Japo wenye Maono ya Kimpira tulisema tumeshatoka, ila yafuatayo kadhaa yamechangia kabisa Kaizer Chiefs FC Kufuzu kwa Aggregate ya 4 - 3

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwanza nianze kwa Kuipongeza Simba SC kwa Kufa Kiume kwa leo nayo Kushinda Goli 3 kwa 0 japo tumetolewa kwa Kanuni ila hatujafungwa bali wote tumeshinda katika nchi zetu.

Hata hivyo kwa Maoni yangu kutokana na Jicho langu la Kimpira na Mtazamo wake baada ya Kuungalia mpira wote kuna Mapungufu kadhaa nimeyabaini na ambayo ndiyo yametugharimu na hata Kushindwa kupata Goli ( Bao ) Muhimu la Nne tumalize Mchezo.

1. FOWADI MZIGO CHRIS MUGALU

Sijui kwa upande wenu ila kwa upande wangu Mchezaji huyu ndiyo Kakosa Magoli mengi ( tena clear chances kabisa ) ambayo yangeamua hatima yetu CAF.

Chris Mugalu kakosa Magoli Matano ambapo Mawili ni ya Vichwa na Matatu ni ya Miguu na hili sasa limekuwa ndiyo tatizo lake Sugu katika Mechi za Kimataifa ( Klabu Bingwa ) au Mechi za Madafu ( Ligi Kuu ya Tanzania )

Nilipoanza tu Kuona nae ameanza tabia za Kikongo za akina Mukoko na Tuisila za Kujiremba sana na kupaka Rangi hadi Kusuka Nywele nikajua Shughuli ndiyo imeisha na imeisha kweli Mguuni mwake sema tu Hirizi yake ya Kupendwa na Kocha Gomez Kisoka ndiyo inambeba na Kumlinda.

2. KOCHA GOMEZ KUTOJIELEWA

Hivi Kocha wa Simba SC Didier Gomez da Rosa ina maana alikuwa hauoni Ubovu wa Mshambuliaji Chris Mushimba Kopa Mugalu na akambadilisha kwa faida ya Timu kwa Kumuingiza ' The Hitman ' Meddie Kagere?

Ni Kocha mzuri sana ila kwa hili la kutopenda Kumchezesha Meddie Kagere ( tena Top Goal Scorer ) wa Simba SC kunatushangaza wengi na pia tunaogopa kuwa hali hii ikiendelea inaweza hata Kumharibu Kisaikolojia Mchezaji husika na hata Kufikiria Kuhama ( Kuondoka ) Simba SC na kuja Kujutia baadae kama ambavyo tulikuja Kujuta ( Kujutia ) kwa Mshambuliaji Amis Jocelyn Tambwe alipoondoka Simba SC yetu.

Kama Kocha Gomez ana Chuki na Kagere nao pia Uongozi uwakalishe Kisesera ( Kitako ) ili wayamalize kwani nimjuavyo ' Bull Striker ' Meddie Kagere yale Magoli ambayo Mugalu kayakosa ( Kipumbavu kama si Kizembe ) kabisa Yeye angefunga yote kama hata si Moja au Mawili.

3. UCHOYO, UBINAFSI NA PAPARA KWA WACHEZAJI WA SIMBA SC

Nina uhakika wa 95% kwa Morali waliyokuwa nayo Wachezaji wa Simba SC leo wangeacha Papara, Ubinafsi na Uchoyo wa kupeana Pasi nilikuwa naziona kabisa ( wazi wazi ) Goli 6 hadi 7.

4. AHADI ZA MO DEWJI KWA WACHEZAJI WA SIMBA SC ZILIWAHARIBU MAPEMA KISAIKOLOJIA

Kila Mchezaji wa Simba SC alikuwa akihaha bila mpangilio ( hasa kwa kukosa Team work ) na hatimaye kila wakifika katika Goli la Kaizer Chiefs FC wanakosea na Kutofunga Magoli ya haraka ili Biashara imalizike tu mapema kwa Mkapa.

