Japo ' Wanachukiwa ' na wengi ila hadi hivi leo bado sijaona Baba wa ' Promo ' Tanzania nzima kama Clouds Media Group

Watu kweli watakuwa wengi ila faida watapataje kwa kiingilio kidogo hivi au sponsor ndio analeta faida?
Wakilipia watu 40,000 kwa shilingi 3000 ni sawa sawa na sh 120m.
Toa kodi ya VAT kama (18m)
Toa malipo wasanii (40m) kima cha chini 1m kila mmoja wako 40
Toa walinzi, polisi, kokodi uwanja, crew, music system,usafiri, generators n.k. (30m)
Promo, perdiem, allowance (10m)
Inabaki milioni 22m tu??

Hizi ni hesabu za makisio tu, inawezekana kuna namna watapata faida zaidi lakini kutokana na kiingilio bado haitakuwa kubwa ukizangatia wanaoenda matamasha ya aina hiyo hawapendi aghali.....

Pengine ndio maana kijana mwenye tamasha lake anapiga maneno kuhusu viingilio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…