January Makamba, uliteuliwa ili usimamie ukatwaji wa umeme?

Sijui ni jambo gani huwa anamwambia mkuu naye anamuamini

Maana umeme unakatika kila mara na mkuu haonekani kuguswa kabisa na hali hii.
Mkuu tangu uwekewe vipande vya chupa kwenye msosi umekuwa mpoleeeee hata dhihaka kwa Chadema, Bavicha na mwamba Mbowe huzitoi tena. Umejichimbia zako huko Longido ndani ndani.

Vipi Sasa lami kuwekwa kutoka Sanya juu hadi Longido? Tuondoe tofauti na itikadi zetu tupaze sauti Maza labda atatusikia.
 

Kuteuliwa kea January Makamba kuongoza Wizara ya Nishati na mara baada ya uteuzi wake kuivunja Bodi ya Tanesco na kuisimika nyingine ikiongozwa na ISSA; ni mkakati wa makusudi wa kutaka kupata sababu za kuanza kuivunja TANESCO kuwa mashirika matatu yanayojitegemea ya GENERATION, TRANSMISSION na DISTRIBUTION halafu baada ya hapo yauzwe!!

Kumbukeni kuwa huyo Mwenyekiti wa sasa wa TANESCO ndio alikuwa dalali wa kuliuza shirika la Simu [TTCL] hivyo uteuzi wake ni wa malengo!!
 
Watz wengi wamejaa ujinga vichwani mwao, utayasikia yakisema mama anaupiga mwingi, anaupiga mwingi kwa kutuletea majina badala ya watendaji,haya huyo January anafanya nini hapo,kuna yule mama wa foreign Mulamula hana lolote, kuna Mchengerwa anasema uongo kila siku eti watumishi watalipwa malimbikizo kabla ya christmas hakuna aliyelipwa anazunguka nchi analipwa pesa anaongea uongouongo tu.Ametutolea jembe Kalemani akatuletea wahuni masela wapiga dili tu,wakate umeme mazima sasa ovyo kabisa.
 
Duuh udalali tena??

Imekula kwetu.
 
Kukatika umeme kunatokana na umasikini wa nchi yako na si vinginevyo. Fanya utafiti utaelewa.
Umasikini sio point hapa, kwasababu hata kipindi cha Magufuli umasikini ulikuwepo na hakukuwa na tatizo la kukatika kwa umeme hovyo hovyo kama hivi leo. Tatizo ni management inagoongozwa na January kama Waziri wa nishati.

Waziri ameonesha dhahiri kushindwa kusimamia hii wizara kinachoshangaza mamlaka ya uteuzi iko kimya juu yake. Hii inaleta maswali mengi sana;

Je hicho kinachofanyika sasa hivi ndio hasa alitumwa kufanya na mteule wake?

Je mamlaka imekaa kimya kwasababu haijui kinachoendelea?

Au Waziri ni mmoja wa wenye chama kama anavyosema Nape kwamba Chama kimerudi kwa wenyewe?
 
Yulr wa foreign ndio hata kusoma hajui[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] ni matapeli tuu na madalali wa wqzungu
 
Kuwa mstaarabu basi unapomjadili Rais. Maneno yako hayana chembe ya busara na ni ya kihuni sana. Ukikosa nidhamu hadharani tena unaibua maswali ya malezi yako. Si sahihi.
 
Hivi hotuba ya Mheshimiwa Waziri wakati anafungua mafunzo ya uongozi mbona hamuileti jamvini?

Anasema uongozi pamoja na mambo mengine ni ule uwezo wa mtu kuelekeza watu na watu kufuata maelekezo yako (kama nilimuelewa vizuri). Najiuliza, wale aliowaelekeza wasikate umeme ndani ya wiki vinginevyo atashughulika na mtu lakini umeme bado unakatwa, Je. Anaturuhusu tutilie mashaka ushawishi wake kwa anaowaongoza?
 
-TANESCO sasa hivi ni majanga,toka Waziri mpya na Bodi mpya viiñgie madarakani,shida siyo kukatika umeme tu,bali hata nyaya za 50mm shirika halina,
-juzi nilikwenda TANESCO Chanika,kuna wateja zaidi ya 300 wamejengewa nguzo, lakini hawajaunganishiwa waya wa 50mm,ili mchakato wa kupewa control number,walipie service line na
-wananchi hawa hawalipi kodi ya majengo,( ambayo inalipwa ) kupitia Luku.
-Mama SSH watendaji wako wanakuhujumu,usifikie malengo ya kukusanya kodi ya majengo.
-Wafanyakazi wa TANESCO wanamajibu ya kuudhi na inavyoonekana,Maharage ameishiwa pumzi mapema na hana jipya jahazi linazama.
 
Anatajwa kwa sababu wengi bado wanajiuliza ilkikuwaje really Samia akamuona January anafaa kuwa waziri wa nishati mtu kama mtu Januari ni mtu mzuri lkn siyo kwa wadhifa huo muhimu
Hapa Kalemani alipaweza sn pamoja na madhaifu ya kibinadamu lakini alikuwa mfuatiliaji kupita kiasi
 
Bibi ushungi aliingizwa cha kike kwa January
 
January Makamba hiyo wizara ni kubwa sana kwake.yeye ilimfaa ile ya utamaduni na michezo au jinsia na watoto.aliyempa hiyo wizara ndio mwenye matatizo sio January.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…