Japhet Koome: Siogopi vitisho vya mahakama ya ICC

Japhet Koome: Siogopi vitisho vya mahakama ya ICC

Kenyan

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
414
Reaction score
314
Inspekta Jenerali wa polisi Japheth Koome amesema kuwa hatishiki na barua iliyotumwa kwenda kwa Mahakama ya kimataifa ICC na upinzani.

Upinzani kupitia Muungano wa Azimio unaoongozwa na Raila Odinga uliandikia ICC barua ukitaka Mahakama hiyo kufungua jalada la uchunguzi kutokana na nguvu nyingi kupita kiasi waliotumia maafisa wa polisi kudhibiti waandamanaji.

Mwanasheria Mkuu wa Upinzani, Paul Mwangi, alitaka ICC kumchunguza Koome akidai alitoa amri ya kuwapiga risasi waandamanaji.

"Sitishiki hata kidogo." Alisisitiza Koome huku akiwataka maafisa wa polisi kutokubali kutishwa na Raila Odinga.

"Natoa rai kwa maafisa wa polisi kusimama kidete na kulinda mali ya wananchi bila ya ubaguzi." Akiongeza Koome alipohutubia Wanahabari nyumbani kwake Kangundo.

Matamshi haya ya Koome yanakuja siku chache tu baada ya Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua kusema kuwa watamlinda IG Koome kutokana na vitisho hewa kutoka kwa upande wa Upinzani.

Gachagua alidai kuwa upinzani unamtisha IG kwa kufanya kazi yake ipasavyo.
 
Back
Top Bottom