Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983


asante mkuu
 
Kwanza ilikuwa. 1964 wanajeshi. Colito[. Lugalo]. Barracks walipofanya rioting. Dar es. Salaam. Halafu lilikuwepo jaribio lililofanywa na. Bibi. Titi. Mohammed na wenzake . By the way,yule. Bibi. Titi alikuwa hajui kusoma na kuandika. Hili jambo nimeambiwa na impeccable sources. Halafu jaribio hilo unalozungumzia ndio la mwisho lililofanywa na. Zakaria. Hans. Poppe. Mwalimu alishtuka sana. Zakaria alipofanikiwa kutoka jela. Akaniambia kwa nini wanamwamini yule wanamtoa jela.
 

Huyu huyu Hans Poppe anayegawa hela Msimbazi??Kweli historia mwalimu mzuri Sana,Andrew kwanini unafikiri Mwalimu hakumwamini Hans Poppe hata hakutaka atolewe lupango?
 
yalikua maasi ya wanajeshi sio mapinduzi.yalizimwa na jeshi la uingereza.kuna kitabu cha paulo sozigwa,kama sikosei alikua mwandishi wa rais ndo kimeelezea vizuri hatua kwa hatua kuhusu kilichotokea.ukitafuta library waweza kukipata.

Naomba title ya hicho kitabu cha paulo soxigwa.
 
Companero,
Si kweli kwamba Oscar ndiye aliyemwokoa na kumficha Mwalimu katika mapinduzi ya 1964. Huyu mtafiti amekosea. Nadhani Kawawa alikuwa na jukumu kubwa zaidi kumshawishi Mwalimu kujificha kuliko Kambona. Kambona hakujua alipofichwa Mwalimu.
Nadhani Kawawa ni lile tukio la mwisho, na ndio jina la simba wa yuda lilipoanzia
 
nini kilitokea hadi baadaye Kambona akakimbia nchi!
 
Alikuwepo na marehem EUGEN MAGANGA cheo chake ni cptn
 
Naomba mnifafanulie Mimi secondary nimeanza mwaka 2004 sasa naomba mniongoze vyema hii history imefichwa sana nakumbuka kunakipindi nilipata nafasi ya kufanyabkazi pale 501JwTz nilikuwa kitengo cha engine room kuna jamaa alinigusia kwamba kuna meja anaitwa kisarika pia alihusika kwenye hiii insu lakini akasamehewa na akashushwa cheo basi naomba msaada wenu
 

Hivi ni huyu Hans Pope wa Simba sports club?
 
Hivi ni huyu Hans Pope wa Simba sports club?
Ndio huyo huyo.Ambaye alikuwa yuko huko UKAWA ni mtu wa TEAM LOWASA na alikuwa bega kwa bega kwenye mbio zake za uraisi.Ndio hao nadhani Kingunge alikuwa akijivunia kuwa Lowasa akishindwa nchi itawaka moto.Lowasa alikuwa na mtandao wa ajabu acha tu.Mungu kainusuru Tanzania
 
tumshukuru mungu
 
Hicho ni cheo kipi mkuu?Maganga alikuwa Luteni.
Alikuwa Captain. Na hivyo ndivyo tulivyomuita tulipokuwa chuoni (UDSM): Captain Maganga. Kuna makala ya Eric Kabendera ambayo imepotosha ukweli na kusema alikuwa Luteni. Ninamfahamu marehemu binafsi.
 
Duh Major Gen Hanspope? Kweli Yerico aliwafuma. Mwanakijiji et al, tuna deni kubwa la kuandika vitabu vya historia ya nchi yetu.
 
This thread made me realize that i didnt know my country although i have two bachelors.. Big up to Yericko Nyerere i always undermined you
 
Hivi mimi humu jamii forum huwa nafanya nini ?? Ni nadra sana kuonekana kwenye mada za aina hii ambazo kimsingi ni elimu ambayo hutaipata popote ,asante waanzilishi wa jamii forum ,shukrani za dhati kabisa kwa wote waliochangia uzi huu ,nimepata kitu kikubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…