Watu wa Saikolojia hawakufanya vyema Kazi yao ya Kuwajenga hasa Kiakili kupelekea Akili zao Kuwaza zaidi Ahadi ya Zawadi na siyo Utulivu na Umakini uliokuwa ukihitajika ( ukitakiwa ) mno katika Mchezo huu wa marudiano Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

5. BERNARD MORRISON KUPENDA KUCHEZA NA JUKWAA ZAIDI NA SIYO KUISAIDIA TIMU KWANZA

Nikiri tu kwamba kweli Kuingia Kwake baada ya Kutolewa kwa Kiungo Punda Muzamiri Yassini ambaye Mechi ilimshinda mapema tu kuliongeza Uhai kwa Timu na Chachu ya Ushambuliaji.

Kinachomgharimu tu Bernard Morrison ni Kupenda kucheza na Jukwaa, Sifa za Kipuuzi na kutokuwa pia na Nidhamu ya Mchezo huku pia akiwa mzito Kukaba pale akipoteza mpira na anautafuta kwa Ulazima Ufalme wa Simba SC wakati bado hastahili kuwa Mfalme kama akina Emanuel Okwi.

6. UFAZA ULIOPITILIZA WA CLATOUS CHAMA AWAPO UWANJANI

Sikatai kuwa ni Mchezaji mzuri sana na ana Kipaji cha Kipekee na hata Goli kafunga ila tatizo moja Kubwa ambalo linaudhi mno kama pia siyo Kukera.

Chama anapoozesha sana Mpira na Timu kwa ujumla na ni Chama huyu huyu pia hawi mwepesi katika kutoa Pasi za Ushindi kwa Wenzake huku akiwa ana Ubaselona ( Ubishoo ) mwingi hata akiwa tu ndani ya 18 na hata ndani ya 6.

7. KUUMIA KWA THADEO LWANGA NA JOASH ONYANGO KULIHARIBU MFUMO MZIMA NA MIPANGO THABITI

Kuumia Kwao ni Pigo kwa Simba SC kwani kuna Mipira mingi ya Kona Simba SC ilipata na kwa nimjuavyo Beki Onyango alivyo mzuri kwa Vichwa angeweza hata Kufunga Goli kama ambavyo mara nyingi amekuwa akifunga kwa Vichwa.

Kabla ya Kuumia Thadeo Lwanga Kiungo chote cha Kaizer Chiefs FC kilikufa na Mwanaume akilimiliki vyema Dimba huku akiwagonga ( akiwapa Chai ) Viungo wa Timu hiyo Pinzani na kupelekea kuharibu kabisa Uchezaji wao na muda mwingi Simba SC Kuutawala Mchezo.

Namalizia kwa kusema Simba SC haijatolewa kwa Kufungwa bali imetolewa kwa Kanuni tu za Uwiano wa Magoli na imeendelea kutuma Meseji barani Afrika kuwa kwa Mkapa ukitua ( ukija ) tu ni lazima utafungwa utake au usitake.

Mwisho ni Ushauri wangu tu Wahusika wakiona unafaa ( unawafaa ) wauchukue kwamba Wachezaji pekee wa Kigeni wenye Msaada na Faida kwa Simba SC ni Chama, Miquissone, Onyango, Kagere, Bwalya, Lwanga na Morrison tu hivyo wengine waachwe ( watemwe ) kisha Waletwe Wachezaji wapya wa Kigeni Watatu ( 3 ) wa maana, tishio na wenye uwezo mkubwa na Kikosi kisibadilishwe bali Kiimarishwe tu.

Sasa nguvu zote ni VPL na ASFC pekee.
 
Esperence mechi ya kwanza kafungwa 2-0, ila mechi ya marudiano leo esperence ndie aliepita.. tukiwaambia mashindano ya caf yana timu zake ni zile zile miaka yote tunaonekana wanafiki
Taratibu naziona tena Timu za Uarabuni ( hasa Al Ahly ) inaenda Kubeba Kombe hili la Ubingwa wa CAF Champions League.

Hata hawa Kaizer Chiefs FC watatolewa.
 
