Uchaguzi 2020 Japo hatuna Tume Huru, CHADEMA watasimamisha wagombea katika ngazi zote akiwemo mgombea urais kwa sababu hizi miongoni mwa nyingine

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Binafsi naamini wapinzani, wakiwemo CHADEMA, wanaelewa vizuri sana kuwa kwa wao kutangazwa washindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu haitokuwa jambo jepesi na litakuwa ni jambo gumu kuliko ilivyowahi kuwa vigumu katika chaguzi zote zilizopita.

Hata hivyo,wataweka wagombea katika ngazi zote huku sababu kuu zinaweza kuwa ni hizi miongoni mwa nyinginezo:

1.Hii ni fursa kwao ya kufanya siasa
Wote tunajua kuwa awamu hii tangu iingie madarakani mwaka 2015, ilizuia mikutano ya vyama vya siasa kinyume na sheria huku CCM ikiendelea kufanya siasa pasipo kubughuziwa.Hivyo,wapinzani watatumia mikutano ya kampeni kuwaeleza wananchi yale waliokuwa wakitaka kuwaeleza kupitia majukwaa ya kisiasa tangu 2015 .

Bila kujali watatangzwa washindi au laa,kwao hii ni fursa ya kuwaeleza wananchi mapungufu ya CCM na serikali yake hii ya awamu ya tano chini ya Magufuli.Ni fursa ya kuwakumbusha na kuwaeleza wananchi juu ya matendo ya watu wasiojulikana kama kuteka,kuua,kupoteza watu,n.k.

Kampeni hizi pia ni fursa ya kuwaeleza na kuwakumbusha jnsi CCM na serikali yake ilivyoshindwa kutekeleza ahadi ya kutoa milioni 50 kwa kila kijiji,jinsi walivyotelekeza watumishi wa umma kwa miaka mitano pasipo nyongeza ya mishahahara kinyume na ahadi zao za kampeni,walivyoshindwa kuwalipa kwa wakati wakulima wa korosho, walivyo kuja na makato katikli ya bodi ya mikopo,n.k.

Kwa kifupi, hii ni fursa kwa wapinzania kueleza haya yote na mengineyo wakati wa kampeni bila kujali kuwa tume hii si huru na kwamba wasimamizi wa uchaguzi ni makada wa CCM lengo likiwa ni kutumia mikutano ya kampeni kufikisha ujumbe kwa wananchi,ujumbe ambao,kwa mikaka karibu mitano, Magu na serikali yake wamekuwa wakiuzuia usiwafikie wananchi kupitia majukwaa ya kisiasa

2.Kupata uhalali wa kuendelea kudai Tume Huru ya Uchaguzi
Yale yote yatakayotokea na ambayo yatakuwa ni kinyume cha sheria za nchi na sheria za uchaguzi,yatatoa fursa na uhalali wa kuendelea kuikataa tume hii iliopo pamoja na kuyapa nguvu madai ya kuwakata Wakurugenzi wa Halmashauri ambao baadhi yao kama sio wote wanaaminika kuwa ni makada wa CCM hivyo hawastahili kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

3.Kutoa fursa kwa dunia kujionea aina za chaguzi tulizonazo katika nchi yetu
Wapinzani wanashiriki huku wakijua dunia itakuwa inatupia macho uchaguzi huu kupitia wawakilishi watakaotumwa kuja kutazama uchaguzi mbali na mataifa kama Marekani kutaka kuona kama ile kauli ya Magu kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki inatimizwa kwa vitendo.Mauzauza yoyote yatakayotokea yatasaidi kuithibitishia dunia kuwa madai ya wapinzani kuhujumuwa katika hizi chaguzi huwa ni madai ya kweli.

4.Ni nafasi ya wapinzani kujipima ni kwa kiasi gani wanakubalika kwa wananchi
Kupitia mikutano ya kampeni,chama cha siasa kinapata fursa ya kujipima ni kwa kiasi gani baada ya miaka mitano kwisha chama husika kinakubalika kwa wananchi na zaidi ni kwa kiasi gani wagombea wake wanauzika hasa kwa nafasi ya mgombea uraisi.

5.Kupima kama siasa za hama hama zimekuwa na madhara kwao na kama zimesaidia chama tawala
Hii itakuwa ni fursa ya kuthibitisha madai kuwa siasa za hamahama zimeua upinzani na kuinufaisha CCM.

6.Kutotoa fursa kwa wagombea wa CCM kushinda bila jasho
Japo tunajua tume si huru huku baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi wakitajwa kuwa ni makada wa CCM,bado si sahihi kuwaacha watangazwe washindi pasipo kupata joto la kwenye kampeni(lazima wahenye).

7.Inawezekana pia wapinzani wana sababu zao za kushiriki huu uchaguzi
Inawezekana kabisa wapinzani hawa teyari wana mipango yao ambayo ili itimie,ni lazima kwanza washiriki huu uchaguzi na kasoro zozote zitazojitokeza, ndio zitawapa uhalila wa kutekeleza mipango na mikakati yao ambayo mimi na wewe hatuijui.Kwahiyo huenda kushiriki kwao ni kama tu kuitega CCM na serikali yake,

Mwisho, ni lazima ieleweke kuwa kuiondoa CCM madarakani ni mchakato, na kushiriki uchaguzi ni sehemu tu ya mchakato husika bila kujali uchaguzi utakuwa huru na wa haki au vinginevyo.
 
