January Makamba, Nape Nnauye na Mwigulu Nchemba, kama mna ndoto za kuja kuwa Marais kwenye Nchi hii basi futeni hizo ndoto

Ndivyo system ya sasa inavyofanya kazi ni ama ulambe asali ufunge mdomo au upambane na dola
Wanaliwa na system zao za kibwege plus roho za kimaskini kwenda shule na kurudi wezi.😂
 
Vijana mmeaminiwa na Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania kwa kupewa uwaziri lakini mnachokifanya kwenye wizara zenu ni madudu tu. Hamjaonesha kuwa mko competent kuweza kugombea nafasi ya Urais hapo mbeleni.

i.
Wafute ndoto zao kwa wananchi gani,hawa hawa wanaofanya uongozi kuwa mabishano ya Simba na Yanga ?
 
Kabisa. Hata wakiongea jambo huoni kama wapo upande wa Wananchi wapo upande wa kujijali wao tu.
 
Ukiona hawafukuzwi maana yake ni utendaji wao unamridhisha aliyewateua
utendaji sio utendaji - wao wanamridhisha aliyewaweka! limits zinazingatiwa na kuwa bendera fwata upepo enough to impress their boss!
 
Wakiamua kugombea urais hakuna mtz yyte WA kuzuia Hilo. Sio wewe sio Mimi Tanzania kama Kuna mwanasiasa umpendi dawa ni moja tu. KUMOMBEA AFE KIFO CHA GHAFLA vinginevyo tutabaki kufarijiana tu JF
 
Kwani inahitaji rocket science kulitambua hili?
Hela za uchaguzi ujao zinakusanywa kwa sababu hatuna vyanzo vingine vya mapato
Hakuna bidhaa za kuuza nje kutuingizia dollars na pesa za kigeni na uchaguzi uko kwenye kona tu
 
Wakiamua kugombea urais hakuna mtz yyte WA kuzuia Hilo. Sio wewe sio Mimi Tanzania kama Kuna mwanasiasa umpendi dawa ni moja tu. KUMOMBEA AFE KIFO CHA GHAFLA vinginevyo tutabaki kufarijiana tu JF
Katiba Mpya itakapatikana muda si mrefu kwa hiyo hiyo ndoto yao ife
 
Katika Jambo Magufuli alijatibu kufanya lenye manufaa ni kuondoa mizizi yote ya wanajiona kama Icon katika Nchi-bahati mbaya baada ya kufariki wamerudi wale wale.
 
Katika Jambo Magufuli alijatibu kufanya lenye manufaa ni kuondoa mizizi yote ya wanajiona kama Icon katika Nchi-bahati mbaya baada ya kufariki wamerudi wale wale.
Kabisa mkuu. Yaani wamekosa maarifa ya uongozi hawa watu. Wao wanapewa vifurushi kupitia kodi zetu, kodi zetu ndizo zinafanya wafanye maamuzi ya hovyo.
 
Hawa uliowataja, ninadhani sisi raia kuwataja kila mara na bila ya Rais kuwaondoa kwa madhaifu yao ya wazi, anawaunga mkono.

Na katika baraza lao la mawaziri, mwenyekiti akiwa ndiye Rais, maovu yote wanayotutendea bila ya kumumunya maneno, yana baraka zake.

Haiwezekeani lijitokeze ombwe la kutisha la uongozi kwa kipindi kifupi hiki cha uongozi wake akae kimya bila kutia neno, ni ngumu sana!

Magufuli aliwaondoa kwa aibu kwa sababu aliona hawafai, Rais wa sasa muda huo yeye akiwa naibu na mshauri mkuu!

Alivyowarejesha kwa kubadili gia angani tukadhani anawafuta machozi ya pole ya kuondolewa kwao kwa uonevu, kumbe walipokea "sakramenti" inayowahusu na hawakustahili msamaha wa "kabila" hiyo.

Asipowapumzisha na akiendelea kuwakumbatia kama vifaranga, wanamharibia sana tena wazi wazi utawala wake huu ambao watu waliuchukulia kama wenye kuleta matumaini.

Jamani, ama ni mbinu ya kumchafua huyu Rais ili nchi isitawalike wao wakamate uongozi?

Maana tukumbuke kuwa, wote hao walichukua fomu za kugombea urais '15 nadhani wana ajenda ya siri inayohusu uchu wa madaraka!

Tunakoelekea hali hii isipobadilika, nadhani itafika pahala waTz wote tutaongea lugha moja bila kujali itikadi zetu za kisiasa, kidini ama kikabila isipokuwa kwa genge dogo la walamba asali ambao ni la wachache na hapo ndipo patakapokuwa patamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…