Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983


Sawa nakubali, Zakaria yupo katika hiyo picha lakini haina maana kuwa anafanya biashara na hao Mafisadi [RIdhwani etc.] isipokuwa kwa vile wote ni wasafirishaji wa mafuta bila shaka wana ushirikiano kupitia chama chao ambamo yeye Zakaria ni kiongozi mkuu!!! Nasisitiza kuwa Zakaria Hans Pope hana ubia wa biashara na wakina Lowassa.
 
nyerere alivyowashika akawaambia nyie si mnajifanya wanaume wa shoka sio,basi niwaonyeshe mimi ni zaidi yenu.ndipo akaamuru wote wahasiwe

Hizo ni porojo zisizo na ukweli wowote.
 
Mbona umemtaja hans pop tu wengine huwajui eeh??? Ngoja nikutajie wengine sasa. KAPTEN EUGEN MAGANGA, KADEGO, MAGII, NA KUNA MMOJA ALIKIMBILIA UINGEREZA jina lake limenitoka kidogo. Kapten eugene maganga tumemzika mwaka juzi kijijini ITAGA MKOA WA TABORA alikua anasumbuliwa na kisukari aliacha watoto wawili ote wa kiume mmoja anaitwa MICKEY EUGEN MAGANGA na RAYMOND EUGEN MAGANGA ndio mimi nilieandika maneno haya. R.I.P EUGEN MAGANGA
 
Naona Mkuu Pasco ameanza kufunguka siondoki hapa hadi Kieleweke,,,!
 
msukuma unayemsema alikuwa anaitwa suleiman matusela kamando..alisamehewa na ameshafariki...aliyetorokea kenya na Uk ni Lugangira..ameshafariki....alitokoroka na ex -pilot/comandoo akitwa Hatii maghee-alishikwa na kurudishwa keko.wengine pia walisamehewa na wameshafariki....pope alikuwa kikosi cha mizinga na kaka yake alikuwa Rubani Airwing.....issue ilitisha sana na kesi yake pia ikiwapa umaarufu wanasheria na ma lawyers...mageuzi ya meanza siku nyingi....
 
Jamani mimi bado narudia OMBI langu hivi kweli hakuna waandishi wa Kitanzania wanaoweza kuandika huu mkasa wa akina Hans Poppe ili kuweka KWANZA kumbukumbu na PILI ili vizazi vijavyo viweze kujifunza kutokana na tukio hili.

Tunataka mzungu aje kutoka ULAYA atuandikie hii party ya history ya nchi yetu apate PhD yake. Halafu "makanjanja" (SIC!) wetu waishie kutafasiri kazi hiyo ya mzungu kwa lugha ya kiswahili!?.

Mbona Wamarekani wameandika vitabu vingi tu kuhusu assassination Kennedy, sembuse hii a failed coup! Waandishi wa Tanzania amkeni jamani.

kama kuna mwana JF yeyote anayefahamu wapi naweza kupata hiki kisa cha akina Hans Poppe naomba anifahamishe. Niko interested kujua ALPHA and OMEGA ya hilo jaribio la mapinduzi. Kisa kizima na wahusika wake.
 
Uhaini ulipangwa 1982, home kwetu ni Drive-in Estate, nyumba yetu na nyumba ya Banyikwa ziliuwa zimeungana tukitenganishwa na ukuta. Hapo ndipo ilipokuwa ikifanyika mikutano ya kupanga mambo!

Habari hizo zilivuja mapema na zilivujishwa na Vijana waliokuwa wakilima michicha na kumwagilia michicha pale mbele ya Flat za Drive INN na Mzee mmoja aliyekuwa akichoma mahindi karibu na nyumbani kwa walikokuwa wakikaa Akina Hans Pope maeneo ya karibu na Highlands Cinema Iringa waliripoti juu ya pilikapilika fulani zisizoeleweka wakachoma utambi!Wanaume wakaanza kujipanga

Na nadhani kuna vitu hawakuvijua vizuri kuhusu hizo flat za Drive Inn!!!

