Jasusi damu zamwagika

Jasusi damu zamwagika

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Robert akiwa kwenye gari lake alianza kulia, akashindwa hata kuendesha akaamua kusimama kando ya Barabara akiwa anabubujikwa na machozi.

Machozi yakawa yanamtiririka Robert huku akizidi kulia kwa uchungu mkubwa, jua lilikua likiwaka huku Watu wakiendelea na shughuli zao lakini kwa Robert ilikua tofauti sana, alijikuta yupo kwenye kisa chenye utata sana.

Alikua amevalia Suti nyeusi, kiatu cheusi lakini sura yake hofu na hali ya majuto ilikua imetanda sana. Akajikuta akipiga usukani kutokana na hali aliyokuwa nayo, akageuka nyuma ya gari.

Kulikuwa na Mwili wa Mtu uliokuwa ukivuja damu, mwili huo hapana shaka ulikuwa ni wa kike kwani ulikuwa na vazi la Shela.

Robert akaliondoa gari pale kando ya ile barabara, sasa akawa barabarani kuelekea alipokusudia huku ile hali ya kulia ikiwa imekata. Simu yake ilikua ikiita mno lakini hakutaka kuipokea, Alipofika mbele akaachana na barabara kuu akaingia barabara ya vumbi ambayo ilikua ikielekea ufukweni.

Robert alipofika juu ya kilima akaongeza mwendo akalitumbukiza gari hilo ndani ya bahari na kuzua taharuki kwa Watu waliokuwa upande mwingine wa ufukwe, kelele na taharuki vikaamka pale Ufukweni, Watu wa uokozi wakawa tayari kwa ajili ya kuzama majini kulitoa gari hilo.

Kwa muda mfupi lile gari lilikuwa limezama ndani ya yale maji ya Bahari ambapo kwa upande ule kulikuwa na kina kirefu ambacho Watu walikuwa hawaendi kuogelea, Punde polisi wakaja pale huku Watu wakiendelea kupigiana simu kuwa kuna gari limezama ndani ya Bahari, kilikuwa ni kituko kwa kila aliyesikia, kila Mtu akataka kujua ilikuwaje.

Polisi wakazungusha utepe wao kuashiria kuwa eneo hilo halikuwa salama kwa wakati huo, ziliwachukua zaidi ya dakika 45 waogeleaji kuchopoa miili miwili. Moja ilikuwa ni ile ya kike na nyingine ilikua ni ya Robert, gari ya huduma ya kwanza ikaichukua miili ambapo yote ilikuwa tayari haina uhai.

Taarifa hii ikawa na mkanganyiko mkubwa kwa Watu walioisikia, haikuhitaji uchunguzi mkubwa sana kugundua kuwa walikuwa ni Wanandoa au watarajiwa, mwili wa Mwanamke ulikutwa na risasi shingoni.

“Ufanyike uchunguzi haraka sana kuhusu hili tukio” Akaagiza mkuu wa Upelelezi.

  • ••••••••
Vilio vilikuwa vimetanda ndani ya kanisa moja lililopo katikati ya Jiji, tayari polisi walikuwa wamefika na kuukuta mwili mwingine uliokuwa umejeruhiwa kwa risasi, ulikuwa ni mwili wa Mwanaume mmoja ambaye alitambulika kama Bosco, naye alikuwa amevalia suti.

Polisi wenyewe walipigwa na butwaa kwa jinsi hali ya vilio ilivyokua imetanda ndani ya kanisa hilo kubwa na lenye hadhi, Watu wengi walikuwa wakisimuliana kilichotokea hapo.

Mama mmoja alikua akilia kwa uchungu huku akiutikisa mwili wa Bosco uliokuwa umeloa damu, shati jeupe alilovaa lilikua limetapakaa damu mno.

“Mwanangu mimi! Eeeh Mungu mtihani gani huu umenipa mimi leo tena mbele ya Kanisa” Sauti ya kilio iliyotoka kwa kwikwi ilimtoka Mama huyo, mmoja wa Askari akapata shahuku ya kumfuata huyo Mama.

“Pole Mama!” Akasema huku akiwaambia watu wa Huduma ya kwanza wauchukue ule mwili kwa ajili ya taratibu za kiupelelezi zaidi.

Lilikua ni pigo lililoamsha kilio chake, Mwili wa Bosco ulikuwa ukiwekwa kwenye gari maalum kwa ajili ya kuupeleka Hospitali, mkononi Askari huyo aliyejitambulisha kama Inspekta Zola alikua ameshikilia karatasi yenye majina ya Watu waliopoteza Maisha kwenye kisa kile cha kutisha. Jina la Robert lilikua la kwanza, la pili ni Sandra na la tatu ni Bosco. Akajiuliza Watu wale walikua kwenye kisa gani kilichopelekea vifo vyao.

Akamfwata Mtu mmoja aliyekua amekaa kando, alikua amejitenga sana na wengine. Kupitia jicho la Kipelelezi Inspekta Zola akagundua jambo, alipomfikia akamuuliza

“Nini kimetokea?” Ilikua ni kama vile ameamshwa kutoka kifo, akajikuta akishtuka sana. Naam! alikuwa ni Mdada mwenye sura ya upole, mweupe mwembamba, kwa jinsi alivyovaa ilikua rahisi kutambua kuwa hakua miongoni mwa Watu waliofika kwa ajili ya ile shughuli pale Kanisani.

“Unaitwa nani?”

“Judith!!”

“Huonekani kama mmoja wa Waalikwa hapa, kimekuleta nini?” Swali hili likaambatana na jicho kavu la kipelelezi

“Mimi?”

“Ndio wewe kwani naongea na nani?” Mdada akakaa kimya bila kujibu chochote huku akionesha kutetemeka, Yule Askari akamchukua Mdada kwa ajili ya mahojiano zaidi pamoja na baadhi ya Watu ambao walitambulika kama ndugu wa Bosco ambaye amefariki kwa kupigwa risasi.

Ilikua ni siku ya majonzi sana, vilio vilitanda hadi kituo cha polisi ambapo baada ya polisi kuwataka watulie ndipo vilio vilipokoma.

“Nini kimesababisha vifo vyao?” Aliuliza Inspekta Zola ambaye alikua makini, mbele yake kulikua na Ndugu zake Bosco na wengine ambao walijitambulisha kama ndugu wa Sandra, yule Mdada alikua amekaa pembeni akiwa katika hali ya hofu.

“Inatisha na kusikitisha Afande, marafiki walioshibana leo wanauwana” akaongea Mama yule ambaye alifahamika kama Ndiye Mama yake na Bosco, kilio kilianza tena ikabidi sasa Inspekta Zola amuondoe Huyo Mama kwasababu asingeliweza kuzungumza chochote zaidi ya kilio.

“Nini kimetokea?” akauliza tena Inspekta Zola akiwatazama walioko mbele yake, mmoja akatikisa kichwa ishara ya kuwa hajui hasa kilichosababisha vifo vya Watu watatu, Inspekta Zola akapata wazo la kumuuliza yule Mdada, akamuita

“Nini kimetokea?” Akamuuliza yule Mdada ambaye hata baada ya kuulizwa alikaa kimya kwa kitambo kidogo kabla ya kuanza kuzungumza.

Chozi likianza kumbubujika akajikuta akianza kuongea.

“Mapenzi! Najiuliza kwanini yameumbwa, kwanini yanatesa, yanafanya Watu wawe maadui, watu wapoteze furaha walizonazo! Ni mapenzi” Kila mmoja alikaa kimya baada ya huyo Mdada kuanza kuzungumza, Familia zote zilizopo pale polisi zilikaa kimya kumsikiliza Mtu ambaye hawakumfahamu.

“Huyu ni Muongo” Akadakia Dada Mmoja aliyekuwa akibubujikwa machozi

“Hebu subiri aongee alafu sisi tutapima maneno yake kama yamejaa ukweli au uwongo” akaongea Inspekta Zola

“Nawaomba polisi mufanye kazi yenu lakini sio kusikiliza maneno ya Mtu huyu, Mdogo wangu Sandra hakuwahi kuingia kwenye vita ya Mapenzi, anaongea Uwongo Mtupu…”

“Mpaka hapa tunapozungumza hakuna aliye hai ambaye anayeweza akatueleza kilichotokea, ni vema tukamsikiliza huyu Binti”

“Una maanisha nini? Mdogo wangu Robert amekufa?” akauliza kwa Mshituko kuhusu Robert ambaye mwili wake uliopolewa Baharini baada ya kulitosa gari lake ndani ya Bahari.

“Sandra na Robert wamekutwa wakiwa tayari wamekufa ndani ya maji, ndio maana nasema tukae kimya kumsikiliza ili kama kuna ukweli unazungumzwa basi ndio utatupa uelekeo wa kujua chanzo cha vifo hivi vya Kutisha” Akajibu Inspekta Zola, taarifa ikaamsha tena vilio

“Nilijua Robert atakuwa salama jamani”

“Nini kimetokea Robert Mwanangu…Nini Babaaa??”

“Bosco mlikuwa mnaficha nini kwenye maisha yenu wanangu?” Zilikuwa ni sauti zilizojaa vilio hadi Inspekta Zola akaamuru sasa watolewe nje ili afanye mahojiano na huyo Mdada ambaye alionesha kufahamu baadhi ya mambo!

“Judith sitaki uingie matatizoni, unaonekana sio mtu mbaya…sura yako inaonesha hujahusika kwenye jambo hili lakini unafahamu kitu..lisaidie jeshi la polisi, nini kimesababisha vifo hivi vya kutisha na ilikuwaje pale kanisani?” Chozi likaanza kumbubujika Judith akiwa anamtazama Inspekta Zola ambaye alikua makini kusikiliza atakacho kisema.

“Judith…unafahamu nini kuhusu Maisha ya Bosco, Sandra na Robert?” akauliza tena Inspekta Zola lakini bado Judith aliendelea kulia.

“Mapenzi yamefanyaje Judith? wewe ni sawa na binti yangu na huwa naumia sana kumuona Binti kama wewe ukiingia kwenye matatizo”

Judith akajifuta mchozi uliokua ukitiririka kwenye mashavu yake akavuta hewa kama Mtu mwenye mafua kisha akamkodolea macho Inspekta Zola

“Tupo mimi na wewe tu, tuongee kama Mtu na Baba yake Judith…Nini kimetokea?” Kauli hii ikamfanya Judith avute hewa, akajisikia uhuru fulani wa kuzungumza. Macho ya Inspekta Zola yaliyokomaa Kijasusi yakawa yana Mmulika Judith ndani ya Chumba kimoja cha mahojiano.

