Japan imeruhusu watafiti kuumba binadamu

Japan imeruhusu watafiti kuumba binadamu

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
𝗝𝗔𝗣𝗔𝗑 π—œπ— π—˜π—₯𝗨𝗛𝗨𝗦𝗨 π—ͺπ—”π—§π—”π—™π—œπ—§π—œ π—žπ—¨π—¨π— π—•π—” π—•π—œπ—‘π—”π——π—”π— π—¨

1_20250128_182723_0000.png

Dunia na maajabu yake!! πŸ‘‹
Nchini Japan mwaka 2019 waliweza kupitisha Utafiti kwa kuweza kuwaruhusu Wanasayansi kuweza kuumba Wanadamu.

retrato-criatura-marina-surrealista_23-2151625954.jpg

Mfumo huo ambao unakusanya viungo vya Wanyama na binadamu ili kuweza kukuza viungo vya binadamu ndani ya mnyama kwa njia ya kupandikiza. Watafiti hao wakiongozwa na Jamaa mmoja anaitwa Hiromitsu Nakauchi.

retrato-criatura-marina-surrealista_23-2151625986.jpg

Utafiti huo unaruhusisha kuingiza seli za binadamu kwenye viinitete vya wanyama (animal embroys) kwa nguruwe na panya, ili kuweza kukuza vya binadamu. Bado kuna wasiwasi wa kimaadili unaweza kujitokeza kuhusu kuchanganya Seli za kibinadamu na Wanyama haswa kwenye ukuaji wa Ubongo.

retrato-criatura-marina-surrealista_23-2151625971.jpg

Sheria mpya imeruhusu utafiti huo kukuza hadi kuwa mnyama binadamu kamili, hivyo kuzua mijadiliano mikali kati ya Sayansi ya Matibabu na uumbaji wa Mungu.

3_20250128_182724_0002.png

Usisahau kutembelea page ya #bongotech255 utajifunza mengi zaidi ✍️
3_20250126_193857_0002.png

#bongotech255 #human #hybrid #humanhybrid #teknoloji #japan #scientist #animal #dunia
 
Ninajichejekesha hapa. Mawe

Ulaya wanatengeneza Steak, kuku bila vichwa, wanauzwa supermarket na kusindika kwenye makop.Yaani teyari wanafanya hivyo, wengine wanasubiri leseni.

Hata hivyo, hujaumbika mpaka umekufa.
Nacheka kana mazuri. Mawe
 
Tunakokwenda panaogopesha sana watu wanaleta mchezo na Mungu waziwazi πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 
Kuna mafanikio yoyote tangu 2019
Waliruhusu 2019 lakini mchakato unaanza kufanya kazi mwaka huu 2025 πŸƒβ€β™‚οΈ japo kuna baadhi ya Taarifa zingine wamesema Siri hawawezi sema lakini kwa ufupi tu wanasema wamefanikiwa kwa asilimia 75%
 
Huko kuzaliana issue; wacha watumie njia mbadala kuijaza nchi.
 
Huyo muazirishaji sijui nani nakauchi Japan mbona Wana majina hivyo
 
Kwa maisha haya ya kibongo kuna watu wanaona Bora wakaumbwe upya Japan
 
Tunakokwenda panaogopesha sana watu wanaleta mchezo na Mungu waziwazi πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
Mkuu hapa tulipo panaogopesha.

Natamani ningeweza kuishi milele, ...ukiondoa ushabiki wa dini....hata kurudi nyuma na kusawazisha mambo fulani yaliyopita. Nasikitika hayo hayawezekani. Labda hao wajuvi wangeweza kulifanya hilo, ningekuwa na mtazamo tofauti. Lakini haya ya ma hybrid, Mawe.

Ila, kwa maoni yangu, naona jinsi mataifa makubwa yatakavyokuja kuporomoka. Mungu hadhihakiwi
 
Kwa maisha haya ya kibongo kuna watu wanaona Bora wakaumbwe upya Japan
Mkulu, nakuhakikishia hakuna binadamu yeyote yule bongo anyetaka akaumbwe tofauti na alivyo umbwa.
Naomba nikuulize kwa heshima na taadhima, ww una maisha gani ya kibongo yanayokufanya utake kuumbwa tena? Ondoa Siasa, Ondoa ubaguzi, ondoa any bias kwenye majibu yako, titaelewana

Kumbuka "hujafa, haujaumbika"
 
Watafanikiwa tu, kama kuna kuku wa kienyeji na kisasa, watashindwaje kwa binadamu?
 
Watafanikiwa tu, kama kuna kuku wa kienyeji na kisasa, watashindwaje kwa binadamu?
Huu mfano wako wa kuku wa kienyeji na kisasa, ni sawasawa tu na mchina anavyozaa na mswahili n.k.hamna jipya sana...
Sema kutengeneza pure binadamu kama sisi..hawawezi na hawataweza: Mwanadamu ni perfect machine - yenye utashi na personal decisions - ni mashine ambayo sio programmed HAKUNA mashine nyingine yoyote inawezakuwa hivyo..
Hata akili mnemba wakati mwingine anajibu kipumbavu mpaka mtu unastuka
 
Mkulu, nakuhakikishia hakuna binadamu yeyote yule bongo anyetaka akaumbwe tofauti na alivyo umbwa.
Naomba nikuulize kwa heshima na taadhima, ww una maisha gani ya kibongo yanayokufanya utake kuumbwa tena? Ondoa Siasa, Ondoa ubaguzi, ondoa any bias kwenye majibu yako, titaelewana

Kumbuka "hujafa, haujaumbika"
Tunasherehesha jukwaa tu mkuu, I'm not serious
 
Huu mfano wako wa kuku wa kienyeji na kisasa, ni sawasawa tu na mchina anavyozaa na mswahili n.k.hamna jipya sana...
Sema kutengeneza pure binadamu kama sisi..hawawezi na hawataweza: Mwanadamu ni perfect machine - yenye utashi na personal decisions - ni mashine ambayo sio programmed HAKUNA mashine nyingine yoyote inawezakuwa hivyo..
Hata akili mnemba wakati mwingine anajibu kipumbavu mpaka mtu unastuka
Wakianzia kwa maiti, kwa kuiwekea mashine ya mapigo ya moyo wanaweza kufanikiwa.
 
Back
Top Bottom