👊 ✌✌✌💥
BTW: Hivi Idris sultan alikuwa anacheka koti au jinsi Tanzania ilivyowapwaya jamaa?
... 😅😅😅😅😅😅!
 
4.Ni nafasi ya wapinzani kujipima ni kwa kiasi gani wanakubalika kwa wananchi
Kupitia mikutano ya kampeni,chama cha siasa kinapata fursa ya kujipima ni kwa kiasi gani baada ya miaka mitano kwisha chama husika kinakubalika kwa wananchi na zaidi ni kwa kiasi gani wagombea wake wanauzika hasa kwa nafasi ya mgombea uraisi.
Sababu hii nilitaka kuipa ufafanuzi zaidi; lakini nikakuta niliyotaka kuyaweka hapa yanaungana vyema na namba saba.
7.Inawezekana pia wapinzani wana sababu zao za kushiriki huu uchaguzi
Inawezekana kabisa wapinzani hawa teyari wana mipango yao ambayo ili itimie,ni lazima kwanza washiriki huu uchaguzi na kasoro zozote zitazojitokeza, ndio zitawapa uhalila wa kutekeleza mipango na mikakati yao ambayo mimi na wewe hatuijui.Kwahiyo huenda kushiriki kwao ni kama tu kuitega CCM na serikali yake,
Kama wapinzani watafanya kampeni zao bila kuwaeleza wananchi umhimu wa kura zao na haki zao za msingi za kuwachagua viongozi wanaowataka watakuwa wanafanya kazi bure.

Ni jukumu la kila mwananchi kujua wajibu wake na haki zake na akatae kwa njia zozote kuporwa haki zake. Na ni wajibu wa wapinzani, bila kujali kama watapigiwa wao kura kuwaelimisha wananchi juu ya haki hizi.

Kama wapinzani watakwenda kwenye kampeni bila ya kusisitiza kwa wananchi umhimu wa kura zao, watulie tu wakiona kura walizopiga zinaharibiwa, basi hawa wapinzani watakuwa wameshindwa kazi yao ya kuwaelimisha wananchi, na watakuwa hawana sababu yoyote, pamoja na hizo nyingine ulizo orodhesha hapo juu kushiriki kwenye uchaguzi wowote.

Ni wananchi ndio watakaokataa matokeo ya Tume kama ushahidi unaonyesha kura zao zimevurugwa
CHADEMA na wenzao kazi yao ni kuwapa elimu na miongozo ya kukataa dhuruma hiyo. Hii ndio kazi ambayo hadi sasa wapinzani wote wangetakiwa wawe wameifanyia mipango imara jinsi ya kuiwwasilisha kwa wananchi wakati wa kampeni.

Ndio maana nina wasiwasi kwamba hawa wapinzani wamefanya maandalizi yoyote hadi kufikia hapa.

Kama watajipeleka tu kwenye kampeni bila ya mikakati waliyoiandaa wwakati wakiwa na nafasi ya kufanya hivyo, miaka mitano yote, basi hawastahiri kamwe kupewa madaraka na wananchi.
 
Mwisho, ni lazima ieleweke kuwa kuiondoa CCM madarakani ni mchakato, na kushiriki uchaguzi ni sehemu tu ya mchakato husika bila kujali uchaguzi utakuwa huru na wa haki au vinginevyo. [emoji109][emoji109][emoji109][emoji123]makala nzuri kabisa

Jr[emoji769]
 
Kwanza serikali haikuzuia mikutano ya siasa. Mliruhusiwa mfanye kwenye majibo yenu, ili kuondo migongano.
Pili tume ya uchaguzi ipo huru na wananchi wanafamu hilo. Na mna kitu gani cha kuwaambia watanzania juu ya Ccm hii. Ambayo imefamya makubwa kwa muda mfupi? Nyie Chadema sasa hivi ni maji ya shingo mnasubili kuzama. Chubwii.
 
Sababu hii nilitaka kuipa ufafanuzi zaidi; lakini nikakuta niliyotaka kuyaweka hapa yanaungana vyema na namba saba.

Kama wapinzani watafanya kampeni zao bila kuwaeleza wananchi umhimu wa kura zao na haki zao za msingi za kuwachagua viongozi wanaowataka watakuwa wanafanya kazi bure.

Ni jukumu la kila mwananchi kujua wajibu wake na haki zake na akatae kwa njia zozote kuporwa haki zake. Na ni wajibu wa wapinzani, bila kujali kama watapigiwa wao kura kuwaelimisha wananchi juu ya haki hizi.