“Unawafahamu vipi hawa Watu?” aliuliza tena Inspekta zola tena bila kuchoka

Judith akanyanyua kinywa chake ili aanze kueleza kilichotokea, mara mlango ukafunguliwa akaingia Polisi mmoja aliyevalia sare za kipolisi, akapiga saluti kwa Inspekta Zola.

“Ripoti ya uchunguzi wa miili ya Marehemu wote Watatu” Akaongea polisi aliyeingia, akamkabidhi baasha Inspekta Zola, akaifungua ili asome ripoti hiyo.

Akazisoma ripoti zote lakini ripoti ya mwili wa Sandra ilimshangaza kidogo licha ya kukutwa kwa risasi sehemu ya shingo pia Mwili ulikutwa na tatuu ya jina la Bosco upande wa kulia wa paja lake lakini pia upande wa kushoto wa paja lake lilikutwa jina la Robert. Inspekta Zola akamtazama yule polisi kisha akarudisha macho yake kwa Judith, akawa na maswali mengi yaliyohitaji majibu ya haraka.

“Sandra alikua na mahusiano na Bosco na Robert kwa wakati mmoja?”

“Ndio”

“Je, Robert na Bosco walikua wakijuana kwenye penzi la Sandra?”

“Hapana”

“Walikua marafiki walioshibana sasa waliwezaje kuishi kwenye penzi la Mtu mmoja?” Akauliza Inspekta Zola, kisha akatazama saa yake tayari usiku ulikua umeingia.

“Afande utahakikisha anakua salama huyu binti hadi kesho asubuhi” akasema Inspekta Zola kisha akaondoka zake pale kituo cha polisi, Judith akachukuliwa kwa maelekezo maalum ya Inspekta Zola akapelekwa sehemu ili apumzike ndani ya kituo kile cha polisi.

  • ••••••••
Nyumbani kwenye familia ya Robert bado vilio vilikua vimetawala kila mmoja akijiuliza Robert alikua amepatwa na nini hadi akawapiga risasi Sandra na Bosco, wote walishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa. Ndugu walikua wakifika kwa ajili ya mazishi ya Robert, pia upande wa Bosco hali ilikua hivyo hivyo, pia kwa Sandra hali ikawa hivyo hivyo.

Hakuna aliyejua hasa sababu ya Marafiki hawa walioshibana kuangukia kwenye kivuli cha Umauti.

Baada ya kutoka kituo cha Polisi Inspekta Zola akaelekea nyumbani kwake, siku hii hakuwa katika hali ya kawaida bali kwenye tafakari nzito kuhusu kisa kile kizito ambacho kilikua mikononi mwake. Taarifa iliyopo kwenye meza yake ilikua ni Robert kumpiga risasi Bosco, kisha kumpiga risasi Sandra na kwenda kujitosa ndani ya Bahari.

Akiwa kwenye chumba chake maalum kwa ajili ya upelelezi akaanza kuvuta picha tofauti tofauti ambazo alikua akizifikiria lakini hakufanikiwa kupata picha halisi ya tukio lile, umri wake wa miaka 60 ulitosha kumwambia kuwa kisa kile kilikuwa na simulizi ya kusisimua ndani yake.

Akachukua karamu na karatasi akaandika ” ROMEO NA JULIET” kisha akafuta kwa kuamini kuwa visa hivyo ni tofauti, akamaliza kwenda kitandani na kujitupa, akajigalagaza hadi Usingizi ulipomchukua.

Asubuhi jua likiwa tayari limetoka akaamshwa na mlio wa simu yake ya mkononi iliyokua pembezoni mwa Kitanda chake. Akaamka na kuipokea, akajua kuwa siku ilikua imeanza. Akajiandaa na kuelekea kituo cha polisi, akaelekea moja kwa moja chumba cha mahojiano akamkuta Judith akiwa anamsubiria.

Kabla hajaanza na Judith, akaikuta baasha pale mezani, hapana shaka ilikua ikimsubira yeye. Alipofungua akakutana na ujumbe mwingine uliomkata maini yake, Naam! haraka akachomoka pale na kumuacha Judith akiwa kwenye uangalizi, akachukua gari yake ndogo na kuelekea Hospitali ambako maiti zilikua zimehifadhiwa.

Akaiomba maiti ya Sandra, ikaletwa kwenye chumba maalum kisha paja la Sandra likafunuliwa, akaiona Tatuu yenye jina la Bosco kisha akaifungua ile taarifa iliyopo kwenye baasha akagundua ufanano wa jambo fulani, pale pale simu yake ikaita. Akaweka miwani yake vizuri kisha akaipokea hiyo simu

“Zola! nafikiri umeupata Ujumbe wangu, Haraka sana anza na upelelezi wa kina…Hawa marehemu watatu huenda wakawa wanahusika na kifo cha Makam wa Rais” Ulikuwa ni ujumbe tata sana kwenye kichwa cha Inspekta Zola, jasho likawa linamtoka.

“Inawezekanaje? Wauwaji wakauwana wenyewe kwa wenyewe?” Akauliza Zola

“Zola, fanya upelelezi wako upesi. Idara yangu ya Usalama wa Taifa inakuamini sana ndio maana sijaona Mtu wa Kumpa hiyo kazi zaidi yako”.

“Oooops! sawa Mkuu” Akajibu kwa utiifu wa hali ya juu sana, Hofu ikatanda na hali ya tahadhari ikapanda kwenye kichwa cha Inspekta Zola, akajua sasa alikua kwenye kazi rahisi iliyogeuka kuwa ngumu kupita maelezo.

Kwenye Tatuu ya Jina ka Bosco kulikua na alama ya vidole viwili, alama hii ilikua maarufu sana miezi michache iliyopita baada ya kutokea kwa vifo vingi vya Watu wa Usalama, na viongozi wa juu wa Serikali, kila aliyeuawa alikutwa na muuli wa alama ile ya Vidole, hapo ndipo wasiwasi ulipoibuka baada ya kukutwa kwa Tatuu kwenye mwili wa Sandra.

Mara moja simu ya Inspekta Zola ikaanza kuita, ilikua ni simu kutoka kituo cha Polisi.

“Unasemaje?” akauliza Inspekta Zola akiwa amesimama kando ya maiti ya Sandra

“Nakuja haraka sana” akasema Zola kisha akachukua gari kurejea kituo cha Polisi, akasikia Milio ya gari za kubebea wagonjwa kutoka kituo cha polisi, maiti zilikua zimezagaa eneo la kituo cha polisi.

Zola hakuamini macho yake, Polisi mmoja akamfwata Zola na kumwambia kuwa yule Binti aliyekuwa akihojiwa ndani ya kituo hicho ndiye aliyekuwa amesababisha madhara yale

“Inawezekanaje binti dhahifu kama yule awashinde zaidi ya Askari 15 na kuwauwa wote?” Akauliza Zola huku akiwa anatazama jinsi maiti zilivyokuwa zikichukuliwa na kuwekwa kwenye Magari ya kubebea wagonjwa.

“Inspekta, Binti anaonekana kuwa na mafunzo ya kimapigano na ujasusi wa hali ya juu sana” Baada ya kusikia hivi Inspekta Zola akaelekea ndani ya kituo, damu zilikua zimetapakaa huku matundu ya risasi yakiwa kwenye miili ya askari waliokuwa tayari wameuawa.

“Amechukua baadhi ya nyaraka kwenye masanduku” akaongeza askari ambaye alikuwa akimfwata Inspekta Zola kwa nyuma, akaingia moja kwa moja hadi kwenye kile chumba cha mahojiano ambacho alimuacha yule Mdada aliyejitambulisha kama Judith, akaona kuna ujumbe juu ya meza, akaufungua ukiwa kwenye baasha akakutana na ujumbe ulioandikwa “KIVULI CHA UMAUTI” alafu alama ile ya vidole ikawa chini ya maneno hayo.

“Uuupsss” Akashusha pumzi kisha akaketi kwenye kiti na kuegemea ile meza

“Ngoma hii ni ngumu sana kuicheza” akajisemea kwa sauti kuu huku akitikisa kichwa chake.

  • •••••••••••••••
Ndani ya Jengo moja refu zaidi katika Jiji hili, kulikuwa na jamaa mmoja aliyeitwa Six, alikua ameketi huku akivuta sigara yake, mwili wa Six ulikua na tatuu nyingi sana za rangi, simu yake ilikua bize sana akionekana kupokea na kutoa taarifa.

Mara akaingia Judith Mdada ambaye alikua kwenye kile kituo cha polisi, alionekana kuwa mwenye msongo wa mawazo. Akafikia kuketi kwenye sofa karibu na Six, Six akatikisa rasta zake

“Mbona uko juu juu sana?” Akauliza huku akizima sigara yake, akatoa moshi mwingi mdomoni

“It’s a bit Strange ( Inatisha kidogo )”

“Kumetokea nini?”

“Walinishtukia ikabidi nipambane kujiokoa pale”

“Oooh! Shit” Six akaongea kwa hasira sana, Mdada aliyejitambulisha kwa polisi kama Judith akavua sura ya bandia.

“Hawajafanikiwa kukufahamu?”

“Yes! hawajanifahamu”

“Ok! Malaika usiye na dhambi” akaongea huku akiwa anapokea nyaraka zilizoibwa ndani ya kituo cha polisi.

Nje kidogo ya Jiji hili, Inspekta Zola alikua akipokea kazi kamili ya kuwasaka waliokuwa wakifanya mauwaji ikiwemo kifo cha Makam wa Rais ambaye alipigwa risasi akiwa nyumbani kwake na kuzua taharuki kubwa.

Mbele yake alikua amesimama Mtu mmoja mwenye umri sawa na wake, wote walikua Wazee wenye utaalam wa upelelezi, Mzee huyu alijulikana kama Dawson maarufu kama Google. Jina hili la utani alipewa sababu ya taarifa nyingi alizonazo ndani ya kichwa chake, licha ya Mzee Dawson kuwa Mtu wa Usalama wa Taifa pia alikua ana kitengo chake cha Siri alichokipa jina la MPA ambacho kilikua kikidili na masuala ya Upelelezi wa kesi kubwa kubwa ndani na nje ya Nchi.

