Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Leo ahsubuhi, mnamo saa mbili Polisi wakiwa katika mavazi ya kiraia walifika nyumbani kwa Dkt, Slaa kwa nia ya kumchukua.
Dkt Slaa ambaye wakati huo alikuwa anasikiliza maoni ya Watanzania kupitia Club House akatoa taarifa mapema kwa baadhi ya Wanadiaspora, ambapo kelele zikaanza kupigwa mitandaoni dhidi ya jatibio hilo
Muda mfupi uliopita nimemsikia Dkt Slaa akitoa maelezo kuhusu jaribio hilo lililofeli. Anasema walikuja polisi wakiongozana na OCD wote wakiwa in civilian clothes, hali waliyomkuta nayo na kwa kufahamu ameshawataarifu Watanzania wenzake, ilibidi wamuombe waondoke naye kwa agizo la RCO.
Aliongea naye kwenye simu na kumueleza hakatai wito lakini asubiri ruhusa ya daktari wake. Dkt Slaa anaendelea na matibabu baada ya vipimo na upasuaji mdogo.
Askari wameshaondoka lakini upo uwezekano kuwa wanaendelea kumuwinda ili kumchukua kimya kimya
Rais na watu wake wamepanick, sasa kila mmoja anayesimama mbele yao wanamhalalishia brutal code.