Acha kudanganya.
Mpira hauna mwenyewe.
Simba wamecheza vizuri na walikuwa na nafasi ya KUPITA.magoli mengi Tu wamekosa.hadi moja imegonga mwamba.
Simba imepata goli 3 tofauti ya goli moja.
Sio mbaya.
Esperence mechi ya kwanza kafungwa 2-0, ila mechi ya marudiano leo esperence ndie aliepita.. tukiwaambia mashindano ya caf yana timu zake ni zile zile miaka yote tunaonekana wanafiki
 
Esperence mechi ya kwanza kafungwa 2-0, ila mechi ya marudiano leo esperence ndie aliepita.. tukiwaambia mashindano ya caf yana timu zake ni zile zile miaka yote tunaonekana wanafiki
Naweza kusema ndio
Ndio kwa sababu takwimu ziko hivyo Afrika magharibi, na kaskazini vilabu vyao hasa kaskazini wanafanya vyema sana.

Hata ulaya CL timu ni zile zile tu. Zikibadilika mara moja au mbili misimu mingine ni zile zile...
 
Acha kudanganya.
Mpira hauna mwenyewe.
Simba wamecheza vizuri na walikuwa na nafasi ya KUPITA.magoli mengi Tu wamekosa.hadi moja imegonga mwamba.
Simba imepata goli 3 tofauti ya goli moja.
Sio mbaya.

Mpira hauna mwenyewe ndio maana esperence, waydad, al ahly wamepita.. hao ni mabingwa kila mara wanapokezana tu. Kaizer mwenyewe kapata zari baada ya kuwatia 4 vibonde wake simba
 
Simba vibonde?
Kuwa funga goli 3 kaizer chiefs mnadhani KAZI ndogo?
Siku utopolo ombeni mechi ya kirafiki na kaiza.
Mpira hauna mwenyewe ndio maana esperence, waydad, al ahly wamepita.. hao ni mabingwa kila mara wanapokezana tu. Kaizer mwenyewe kapata zari baada ya kuwatia 4 vibonde wake simba
 
Angeweza kufungua
Angeweza kupiga pasi
Angeweza kupiga krosi
Angeweza
Angeweza
Angeweza............
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Washafungwa na kuondolewa mashindanoni basi wajipange upya msitafute justification,Simba Wana maneno meeengi ndo yamawagharim yan wanajiona wanauwezo sana kumbe hovyo tu.

Game ya kwanza kule SA walienda wakijiamini baada ya kuaminishwa na mpuuzi wanaemwita msemaji wao eti oooh KC ni utopolo mara wapo nafasi ya 10 lkn walichokutana nacho wamekoma.

Moja ktk post zake msemaji wao anasema "zingeongezwa dakika 10 tu walikuwa wanafungwa". Yaan hakujua kuwa mpira ni dakika90? Hizo dkk 10 zinaongezwa kutoka wapi kama sio upuuzi ni nini?

Mi nadhan masuala ya kiufundi aachiwe kocha huyu mropokaji wao anasababisha mnakufa kiboya
 
tujikumbushe utopolo walipopangwa kundi gumu kabisa la hatari wakiwa na gor mahia na rayon ya rwanda tena kombe la shirikisho dah kudadadeki majinga ni majinga tu milele na milele amina
fungu la kukosa.PNG
 
tujikumbushe utopolo walipopangwa kundi gumu kabisa la hatari wakiwa na gor mahia na rayon ya rwanda tena kombe la shirikisho dah kudadadeki majinga ni majinga tu milele na milele aminaView attachment 1794598
Hilo ndo tatizo la wajinga yaan kwakuwa yanga walifanya vibaya basi unajificha kweny kivuli hicho? Hapa linazungumzwa Simba kutolewa kwny mashindan ww kwa upumbavu wako unalinganisha na yanga.
 
Kuna watu duniani wanasumbuliwa na wivu tu, yaani kwa kiwango kilichoonyeshwa na simba msimu huu nina imani yanga watafika level hii miaka 50 ijayo! Eti simba wana midomo, yaani waache kufurahia uzuri wa timu yao, yanga mjifunze kupitia simba kwa nafasi tunazowapa kushiriki club bingwa Africa bila kuwa mabingwa kwani kwa utopolo huo si rahisi kuwa mabingwa wa nchi hii kwa miaka kumi ijayo!
 
