Uchaguzi 2020 Japo Magufuli atashinda lakini ilitakiwa ashindwe

Uchaguzi 2020 Japo Magufuli atashinda lakini ilitakiwa ashindwe

Mleta mada amefanya analysis nzuri sana na ametoa ushauri mzuri sana kwa wanaomshauri mheshimiwa wafuate ushauri huo na atachaguliwa tena na atabadilika. Nia yake ni nzuri ila medhodology ya utekelezaji wake labda na aina fulani ya hasira ama chuki ama ubaguzi. Haya ayaache! Otherwise katenda mazuri lakini uhuru wa mtu ni muhimu zaidi!
 
Alichoandika mleta mada kwenye post namba moja kiko wazi sana. Rais alituma pole kwa Lisu mara moja tu ili kuhadaa umma kuwa ameguswa. Lakini ukweli ni tofauti. Tuna akili timamu ya kujua mambo. Ameruhusu mikutano sio kwakuwa anapenda ila kwa sasa inamlazimu, lakini hata kufungia mikutano hakufanya kisheria, bali ni matumizi mabaya ya madaraka.

Huu utetezi kuwa kinachomuudhi ni lugha za matusi sio kweli, maana hata yeye huwa anatumia sana lugha hizo, labda useme mtenda akitendewa hujisi kaonewa. Na hakuna siku amewahi kutukaniwa mama yake kwa maana ya matusi. Kama kweli hapendi lugha ya matusi, wakati wa kampeni za 2015 akiwa jukwaa moja na mh. Msukuma, huyo Msukuma alisema Lowassa kajinyea na bado alikuwa anachekelea, na hakumchukulia hatua yoyote huyo Msukuma, usidhani hatukumbuki hili, achia mifano mingi ya dhahiri kuhusu yeye kufumbia macho matusi ya watu wa chama chake. Kwenye siasa vijembe na kejeli ndio sehemu yake, labda kama kaingia kwenye mchezo asiouweza.

Hilo la huruma sio kweli, maana anaowasemehe ni wale anaotaka kuwatumia kwa kiki ya kisiasa kuwa ni mtu mwenye huruma. Hana hofu yoyote ya Mungu, bali kutokana na background yake alikuwa ni mtu muhudhuriaji wa kanisa, hivyo kwenye ubongo wake kulijengeka hali ya kumtamka Mungu. Hofu ya Mungu sio kupiga picha ukiwa kanisani unasali, na kuita viongozi wa dini kufungua mikutano kwa sala. Hizo mbinu ni kutengeneza watu kisaikolojia kuwa yeye ni mcha Mungu, jambo ambalo si kweli. Mtu mcha Mungu utamuona kwa matendo sio kwa maigizo. Toka ameingia madarakani, chaguzi zote za nchi hii tumeshuhudia, ukatili, uhayawani na ushenzi wa kiwango cha juu. Kwa mtu mcha Mungu haya yasingeonekana. Rejea kilichotokea uchaguzi wa SM, na pitia historia yake alipokuwa mbunge alikuwa anashindaje. Usichanganye huruma na wajibu wake, kusimamia ukusanyaji wa kodi, utendaji kazini nk hayo ni majukumu yake, na analipwa mshahara kwa hayo, This has nothing to do na huruma.

Hiyo miradi ya maendeleo ni jukumu la mkusanya kodi yoyote, hata wakoloni walifanya. Je kwakuwa amesimamia miundombinu kadhaa basi ndio alazimishe box la kura kupitisha watoa rushwa wa chama chake? Ndio aminye uhuru wa vyombo vya habari? Kila siku anatunga sheria kandamizi ili atawale watu kwa shuruti, ni kipi cha hatari watu kusikiliza redio za nje, ambacho hakikutokea enzi za Mwinyi, Mkapa au Kikwete, ila chini yake kitatokea? Tulishatoka dunia ya kuburuzwa na kiongozi, tunataka tumchague tunayemtaka sio kwa shuruti yake.

Ni hivi boss, Ni vyema ikafahamika kuwa ccm sio chama cha kizazi hiki, sio kwamba ccm haijafanya kitu, maana hata wakoloni walifanya mambo kadhaa. Bali kizazi hiki kinataka mabadiliko hasa ya kimfumo, na kwa bahati mbaya Magufuli na ccm yake wanajenga miundombinu wakidhani hayo ndio mabadiliko yanayotakiwa na kizazi hiki. Miundombinu sio mabadiliko, bali ni wajibu wa serikali yoyote inayokusanya kodi, tena hii ni kazi endelevu. Pls, Magufuli ashauriwe vyema kwenye hili, vinginevyo ataendelea kuweka sheria nyingi kandamizi, ataleta miundombinu na mambo mengine, lakini atakuwa haijakidhi mahitaji ya kizazi hiki ya mabadiliko. Nadhani kwa bandiko hili utafikisha ujumbe sehemu husika.
 
