Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218

Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218

Hapa nakuunga mkongo. Ukiwauliza wanaoulinda huo muungano umeleta faida gani hawana majibu. Umaskini Zanzibar umezidi. Zanzibar ingeungana na nchi mama yao Oman leo hii Zanzibar ingekuwa kama Muscat. Utajiri wa mafuta ungechuruzika mpaka kufika Zanzibar. Makosa ni kuungana na nchi fukara iliyoitwa Tanganyaika iliyojaa watu wenye ukabila, ukanda, udini, ubaguzi, ufukara wamebaki kuirudisha nyuma Zanzibar na siasa chakavu.

#FreeZanzibar
Mwishowe mtaja olewa sasa hivyo,kwa mwendo huo,yaani kila kitu Oman wawaletee tu nyie mkalishe kitako Ivyooo!,Mshukuru muumba mmekingwa na balaa kubwa.
 
Kwani Tanzania mna akili,big up Kenya ,Mliisha sahau KANU
 
Hoja zako zipo wapi?
Je, Zanzibar wana Bajeti ya Ulinzi , Mambo ya ndani, nje, Wizara za muungano na taasisi zake?

Je, mikopo inayochukua ambayo si tatizo, watarudisha kwa utaratibu gani?
Ikiwa hawawezi kumalizana na Tanesco, mabilioni wanayokopa nani atakayelipa? Mtanganyika!

Tunasema, wakati umefika turudi rasimu ya Warioba ya mambo 7 . Tanganyika isimame na kujisimamia na Zanzibar nayo ijisimamie ikakope mtrilioni kadri inavyoweza.
Hoja zako zipo wapi?
Je, Zanzibar wana Bajeti ya Ulinzi , Mambo ya ndani, nje, Wizara za muungano na taasisi zake?

Hoja yangu ni kwamba hayo mambo uliyoyataja ni masuala ya Muungano, yanahudimiwa kutokana na mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hayahudumiwi na Tanganyika wala na Zanzibar. Zanzibar Ina Mambo yake ya kuhudumia.

Kuna sehemu umetaja kwamba elimu sio suala la Muungano. Hapo umepotosha. Elimu ya msingi ndio ambayo sio ya Muungano.

Umezungumzia wanufaika wa Bodi ya Mkopo wa Elimu ya Juu kuwa Mkopo ule kwao ni Grants. Hivi hua mnalipwa kuandika uongo na kueneza chuki kwa wananchi?

Na hata habari ya umeme umeizungumzia ki upotoshaji.



Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Serikali ya Japan imeipatia Tanzania mkopo wa shillingi billion 761.8 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo nchini!

Katika mkopo huo kisiwa cha Zanziba kimepewa mgao wa Tsh billion 218+

Kazi iendelee...

=====

View attachment 2108391

Serikali ya Tanzania na Japan zimesaini mikataba mitatu ya mkopo na msaada yenye thamani ya Yen za Japan bilioni 37.9 sawa na takriban shilingi bilioni 761.8 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ukarabati wa Bandari ya Kigoma, uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na Ujenzi wa Barabara ya Arusha-Holili.

Mikataba hiyo imesainiwa jijini Dar es Salaam, kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan, Bw. Naofumi Yamamura, kwa naiaba ya Serikali ya Japan.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mikataba hiyo, Bw. Tutuba alisema kuwa Mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma utatekelezwa kwa msaada wa Yen za Japan bilioni 2.73 sawa na takriban shilingi bilioni 54.79, ukihusisha Ukarabati wa gati za mashariki na kaskazini mwa Bandari ya Kigoma, ukarabati wa majengo ya kushushia abiria na mizigo, ukarabati wa barabara zilizopo katika Bandari hiyo na ujenzi wa majengo mapya ya abiria na mizigo.