Manara mwingine huyu....hiyo nafasi mpen mwadui FC sio lazima mumipe Yanga nyie si ndo mnagawa nafasi
 
Kwanza nianze kwa Kuipongeza Simba SC kwa Kufa Kiume kwa leo nayo Kushinda Goli 3 kwa 0 japo tumetolewa kwa Kanuni ila hatujafungwa bali wote tumeshinda katika nchi zetu.

Hata hivyo kwa Maoni yangu kutokana na Jicho langu la Kimpira na Mtazamo wake baada ya Kuungalia mpira wote kuna Mapungufu kadhaa nimeyabaini na ambayo ndiyo yametugharimu na hata Kushindwa kupata Goli ( Bao ) Muhimu la Nne tumalize Mchezo.

1. FOWADI MZIGO CHRIS MUGALU

Sijui kwa upande wenu ila kwa upande wangu Mchezaji huyu ndiyo Kakosa Magoli mengi ( tena clear chances kabisa ) ambayo yangeamua hatima yetu CAF.

Chris Mugalu kakosa Magoli Matano ambapo Mawili ni ya Vichwa na Matatu ni ya Miguu na hili sasa limekuwa ndiyo tatizo lake Sugu katika Mechi za Kimataifa ( Klabu Bingwa ) au Mechi za Madafu ( Ligi Kuu ya Tanzania )

Nilipoanza tu Kuona nae ameanza tabia za Kikongo za akina Mukoko na Tuisila za Kujiremba sana na kupaka Rangi hadi Kusuka Nywele nikajua Shughuli ndiyo imeisha na imeisha kweli Mguuni mwake sema tu Hirizi yake ya Kupendwa na Kocha Gomez Kisoka ndiyo inambeba na Kumlinda.

2. KOCHA GOMEZ KUTOJIELEWA

Hivi Kocha wa Simba SC Didier Gomez da Rosa ina maana alikuwa hauoni Ubovu wa Mshambuliaji Chris Mushimba Kopa Mugalu na akambadilisha kwa faida ya Timu kwa Kumuingiza ' The Hitman ' Meddie Kagere?

Ni Kocha mzuri sana ila kwa hili la kutopenda Kumchezesha Meddie Kagere ( tena Top Goal Scorer ) wa Simba SC kunatushangaza wengi na pia tunaogopa kuwa hali hii ikiendelea inaweza hata Kumharibu Kisaikolojia Mchezaji husika na hata Kufikiria Kuhama ( Kuondoka ) Simba SC na kuja Kujutia baadae kama ambavyo tulikuja Kujuta ( Kujutia ) kwa Mshambuliaji Amis Jocelyn Tambwe alipoondoka Simba SC yetu.

Kama Kocha Gomez ana Chuki na Kagere nao pia Uongozi uwakalishe Kisesera ( Kitako ) ili wayamalize kwani nimjuavyo ' Bull Striker ' Meddie Kagere yale Magoli ambayo Mugalu kayakosa ( Kipumbavu kama si Kizembe ) kabisa Yeye angefunga yote kama hata si Moja au Mawili.

3. UCHOYO, UBINAFSI NA PAPARA KWA WACHEZAJI WA SIMBA SC

Nina uhakika wa 95% kwa Morali waliyokuwa nayo Wachezaji wa Simba SC leo wangeacha Papara, Ubinafsi na Uchoyo wa kupeana Pasi nilikuwa naziona kabisa ( wazi wazi ) Goli 6 hadi 7.

4. AHADI ZA MO DEWJI KWA WACHEZAJI WA SIMBA SC ZILIWAHARIBU MAPEMA KISAIKOLOJIA

Kila Mchezaji wa Simba SC alikuwa akihaha bila mpangilio ( hasa kwa kukosa Team work ) na hatimaye kila wakifika katika Goli la Kaizer Chiefs FC wanakosea na Kutofunga Magoli ya haraka ili Biashara imalizike tu mapema kwa Mkapa.