Walifanana sana tabia zao, walikua walevi wa sigara na nyakati fulani walikua wakitumia pombe kali, ilikua ni kawaida kwao tangu wakiwa vijana kwani kazi waliyokua wakiifanya iliwafanya watumie akili nyingi ili kupambana na uharifu,

“Kuna kundi linaitwa MAFIA GANG, ni kundi maalum kwa ajili ya Ugaidi…Mkuu wa kundi hili anaitwa John Brain ni mzungu anayeishi Uskochi, Kazi yake ni kuratibu mauwaji. Amefanya kazi katika Nchi nyingi na sasa yupo hapa Nchini ndiye anayeratibu mauwaji ya viongozi kwa maslahi yake binafsi. Mwaka 2003 nchini Congo walifanya mauwaji mengi sana, nakuamini Zola ndio maana nataka ufanye upelelezi wa kina, ukomeshe kabisa kundi hili hapa Nchini” Yalikua ni maneno ya Mzee Dawson yalitoka na moshi wa sigara.

“Kila kitu kipo tayari kwa ajili yako Zola, unahitaji kuikomboa Nchi yako. Nakufahamu vizuri linapokuja suala la kesi tata” Akamaliza kwa kumtakia kila la Kheri kwenye jukumu lake zito la kuliondoa kundi la MAFIA GANG lakini kichwani bado alikua anauwaza ule mkasa wa akina Robert, akajiuliza waliingiaje huko na nini kilipelekea wauwane.
 
Ilipoishia “Kuna kundi linaitwa MAFIA GANG, ni kundi maalum kwa ajili ya Ugaidi…Mkuu wa kundi hili anaitwa John Brain ni mzungu anayeishi Uskochi, Kazi yake ni kuratibu mauwaji. Amefanya kazi katika Nchi nyingi na sasa yupo hapa Nchini ndiye anayeratibu mauwaji ya viongozi kwa maslahi yake binafsi. Mwaka 2003 nchini Congo walifanya mauwaji mengi sana, nakuamini Zola ndio maana nataka ufanye upelelezi wa kina, ukomeshe kabisa kundi hili hapa Nchini” Yalikua ni maneno ya Mzee Dawson yalitoka na moshi wa sigara.

“Kila kitu kipo tayari kwa ajili yako Zola, unahitaji kuikomboa Nchi yako. Nakufahamu vizuri linapokuja suala la kesi tata” Akamaliza kwa kumtakia kila la Kheri kwenye jukumu lake zito la kuliondoa kundi la MAFIA GANG lakini kichwani bado alikua anauwaza ule mkasa wa akina Robert, akajiuliza waliingiaje huko na nini kilipelekea? Endelea

SEHEMU YA PILI

“Oooh! Jesus!” Akasema Zola huku akilikodolea macho gari la kifahari la Mzee Dawson ambalo lilikua likitokomea, mkononi alikuwa ameshikilia bahasha nyeusi ambayo ilikua maalum kwa ajili ya kazi za siri, alijua ni vitu gani vitakuwepo kwenye Bahasha hiyo.

Safari ya Inspekta Zola ilimchukua masaa takribani matatu kufikia yalipo makazi yake ya siri ambayo alikua akiyatumia kwenye upelelezi kila alipopata kazi ngumu mbele yake alijificha kwenye makazi hayo ambayo aliyapa jina la HOME TOWN.

Lilikua ni jumba lililopo karibu na fukwe ya Bahari ya Hindi, alichagua eneo hili sababu lilikua tulivu sana, licha ya kuwa ni eneo ghali sana lakini alimudu gharama ambazo alikuwa akilipiwa na kitengo cha Siri cha Mzee Dawson ( MPA )

Akabandua karatasi zilizopo kwenye ubao maalum, kisha akabandika karatasi nyeupe akachora kwa kalamu na maandishi yakapata kusomeka kama MAFIA GANG akimaanisha ndio kwanza alikua akiingia kazini kwa ajili ya kupambana na kikosi hicho hatari cha Bwana John Brain.

Ilikua tayari usiku umeshaingia, akapiga simu kwa Waangalizi wa zile maiti Hospitali kuwa hazipaswi kutolewa hadi pale upelelezi utakapo kamilika, Hivyo familia zisubirie kwanza kabla ya maiti za akina Robert kupatikana kwa ajili ya mazishi, alikua na lengo lake ndani ya kichwa chake kilichojaa nywele za mvi, akakuna kidevu chake baada kuwa tayari ametoa maelekezo muhimu sana.

Inspekta Zola licha ya kuwa umri ulikua umeenda kidogo lakini alikua akipenda sana visichana vidogo vidogo, akaondoka kwenye makazi yale akaelekea Baa kwa ajili ya kupata mvinyo na kuangalia Mwanamke wa Kustarehe naye usiku huo.

Akaagiza White Wine huku akikodolea macho baadhi ya visichana vilivyokua ndani ya Baa hiyo, alipomaliza kunywa akawa ameshapata Msichana wa kustarehe naye usiku huo ambapo akaelekea Kwenye Hoteli moja iliyopo mita kadhaa kutoka kwenye makazi yake ya siri. Akastarehe naye kisha akamuondoa usiku huo huo, akabadili hoteli ambako alilala hadi asubuhi.

Aliamka na uchovu kiasi, akapata Kahawa kisha akaondoka hotelini hapo akaelekea Hospitali, akaagiza iletwe maiti ya Sandra. Akaanza sasa kuikagua rasmi kwa kutumia jicho lake kali la kijasusi, akiwa amevalia miwani yake ya macho akagundua jambo, akaagiza mkasi na kisu, akavalia gloves kwanza.

Akawaambia Watu wa Maabara waongeze mwanga wa taa, wakafanya hivyo. Akaona alama kwenye sura ya Sandra ambayo ilionesha kuwa sura ile haikuwa halisi. Akafwatisha ile alama kwa kisu ndipo akaona sura ikijivua. Wote waliokuwa ndani ya chumba cha Maabara wakaingiwa na ganzi, lilikua ni jambo lililo hitaji umakini wa hali ya juu zaidi.

Sura ilipovuka wakaikuta sura nyingine kabisa, pale pale akavua gloves akachukua simu na kupiga picha kisha akapiga simu kwenye kitengo cha siri cha Mzee Dawson ( MPA )

“Nahitaji wataalam wa Maabara haraka sana kwenye Hospitali ya ST. James karibu na chuo cha Biashara” Ilikua ni sauti yake iliyojaa umakini zaidi, haraka wale wataalam wakawa wamewasili hospitalini hapo

“Chunguzeni maiti mbili za Robert na Bosco, vueni sura zao za Bandia kisha mpige picha mnitumie” Akawaachia maagizo, Inspekta Zola akaondoka pale Hospitalini akiwa na jambo jipya ndani ya akili yake, sasa ndio akawa na mashaka juu ya wapi walipo Akina Robert wa ukweli na kwanini wale wajitoe muhanga kupoteza maisha yao?

“Kuna jambo limejificha sio bure” Akasema Inspekta Zola akiwa kwenye gari yake, alikua akielekea ofisini kwa Mzee Dawson ambaye ni mtaalam wa Taarifa kutoka usalama wa Taifa.

“Naam! Zola , kuna jipya umeligundua?” akauliza Mzee Dawson baada ya kukutana ana kwa ana na Inspekta Zola

“Dawson!! hili jambo lina mchakato wa hatari unaohitaji utulivu zaidi”

“Hilo ndilo nililotegemea kulisikia kutoka kwako Zola, hii sio kazi ya kitoto ndio maana nimeileta kwenye meza yako, umekutana na kazi nyingi za hatari na zote umefanikiwa, hili haliwezi kuwa jepesi pia”

“Maiti zile zina sura za Bandia, inaonesha kuna mwamvuli wa Kifo uliotumika hapa ili kupumbaza akili za kipelelezi”

“Una maana maiti sio halisi kwa sura tambuliwa?”

“Ndio, hii moja wapo” Akamuonesha sura iliyokutwa kwenye maiti iliyotambuliwa kama Sandra.

“Wauwaji ni Watu wenye akili kubwa sana na inaonesha ni wazoefu wa hii kazi Zola, unatakiwa kuwa makini sana endapo watakugundua hali itakua mbaya, unatakiwa upate sura ya Bandia ili kuficha uhalisia wako” Akasema Mzee Dawson akionesha kuanza kulitazama jambo hilo kwa jicho la tatu.

********

Ndani ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa, Six na yule Mdada aliyejitambulisha kwa Inspekta Zola kama Judith lakini huku alikua akiitwa Malaika walikua wakisubiria ugeni ndani ya Uwanja huu.

Malaika alikua kwenye sura yake halisi, akionekana kama mdada mwenye majivuno sana, shingo yake ilikua na tatuu ya maua ya rangi aina ya Rose, iliwabidi kukaa hapo kwa zaidi ya nusu saa. Punde wakapata kumuona Mtu waliyekuja kumpokea, alikua ni Mzungu mwenye kibegi kidogo.

Safari ya kutoka Uwanja wa ndege kuelekea kwenye makazi yao ya siri ilianza, Mzungu alipofika kwenye gari akavua sura bandia. Yes! huyu ndiye John Brain ambaye idara nyingi za Usalama Duniani zilikua zikimtafuta lakini ilikua ngumu sana kumnasa, licha ya kuwa yeye ndio Bosi wa kundi la MAFIA GANG lakini pia alikua akipokea oda kutoka kwa Mabosi wake ambao walikuwa wa siri sana.

“Umefanikisha kuchukua nyaraka?” akauliza John Brain huku akiwa anaiweka ile sura ndani ya begi lake dogo ambalo lilikua na sura nyingine za Bandia ambazo alikua akizitumia mara kwa mara ili kuficha utambulisho wake.

“Nimefanikisha lakini kuna Mpelelezi mmoja makini anafwatilia jambo hili”

“Dammn!! niliwaambia mnatakiwa kwanza kusafisha kikosi cha Usalama wa Taifa ndipo kazi nzito ianze” John Brain akachukua nyaraka na kuanza kuzipitia, alifahamu lugha zaidi ya 20 hivyo hakupata shida pindi alipokuwa akiratibu mpango fulani kwenye Nchi tofauti tofauti.

  • ••••••••
Ndani ya Ikulu, Mzee Dawson alikua akifanya mazungumzo na Rais wa Nchi ili kujua wamefikia wapi. Ilikua ni lazima wadhibiti MAFIA GANG kabla haijaleta mpasuko na taharuki kwa Wananchi, tayari Watu ambao hawakua Usalama wa Taifa walianza kufa, vifo vya Askari 15 ndani ya kituo cha polisi ilikua ni miongoni mwa taarifa zilizomkasirisha sana Rais.

