Jaribio sahili unaloweza kulifanya na watoto kutengeneza upinde wa Mvua

Jaribio sahili unaloweza kulifanya na watoto kutengeneza upinde wa Mvua

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Habari wana JF,

Leo ninawaleteeni sayansi ya upinde wa mvua. Hivi unafahamu ni kwa vipi upinde wa mvua hutokea? Na ni kwa nini watu wakiona upinde wa mvua husema bila wasiwasi kwamba "mvua haitanyesha, si unaona li upinde la mvua lilee"

Naandika mada hii baada ya kusikia kisa cha bodaboda wa mahala fulani (ila hizi akili za baadhi ya hawa maafisa usafirishaji aseee!!😄) waliamua kujaza mafuta pikipiki na kuwasha kuufuata hadi wafike penye upinde wa mvua. Sijui waliupata ama nini. Anyway tuachane na akili za boda. Turudi kwenye sayansi.

Nadharia nyuma yake: Upinde wa mvua hufanyizwa na mwanga wa jua unaodunda na kupindishwa katika nyuso za ndani za matone meengi ya maji ya duara. Kiufupi natone ya maji hujifanya kama prisimu ndogondogo. Kwa hivyo mtu akitimiza mahitaji hayo atauona upinde wa mvua hapo hapo alipo. Eaaasy.
Screenshot_20240422-112311_Chrome.jpg


Jaribio sahili: UPINDE WA MVUA

Kusudi: Kutengeneza upinde wa mvua wa bandia nyumbani.

Vifaa: Pampu ya kuspray au mdomo tu unatosha.

Screenshot_20240422-091833_Gallery.jpg

Maji safi na mwangaza wa jua.

Screenshot_20240422-092539_Gallery.jpg

Njia
-Chagua mahala penye jua na uwazi wa kutosha
-Kisha jaza maji safi mdomoni au katika chupa ya kuspray uliyonayo
-Geuza kisogo kilielekee jua mojakwamoja, macho yako yatazame upande kivuli chako kilipo usawa huohuo wa macho.
-Baada ya hapo puliza matone kufanyiza matone meengi katika kieneo cha mbele ya uso wako.
-Tazama, upinde wa mvua utajitokeza katikati ya matone 🤯

Unaweza kufurahia jaribio hili na wanao nyumbani au mwalimu akafanya na wanafunzi wake kuwajengea udadisi na kupunguza maelezo yoyote ya kishirikina waliyokuwanayo kabla labda.

Matokeo: Upinde wa mvua umejitokeza kwa muda kiasi na kutoweka pale matone yanapokata
Screenshot_20240422-091850_Gallery.jpg


Hitimisho: Upinde wa mvua waweza kuonwa mwanzo na mwisho wake hapohapo ulipo nyumbani. Haya ni matokeo ya kawaida kabisa ya matone ya mvua kutawanya mwangaza wa jua ulioundwa kwa mianga na miale yenye kasi tofautitofauti, na hivyo kupindishwa kwa kiwango tofauti tofauti.

Ahsanteni.
 
Unapulza matone ukiwa usaw (uso kwa uso ) ukiwa unatazam jua?
Hapana.

Ni kisogo ndio kielekee jua.... macho yatazame mbele yaani ule upande ambao kivuli chako kinaelekea
 
Nadhani utakuwa mwalimu wewe au kijana wa sayansi dadisi.

Hata hivyo hongera safi sana.
 
Nakubali 💯
IMG_5575.jpeg

Nadharia nyuma yake: Upinde wa mvua hufanyizwa na mwanga wa jua unaodunda na kupindishwa katika nyuso za ndani za matone meengi ya maji ya duara. Kiufupi natone ya maji hujifanya kama prisimu ndogondogo. Kwa hivyo mtu akitimiza mahitaji hayo atauona upinde wa mvua hapo hapo alipo. Eaaasy.
 
Back
Top Bottom