kabla ya hiyo nilituma hii ikaondolewa:
Ndugu wanajamvi, waislamu hawahesabiwi kwa sensa isiyo na kipengele cha dini, tunajua pia kuwa BAKWATA watahesabiwa. Ni wazi kuwa serikali inaweza kufanya chochote lakini haiwezi kuwalazimisha watu kufanya chochote, haikuwa hivyo tokea mamlaka zilipoanza kuwepo duniani. KWA HILI LA SENSA YA MWAKA HUU TUNASEMA, WAISLAMU HAWATAHESABIWA BAKWATA, WAKRISTO NA WAPAGANI WAMEKUBALI KUHESABIWA
- Kwa nini kipengele cha sensa kiliondolewa?
Inasadikika kuwa sensa ya mwisho kufanyika wakati wa ukoloni Tanzania ilikuwa na Waislamu asilimia 60, Tukisema kuwa serikali ilikiondoa kipengele hiki kwa sababu maalumu ikiwemo kuwa na nafasi ya kuendeleza na kusadikisha takwimu za uongo ili kushamirisha Mfumo Kristo (MK) Tanzania tunakosea?
- Kwa nini taasisi mbalimbali za serikali na binafsi zimekua zikitoa takwimu za watu na dini zao?
Mfano 0fisi ya waziri mkuu inadai wakristo ni 45%-waislamu 35%. TBC1, imetangaza wakristo ni 52%-waislamu 32%.Bodi ya watalii -
Christianity and Islam are the predominant religions of Tanzania. About 40-45% of the population practice Christianity, about 35-40% practice Islam.,Tovuti kikatoliki (
RCNet) waislamu 34%- na wakristo ni 44%
Na hapa kuna hoja mbili,
a) kwa nini takwimu zinatofautiana? na b)kwa nini pamoja na kutofautiana zote zinaonesha wakristo ni wengi kuliko waislamu?
Kwa kawaida jambo la uongo lazima hukwama, takwimu zinatofautiana kwa sababu ni za uongo, Zote zinaonesha wakristo ni wengi kwa sababu za kukidhi matakwa ya MK.
Mkurugenzi wa TBC alipoulizwa kuhusu takwimu katoa wapi aliishia kuomba radhi, kakosea, swali ni je kakosea nini? Amekuwa akikosea mambo mangapi ya kitaifa kwa ujumla wake kama lilivyo hili? Huu ndio MK
3.Kwa nini kiwepo kipengele cha kuhesabiwa kwa nyumba za ibada?
Waislamu wakisema kuwa kuhesabiwa kwa nyumba za ibada pekee kunaweza kutumiwa na wapotoshoshaji wa Umma kupitia MK, kuwa Wkristo ni wengi kwani siku hizi kuna utitiri wa madhehebu kikristo na makanisa binafsi hata kama yana waumini wachache achilia mbali uyoga wa makanisa yanojiita ya wokovu? Kwa nini nyumba za ibada na sio na wanaoabudu humo?, Serikali inataka kugawa misala misikitini na mabench kanisani?
Waislamu wa leo ni tofauti na wa enzi hizo, wanajua wanachokifanya na hili la sensa ni moja na mengine yatakuja,hatuhitaji kumtafuta kiongozi wala Sheikn Ponda kwa hili, elimu tulishapata , macho yalishafumbuliwa na Tunaelewa athari za mfumo Kristo katika jamii
- Tulisadikishwa kuwa waislam hawakusoma, kumbe data zinaonesha NECTA inawapunguza
- Tukasadikishwa kwamba hawajengi Mashule na Hospitali ila wanajenga misikiti, kumbe wenzetu wanajenga kupitia fedha wanazopewa na serikali hii hii kupitia MoU
- Tukasadikishwa kuwa nchi hii haina dini , kumbe serikali yetu ina mfumo Kristo ambao haukuandikwa popote lakini unafanya kazi zake kwa siri na waziwazi
TUMEKATAA KWENDA KWA MATAKWA YA MK, NARUDIA WAISLAMU HATUHESABIWI.