ni kijana?😁😁😁Hawezi kufa njaa. Bado kijana na kuna vyeo vingi serikalini ( ubalozi, Mkuu wa Taasisi n.k.) na kwenye Chama.
Amandla...
Nimeona, na Makamba ni King au Queen!??Kuna chess inachezwa.
Amandla...
Labda kwake huyo ujana una maana nyingine.Hivi mtu wa 28 January, 1974 ana miaka 51 ni kijana?😁😁😁
Unatumia vigezo gani?
Katika siasa ni kijana. Watu wanagombea hata wakiwa na miaka 70 hadi 80. Kuna mwengine anagombea urais akiwa na miaka 90.Hivi mtu wa 28 January, 1974 ana miaka 51 ni kijana?😁😁😁
Unatumia vigezo gani?