Kama wapinzani watakwenda kwenye kampeni bila ya kusisitiza kwa wananchi umhimu wa kura zao, watulie tu wakiona kura walizopiga zinaharibiwa, basi hawa wapinzani watakuwa wameshindwa kazi yao ya kuwaelimisha wananchi, na watakuwa hawana sababu yoyote, pamoja na hizo nyingine ulizo orodhesha hapo juu kushiriki kwenye uchaguzi wowote.

Ni wananchi ndio watakaokataa matokeo ya Tume kama ushahidi unaonyesha kura zao zimevurugwa
CHADEMA na wenzao kazi yao ni kuwapa elimu na miongozo ya kukataa dhuruma hiyo. Hii ndio kazi ambayo hadi sasa wapinzani wote wangetakiwa wawe wameifanyia mipango imara jinsi ya kuiwwasilisha kwa wananchi wakati wa kampeni.

Ndio maana nina wasiwasi kwamba hawa wapinzani wamefanya maandalizi yoyote hadi kufikia hapa.

Kama watajipeleka tu kwenye kampeni bila ya mikakati waliyoiandaa wwakati wakiwa na nafasi ya kufanya hivyo, miaka mitano yote, basi hawastahiri kamwe kupewa madaraka na wananchi.
Hili sio geni, tumeshaliona kwenye majimbo kama Arusha Mjini na Mbeya Mjini, wananchi wa huko wanavyofanya; kiukweli kuanzia wakati wa kampeni mpaka kuelekea uchaguzi wenyewe na baada ya uchaguzi hali ya hewa hubadilika sana, wengi hujikuta ari ya kutaka mgombea wao wa upinzani ashinde huongezeka, na hili husababisha pressure kwa watawala na vyombo vyao bya usalama.

Kimsingi naunga mkono hoja; Chadema ni vyema washiriki uchaguzi, lolote litakalotokea baada ya hapo ndio watakuwa wamepata platform yakulihubiri mbele ya safari, but huwezi kususia uchaguzi halafu uje uwaambie wananchi na jumuia ya kimataifa nilijua nikishiriki wataniibia kura, siasa ni muendelezo wa matukio, haiwezi kusimamishwa kwa tukio moja.
 
Kumbe kusimamisha wagombea tu.mbona hata TADEA na NLD wanasimamishaga.
 
Wananchi wengi tutapenda kuona mikutano isiyo na figisu yenye usawa kwa vyama vyote ila wasiwasi una kuja he,polisi hawatawashusha wapizani majukwaani kwa kisingizio Cha uchochezi?
 
Kwanza serikali haikuzuia mikutano ya siasa. Mliruhusiwa mfanye kwenye majibo yenu, ili kuondo migongano.
Pili tume ya uchaguzi ipo huru na wananchi wanafamu hilo. Na mna kitu gani cha kuwaambia watanzania juu ya Ccm hii. Ambayo imefamya makubwa kwa muda mfupi? Nyie Chadema sasa hivi ni maji ya shingo mnasubili kuzama. Chubwii.

Yaani unajitoa ufahamu Kabisa,eti Tume huru? Kisa tu inaipendelea CCM ,Kubalini Iwe huru muone!!
 
Sababu hii nilitaka kuipa ufafanuzi zaidi; lakini nikakuta niliyotaka kuyaweka hapa yanaungana vyema na namba saba.

Kama wapinzani watafanya kampeni zao bila kuwaeleza wananchi umhimu wa kura zao na haki zao za msingi za kuwachagua viongozi wanaowataka watakuwa wanafanya kazi bure.

Ni jukumu la kila mwananchi kujua wajibu wake na haki zake na akatae kwa njia zozote kuporwa haki zake. Na ni wajibu wa wapinzani, bila kujali kama watapigiwa wao kura kuwaelimisha wananchi juu ya haki hizi.

Kama wapinzani watakwenda kwenye kampeni bila ya kusisitiza kwa wananchi umhimu wa kura zao, watulie tu wakiona kura walizopiga zinaharibiwa, basi hawa wapinzani watakuwa wameshindwa kazi yao ya kuwaelimisha wananchi, na watakuwa hawana sababu yoyote, pamoja na hizo nyingine ulizo orodhesha hapo juu kushiriki kwenye uchaguzi wowote.

Ni wananchi ndio watakaokataa matokeo ya Tume kama ushahidi unaonyesha kura zao zimevurugwa
CHADEMA na wenzao kazi yao ni kuwapa elimu na miongozo ya kukataa dhuruma hiyo. Hii ndio kazi ambayo hadi sasa wapinzani wote wangetakiwa wawe wameifanyia mipango imara jinsi ya kuiwwasilisha kwa wananchi wakati wa kampeni.

Ndio maana nina wasiwasi kwamba hawa wapinzani wamefanya maandalizi yoyote hadi kufikia hapa.

Kama watajipeleka tu kwenye kampeni bila ya mikakati waliyoiandaa wwakati wakiwa na nafasi ya kufanya hivyo, miaka mitano yote, basi hawastahiri kamwe kupewa madaraka na wananchi.
Bila shaka watakuwa wamekusoma mkuu.Ushauri huu ni mzuri na binafsi nauunga mkono.
 
Back
Top Bottom