Hapa ntajikita kujadili mambo ya (EI) yaani emotional intelligence. Bila shaka kila mtu atakubali kwamba Rais wetu ana tatizo la emotional intelligence, hivyo kusababisha kuonesha hisia zake hata sehemu ambayo haikustahili.

Rais Magufuli, ni mtu ambaye anajitoa kwa kiasi fulani, japo wapinzani wake wamekuwa wakimkosoa kwa mambo mengi sana. Kwa mtizamo wangu hayo husababishwa na (modality & methodology) anazotumia kutekeleza matamanio yake, huenda lengo lake likawa jema kabisa lakini kwa sababu anatofautina mtizamo na wapinzan wake basi hujikuta anapingwa sana. Rais Magufuli, anamini yupo sahihi kwa anayoyafanya huku akiungwa mkono na wananchi kwa kiasi fulani.

Licha ya harakati nying za Rais Magufuli, kuiletea Tanzania maendeleo, lakini imeonekana watanzani bado hawaelewi methodology & modality anazotumia. Hii imepelekea kuwepo kwa upinzan AMBAO haukutarajiwa kabisa. Hili limeonekana baada ya ujioa wa hasimu mkubwa wa Magufuli kwenye siasa za Tanzania ndugu Tundu Lissu. Kwa kiasi fulani ndgu TL ametia hamsha hamsha kweny siasa za Tanzania, mpaka kufikia wachambuzi wengi na waumini wengi wa demokrasia kuona sasa kutakuwa na upinzan wenye nguvu kuelekea uchaguzi wa October.

Lakini tujiulize, je Rais Magufuli anafurahia haya yanayoendelea kuonekana tangu ujio wa Tundu Lissu pale uwanja wa ndege mpak huko mikoani? Rais ni mtu anaye penda kujituma kwake, kuoneshwe kuthaminiwa, anataka ashukuliwe, apongezwe na kusifiwa, na hapa ndipo furaha yake ilipo. Lakini kwa kinachoendelea kuelekea uchaguzi wa October, Rais Magufuli ataona watanzani ni watu ambao hawana shukran wala hawastahili kufanyiwa jema lolote, hivyo hali hii kusababisha Magufuli kuwachukia baadhi ya watanzani wazi wazi kama alivyoonesha baadhi ya maeneo kweny kipindi cha uongozi wake.

Rais Magufuli, anasahau mambo ya demokrasia linapokuja swala la yeye kutopongezwa na kusifiwa kwa alichofanya. Kwa vile Rais ana tatizo la emotional intelligence (EI) basi tutegemee ubaguzi mkubwa, majibu mabaya kwa wananchi baada ya uchaguzi, kejeli na pengine kuongeza kibano zaidi kwenye mambo mbali mbali. Sasa ili kuepusha yote haya, ambayo yataacha makovu mengi baada ya yeye kuondoka 2025, ilitakiwa ashindwe kweny uchaguzi huu wa 2020.

Nimalizie kwa kuwashauri watu wa Public relations, kutoka ofisi ya Rais kumfanyia counseling Mh Rais, ili achukulie ushindani wa kisiasa kama njia ya kufikia maendeleo, maana licha ya kuahidi kumaliza upinzan ifikapo 2020, lakini bado kuna upinzan mkubwa tena imeonekana watu ndio wana moto zaidi ya 2015.

Huu ni ukweli wa dhahiri, ngoja niwaite wapambe wake wajionee ukweli wa mambo, ambao wapambe wa Magufuli hawataki usikike.
 
Nani angetakiwa kumshinda??
 
wapinzani wa kweli wa awamu hii ni wapenda :amani,maendeleo,haki,demokrasia na wale wote wenye akili zilizopevuka! Kodi za watanzania zinatumika kununua majogoo mitaani wakati hospitali hazina madawa,kodi zetu zinatumika hovyo....simply wapinzania wa awamu hii ni watanzania wenyewe ....tena walipa kodi!
Hapa unadanganya.

Ukosoaji wa aina hii ndio unatufanya hata kama Magu ana mapungufu tumchague. Ukisema dawa hosp hazipo unachukua mlinganisho gani? Leo Hosp zipo nyingi na dawa zipo kuliko vipondi vyote.

Ukosema mzunguko wa hela mtaani umepungua nitakuelewa
 
Back
Top Bottom