“Bandari ya Kigoma ilijengwa katika kipindi cha mwaka 1912–1927 na imekuwa bandari muhimu katika kusafirisha mizigo na abiria kwenda nchi jirani za Burundi, DR Congo, Zambia na mikoa iliyopakana na Kigoma, hivyo kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo kutachangia kuongeza ufanisi wa Bandari, kutoa fursa za ajira, kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kuchochea shughuli za kiuchumi na kuchochea biashara kati ya Tanzania na nchi hizo jirani” alisema Bw. Tutuba

Alisema kuwa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji Zanzibar, utatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Yen za Japan bilioni 10.86 sawa na takriban shilingi bilioni 218.382 ambapo mradi huo utahusisha kujenga na kukarabati miundombinu ya maji Mjini Zanzibar.
Na kwenye kulipa zanziba watalipa walichochukuwa au inakuaje???
 
bakizeni machogo yenu hukohuko bara, mna vichwa kama Thierry Henry nchi nzima, nyie watu gani?
Wewe fala mtwana, mpumbavu usiye na akili kama wazanzibar wenzako nyamaza KIMYA. Mnaweza nini ninyi mabasha watupu huko mnanuka wapumbavu ninyi. Wewe kichwa chako kikoje wewe mtumwa mwenye bwana wa kiarabu.
 
Bila katiba mpya mtarajie zaidi ya hayo. From Chato to Zanzibar.
 
Kwani huu Muungano sisi tunaung'ang'ania una faida gani na sisi, kidhati kabisa mie sioni faida kwetu kwenye huu muungano, halafu kibaya zaidi ni sisi ndio tunafosi, wazanzibar wakitaka nchi yao inakuwa msala.

CCM inauhitaji sana huu muungano kama ulivyo no matter the cost. Na kwa vile hakuna mwenye ubavu wa kubadilisha, it’s a done deal.
 
Na infact Zanzibar kama visiwa vingine ingeshakuwa kama Dubai kitambo Sana ni vile Bara ndio wanaizuia..

Visiwa Maskini hapa Duniani ni Zanzibar na Commoros ila wakikaa peke yao Utalii wote ni Zanzibar.
Nini kimeizuia Comoro kuwa kama Dubai?
 
Inayokopa ni Tanzania.
Inayolipa au kutakiwa kulipa ni Tanzania hiyo hiyo.
Hakuna sehemu Tanganyika au Zanzibar inalipa au itatakuwa kulipa madeni yaliyokopwa na TANZANIA.

Mkitaka kuhuisha hizo ndogo zenu kwanza vunjeni Muungano kila nchi iwe huru, halafu kama mnaona bado Muungano mnauhitaji anzisheni shirikisho full stop


Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Na iwe hivyo. Kwa nini kaka mkubwa akope na mdogo ale tu bila kulipa?
 
Na iwe hivyo. Kwa nini kaka mkubwa akope na mdogo ale tu bila kulipa?
Anaekopa hapo ni baba sio Kaka mkubwa.

Kaka mkubwa nae huwa anakopewa kwenye biashara zake zisizoihusu familia namlipaji ni huyo huyo baba.

Umeipata hiyo au nikufafanulie?

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Hii hatari, mbona Zanzibar wamechukua mgao mkubwa hivyo?
Hadi kufika 2025, Zanzibar itakuwa kama Dubai! Nchi inayokopa ni Tanzania na walipaji ni Tanzania!! Zanzibar haiwezi kudaiwa maana haijakopa Zanzibar!!
 
Hadi kufika 2025, Zanzibar itakuwa kama Dubai! Nchi inayokopa ni Tanzania na walipaji ni Tanzania!! Zanzibar haiwezi kudaiwa maana haijakopa Zanzibar!!
Na mwaka huo Tanganyika itakuwa Kama China.
Nchi inayokopa ni Tanzania na walipaji niTanzania. Tanganyika haiwezi kudaiwa maana si iliyokopa. Nadhani tunaelewana

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Usinikumbushe wakati
Yani wangekuwa wanalipa deni kama sisi isingekuwa shida sema ni kwamba hata umeme kulipa huwa unawashinda!
Kiongozi wa juu wa Zanzibar bila kumung'unya maneno alisema tuko tayari mtukatie umeme tutawasha vibatari!! Baada ya kuona hawawezi kulipa deni la umeme!!
 
Nadhani wao wako mil 1 huku Bara tuko mil zaidi ya 40....
 
Wajinga ni sisi ndio tuliwao. Acha tuisome namba
 
Back
Top Bottom