Mcqueenen
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 6,843
- 11,702
Anaweza kuwa amechoka, amesusa, amenuna, amekasirika, amekwazika, ana kinyongo, anaumwa, ana msongo wa mawazo. Si unajua mabinti na vijana wa siku hizi wana mambo mengi? Si unajua siku hizi maisha yanaenda kasi? Kwahyo yeye akikasirika, akinuna, akisusa, wewe jaribu upole.
Najua unamuona yupo anasubiria tu, tena anasubiria kwa hamu vitu ambavyo huenda hatokuja kuvipata. Lakini akiwa bado anavisubiria na kuvihangaikia, wewe jaribu kumuonesha upole.
Wala hizo siyo hisia zake tu, unatakiwa utambue kuwa ni kweli na yeye ana vitu vinampa majonzi, kuna vitu anavijali. Ambavyo wakati mwingine hivyo vitu vinamuumiza au kumuangusha. Lakini yale maneno matamu, ukiyasema kwa upole inarahisisha, inamrahisishia kuubeba ugumu wa maisha.
Chukua huu ushauri, hautajutia, tena hawa mabinti na vijana huwa hawasahau kwasababu mapenzi ndiyo chanzo chao kikuu/pekee cha furaha.
Halafu ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya tu ni kujaribu kuwa mpole. Muoneshe unampenda, mwambie hakuna mwingine, mkumbatie, usimkaripie, mfurahishe, usimkwaze mbusu, usimnunie, mlegeze, usimuumize, mpe zawadi, usimpuuzie, jaribu upole.
Najua kuna muda na wewe unakuwa busy, kuna muda anakuudhi, kuna muda unamuigizia, kuna muda unavunga eti wewe ni badguy siyo nice guy.
Lakini ninachosema usisahau pia kuna muda unatakiwa kuwa halisi, kuna muda unatakiwa kuonyesha hisia zako, kuna muda unatakiwa kujishusha, kuna muda unatakiwa kumbembeleza, kuna muda unatakiwa ujaribu kuwa mpole.