rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,784
- 23,312
Kwanini sintoshoriki zoezi la sensa
mimi ni mkiristo wa dhehebu la rc.katika mafundisho yetu yesu alizaliwa wakati wa zoezi la sensa hivyo imani ya dini yangu haipingani na zoezi hilo.
Pia naelewa zoezi hili ni muhimu kwa ajili ya serikali kujua idadi ya watu wake ili iweze kupanga mipango ya maendeleo kulingana na idadi hiyo.
Pamoja na kutambua yote hayo nimeamua kutoshiriki zoezi hilo kwa sababu kuu zifuatazo
kama serikali iliweza kulazimisha tununue ndege ya thamani hata kama wananchi watakula nyasi zoezi hili ni kiini macho.serikali makini inajali huduma muhimu za wananchi na sio huduma za mtu mmoja mmoja.
Kama serikali imeshindwa kuwalipa madokta na walimi kwa kisingizio haina pesa na wakati huo huo imeendelea kuwaongeza wabunge marupurupu na posho zao pia imeendelea kununua magari ya thamani,kuongeza mikoa,wilaya na kuwa na baraza kubwa la mawaziri bado zoezi la sensa halina maana.
Kama viongozi wa serikali na wabunge wanaendelea kupelekwa kutibiwa india badala ya kuimarisha hosptal zetu sijui wanataka wajue idadi yetu ili wafanyeje.
Kama bajeti za wizara nyeti kama afya na elimu hazitengewi bajeti ya kutosha ni mipango gani watakayoipanga baada ya kutuhesabu
sababu ni nyingi siwezi kuzitaja zote nitawachosha ila kesho sihesabiwi