Fungakazi ilikuwa lile eneo la Msasani bonde la Mpunga karibu na mradi wa chumvi ulipokuwepo ambako wafanya mapinduzi walitaka kuangalia na kuweka vifaa vyao vya kumtandika nyerere katikati ya magugu maji ili wamrarue akienda nyumbani au akienda ofisini.Hawakujua kuwa lile pori la magugu maji wamakonde walikuwa wakitumia kucheza watoto wao wa kike na KUlikuwa na wanaume wa kimakonde waliOkuwa wakikaa juu ya magorofa yasiyoisha kuangalia eneo lile na kufukuza watu wasisogee eneo la mambo yao.Walipowaona wanaangalia karavati na kuzunguka zunguka eneo lile wakawaripoti kuhusu pilika zisizo za kawaida mitego ikaanza kuwekwa taratibu.
 
Magazeti ya Rai enzi zile walikuwa na makala kibao kuhusu haya mapinduzi.Yalishaandikwa sana sema labda ni bwamdogo flani.

 

Nyerere huwa sielewi kwa nini alikuwa mtu wa kusamehe sana waliokuwa wakitaka kumpindua! yaani nasikia kuna askari moja alisema Kambona lazima niende uingereza nikamwue utake usitake wakati ule Nyerere anasumbuliwa na mpaka wa Malawi na Kambona Mnyasa koko anaendelea na harakati za kutaka kumpindua nYerere Uingereza.

Alichofanya Nyerere alimwambia nimekwambia nimemsamehe usimwue Kambona. Alipoona kapania Akamtoa jeshini akampeleka uraiani kushika vyeo vya kisiasa na akampiga marufuku ya kusafiri nje ya nchi!

Kuna wakati huwa nadhani Nyerere alikuwa mkatoliki mno angekuwa mwingine au angeua hadi basi!
Nyerere uwezo wa kusamehe unashinda hata wa Mandela.
 

Nilisoma makala hio miaka ya 2000 mwanzoni nadhani kama sio mwishoni mwa miaka ya tisini....mwaka jana nilienda habari coorperation kuulizia kama naweza kupata makala hizo, cha kushangaza wakaniambia niende maktaba ya taifa huwa wanaweka kumbukumbu za magazeti....sikuwa na muda so sikufuatilia zaidi.
 
This is a smart chap and hard working person. He has got big influential power that is why he survives in the business and thrives as well. Probably he is still connected to the system he tried to turn against during Nyerere's time. Who knows?
 
Unadhani aliamka tu asubuhi akaorganise wenzake wakampindue Rais bila kuwa na back-up ya wanasiasa na wafanyabiashara nyuma yake? Ana bahati lile jaribio walilifanya kwa Nyerere, ungekua utawala wa nchi nyingine hizi za kiafrika hata mahakamani kesi zao zisingeenda!

 
Baadhi wanaojua vzr hii stori wanakuja kubeep then wanakimbia!
cc;Pasco,The East africa Eagle,
 
Zakaria Hans pope alikuwa kwenye mizinga yeye alipangwa kupiga mizinga msasani kwa mwalimu endapo mapinduzi yangefanikiwa!
 

Kweli Kabisa kwa sie wazamani pale msasani bonde la mpunga walipojenga May Fair plazza walikuwa wanavuna chumvi pale miaka ya 70's.
 
Kama kuna mwandishi atataka kuandika Kuhusu kadhia hii amtafute Balozi Augstin Mahiga wakati ule alikuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anaijua movie yote mwanzo mpaka mwisho.
 
Why not wakati wafanya Biashara wenyewe ndio hao mawaziri?
Umesahahau ya Maige na kununua nyumba ya 500Mil kusingizia Biashara ya Malori ?

By the way hawa wakina Hans ni Proxy tu wenyewe ni Viongozi serekalini.
Kaptain Kadege na Maganga,Rugakigira wako wapi? Mafanikio ya HansPope yanatokana na msingi wa famiia yao kwa ujumra.Kabra ya huu hawa wagiriki warikuwa tayari matajiri.Mahaini mengine warifariki au kuwa maskini manake warikuta kira chao kimechakaa na hawakuwa na jinsi ira urevi na uzinzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…