Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Waziri wa Nishati, January Makamba, amesema kuwa, majadiliano yanayohusu Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia baina ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji Kampuni ya Shell ya Uholanzi na Equinor ya Norway na washirika wao yamekamilika na kwamba sasa wataalam wapo katika kazi ya kuandika mikataba ya mradi huo.
Waziri wa Nishati ameyasema hayo tarehe 06 Machi, 2023 jijini Arusha wakati akitoa vipaumbele vya Wizara katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati ambapo pamoja na masuala mengine ya kiutumishi, Baraza hilo limepitia Mpango wa Bajeti wa Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/2024.
“Mazungumzo ya mradi huu wa LNG yamekamilika na wataalam kwa sasa wanaandika mikataba mikubwa miwili yenye masuala mengi ikiwemo ya kiufundi, Mkataba mmoja ni wa Nchi Hodhi (HGA) na mwingine ni mkataba uliounganishwa wa vitalu vya Gesi Asilia Namba I,II na IV ambavyo gesi yake itatumika kwenye mradi wa LNG, kila mkataba una takriban kurasa zaidi ya 600, hii si kazi ndogo ila nimewasisitiza wamalize kazi mwezi huu ili kuweza kuendelea na hatua nyingine za utekelezaji.” Amesema Makamba
Amesema kuwa mradi huo ambao uwekezaji wake ni zaidi ya Shilingi Trilioni 70 utaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi nchini na utaifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazochangia katika usalama wa nishati duniani hivyo amewataka Watendaji wa Wizara ya Nishati kuendelea kusimamia utekelezaji wa mradi huo.
Makamba ametaja mradi mwingine unaoendelea kutekelezwa ni wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania ambapo kwa sasa shughuli mbalimbali za maandalizi ya ujenzi zinaendelea na mwezi uliopita Serikali imetoa kibali cha ujenzi wa bomba hilo kwa kampuni ya EACOP na kwa sasa inaendelea kukamilisha taratibu za kupata pesa za kutekeleza mradi huo ambazo zimefikia mwishoni.
Ameongeza kuwa, zoezi la ulipaji fidia kwa watu 9800 katika mkuza wa Bomba la mafuta zinaendelea ambapo mpaka sasa shilingi Bilioni 29.2 zimelipwa kati ya shilingi Bilioni 30 zilizokuwa zinahitajika kwenye ulipaji fidia na matarajio ni kwamba ujenzi unatarajiwa kuanza kabla ya mwisho wa mwaka huu.