Huwa sipendi kumjaji mtu kwa sababu ya dini yake,dini haibadilishi genetic make up ya mtu.Waisilamu ,wakristu,wapagani wote hawa wana one thing in common(wote ni watanzania).Tuwekeni maslahi ya nchi kwanza tutafanikiwa, udini ukabilia kwangu mimi mtu anayeendekeza haya namuona anahitaji msaada.Na ninautilia mashaka ufahamu wake,matatizo hayaletwi na dini matatizo tunayasababisha wenyewe.Ni kawaida wanadamu kutafuta mtu wa kumlaumu au kitu cha kutumia kama sababu ya kushindwa kwetu kufanya jambo fulani.Angalieni hata nchi za kiislamu au za kikiristu tu, je zinaishi kwa amani?Si kweli matatizo yapo siku zote,tutauana wenyewe kwa ujinga wetu.Siwezi kuwa kama wewe na wewe huwezi kuwa kama mimi,hata kwenye ndoa watu hutofautiana ijekuwa sisi.Tujifunze tubadilike,tutofautishe mawazo ya mtu na hali halisi ya mambo ilivyo(opinions and facts).Mi nimesoma na waisilam,wakristo na wapagani pia,huwa namshangaa mtu akisema watu fulani(anataja dini) ni wajinga au vilaza.Kila mtu anaujinga wake kwa sababu hakuna ajuae kila kitu.Watu ambao hujadili mambo haya wengi wao maisha yanawasumbua,mtafute mtu aliyefanikiwa utaona anamtizamo tofauti wa mambo haya.Tusiwapotoshe watu kwa kuwa na misimamo ambayo haijengi nchi kwa manufaa yetu binafisi.We have to learn to see what others are seeing instead of accusing them,you are wrong ,we are right.Wengi wetu tuko kwenye dini ambazo tumezaliwa tukawakuta wazazi wetu wanaamini,je ulishawahi kuwauliza wazazi wako kwa nini wanaamini hicho wanacho amini?Action speaks louder than words,ukitaka kumvutia mtu huko uliko kiimani siyo maneno yako bali matendo yako yatamvutia zaidi.Learn to walk the talk.
Naheshimu uhuru wa mtu wa kuabudu,watanzania wenzangu tubadilike,si vizuli kumwita mwenzako (waktristu/waisilam/wapagani) ni vilaza.Umefavya research? Au unasema kwa sababu unamdomo wa kuongea.
Tanzania kwanza,tanzania kwanza.Tanzania hatuendelei kwa sababu maslahi ya nchi ni ya mwisho,hivyo hivyo hata viongozi wetu maslahi ya chama kwanza ya nchi baadaye.Itaendelea kutucost.
Kuna vitu ambavyo huwezi kuvibadilisha na huna control navyo,kwa mfano hukuchagua uzaliwe ktk familia uliyopo sasa au katika bara ulilopo sasa,au wazazi wako wawe hao,kama zingekuwepo form za kujaza kabla ya kuzaliwa naamini ungechagua kitu tofauti.
God created us all,mwanadamu atajiangamiza mwenyewe taraatabu kutokana na matendo yake."We can choose our actions but we can not choose the consequencies of our actions".
Tufikilie kabla ya kupost vitu,impact yake,tutaelewekaje kwa wenzetu,wenzetu watajisikiaje.Be considerate.
Ni hayo tu.