Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Mkuu give credit where it is due, Kambona ndiye aliyemsaidia Nyerere. Na ndio maana tunasisitiza kuwa hawa walikuwa washikaji hadi Nyerere akawa ndiye aliyemtoa bibi harusi wa Kambona siku ya harusi yake. Picha zipo zimejaa tele kwenye gazeti la Drum mlilolifungia!
Ni suala la ushikaji au majukumu ya kikazi?
 
Baba yake aliuwawa mwaka 1971 wakati wa vita iliitwa ya MUTUKULA muda kidogo baada ya kumpindua Obote. Mzee Hanspope alikuwa RPC mkoa wa ziwa magharibi sasa Kagera. Mwili wake ulifichwa Mulago Hospital mpaka 1979 ukardishwa na kuzikwa Iringa.
Kwanini mwili ulifichwa? Na kwanini miaka mingi hivi?
 
Hadithi za kutengenezwa huwa tamu sana!! Hivi waasi waliokuja kuachiwa na mzee Mwinyi ni kina nani?

Hadithi za kutengenezwa? Hebu jaribu kuielewa historia ya Tanzania nje ya milango ya shule.

Hizo si hadithi za kutengeneza. Baadhi yetu tulikuwa tunazisikia kwenye radio.
 
Hadithi za kutengenezwa? Hebu jaribu kuielewa historia ya Tanzania nje ya milango ya shule.

Hizo si hadithi za kutengeneza. Baadhi yetu tulikuwa tunazisikia kwenye radio.
Kama ambavyo tulisikia "Rais anachapa kazi... au mlitaka mmuone anazurula Kariakoo..." ikiwa utaamini kila unachoambiwa pasina kujipa muda wa kudadavua... utalishwa tangopori ...aaah hapana "...za kuambiwa...!!
 
Hadithi za kutengenezwa? Hebu jaribu kuielewa historia ya Tanzania nje ya milango ya shule.

Hizo si hadithi za kutengeneza. Baadhi yetu tulikuwa tunazisikia kwenye radio.
Kama ambavyo tulisikia "Rais anachapa kazi... au mlitaka mmuone anazurula Kariakoo..."
 
Kama ambavyo tulisikia "Rais anachapa kazi... au mlitaka mmuone anazurula Kariakoo..."

Kama unazungumzia matukio haya matatu ya majaribio ya kuleta mageuzi/mapinduzi haya siyo drama:
1. Lile la 1964 kuna uncle wetu mmoja ndiyo kwanza alikuwa amerudi kutoka UK mafunzoni, ile mutiny ilimkumba akafukuzwa kazi.

2. Hilo la 1969/71? Tulikuwa tunasikiliza kwenye vyombo vya habari. Masikini Bi Titi hakuwahi kueleza lolote kuhusu kipindi chake alipokuwa jela kwa hivyo tumepoteza historia.

3. La 1983 niliisoma ile story ya Maganga kwenye Rai. Aidha niliwahi kusoma story ya Lugangira na jinsi alivyokamatishwa na Yahya Husein kiujanja hivi.
 
Mitaani kuna vijiwe aina mbili... vijiwe vya wavuta bange na vijiwe vya wanywa kahawa kote kuna vijiredio!!
Taarifa za redio zikaendelea kusema kuwa "Idi Amini alikuwa akila nyama za watu!!" Zilikutwa kwenye friji!!!
 
Niliwahi kusoma kitabu ‘State of blood’ ambacho kiliandikwa na aliyekuwa Waziri wake mmoja aliyekuwa mkimbizi kipindi kile.

Aliandika kwamba ndani ya friji lake la ofisini alikuwa amehifadhi kichwa cha mtu (nimesahau kama kilikuwa cha his murdered wife au boyfriend wake). Alikuwa anapenda kufungua lile friji ili mualikwa aweze kuona nini kingemtokea kama angekuwa mbishi.

To be fair siku moja niliona mahojiano baina ya binti yake mmoja na mtangazaji wa tv moja USA. Yule mtangazaji alimuuliza hilo suali na binti alikataa na kusema ilikuwa ni propaganda za western media kuharibu jina lake.
 
Japo historia haisemi wazi juu ya mambo mengi sana Tanganyika na Tanzania ya leo, lakini Mwalimu Nyerere tangu awe kiongozi wa nchi hii amenusurika mapinduzi MATATU,

Moja ni la mwaka 1964, lapili ni la mwaka 1970 na la mwisho ni la mwaka 1980 (Sina uhakika sawa na hiyo miaka)

Jaribio la kwanza ndilo lilipelekea kuundwa kwa JWTZ na lilizimwa kwamsaada wa Malkia wa Uingereza aliyetuma makomandoo maalumu na wakafanikiwa, Jaribio la pili ndilo lililopelekea kuundwa kwa Usalama wa Taifa na kikosi maalumu cha ulinzi wa Rais,

na jaribio la mwisho ndio lilipelekea kubadili sera ya usalama wa Taifa kwa kuwapandikiza kila kwenye sekta na kuwa kila mtu ni mlinzi wa nchi hii (usalama)

Sikumbuki vema lakwanza kama liliongozwa na nani lakini Kambona ndie alimficha Mwalimu, lapili sikumbuki vema, lakini la mwisho liliongozwa na baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Anga cha Ukonga Banana,

Na mipango yao iliharibikia palepale Banana baa baada ya mmoja wao kulewa na kuanza kuongea hovyo hasa akisema yeye anataka cheo cha uwaziri mkuu!