“Dawson! Unasifika kwa Ujasusi, tayari kazi hii iko mikononi mwako na hakuna namna tunaweza kufanya bali kusikiliza maendeleo yako” Yalikua ni maneno ya Rais, Mzee Dawson alikua akichezea karamu kuonesha alikua akitafakari namna ya kumjibu, Rais akagonga meza kama ishara ya kuhimiza kupata jibu kutoka kwa Mzee Dawson

“Kazi iko kwenye mikono yangu Mkuu, ni lazima nilifyeke kundi hili kabla halija leta madhara zaidi”

“Madhara zaidi? tayari wameleta madhara na hofu imetanda kwa watendaji wa Serikali, najiuliza ni Watu wa namna gani hawa wameweza kuingia kwenye nyumba ya Msaidizi wangu ( Makam wa Rais ) na kufanya mauwaji bila Askari na walinzi wengine kujua, hali sio shwari Dawson” Rais akapaza sauti iliyoambata na kukauka kwa koo lake, akahitaji maji ya Baridi kutoka kwenye friza, Dawson akampatia maji kwenye glasi, yalikua ni maongezi ya siri kati ya Dawson na Rais huyu. Baada ya kumaliza kunywa glasi moja ya maji baridi, akawa ametuliza mzuka wake.

“Dawson! nakuamini” akasema Rais akiwa anaweka glasi juu ya meza kisha akavuta tai yake

“Sitakuangusha Mkuu ni jukumu langu zito, nimekula kiapo kuilinda nchi yangu” akasema kwa utii na heshima kubwa mbele ya Rais huyu Kijana

“Wanataka nini?”

“Mapema tutalibaini hilo, kuanzia hapo tutawadhibiti Mkuu. Wamefanya mauwaji Nchi nyingi lakini hapa wameingia sehemu isiyo salama kwao, nakuhakikishia nitawafyeka haraka iwezekanavyo”

“Dawson! Nchi inakuangalia wewe na kitengo chako cha Usalama wa Taifa” Akamaliza kwa kumrunusu Dawson akaendelee na majukumu yake mazito, jasho likiwa linamvuja…Mzee Dawson akachukua Lifti kushuka chini, akaingia ndani ya gari yake.

Jua lilikua tamu sana siku hii, hali ya ubaridi ikiwa inachukua nafasi kubwa. Inspekta Zola akaelekea nyumbani kwa Marehemu Robert, Waombolezaji walikua wengi sana lakini Zola akahitaji kuonana na Mama yake na Robert, akaoneshwa mahali ambapo Mama huyo alikuwepo.

“Pole Mama, Naitwa Inspekta Zola nafikiri unanikumbuka?” akaongea baada ya kuketi, akahitaji kuzungumza na Mama yake Robert pekee, waombolezaji wengine wakaamriwa kutoka.

“Mara ya Mwisho ulionana wapi na Robert?” Mama akafuta chozi lake, akajiweka sawa kuongea

“Nilizungumza na Robert kupitia simu, akaniambia nije huku kwa ajili ya harusi yake. Nilichelewa kufika huku kutokana na mazingira yaliyo nje ya uwezo wangu, Alinisistiza sana natakiwa kuwepo lakini nilifika siku ya harusi…”

“Ulionana na Mwanao baada ya kufika?”

“Hapana, alipofika kanisani hakupata hata kunitazama. Ndio tukio likatokea…”

“Mwanao alikua anafanya kazi gani?”

“Robert alikua na duka la kuuza Maua mjini, ndio biashara yake ya muda mrefu”

“Unamfahamu vipi Bosco?” Mama akaanza kulia, Zola akajitahidi kumtuliza

“Bosco ni kama Mwanangu, walikuwa wakija pamoja kunitembelea, sijui wamepatwa na nini hadi wakauwana” Inspekta Zola alipomaliza kuzungumza na Mama Robert, akaelekea kuonana na Mzee Dawson ambaye alimpigia simu kuwa kuna ujumbe kutoka kwa Rais

Ndani ya mkoba wa Inspekta Zola kulikua na sura za bandia ambazo alikua amepewa na Mzee Dawson ili kuficha uhalisia wake, alipofika kwenye gari akaivaa kisha akaelekea kuonana na Dawson.

Kama kawaida yao walikutana sehemu iliyojificha huku wakipata pombe ambayo kwao waliita kama kifungua kinywa, sura ya Mzee Dawson ilikua imekosa neema ya furaha, tabasamu lake halikuonekana hata chembe na kumfanya Zola atamani kusikia kutoka kwa Mzee Dawson ( Google )

“Hali ni mbaya Zola, Mkuu amewaka sana leo anahitaji kazi iishe ndani ya muda mfupi vinginevyo anaweza akaajili Watu kutoka nje ya Nchi kwa ajili ya upelelezi wa kina kuhusu MAFIA GANG” akasema kwa sauti iliyotoka kwa vituo vituo huku akiwa anameza funda za pombe

“Dawson! umenipa kazi ndani ya masaa 24, ndani ya Upelelezi huu kuna visa tata sana ambavyo vinahitaji umakini wa hali ya juu sana vinginevyo tutakuja kupoteza kila kitu”

“Kuna Mtu nitakuunganisha naye, ni rafiki yangu wa muda mrefu anaitwa Pacho…atakusaidia baadhi ya mambo ili kuendana na muda”

Punde simu ya Mzee Dawson ikaanza kuita, akaisikilizia kwa miito mitatu kisha akaipokea na kuiweka kwenye sikio lake lililojaa Usikivu wa kupokea taarifa, alichokisikia kilimshtua sana mara simu ikakatika.

“Barabara namba 8 kuna mauwaji yametokea ya Afisa wa Usalama akiwa anatoka kanisani” Ilikua ni sauti ya Mzee Dawson iliyotawaliwa na utulivu sana

“Ooh God”

“Ndio hivyo Zola, hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa wiki hii na kuendelea”

“Ngoja nielekee eneo la tukio” Inspekta Zola akajikusanya na kuondoka pale akimuacha Mzee Dawson akiendelea kugida pombe kali.

Yalikua ni majukumu yake ya kazi, akafika eneo la tukio na kuukuta mwili wa Afsa aliyeuwa ukiwa juu ya daraja, gari ya Afsa huyo ikiwa imesimama katikati ya Barabara na kusababisha msongamano.

Taratibu za kiusalama zikaanza mara moja huku mwili ukichukuliwa na kupelekwa Hospitalini, mara simu ya Zola ikaingia ujumbe kutoka kwa wataalam wa Maabara kutoka kwenye kitengo cha Siri cha Mzee Dawson kilichoitwa MPA, akapewa taarifa juu ya Maiti ya Robert na Bosco.

Milii ile ilikuwa ndio pekee yenye sura halisi tofauti na Maiti ya Sandra ambayo ilikutwa na sura bandia, akajikuta akiwa njia panda hajui aanze na lipi amalizie lipi, simu yake ikaingia ujumbe mfupi kutoka kwenye namba ambayo ilikuwa ya siri

“ZOLA TOKA ENEO HILO HARAKA SANA” Ujumbe ulisomeka hivyo, akajaribu kutafakari kwa kina lakini hakupata majibu kwa haraka, akajaribu kuujibu ujumbe huo lakini hakufanikiwa kupata majibu. Kwa akili yake ya kipelelezi akajuwa mara moja yupo Mtu anayemuona pale, haraka akaondoka pale na kuelekea kwenye gari lake ambalo lilikuwa kando na eneo lile, mara akasikia mlipuko mkubwa. Alipogeuka akaona gari moja ikiwa inawaka moto, ndio gari ambalo alikuwa karibu nalo pale alipokuwa amesimama eneo la tukio.

Hapo akafanikiwa kujua kuwa kuna Watu wanamfuatilia kwa karibu sana lakini akawa na maswali mengi kuwa ni nani aliyemuokoa kwenye ile hatari? Mlipuko ulisababisha majeruhi wengi sana ambao walikuwa ni Askari na wapita njia.

Alipofika kwenye gari yake akapata shahuku ya kutaka kumfahamu aliyemuokoa kwenye kifo, akachukua simu yake na kujaribu kuujibu ule ujumbe lakini hakupata majibu mengine, akamtafuta Mzee Dawson na kumtaarifu juu ya tukio hilo la mlipuko

“Aliyekuokoa anaitwa Pacho, ndiye msaidizi wako kwenye majukumu”

“Oooh! niliona kifo changu pale”

“Kuwa makini sana, Watu wa Usalama wanauawa sana….” yalikua ni maneno ya mwisho ya Mzee Dawson kisha simu ilikatika, ikampa wasaa Inspekta Zola kuelekea kwenye makazi yake ya Siri karibu na ufukwe.

Masaa mawili baadaye yalimkuta Inspekta Zola akiwa amekalia kiti kwenye makazi yake ya siri, mbele yake kulikuwa na meza nyeusi ngumu iliyotengenezwa kwa kioo. Alionekana kuzama kwenye lindi la mawazo, akafikiria namna Muuwaji alivyokuwa akifanya mauwaji kila kukicha, bado alitakiwa kujuwa ni wapi alipo Sandra wa Ukweli kama Bosco na Robert ni Watu halisi, presha ya Rais ya kulazikisha kazi ifanyike upesi ilimkasirisha sana.

