Japo walisema Yule ni katili huyu wa sasa akidondoka hata nusu ya watu hawa hapati.

Inauma sana kwakweli, na ndio maana sasa hivi kila mtanzania anapambana kadri awezavyo aingie kwenye system hili asipitwe na ulaji.
 
Erythrocyte ukitaka kufaulu katika siasa za TZ kwa zama hizi usimponde JPM vinginevyo utaingia kwenye vitabu vyeusi. Raia wa kawaida huwezi ukawaambia chochote kuhusiana na JPM kwa sababu alichokuwa anakiongea kwa ajili yao walikuwa wanakiona anakifanya sio blah blah za demokrasia, haki, amani, uzalendo na takataka zote.

Nyeupe ni nyeupe sio kupindisha; kumbuka hata somo la 'Criminology' lianzishwa baada ya wanasiasa waliokuwa wanapigania demokrasia na wanaopinga kuanzisha uhalifu dhidi ya raia kwa maslahai ya kupata sifa za kijinga na madaraka ili wapore rasilimali za umma.

Ninakushauri wewe CDM ujihadhari kueneza chuki dhidi ya hayati JPM; you won't achieve your goals, certainly I can guarantee you on this, the breakthrough is very narrow!!!
 
Ana kwao ana dini yake ana watu wake ,wala haijalishi unazikwa na watu wangapi wala huku hakuhitajiki sanduku.
 
Kwangu ni Ni Rais bora na mfano mzuri kwa jamii zote duniani ......,Hua sipendi hata kuangalia picha zake maana hua napata maumivu makali sana nikona nchi ilivyo kwa sasa...
 
Umesoma kitabu cha Kabendera?
 
Umesoma kitabu cha Kabendera?
Yule mwenye hallucination ya utisho wa kimamlaka wa JPM na hachani nywele au aliyekuwa kwenye vilabu vya mpira?
Jitahidi kupanua ubongo wako usiendekeze itikadi za kisiasa uchwara. Pitia mawazo ya kila mtu yawe hasi, chanya au udete kisha chakata na usimamie ukweli sio ushabiki wa kumtukana na kumtuhumu mtu bila ushahidi!!

Wale walioandika kitabu kuhusu JPM na Chato wamefika wapi na ujinga waliowekeza kwenye kitabu chao?
 
Mwenyezi Mungu tunaomba ufyekelee mbali dikteta mke anayeendeleaa kumwaga damu za Watanganyika kwa kutumia polisiccm
 
Maoni yako yamepokelewa.
 
Umeongea kitu kikubwa kaka ambacho wapinzani hawakijui au wanakijua lakin wanakipuuza.

Nimeshawahi kuwaambia humu mara kibao tu kwamba hili wapinzani kutunza imani yao kwa wabongo hawatakiwi kabisa kumpondea pondea JPM au kumlinganisha linganisha na Samia tena katika minajiri ya kumfanya Samia aonekane ni bora...

Kitendo cha wao kuendelea kulazimisha chuki kwa marehemu JPM, huku kuna mambo mengi tu ya ovyo yanayofanyika kwenye awamu ya sasa kinatoa tafsiri kwamba wao bado wanaumizwa zaidi na awamu ya tano kuliko hata uozo wote unaofanywa na awamu ya Samia. Wanasahau kwamba JPM licha ya mapungufu yake lakini alikuwa na mpaka sasa bado ni kipenzi cha watu.


Hivyo basi kuendelea kumg'ang'ania JPM ni kujitafutia chuki kwa wabongo na mwisho wa siku wataonekana hawana la maana ni bora tuendelee tu n ccm.
 
Kwanza hicho kitabu cha kabendera ni watanzania wangapi waliokisoma au ambao wana uwezo wa kukisoma?? Na uthibitisho wa tuhuma zote zilizopo mle uko wapi???? Au tuamini tu eti kisa kibendera kasema sijui kwa kuwa yeye ni investigative journalist??

Ndio ujue hawa wapinzani wetu ni mabogasi sana na kwanin wabongo wataendelea kumpuuza, na wao wataendelea kuwa wapinzani licha ya ccm kukosa sifa ya kuliongoza taifa hili.
 
Kwa akili yako kisoda unadhani wote hao walikuwa wamekwenda kumuona kwa vile wanampenda?

Halafu duniani ukiishi kufurahisha kila mtu huwezi kufanikisha kitu. Wewe fanya linalofaa kisha sepa mbele. Watanzania wenyewe hawa hawana shukrani.

Huyo bwege Mwendazake alisomamisha shughuli za vyama na ruzuku akawanyima. Kuna watu walikuwa jela wengi tu na akina Tundu na Lema walikuwa ukimbizini.

Amekuja huyu wa sass kawatoa ukimbizini, kawafutia makesi, kawaruhusu mikutano na kawapa ruzuku, ndiyo kwanza mnamtukana kila tusi.
 
Alikuwa mzuri kwenye miundo mbinu, ubaya hakuwa na utu. Vifo kama vya sasa, jela, risasi nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…