Japo hakuna ajuaye sababu za kutwaliwa kaka, isipokuwa yeye, kuna watu saw it coming, wakasema, wakapuuzwa, akatwaliwa. Dada ukisikia usipuuze hili

Japo hakuna ajuaye sababu za kutwaliwa kaka, isipokuwa yeye, kuna watu saw it coming, wakasema, wakapuuzwa, akatwaliwa. Dada ukisikia usipuuze hili

Mwaka wa uchaguzi , Kuna mambo mengi Sana. Lakini ngojea tuone " the voice from within " inamwambia nini
Mungu Muumba asolala Wala kusinzia Amchukue mkononi mwake Amvushe salama. Jicho la Dubu, Simba Wala mbwa mwitu halitamwona.
 
Wanabodi,

Haya ni miongoni mwa mabandiko yangu ya kikubwa, weka mbali na watoto, hakuna kutaja taja majina.

Hili ni bandiko la kumhusu yule Kaka yangu, aliyetwaliwa. Japo hakuna binaadamu yeyote ajuaye sababu halisi za kutwaliwa kwake, isipokuwa YEYE mwenyewe pekee, ndie Aliyetoa, kisha Akatwa, ila kuna watu, “Saw It Coming!“ wakasema, wakapuuzwa, as a result, Kaka akatwaliwa!.

Sasa hao watu wenye jicho hilo la tatu, wanaviona viashiria vya same same likely scenario na wanasema kwa nia njema na dhamira safi ya kumsaidia huyu Dada.

Dada yangu mpenzi, nakuomba sana, ukisikia kitu, sio lazima ukizingatie kila utakacho sikia, maana utasikia vingapi?, ila sikiliza kila utakacho sikia, na ukiisikia sauti kutoka ndani yako, the voices from within, ikimwambia kitu, aifanyie tathmini hiyo sauti kama ni sauti ya YEYE Mwenyewe, au ni yeye tuu!, ikitokea ni sauti kwake YEYE, then, usiipuuzie!.

Leo asubuhi nikiwa bafuni naoga ili kwenda kwenye shughuli zangu, nikaisikia sauti, voices from within, ikiniambia, ukisikia kitu, mwambie tuu Dada yako, kuna watu wamemzunguka, wakimwimbia nyimbo za sifa na mapambio, huku wana jicho la tatu, kuna vitu wanaviona, hawamwambiii, wameamua kunyamaza, hawasemi ila ukweli wanaujua, na wana uwezo wa kumsaidia kwa kumwambia ukweli, ila wanachelea labda Dada atakasirika.

Sauti hiyo imeniambia Dada akiambiwa, akisikiliza, itamsaidia, ila akisikia akapuuza, yule YEYE, anaweza kufanya jambo!.

Paskali
Sisi wengine tunawaheshimu sana nyie mnakuja na hizo sauti from within.
Malaika ndiyo nyinyi hivyo sisi tunakaa mguu sawa tu ili isiwe surprise.
 
Ikiwa ni uasi, au usaliti wa aina yoyote hauna nafasi. Fikiri, mtu anavyojisikia na kuumia anaposalitiwa. Hakuna unafiki,usaliti Wala Hila itafanikiwa Mwaka huu2025 Mark these words.
 
Sikuwa fan mkubwa wa anko mwendazake lakini nafsini nilikuwa najua anapigana vita nzito sana ya nje na ya ndani. Na approach aliyoitumia ya kuwa open book naamini alikuwa anajua kitu anachofanya ni suala la kufa ama kupona..

Kwa hiyo alijitahidi kuzuia kitu alichokiona kikimkaribia ila si kwamba hakujua. Alijua
Atleast alikubali kuwa one day i will be no longer with you but he still did whats right according to his beliefs.
 
Tatizo ni makubaliano ya baadhi ya watu yanamponza, halafu yeye ni mtu kati hivyo anaona aibu kusaliti huo upande ingawa dhamira yake kabisa anajua hatakiwi ila anakomaa. Sasa sijui hiyo pir ni kabla au baada. Kibaya sana yeye alidharau na kudhihaki kifo cha kaka yake aliyekuwa anampenda ambaye aligombanishwa naye, sasa sijui pia wale vijana wa tope walimaanisha kumtusi mwenyekiti kuhumhusisha na kufukuliwa mitaro hahaha ila hakika chama chetu kina kazi ngumu kidogo, wapanga strategies wana mapungufu
Ukiwa upande wa shetani lazima akumalize tu
 
Kuna watu humu jamvini hupaswi kabisa kupuuza wanachokiandika akiwemo Paschal, TumiaAkili, Britanicca, TumainiEl, Maharagwe sijui ya ukweni nk.
Kama huna cha ku comment busara ni kuwa msomaji tu.
Ulivyomtaja huyo TumainiEl nimekuona hamnazo ama hufuatilii vizuri mambo wanayoandika watu humu.

Huyo ni wale walokole machizi
 
Sema CCM imechokwa mtandaoni humu ila huku mtaani ya moto sana sana
Laiti ungejua jamii ya humu ndio ile ile iliyoko mtaani usingesema haya uliyoyasema. Tofauti ni kuwa kui diss CCM mtaani imekuwa ni nongwa kwahio zinasikika sauti za upande mmoja wa wale wanufaika tu.

Majority ya walalahoi hawataki hata kuisikia. Ila hawaongelei mbovu kwa sababu za kiusalama. Hamna anayetaka kuacha mkewe na watoto kwa chuki za wapambe tu.
 
Mleta mada kaja na ushauri mzuri, ila sasa je ushauri wake unaweza zingatiwa, Binafsi kiroho ninayo mengi tu Mungu wangu amenionesha wala sio leo , ila hata nikiyasema nani wakuyasikiliza , hakuna cha kupanga hapa
Mimi naonaga watu wa aina yako ni wasanii na matapeli. Kama sio basi mna tabia ya MAJIVUNI na UNAFIKI , kama unafaham jambo na kama una nia njema kwanini usiliseme, kama unajua halaf unasema huna haja ya kusema ina mana Gani Sasa ni kama umekuja kutuchora na kutukebehi au kujionesha kua unajua sana ya rohoni. Unadhani ni wewe pekee TANZANIA hii anayejua, watu wameshachungulia na wanajua, baadhi wamekaa kimya na wengine wameanza kusema, wanachokijua au walichokiona au wanachoona, ila waliokaa kimya hawajjaja kujimwambafai kua wanajua sana halaf waseme hatusemi, ni matured enough kukaa kimya.
 
Sasa tutegemee nini kama anazungukwa na kuwasikiliza watu kama Steve "Nyerere", Shilole, ma bongo Flava nk?
Jana nimetoa machozi kumuona Rais wangu eti anasimamishwa kumpongeza Ally Kiba na Diamond wakiimba.
Advisors wamemfanya kiongozi wetu mkuu to go that much low kweli? Maana hao ndio wanasimamia kila afanyacho.
Tutaanza kuamini utabiri wa Wanajimu bure! Kama ule alioutoa shehe Yahaya kabla hajafa.
Yule Sheikh alikuwa ni mtaalamu kweli kweli wa Elimu za Nyota !
 
Back
Top Bottom