*****************

Anga lilibadilika kuwa jeusi machoni pa Idara za usalama wa Taifa, Mauwaji ya Polisi na Maafisa yalitaarifiwa kila kona ya Jiji, Hofu ikachukua nafasi kubwa kila mmoja akijiuliza ni nani atafuata Kufa. Ujio wa John Brain Nchini ulikuwa na lengo moja kubwa, akakutana na Vijana wake wawili aliowatumainia sana mmoja aliyeitwa Six na mwingine aliyeitwa Malaika akawaambia

“Wakati Polisi wanahangaika kutafuta ufumbuzi wa vifo hivi vya utata sisi tutakuwa bize kumalizia mpango wetu hapa Nchini, Rais wa Nchi hii alitutuma kazi na tumeimaliza sasa kwanini idara yake inamshikilia Jamaal?” Alihoji John Brain

“Huyu Kenge anayeitwa Zola atakuwa kikwazo kikubwa sana kwenye mpango huu, lazima aondoke kwanza” Alisema Malaika akakumbuka jinsi Inspekta Zola alivyo makini

“Udhaifi wa Zola ni Wanawake, kilevi chake kitamuuwa muda mchache ujao” Alisema John Brain aliyeonekana kujaza mambo mengi kichwani pake

“Kazi hiyo niachieni mimi” Six akaomba apewe huo mpango wa kuondoa uhai wa Inspekta Zola

“Unatakiwa kuwa makini sana sababu kwa namna alivyo huyo Mtu si rahisi akamuamini Mtu kwa Mara ya kwanza, unapaswa pia kujuwa kuwa ukibainika basi kila kitu kitaharibika. Zola ni Jasusi mbobezi, kabla hujampeleleza anakuwa tayari amekupeleleza.” Alisema John Brain, kisha Malaika kasema

“Zola anatumika kama Mwanvuli wa Serikali katika kutekeleza mipango ya siri, najiuliza aliwezaje kukwepa mtego wa Bomu”
 
Ilipoishia “Unatakiwa kuwa makini sana sababu kwa namna alivyo huyo Mtu si rahisi akamuamini Mtu kwa Mara ya kwanza, unapaswa pia kujuwa kuwa ukibainika basi kila kitu kitaharibika. Zola ni Jasusi mbobezi, kabla hujampeleleza anakuwa tayari amekupeleleza.” Alisema John Brain, kisha Malaika kasema

“Zola anatumika kama Mwanvuli wa Serikali katika kutekeleza mipango ya siri, najiuliza aliwezaje kukwepa mtego wa Bomu”Endelea

SEHEMU YA TATU

Yalikuwa ni maswali waliyoulizana, Muda huo Inspekta Zola alikuwa kwenye gari yake akiwa anaelekea nyumbani kwa Marehemu Robert. Kichwani akiwa na mawazo lukuki akajikuta akimfikiria Msichana aliyeuwa polisi katika kituo cha polisi tena kwa Ustadi ambao hata Komando asingeliweza kufanya. Akatikisa kichwa chake kisha katabasamu tuu

Akaanza kuvuta picha namna Msichana yule aliyejitambulisha kama Judith alionekana, alikuwa mwembamba, mweupe na mwenye sura ya upole sana. Pasipo kujuwa kuwa picha aliyokuwa akiiwaza Zola haikuwa halisi kwani, hakuitwa Judith bali alikuwa akiitwa Malaika, sura ile haikuwa halisi.

Alikanyaga mafuta bila kujuwa alikuwa akiwindwa sana auawe, dakika Thelathini na tano baadae alikuwa akiegesha gari lake katika uwa wa nyumba ya Robert. Huzuni ilikuwa imetanda sana, Mama Robert alipomuona Zola alimtambua kama Polisi aliyekuwa akifwafilia tukio la vifo vile, akamkimbilia na kumwambia

“Mnipe mwili wa Mwanangu nimzike, Mnipe mwili nawaomba sana”

“Mama hebu tulia, nimekuja kwa ajili ya kuzungumza na wewe. Hebu futa machozi Mama” Alisema Inspekta Zola akiwa amemshika mabega Mama Robert

“Hebu tuongee vizuri” Zola akapepesa macho yake, kulikuwa na Watu wengi pale Msibani akaona sehemu ambayo ilikuwa tulivu bila Watu, akamsogeza Mama yake Robert huko

“Mama hebu nieleze vizuri tukio lilitokeaje? Kuna utata sana katika jambo hili” Alisema Zola huku akiwa makini kutaka kusikia ambacho Mama Robert angesema

Mama Robert akajifuta chozi na kujituliza kidogo kabla ya kumsimulia Zola

“Tulikuwa kanisani wakati tunasubiria ndoa iweze kufungwa, ili Mwanangu Robert amuowe Sandra. Nilishtuka kusikia mlio wa Risasi, nilipogeuka nikamuona Mwanangu akiwa ameshikilia Bastola huku miili miwili ya Bosco na Sandra ikiwa chini, katika hali ya taharuki kila mmoja akipiga kelele za woga, Robert aliubeba mwili wa Sandra na kuondoka nao akiwa analia” Mama Robert alianza kulia kwa uchungu hadi Inspekta Zola alijikuta akidondosha chozi lake kwa jinsi ambavyo Mama Robert alikuwa akilia kwa uchungu.

“Naomba msaada wako niipate maiti ya Mwanangu Robert ili nimzike Mimi”

“Sawa! Mwili wa Robert utaupata baada ya kumaliza uchunguzi ambao kwa asilimia kubwa naweza kusema Umeisha, nisaidie namba ya Mama Sandra ili niweze kuzungumza nae”

Zola akapewa namba akaelekezwa anapoishi Mama Sandra, akamuaga Mama Robert kisha akaingia kwenye gari yake ambayo ilitengenezwa maalum kwa ajili ya kuzuia risasi kuingia, gari hili lilinunuliwa na Mzee Dawson kwa ajili ya kazi za kipelelezi.

Mwendo wa dakika arobaini na nane, Zola alikuwa ameshafika alipoelekezwa, haikuhitaji sana ujuzi wa kutambuwa kuwa eneo hilo lilikuwa na tatizo licha ya ukimya na uchache wa Watu uliopo pale. Zola akajipenyesha hadi Ndani ambako Mama Sandra alikuwepo lakini kabla hajafika huko alikutana na Baba Sandra ambaye alimtambua Zola kabla hata hajajitambulisha.

“Umefanikiwa kujuwa chanzo cha kifo cha Binti yangu?” Aliuliza Baba yake Sandra ambaye alikuwa na umri sawa na Zola

“Ngoma ngumu lakini tutafikia tamati hivi karibuni”

“Tutashukuru sana ili tuweze kumpumzisha Sandra katika nyumba yake ya milele na hayo mengi tutayaachia jeshi la Polisi”

“Usijali! Nimekuja kuzungumza kidogo na Mama Sandra, hapana shaka yupo Kushoto chumba cha mwisho” Alisema Inspekta Zola huku akiachia tabasamu la kazi

“Jicho lako la kipelelezi liko sahihi Afande, nenda tuu kazungumze nae” Zola aliposikia kauli ya utii namna ile aliona amtamzame Mzee huyo Usoni pake, akahisi jambo lakini akaliweka kiporo kichwani pake. Hata alipokaribia mlango wa chumba alichopo Mama Sandra aligeuka na kumuona Baba yake Sandra akiwa bado anamfwatilia Zola kisha alipoona Zola amegeuka akajifanya kuondoka pale. Zola akagundua jambo fulani, akabisha hodi kisha akaruhusiwa kuingia chumbani

“Pole Mama! Samahani naomba wote mtoke ili nizungumze na Mama Robert, Naitwa Inspekta Zola” Alisema kisha akatoa kutambulisho, Watu walioko mle waliondoka taratibu huku Zola akipata nafasi ya kuangalia picha iliyopo Ukutani, ilikuwa ni picha ya Sandra akiwa shuleni

“Hapana Shaka huyu ni Sandra katika umri wa ukuaji wake?” Alihoji Zola huku akiendelea kuiangalia, Mama Sandra akaitikia kwa masikitiko

“Ndio…Ameondoka nikiwa namuhitaji Mwanangu” Aliposema alijikuta akianza kulia upya ni kama vile aliweka chumvi kwenye kidonda kibichi, Zola alisogea kisha aliketi chini kwa mtindo wa kufunga miguu yake kama Waislam wakaavyo.

“Mwanao alipaswa kuolewa na Robert, lakini Huyo Robert aliondowa uhai wake kabla hata ya harusi. Unafahamu nini kati ya hawa Watu watatu yaani Bosco, Robert na Sandra Mwanao”

“Sandra alifahamiana na Robert muda mchache sana ndipo akasema anataka kuolewa, lakini Robert na Bosco inasemekana ni marafiki wa muda mrefu sana”

“Vifo vyao unaweza ukahisi vinatokana na nini Mama?” Mama Sandra alitikisa kichwa chake kisha akasema

“Ni ngumu sana kwa jinsi ambavyo walikuwa wakija hapa na kuongea kwa furaha sana, sijui nini kimesababisha haya yote”

“Asante Mama! Hii ni namba yangu ukipata chochote nijuze, mtapewa mwili wa Sandra kwa ajili ya maziko huku uchunguzi mwingine ukiendelea” Zola alijizoa na kuondoka pale huku akili yake ikianza kumtafakari Baba yake Sandra kwanini alikuwa akimtazama sana?

Akiwa kwenye gari Zola alionelea aelekee Hospitali ambako miili ile ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi, alipofika alikutana na mtaalam wa Maabara kutoka katika kitengo cha MPA Cha Mzee Dawson akamwambia kuwa ile miili miwili ipelekwe kwa wahusika kwasababu ni miili halali ya wahusika

Zola aliondoka Hospitali na kuelekea katika makazi yake ya siri ambayo Watu wengi walikuwa hawayafahamu, wakati anafika akakumbuka kuwa ujumbe wa picha ulikuwa umeshatumwa, akaingia chumba cha siri kwa ajili ya kufanya alichokusudia, alihitaji kujuwa ule mwili bandia ni wa nani. Akaingiza picha katika mashine yake ya Kazi akapata majibu yaliyomfanya afunge safari nyingine kuelekea Chuo Kikuu cha Sayansi ya Mifupa.

“Namuulizia Anastanzia Nyange” Aliuliza Zola akiwa ameketi mbele ya Mkuu wa Chuo hicho ambaye macho yake yalikuwa yametua kwenye sura ya Zola

“Anastanzia Nyange?” Aliuliza Mkuu wa Chuo ambaye alikuwa na kitambi

“Ndio, picha yake hii hapa” alimuonesha picha

“Ameenda Field na wanachuo Wenzake Kaskazimi Mashariki mwa Mkoa jirani”

“Ok asante” Zola aliondoka pale, nyuma yule Mkuu wa Chuo akanyanyua simu ya mezani akapiga sehemu akaisikilizia hadi ilipopokelewa kisha akasema

“Amekuja hapa muda sio mrefu anamuulizia Anastanzia Nyange” Aliposema hivyo hakuhitaji kusikiliza sauti kutoka upande wa pili akakata simu kisha akaweka mikono yake juu ya meza huku akionekana kuzama katika tafakari nzito sana.