Enzi hizo 1980+ mmoja wa makamanda wa usalama wa taifa aliyeongoza kuwadhibiti waasi hao ni Mabere Marandu,

Na alifanikiwa kuongoza oparesheni za kumsaka na kumuua mmoja wa makomandoo ambae alikuwa ameandaliwa rasmi kumuua Nyerere,

Mapambano yalikuwa ni makubwa kutoka airport hadi kinondoni ulipo ubalozi wa Marekani sasa ndipo walipofanikiwa kumuua!

Jambo la kuwashangaza waasi wale (wanajeshi) wote Mwalimu aliwaita ikulu,

akamwambia kiongozi wa mapinduzi yale (simkumbuki) kuwa

"Shika bunduki uniue wewe mwenyewe kwamkono wako ili uwe rais wa nchi hii"

jamaa aliomba radhi huku akitambaa kisha mwalimu akasema

"nimewasamehe wote"

na aliwapa vyeo na kazi, wengi walikwenda kuwa mabalozi wa Tz nchi za nje!

Sisi hapa tunasema kama porojo tu, lakini yapo mengi sana nyuma ya pazia!

Watawala wanahisi kuyataja ni kama kuharibu sifa ya Tanzania na wengine wanaona kama itaharibu sifa ya Mwalimu.

Mimi binafsi nafikiri kama yatasemwa hadharani yataongeza sifa ya Mwalimu Nyerere na utawala wa ccm ya kale!

Atakuwa ni kiongozi pekee barani afrika na duniani aliyenusurika majaribio matatu ya uasi,

Atakuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kuwasamehe waasi kwa mda huohuo wa uasi (baada ya kuwakamata) na kuwapa kazi nyingine za kitaifa

Atakuwa ni kiongozi pekee duniani aliye ng'atuka kwa amani na kwenda kuishi kijiji tena bila hata ulinzi, akitembelea land rover ya shamba miaka mitano tu baada ya jaribio kali la mapinduzi ya Banana Ukonga!

Hizo zote zilikuwa ni sifa zake ambazo watawala wa leo kwa makusudi ama kwakujua au kutojua wamefifisha nyota ya mwana wa Afrika mbele ya uso wa mataifa!

Na kwakuwafahamisha tu ni kuwa mmoja ya wanajeshi hao walioasi ni Meja Gen Hans Popi yule mwenye Sams Super Store pale Mbezi Makonde!

Kwakifupi hayo ndiyo ninayafahamu,
@Yericko Nyerere zamani ulikuwa na IQ kubwa well done kijana, lazima unajua mengi vile wewe unasoma vitabu.

Ongeza nyama hasa tunapomlilia mwana harakati huyu Hanspope.

I hope Hans alisababisha Pili Misana kupigwa chini na wajumbe alipojitosa Viti maalum, mwendazake alinusa mapinduzi through her.

Anyways Nampenda Mwalimu Nyerere, Endelea kupumzika Mtakatifu.
 
Sababu kubwa ya Nigeria kuja kulinda amani ni kwamba Nyerere aliamua kuvunja jeshi la KAR na kujenga JWT. Ilikuwa ni aibu kwake kwa Uingereza kuzima yale maasi. Waingereza walitaka kubaki waongoze jeshi letu Nyerere akakataa akawaita Wanigeria waje kusaidia kujenga na kutoa mafunzo kwa jeshi jipya la wananchi wa Tanzania.
Hilo jaribio bila Uingereza hadithi ingekuwa tofauti
 
@Yericko Nyerere zamani ulikuwa na IQ kubwa well done kijana, lazima unajua mengi vile wewe unasoma vitabu.

Ongeza nyama hasa tunapomlilia mwana harakati huyu Hanspope.

I hope Hans alisababisha Pili Misana kupigwa chini na wajumbe alipojitosa Viti maalum, mwendazake alinusa mapinduzi through her.

Anyways Nampenda Mwalimu Nyerere, Endelea kupumzika Mtakatifu.

Wakubwa waliowatuma hao vijana pengine ndio Mwalimu aliwasamehe. Nyerere was a character. Yule Mzee alikuwa beyond some of todays imaginations.

Ndio maana aliwapa za uso hawa machief ambao wengine tunafikiri wana uwezo wa kusafisha nyota zetu🤣🤣🤣😍😍
 
Back
Top Bottom