Uchaguzi 2020 Japo ni mchungu 'Kumesa' lakini ndio ukweli wenyewe; watakaorudi Bungeni ni 'wa kijani', kubali kataa. Mwenye masikio na asikie!

Pole nadhani hujui unachokijua.
 
Wapinzani watakuwepo,Ila wapinga maendeleo na vibaraka wa mabeberu ndio wasio takiwa
 
Watarudi kwa sababu na wewe unashiriki dhambi hiyo kwa uandishi wako
Unafurahia machungu ya wengine
Hebu punguza kebehi zako wakati mwingine
Unakera
Kulia kwangu leo imegeuka furaha kwako

Unabariki dhuluma za sisiem
Hali ikiwa ndivyo si you usishangae
 
Japo siungi mkono utawala wa ccm kwa muda wote ila upande wa upinzani umefeli kwa kiasi kikubwa sana.

Wangejikita kwanza kujenga msingi imara ndio wagombanie madaraka.

Wangejikita kuingia mioyoni mwa watanzania wengi badala wa hawa wa mihemko.

Wangejikita kufanya maendeleo kwa wananchi ama sehemu walichaguliwa badala ya kupambana na serikali ccm na polisi.

Wangejinyima kile walichonacho kama sadaka kwa watanzania ama jamii kama kujenga madarasa vyoo ofisi vifaa.

Hata kwenye huduma za afya walao hata panadol kwa zahanati ya uma nk

Hata kuhamasisha usafi kwenye jamii,msaada kwenye majanga nk, mfano hili la korona sijakia hata wakitoa hata barakoa moja kwa muhudumu wa afya.


Nichukulie mfano wa morogoro mjini nilikoishi mbunge akiwa azizi abood na kawe jimbo ninaloishi sasa.

Abood alikua akishuka mpaka chini kabisa mpaka kuwasaidia wakina mama kuchambua dagaa sokoni akihamasisha usafi na kutatua kero zilizo ndani ya uweza wake, achilia mbali kutoa baadhi ya magari yake kwenye misiba japo unaweza kuhesabika sio msaada lakini mkono mtupu haulambwi.

Hapa kawe kama jimbo bunju kama kata sikuwahi kusikia jambo lolote kuhusu mbunge kwa miaka 3 niliokaa hapa, kama imekuwepo na sijapata taarifa nisamehewe.


Lakini kunatofauti kubwa mno.
 

Paskali ni kuwa umeamua kuanzisha uzi kuwa hiyo nia ya Magufuli kunajisi uchaguz, ili wanaccm tu ndio warejee bungeni ndio umeijua sasa? Mbona hilo alitamka wazi toka alipoingia madarakani, na amekuwa akitekeleza tokea kwenye chaguzi za marudio, na hata huu uchaguzi wa serikali za mitaa.m? Halafu ww ndiyo unasema hii ni ccm imara na inayokubalika! Kutoka kwenye haya madaraka yanayotumuka vibaya, humo ndiko kura za ccm zilipo.
 

Kama huna ujualo ni vyema kukaa kimya. Wapinzani sasa hivi ni marufuku kutoa chochote kwenye jamii kwani inaonekana watakubalika sana kwa wananchi. Tumeona kwa macho yetu misaada na michango ya wapinzani ikizuiwa, na hata kukataliwa kwa amri toka juu. Sasa hivi ni ngumu mpinzani hasa cdm, kukubaliwa kufanya lolote la maendeleo kwenye eneo lake eti kisa itakubalika. Hizi siasa za kishenzi zimekuwa wazi sana kipindi hiki cha awamu ya tano. Inaonekana una ufahamu mdogo sana wa uhalisia, ndio maana umeandika hiki ulichoandika.
 
Mayalla

Chukua fom ndugu
 
Unataka kuniambia mkakati wa CCM uliopo wa kumfanya Mbatia kuwa KUB wa Bunge lijalo siyo wa kweli? Labda ungesema wapinzani watarudi ila siyo kwa kiwango kikubwa Kama ilivyokuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…