Zola kabla hajaondoka pale Chuoni alikutana na Mwanachuo mmoja akamuuliza kama anamfahamu Anastanzia, yule Mwanachuo akamwambia Zola kuwa anamfahamu Anastanzia lakini hakuonekana hapo chuoni kwa siku saba. Zola akajitambulisha kuwa ni polisi akamuomba Yule Mwanachuo amueleze mahali ambapo Anastanzia alikuwa akiishi

“Anaishi na Rafiki yake sio mbali sana ni nyuma ya Hoteli mpya ya Sub Marine, ukifika utaona jengo la Njano lina vigae ndio hapo hapo”

“Asante sana” Zola alifunga safari nyingine ya kuelekea huko alipoelekezwa, alitumia dakika ishirini pekee kufika akakutana na Mtu nje ya nyumba hiyo hapana shaka alionekana kuwa mwenyeji hapo, Zola akamuuliza

“Nimemkuta Anastanzia?”

“Salimia kwanza, waungwana husalimia sasa unapouliza tu Hata hujui unayemuuliza kama ni Mzima au la” alifoka Mtu huyo ambaye alikuwa ni Msichana wa Makamo tuu.

“Samahani! Namuulizia Anastanzia”

“Chumba chake kile pale” alioneshwa kisha Zola akashuka kwenye gari na kuelekea kubisha hodi.

Kiatu cheusi cha Zola kilikuwa kinang’aa na kumfanya msichana huyo kujuwa kuwa Mwanaume huyo alikuwa na pesa sana, kisha akapeleka macho yake kwenye gari ya Zola kisha akaingia chumbani kwake.

Muda huo zola alikuwa akibisha Hodi huku macho yake ya Kijasusi yakiangaza huku na kule, ukimya uliomuitikia ulimpa wazo la kujaribu kufungua pale ili aweze kuchunguza vizuri, akarudi kwenye gari yake kisha akafungua begi dogo akatoa rundo la funguo za Bandia, akachagua ambayo iliendana na kitasa cha pale Mlangoni. Akarudi mlangoni na kufungua taratibu sana bila hata sauti ya kufungua kusikika, sekunde chache akajikuta amefanikiwa kuingia ndani. Alikuwa makini sana, sehemu hiyo ilikuwa na chumba na sebule.

Muda huu alikuwa pale sebleni, palionekana kuwa tulivu sana huku feni ikiwa inaendelea kupepea, ilimfanya aamini kuwa kulikuwa na Mtu aliyekuwa akiishi pale, akili yake ikayakumbuka maneno ya yule mwanachuo kuwa Anastanzia alikuwa akiishi na rafiki yake, Zola alimuhitaji zaidi huyo rafiki yake sababu alishafanikiwa kujuwa kuwa Anastanzia amekufa katika lile tukio kule kanisani, akanyata taratibu aliposikia mlio wa simu ukilia kutokea chumbani, akapinda mkono akachomoa Bastola yake yenye kiwambo cha kupoza sauti ya risasi itokapo.

Akageuka nyuma kuhakiki kuwa hakukuwa na Mtu pale sebleni, kisha akaanza kuelekea chumbani ambako ile sauti ya simu kuita ilikuwa ikiendelea kusikika. Akameza mate taratibu huku kijasho cha umakini kikiendelea kutiririka katika paji lake la Uso, Kisha kwa mwendo wa haraka akaingia chumbani huku akiangaza Bastola yake huku na kule, kitandani aliona Mtu akiwa amelala huku sura ya huyo Mtu ikiwa inatazama ukutani na kumpa wakati mgumu Zola kujuwa ni nani aliyelala pale, taswira ilionesha ni Mwanamke kisha akili na moyo wa Zola ukajipa tumaini la kumpata rafiki wa Anastanzia ambaye anaweza kuwa Mwangaza wa kumpa mwanga Zola kuhusu kesi ile ya Utata sana iliyoibua taswira ya nani alihusika na kifo cha Makam wa Rais..

Bastola ikiwa mbele Zola alionekana kuwa makini huku akizidi kusogea karibu na Mtu huyo ambaye hakumtambua hadi muda huo, alipomfikia akamgeuza kwa kutumia bastola yake, mambo haya aliyafanya akiwa na unri wa miaka zaidi ya 50 sijui alipokuwa kijana Zola alikuwa hatari kiasi gani kwenye upelelezi wake, akashusha miwani na Bastola yake taratibu akapelekea kidole eneo la shingo kisha kwenye pua, ubaridi wa Mtu huyo ulionesha kuwa alikuwa amekufa muda mrefu sana, povu ililikuwa likimtoka puani, alipomchunguza vizuri aliona ile alama ya vidole kwenye paja la Marehemu.

“Shit!” Alisema huku akili yake ikimpa majibu kuwa waliohusika na matukio ya kikatili, waliomuuwa Makam wa Rais ndio waliosababisha kifo kile, haraka Zola akachukua simu yake na kumpigia Mzee Dawson ambaye alimpa kazi ile iliyojaa utata sana, Simu hiyo ilipokuwa ikiita Mzee Dawson alikuwa akistarehe na Msichana mmoja nyumbani kwake, alipoona simu ya Zola akaacha kisha akamwambia Msichana huyo avae aondoke haraka. Mzee Dawson akajitupa kitandani akiwa hoi kisha kapokea simu ya Zola

“Unasemaje Zola?” Aliitika Mzee Dawson kwa sauti ya uchovu sana

“Unapaswa nawe kuingia kazini, vinginevyo mambo yanaweza kuharibika kabisa. Nilikuwa nafuatilia kuhusu vifo vya utata vilivyotokea kanisani, mmoja wa Watu ambao wangeliweza kunipa Mwangaza wa kesi hii nimemkuta akiwa amekufa nyumbani kwake, Watu hawa wapo macho na wananifuatilia”

“Nilikueleza kuhusu hilo Zola, nilikupa pia msaidizi ili akusaidie lakini cha ajabu hutaki kuwasiliana naye kabisa, unataka niingie kwenye majukumu hayo?”

“Dawson unajua fika huwa simuamini Mtu katika mambo yangu, napenda kufanya kazi mwenyewe lakini hili linahitaji utulivu zaidi kitu ambacho maadui zetu hawataki kunipa”

“Aaaah Zola” ilisikika sauti upande wa Mzee Dawson, ikionesha alikuwa akijigeuza.

“Hebu fanya taratibu tuonane ana kwa ana Mzee Dawson, nahisi kuchanganikiwa sasa” Zola alikata simu bila kusikiliza sauti ya Mzee Dawson, baada ya hapo akapiga simu sehemu nyingine ndani ya kitengo cha siri cha Mzee Dawson kinachoitwa MPA, akaomba madaktari waweze kufika eneo la tukio, akawapa Ramani kamili lilipo eneo hilo.
 
Ilipoishia “Aaaah Zola” ilisikika sauti upande wa Mzee Dawson, ikionesha alikuwa akijigeuza.

“Hebu fanya taratibu tuonane ana kwa ana Mzee Dawson, nahisi kuchanganikiwa sasa” Zola alikata simu bila kusikiliza sauti ya Mzee Dawson, baada ya hapo akapiga simu sehemu nyingine ndani ya kitengo cha siri cha Mzee Dawson kinachoitwa MPA, akaomba madaktari waweze kufika eneo la tukio, akawapa Ramani kamili lilipo eneo hilo. Endelea

SEHEMU YA NNE


Hakuwa na muda wa kukaa pale, akatoka taratibu hadi nje, akayaangalia vizuri mazingira yale kwa jicho na akili ya kipelelezi akajua tu kifo kile kimetokea masaa machache yaliyopita na kwa vyovyote mwenye chumba kilichokuwa kinaangaliana na mlango lilikofanyika tukio atakuwa labda amesikia au kuona chochote kile, akakumbuka kuwa mlango huo ulifungwa na funguo kuondolewa, akajiuliza haraka akiwa analitazama dirisha la Chumba jirani

“Kama funguo imetolewa maana yake kuna Mtu amefunga mlango na kumfungia Mtu ndani, Nani amefanya hivi?” Akapata akili ya kusogea chumba cha jirani, alipogonga akatoka yule Msichana ambaye alimuelekeza chumbani kwa Anastanzia, yule Mdada alipomuona Zola akaanza kujishebedua kwa kuhisi kuwa Zola alikuwa akimtaka, alionekana kuvutiwa na Mzee Zola kutokana na muonekana wa kitajiri alionao bila kujuwa kuwa alikuwa amesimama mbele ya Mtu hatari kwa upelelezi

“Nilijua tu utakuja kwangu, Anastanzia sio aina ya Mwanamke ambaye anakufaa wewe. Wazee kama nyie mnatakiwa kupetiwa vizuri ili msiwe na mawazo ya kufa kufa” Alisema huku akitabasamu mbele ya Zola, kisha Zola akamuuliza yule msichana

“Mara ya mwisho umemuona Anastanzia lini?” Mdada akaacha kujishebedua baada ya Zola kuonesha sura ya mbuzi

“Wiki sasa sijamuona ila rafiki yake si umeonana nae? Maana nimekuona ukitoka humo ndani” Zola akatoa kitambulisho cha uaskari akamuonesha yule mdada kisha akamuuliza

“Unaitwa nani?” Mdada akawa anatetemeka

“Naitwa Scolastica”

“Rafiki yake Anastanzia amekufa, naomba uniambie ni nani umemuona akiingia au kutoka mle ndani kabla yangu Mimi”

“Kulikuwa na Mkaka mmoja hivi, aliingia kisha akafunga mlango akatoka, sikumuona tena”

“Anafananaje?”

“Mrefu kiasi, mweusi ana rasta”

“Sikia, watakuja polisi kuchukua mwili wa Marehemu, asante kwa ushirikiano wako” Zola akaingia kwenye gari yake akatokomea eneo hilo, akawasiliana na Mzee Dawson ili wapate kukutana na kuzungumza, Mzee Dawson kama kawaida yake akamueleza Zola wakutane sehemu ya siri.

Alipofika Zola, Mzee Dawson aligundua ni jinsi gani Zola alikuwa katika nyakati ngumu ambayo hakupata kumuona nayo, akamimina mvinyo kwenye glasi na kumpatia, akapiga funda moja la mvinyo ukawa umeisha kwenye Glasi, kisha akaitua Glasi hiyo mezani kama Mtu aliyechoshwa na kinachoendelea.

