DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mwanasiasa kijana na mtaalamu wa masuala ya udhibiti wa bidhaa za tiba, Japhari Saidi, amechukua rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Jimbo la Singida Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Japhari amesema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira yake ya kurudisha huduma kwa jamii iliyomlea na kumpa msingi imara wa elimu na uongozi.
“Mafanikio yangu yametokana na nguvu na jasho la wananchi wa kata zote za Singida Mjini waliojitolea kujenga shule ya Utemini na Dr. Salmin nilikosoma. Sina cha kuwalipa zaidi ya kurudi nyumbani na kutoa nguvu na jasho langu kuwatumikia,” amesema Japhari.
Japhari ni mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na pia ana Shahada ya Uzamili katika Bioteknolojia, Ubunifu na Sayansi ya Udhibiti kutoka Chuo Kikuu cha Purdue, nchini Marekani.
Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 12, amehudumu katika Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kuanzia nafasi ya Mkaguzi wa Dawa Daraja la II hadi kufikia hadhi ya Mkaguzi Mwandamizi. Anaamini kuwa uzoefu alioupata katika sekta ya afya utamwezesha kushirikiana na wananchi kuleta maendeleo jumuishi na yenye tija kwa Jimbo la Singida Mjini.
chanzo: Jambo TV