Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,294
- 10,970
- Thread starter
- #161
Una misemo mikali sanaKuna watu wana damu ya uongozi na kuna wanaojipaka mafuta ya uongozi. Mwenye damu hata ukimwamsha usingizi usiku wa manane, jibu lak linasikilizwa kwa uhakika na kuwekwa maananani na anaowaongoza; yule mwenye kujipaka mafuta, ukimwamsha usiku wa manane atatoa jibu ambalo watu hawatatilia maanani mpaka akaoge ajipake mafuta kwanza. Na hata akishajipaka mafuta ya uongozi, akipigwa jua kidogo tu akatoka jasho au akinyeshewa mvua, mafuta yote yanaondoka anakuwa yule yule asiyetiliwa maanani.