“Dawson! Hili jambo ni zito sana, kulifahamu lilipo kundi la Mafia Gang, na kuwajua Watu hao inakuwa kazi ngumu sana. Sijui ni mafunzo ya namna gani watu hao wanapatiwa kabla ya kutekeleza jambo fulani” Alisema Zola huku akakunja midomo yake, akampa Glasi Mzee Dawson ili amuongeze mvinyo, ukamiminwa mvinyo kwenye Glasi ya Zola haraka kisha Dawson akakaa vizuri ili amjibu Zola, kwanza akajikoholesha kisha akasema

“Mauwaji yaliyofanywa na Mafia Gang huko Congo yanatisha sana, hapa bado kabisa hawajavuruga kisawasawa! John Brain kama lilivyo jina lake ni Mzungu hatari sana Zola, nahisi yupo hapa Nchini na kuna mpango wanautekeleza, umejaribu kufuatilia ni mafaili gani yaliibiwa na huyo Msichana katika kituo cha polisi” Zola alitikisa kichwa kuashiria hakufuatilia suala hilo, Dawson akapiga tena fundo la Mvinyo kisha akabeua kidogo

“Zola ninayemjua Mimi hawezi kukosa kujuwa mambo kama hayo, akili yako haipo kabisa Zola, John Brain ana akili sana na anachezea ubongo wako! Huenda ameshakujua na kukufuatilia, anachofanya ni kukuchezesha, hapa kuna mambo mawili huenda yanafanyika kwa wakati mmoja”

“Mambo gani hayo?”

“Wananunua Muda wako na muda wa Wapelelezi wengine ili watekeleze mipango yao, hata haya mauwaji yanayotokea huwenda wanakuhadaa ili usipate muda wa kutuliza akili yako, wanajuwa wewe ni hatari kiasi gani, hilo lipo wazi Zola”

“Hili suala linaninyima usingizi Dawson, nahisi nipo katika chumba chenye giza ambacho siwezi kuona kuna nini ndani yake hata kusikia sauti inayonipa ishara, nahisi kushindwa”

“Ha!ha!ha! Zola, huwezi kukata tamaa mapema hivi, umekula kiapo cha kulinda Taifa hili ikiwemo kupambana na Watu aina ya John Brain, nafikiri muda unaenda, umekuja na gari yako?”

“Ndio”

“Tuitumie sasa hivi”

“Tunaenda wapi?” Aliuliza Zola huku akimtazama kwa makini Mzee Dawson ambaye tayali alionekana kuwa ameshaanza kulewa lakini alimjuwa sawa sawa jinsi alivyo, akilewa huwa anaamuwa mambo kwa kutumia akili sana.

“Tunaenda Hospitali kuruhusu ile Maiti moja iliyosalia kwenda kuzikwa”

“Tutawapa vipi Maiti ambayo si yao, kumbuka ile ni Maiti ya Anastanzia na sio Sandra”

“Tunairudisha sura ya Bandia kama ilivyo Mwanzo, huu sio wakati wa wao kujuwa ukweli, acha waamini wanamzika Mtu wao” Waliitumia gari ya Zola hadi walipofika Hospitali, tayari maiti mbili zilikuwa zimeruhusiwa kwenda kwa wahusika ambazo ni Maiti ya Bosco na Robert.

Wakasimamia zoezi la kuveshwa sura kwa Mwili wa Anastanzia, dakika chache muonekano ulibadirika,

“Yes! Acha wamzike wanayemuamini huku sisi tukiwa bize kufuatilia” Alisema Dawson kisha alikohoa kama kawaida yake, Zola akampa kitambaa akawema mdomoni lakini alipokitoa ilionekana damu katika kitambaa hicho cheupe kuashiria kuwa mapafu ya Mzee Dawson yalikuwa katika hali mbaya

“Usijali” akasema Dawson, kisha Zola akapiga simu kwenye familia ya Mama Sandra ili waende kuuchukuwa mwili walioamini ni wa Sandra ili wakauzike.

“Naingia kazini sasa Zola, tuna muda mchache sana kuhakikisha Nchi inakuwa shwari” alisema Dawson na kumfanya Zola atabasamu maana mzigo ulikuwa ukimuelemea sana. Siku iliyofuata Mazishi ya Sandra yalifanyika, Zola alikuwa miongoni mwa waliohudhuria lakini uwepo wa Zola msibani ulikuwa na melengo makuu mawili, moja kuhakikisha familia haitambui kama anayezikwa si Sandra, jambo la pili aliamini kama Mpango ule ulisukwa basi wasukaji wangefika pale Msibani kwa ajili ya kufuatilia, lakini Pia Zola alimtilia shaka Baba yake Sandra akiamini anajuwa jambo fulani.

Akiwa ameketi alivalia miwani nyeusi na sura ya Bandia kama alivyoambiwa na Mzee Dawson kuwa Huenda Mafia Gang wameshamjuwa ndio maana walitaka kumuuwa katika jaribio la bomu, hakutambuliwa na yeyote pale lakini alionekana kuwa miongoni mwa waliokuja Msibani, Watu walikuwa wengi mno. Kifo kile kilishika mioyo ya wengi.

Naam!! Zola alikuwa bize sana kuhakikisha anazungusha macho yake kila kona, macho yake yakajikuta yametua kwa jamaa mmoja ambaye naye alikuwa bize sana kuzungusha macho yake, Zola hakufanikiwa kugundulika baada ya kubadilisha sura kisha kuvaa miwani, ingehitaji utaalam mkubwa sana kumtambua. Kilikuwa ni kipindi ambacho Msemaji wa Familia alikuwa akiwashukuru Watu waliokuja pale kwa ajili ya maziko ya Sandra ambaye alizikwa pale pale nyumbani kwao, Zola hapo ndipo akajithibitishia kuwa familia ya Sandra haikusanuka kuwa walikuwa wakizika Maiti ya Mtu mwingine, lakini hakusita kukubali uwezo wa Maadui zao ambao walifanikiwa kuuhadaa ulimwengu wa vipofu ambao macho yao hayakuweza kuona mbali zaidi ya Jicho la kipelelezi lenye mafunzo ya kijeshi ambalo Zola alikuwa nalo.

Kwa mantiki hiyo, Maadui walifanya tafiti zao kabla ya kumtumia Anastanzia kuvaa sura ya Sandra maana miili yao ilifanana sana ndio maana hawakuweza kuhisi kama kuna tatizo, akashusha pumzi zake, alijuwa ilitumika akili kubwa sana pale hadi Anastanzia akaingizwa kwenye mwanvuli ule wa Umauti, swali lililomjia akilini mwake haraka ni wapi alipo Sandra mwenyewe?. Aliporejesha macho eneo la yule jamaa aliyekuwa akimfuatilia, aliona kiti kikiwa kitupu kabisa, akaangaza huku na kule bila mafanikio yoyote ndipo akaona ni bora atoke nje ili apeleleze yule jamaa ni nani na kwanini alikuwa akichezesha yale macho ya kipelelezi, akamkubuka sawasawa jamaa huyo mwenye upara na ndevu nyingi.

Alinyanyuka kutoka kitini kama Mtu aliyemaliza tukio la mazishi, hakutaka kuonesha dalili zozote kuwa alikuwa akifuatilia chochote maana aliamini Maadui walikuwepo pale Msibani, akiwa anatoka aligongana na Mwanamke mmoja mrefu, mweupe na mwenye nywele nyingi.

“Samahani?” Alisema Mwanamke huyo ambaye alikuwa na uzuri wa kutosha, macho ya Zola yakautalii mwili wa Mwanamke huyo bila stara

“Usijali!” Akasema Zola kisha akatoka pale taratibu bila kugeuka nyuma.

Yule Mwanamke alimtazama sana Zola hadi alipozama, kisha akaketi kitini. Zola alipofika nje alimuona yule jamaa akizungumza na simu kisha akaingia kwenye gari, Zola hakuchelewa naye akaingia kwenye gari na kuanza kumfuatilia jamaa huyo ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote ule maana hata alivyoendesha gari hilo ilionesha wazi kuwa alikuwa katika hali ya kawaida, akaingia Barabara ya tano kisha akashika barabara kuu ambayo ilikuwa ikitoka Uwanja wa ndege kuelekea eneo ambalo lilikuwa na Hoteli nyingi za nyota tano.

Bila kupoteza muda Zola alimpigia Dawson simu, akamueleza hali ilivyo kisha akasubiria jibu la Mzee huyo.

“Washa GPS ya Gari” ilisikika sauti kutoka upande wa pili, ikampa ishara Zola kuwa Mzee Dawson alikuwa na maelekezo maalum ya nini cha kufanya.

“Nakuona!” Alisema Dawson kisha alikata simu mara moja, baada ya dakika tano akampigia tena na kumwambia

“Fuata maelekezo yangu, kuwa makini hao Watu wana akili ya ziada sana wakati mwingine Watu hawaamini kama Huyo Mzungu ni Binadamu, wana akili iliyozidi…unaweza kuwa umetegwa, kabla ya kutoka Msibani hakuna ishara tata?” Alimpa wakati wa kufikria, Zola akasema

“Nilikuwa makini kuliko kawaida, hakuna aliyeniona ila wakati natoka…” Ukimya ukatawala, Mzee Dawson akamuuliza Zola

“Enhee ilikuwaje?” Zola akafikiria alipokuwa akitoka pale aliparamiana na Mwanamke mmoja mzuri sana, hakutaka kulisema hilo akiamini sio ishara ya kumueleza Mzee Dawson

“Sio ishara!”
 
Ilipoishia “Fuata maelekezo yangu, kuwa makini hao Watu wana akili ya ziada sana wakati mwingine Watu hawaamini kama Huyo Mzungu ni Binadamu, wana akili iliyozidi…unaweza kuwa umetegwa, kabla ya kutoka Msibani hakuna ishara tata?” Alimpa wakati wa kufikria, Zola akasema

“Nilikuwa makini kuliko kawaida, hakuna aliyeniona ila wakati natoka…” Ukimya ukatawala, Mzee Dawson akamuuliza Zola

“Enhee ilikuwaje?” Zola akafikiria alipokuwa akitoka pale aliparamiana na Mwanamke mmoja mzuri sana, hakutaka kulisema hilo akiamini sio ishara ya kumueleza Mzee Dawson

“Sio ishara!” Endelea

“Sawa endelea kuwa makini na gari hilo” Gari hiyo ndogo nyeusi iligota katika moja ya hoteli maarufu sana Mjini hapo iliyoitwa Sarafina Hotel, Muda huu jamaa mwenye upara alikuwa akishuka bila kuonesha wasiwasi wowote huku Zola akiwa anatafuta sehemu rahisi ya kupaki Gari yake, Jamaa wa upara akaingia kwenye lifti wakati Zola akiwa amejibanza mahali anamchungulia, haraka akapandisha ngazi kuelekea juu kwa spidi ambayo kila mmoja alishangaa kwa Mzee kama Zola kupandisha zile ngazi kwa spidi kubwa kama umeme, Naam ilikuwa ni kawaida kwake kutokana na mafunzo aliyoyapata zamani nchini Mexico na Cuba.

