Japan waendelea na utamaduni wao wa kusafisha chumba cha kubadilishia nguo baada ya mechi

Japan waendelea na utamaduni wao wa kusafisha chumba cha kubadilishia nguo baada ya mechi

Hawa watu wana Discipline sana kuanzia kwenye muonekano wao, Ukataji wa nywele, uvaaji na hata ngozi no Tattoo.
Hawazingatii kingine chochote zaidi ya Malengo na Nidham.
ELIMU YA URAIA NA MAADILI HUKO INAFANYA KAZI.
 
Japan kwa mara nyingine wameacha chumba chao cha kubadilishia nguo kikiwa katika hali ya usafi wa hali ya juu baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Uholanzi, Moja ya mila na desturi bora zaidi katika ulimwengu wa soka.
Baada ya mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia dhidi ya Uholanzi, kwa mara nyingine tena wamekiacha chumba hicho kikiwa safi wa kupindukia.

Na hii si mara ya kwanza. Huwa wanafanya hivi kila mara. Wanaichukulia tabia hii kama ustaarabu wa kawaida kabisa na ishara ya heshima kwa wengine, huku mashabiki wao nao wakikusanya na kusafisha taka zote walizoacha uwanjani.

Kongole kwao, wako vema
 

Ningeishi Japan ningeinjoy sana,hao ni mimi kabisa yani,huwa sometime natamani hata kusafisha mtaani kwangu ambako watu ni wachafu​

 
Back
Top Bottom