Watu wa Saikolojia hawakufanya vyema Kazi yao ya Kuwajenga hasa Kiakili kupelekea Akili zao Kuwaza zaidi Ahadi ya Zawadi na siyo Utulivu na Umakini uliokuwa ukihitajika ( ukitakiwa ) mno katika Mchezo huu wa marudiano Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

5. BERNARD MORRISON KUPENDA KUCHEZA NA JUKWAA ZAIDI NA SIYO KUISAIDIA TIMU KWANZA

Nikiri tu kwamba kweli Kuingia Kwake baada ya Kutolewa kwa Kiungo Punda Muzamiri Yassini ambaye Mechi ilimshinda mapema tu kuliongeza Uhai kwa Timu na Chachu ya Ushambuliaji.

Kinachomgharimu tu Bernard Morrison ni Kupenda kucheza na Jukwaa, Sifa za Kipuuzi na kutokuwa pia na Nidhamu ya Mchezo huku pia akiwa mzito Kukaba pale akipoteza mpira na anautafuta kwa Ulazima Ufalme wa Simba SC wakati bado hastahili kuwa Mfalme kama akina Emanuel Okwi.

6. UFAZA ULIOPITILIZA WA CLATOUS CHAMA AWAPO UWANJANI

Sikatai kuwa ni Mchezaji mzuri sana na ana Kipaji cha Kipekee na hata Goli kafunga ila tatizo moja Kubwa ambalo linaudhi mno kama pia siyo Kukera.

Chama anapoozesha sana Mpira na Timu kwa ujumla na ni Chama huyu huyu pia hawi mwepesi katika kutoa Pasi za Ushindi kwa Wenzake huku akiwa ana Ubaselona ( Ubishoo ) mwingi hata akiwa tu ndani ya 18 na hata ndani ya 6.

7. KUUMIA KWA THADEO LWANGA NA JOASH ONYANGO KULIHARIBU MFUMO MZIMA NA MIPANGO THABITI

Kuumia Kwao ni Pigo kwa Simba SC kwani kuna Mipira mingi ya Kona Simba SC ilipata na kwa nimjuavyo Beki Onyango alivyo mzuri kwa Vichwa angeweza hata Kufunga Goli kama ambavyo mara nyingi amekuwa akifunga kwa Vichwa.

Kabla ya Kuumia Thadeo Lwanga Kiungo chote cha Kaizer Chiefs FC kilikufa na Mwanaume akilimiliki vyema Dimba huku akiwagonga ( akiwapa Chai ) Viungo wa Timu hiyo Pinzani na kupelekea kuharibu kabisa Uchezaji wao na muda mwingi Simba SC Kuutawala Mchezo.

Namalizia kwa kusema Simba SC haijatolewa kwa Kufungwa bali imetolewa kwa Kanuni tu za Uwiano wa Magoli na imeendelea kutuma Meseji barani Afrika kuwa kwa Mkapa ukitua ( ukija ) tu ni lazima utafungwa utake au usitake.

Mwisho ni Ushauri wangu tu Wahusika wakiona unafaa ( unawafaa ) wauchukue kwamba Wachezaji pekee wa Kigeni wenye Msaada na Faida kwa Simba SC ni Chama, Miquissone, Onyango, Kagere, Bwalya, Lwanga na Morrison tu hivyo wengine waachwe ( watemwe ) kisha Waletwe Wachezaji wapya wa Kigeni Watatu ( 3 ) wa maana, tishio na wenye uwezo mkubwa na Kikosi kisibadilishwe bali Kiimarishwe tu.

Sasa nguvu zote ni VPL na ASFC pekee.
Kwanza,nakuuliza wewe ni kocha kwa kusomea au ni mradi tu unaenda uwanjani na kutizama mpira?
Unajua kuwa kukosa magoli hata wachezaji wa kimataifa wanakosa lakini kocha huwaacha uwanjani,kwani wanatisha madefenda wa timu pinzani
Match analyists watafanya uchambuzi baadae na pia tutapata mafunzo kutokana na kushindwa
 
Back
Top Bottom