Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Nchi ya Japan itatumia zaidi ya dola za Kimarekani milioni 1.83 kwenye mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Shinzo Abe baadae septemba 27 mwaka huu.
Uratibu na gharama zote za mazishi kwa kiongozi huyu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi kuliko mawaziri wakuu wote nchini humo yataandaliwa na kugharamiwa na serikali kwenye hatua zote.
Abe alifariki kwa kupigwa risasi akiwa na umri wa miaka 67 wakati akihutubia hadhara moja nchini humo.
Mazishi hayo yanayo kadiriwa kuhudhiriwa na zaidi ya watu 6000 yanakutana na pingamizi kubwa kutoka kwa watu wengi nchini humo ambao hawataki yafanyike kitaifa kwa kuwa siyo kawaida ya nchi hiyo.
Mtu mmoja ameripotiwa kujichoma moto karibu na Ofisi ya Waziri Mkuu nchini humo kama sehemu ya kuonesha kutokuafikiana na mpango huo.
Aljazeera