Japhet Hasunga (Mbunge wa Vwawa): Tatizo la Ajira litakuwa bomu kubwa lisipowekewa mikakati

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga amesema Vijana wengi wana wamesoma hadi ngazi ya Chuo na kupata Elimu lakini Ajira imekuwa changamoto. Akizungumza Bungeni amesisitiza hatua zisipochukuliwa, litakuja kuwa bomu kubwa.

Amefafanua, "Serikali imesema itatoa Ajira zaidi ya 32,000 lakini hiyo itakuwa hatua moja. Vijana wanaomaliza ni takriban 90,000 - 100,000 kwa Mwaka kwahiyo haitoshi. Pia, sehemu wanayoenda kuajiri zaidi ni Elimu na Afya. Zipo Taaluma nyingine zinahitaji kutoa Mchango lakini Ajira inaendelea kuwa tatizo".
 
Mama akae na Mkwere amuulize aliwezajewezaje achukue mbinu pale, lakini serikali haiwezi kuondoa hili janga 100% hivyo waendelee na mwendo huu huu wa kuwavutia wawekezaji waje wawekeze ili kutoa fursa za ajira, na pia zitungwe sheria ambazo zitawalinda wawekezaji tusiwe unpredictable akija kiongozi fulani anaona private sector ni ya kuikamua akija mwingine anaona private sector ni muhimu tuwe na strong policy kwenye uwekezaji.
 
Vijana kazi zipo za kumwaga akili yako tuu, uncle wangu analima acre tano za vitunguu ana pesa sana huo ni mfano tuu
 
Mkwere nilimuogopa pale 2015 alipoajiri walimu 46( elfu arobaini na sita) bila kutuma maombi
 
Vijana kazi zipo za kumwaga akili yako tuu, uncle wangu analima acre tano za vitunguu ana pesa sana huo ni mfano tuu
Wewe au ndugu zako wengine,wamelima kiasi gani na ni matajiri wa levo zipi?
 
Mimi silimi, uncle wangu analima ana pesa nyingi sana , najua anaweza kukuajiri akakulipa kuliko mshahara wa serikali
 
Back
Top Bottom