Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Jaribio la kwanza ni kuwaengua wapinzani kwa visingizio vya mapingamizi yasiyokuwa mbele wala mkia ili kujihakikishia Idadi ya wabunge wanaosubiri kuapishwa baada ya Uchaguzi hapo October. Hiii hujuma wapinzani wanapimwa wanaweza kufanya nini ikiwa watafanyiwa hivyo.
Jaribio la pili ni kuwapora ushindi wao kupitia sanduku la kura ambapo hawatatangazwa hata kama mtu ameshinda. Hili litakuwa na mafanikio makubwa kama jaribio kwa kwanza litafanikiwa. Kama jaribio la kwanza litakwama kwa misimamo imara ya wapinzani, basi hata kwenye sanduku la kura watu wataheshimiana na watakaoshinda kwa haki watatangazwa. Kwahiyo wapinzani wakishindwa kupangua jaribio la swali basi mambo yanaweza yakawa magumu zaidi mbeleni.
Haya yote ni baada ya kuona ile mipango yao ya wasimamizi kutokuwepo kwenye ofisi zao limeshindikana kufuatia NEC kutoa karipio kwa wasimamizi kuwepo ofisini muda wote na kinyume na hapo watafukuzwa kazi.