Alipofika Floo ya pili alipokelewa na ukimya, akili yake ikamwambia kuwa Jamaa wa upara atakuwa Floo ya juu yake yaani ya tatu, basi Zola kwa spidi ile ile alizidi kupandisha ngazi na kuendelea kustaajabisha Watu aliopishana nao, mwisho wa Floo ya pili alimuona jamaa wa Upara akikata kona upande wa kushoto, Zola hakutaka kupoteza muda alizidi kumfuatilia ili ajuwe Jamaa yule alikuwa akienda wapi, huku akili yake ikimwambia kuwa ni miongoni mwa wale waliousuka ule mpango wa vifo vya Robert na Bosco na hatimae kumtumia Anastanzia kama mchezo wa kuigiza ili kuficha jambo ambalo kwa asilimia kubwa lilifanikiwa. Alipokata kushoto alianza kuhisi hali ya tofauti, achilia mbali ukimya bali kulikuwa na milango miwili ambayo ilikuwa wazi tena ikiwa inacheza kuashilia kuwa ilikuwa imeguswa sekunde chache zilizopita.

Zola akakunja mkono wake wa kushoto ambao alipendelea kuuita Mkono Wa Mungu, kisha akachomoka na Bastola yake yenye kiwambo maalum cha kuzuia mlio wa risasi kutoka, tayari alikuwa na hisia kuwa alikuwa ameingizwa mtegoni, akachomoa Ear phone masikioni baada ya kuhisi mawasiliano kati yake na Mzee Dawson yalikuwa yanasuasua na hakutaka kuzungumza kwa sauti kubwa, Kitendo cha Zola kuchomoa zile Ear Phone masikioni kilimpa ishara Mzee Dawson, akahisi pengine Zola yupo kwenye mtego wa kifo, haraka akachukua gari kuitafuta Sarafina Hoteli ilipo, Naam! Zola alikuwa akinyata kama paka aliyekuwa akimvizia panya ili aweze kumla, alipiganisha akili yake huku macho akiwa anayaelekeza kwenye ile milango miwili iliyo wazi

Akauchagua mlango mmoja akaingia taratibu kisha akafunga mlango bila kuruhusu sauti ya kufungwa kwa mlango huo kusikika, mbele aliona kuna korido iliyo kimya sana, akawa anaifuata. Alikuwa amejikunja kama duma vile huku akijuwa kuwa kosa lolote atakalo lifanya linaweza kuondoa uhai wake, akaupita mlango wa kwanza na wa pili, akili ikamwambia aufungue mlango wa tatu, alikuwa ni mwenye hisia kali kama Mbwa wa polisi vile, alihema taratibu sana, alifundishwa kuwa kuhema kwa nguvu kunaweza kusababisha shabaha kwenda tofauti jambo ambalo hakutaka litokee pale, akiwa ameshikilia kitasa hicho huku akivuta taratibu Zola alikutana na teke kali lililomnyumbisha na kusababisha bastola yake kuanguka chini, akiwa anataka kuiokota Bastola hiyo ilipigwa teke na kuburuzika mita kadhaa, Ndipo Zola akajuwa sasa yupo katika hatari mno, kwa umakini akageuka taratibu kumtazama aliyempiga teke.

Alikutana na sura ya Malaika, ambaye yeye alimtambua kama Judith tena alikuwa katika sura bandia ambayo Zola alikuwa akiijuwa. Mzee Zola akayakumbuka maneno ya polisi aliyempigia simu na kumtaarifu juu ya mauwaji ya polisi katika kituo cha polisi, akautumia muda huo kuyatazama maungio ya Msichana huyo mwembamba lakini hatari sana akagundua ana ujuzi mkubwa wa kareti.

Zola hakutaka kupoteza muda wake japo alijuwa Msichana huyo ni hatari sana kwake, akakunja mguu na kutupa teke lililofika hadi kwenye mbavu za msichana huyo ambaye aliudaka mguu wa zola kisha akaukunja na kumsababishia Zola maumivu mkali, akapigwa kwenye ngoko ndipo Zola alipotoa sauti ya maumivu, akauvuta mguu haraka ili usivunjwe, akawa na maswali mengi kichwani aliyotaka kumuuliza Msichana huyo lakini aligundua kuwa hana muda wa kupoteza hapo.

Akaweka mikono yake vizuri ili aweze kutupa shambulio, Malaika akajirusha na kutua kwenye mikono ya Mzee Zola ambayo ilikuwa imekazwa, kisha akavingirika na kumpa teke la uso Mzee Zola akaangukia pembeni, akamfuata na kuanza kumpiga sehemu ya tumbo huku akimwambia

“Wewe ni mahiri sana kwa upelelezi lakini mwisho wa kuifanya kazi hiyo ni leo, nakuuwa Hapa ili kupeleka ujumbe kwa aliyekutuma” Zola alikuwa akigugumia kwa maumivu, haraka akauvuta mguu wa Malaika na kumuangusha akapata muda wa kujipanga upya,,, safari hii Zola hakuwa na bahati kabisa, Malaika aliutumia ujuzi wake wa mapigano na kumpiga kisawa sawa Zola hadi akatema Damu, akamuinua na kumkaba shingoni huku akiwa amemgandamiza ukutani, Zola akaitumia nguvu chache iliyobakia akampiga teke sehemu nyeti ikawa auheni kwake, Malaika akaanguka chini haraka akajiokota, ni kama vile alikuwa amemchokoza basi Zola alikutana na Ngumi za uso mfululizo hadi akachanganikiwa

Akajikuta muda mchache ameanguka chini na kushindwa kuinuka, Malaika alipoona Zola hawezi tena kurudisha majibu ya mpambano huo uliopigwa kisiri ndani ya Hoteli hiyo, akavua sura ya Bandia ndipo Zola akapata kuiona sura halisi ya Mwanamke huyo.

“Naitwa Malaika! Najua huna uwezo wa kufanya chochote hapo Zola sababu zimebakia sekunde chache nikupoteze, kama ulifikiria kuwa mtaweza kupambana na Mafia Gang basi huu uwe ujumbe kwa wajinga wenzako, Mtakufa wote endapo mtaendelea kutufuatilia” Malaika akachomoa kisu chake kutoka katika mfuko wa koti alilovaa, akamsogelea Mzee Zola akamwambia

“Kwakuwa umefanikiwa kunijuwa basi huna haki ya kuendelea kuishi” Malaika akanyanyua kisu ili amchome Zola sehemu ya moyo, Ghafla alisikia mlango ukifunguliwa huku risasi zikimiminwa mfululizo, akajirusha na kuanza kukimbia kwa kuzikwepa hadi akazama kwenye korido, alikuwa ni Mzee Dawson ndiye aliyemsaidia Zola pale vinginevyo Zola angeuawa pale.

“Pole Zola” alisema huku akiwa amempa mkono Zola aweze kusimama, akamsaidia akasimama kisha Dawson akaiendea Bastola ya Zola ambayo ilikuwa sakafuni akampatia

“Mshenzi yule alikuwa anaondoa uhai wangu na kama sio wewe basi mgekuja kuchukua maiti yangu hapa”

“Bado siamini kama msichana yule amekukalisha chini Zola!”

“Dawson! Niliposikia hadithi ya yule Msichana ya kuuwa polisi zaidi ya 15 katika kituo cha polisi nilifikiria ni utani lakini leo nimeamini kwanini aliwashinda polisi, ana ujuzi wa Kareti kitu ambacho ni hatari zaidi kwetu”

“Oooh!! Mungu wangu, hatuna muda wa kupoteza hapa, tuondoke” Alisema Mzee Dawson, mara moja wakashuka hadi chini kila mmoja akaingia kwenye gari yake na kuelekea alipopafahamu.

Zola alikuwa na hasira sana akiwa ndani ya gari, kupigwa na Malaika kulimuumiza sana lakini alifanikiwa kuijua sura halisi na jina la huyo Mwanamke ambalo ni Malaika, akili yake ikamtuma aelekee kituo cha polisi, Mkono mmoja ulikuwa na maumivu makali sana lakini alijikaza, alichotaka kujuwa ni mafaili gani yule Malaika aliyaiba ndani ya kituo cha polisi, akaambiwa kuwa mafaili hayo yalikuwa ya kesi moja iliyoshikiliwa na kitengo cha Ikulu.

Kesi hiyo ilimuhusu jamaa mmoja aliyeitwa Jamaal, ambaye alikamatwa siku moja baada ya tukio la kuuawa kwa Makam wa Rais kutokea, Historia ya jamaa huyo ilimuelezea kuwa ni Mtu aliyepitia mafunzo maalum ya kijeshi ya ulengaji wa shabaha ya masafa marefu na upiganaji, alikamatwa katika uwanja wa ndege baada ya msako mkali uliokuwa ukiendelea.

Baada ya kumnasa walikuta Bunduki na risasi ambayo ilitumika kumuuwa makam wa Rais, moja kwa moja alishtakiwa kwa kosa hilo na kufungwa kwa siri katika gereza moja la siri sana, Jamaal alikutwa na vitambulisho vilivyomuonesha kuwa ana Uraia wa Nchi nane ikiwemo Marekani na Ukraine jambo ambalo liliwashangaza sana lakini Jamaal alizungumza lugha nyingi vizuri sana japo alikuwa na asili ya Somalia. Pia taarifa ilienda mbali zaidi na kusema kuwa Jamaal alikutwa na vitambulisho vya kijeshi vilivyoonesha kuwa aliwahi kulitumikia jeshi la Israel na Palestina ndani ya miaka miwili,

Zola alikaa chini na kujishika kichwa chake kisha akauliza

“Kwasasa Jamaal anashikiliwa gereza gani?” Swali hili lilimfanya polisi aliyekuwa akimueleza Zola akae kimya kidogo kisha akasema

“Gereza lipo Ikulu ya Nchi, sisi hatuhusiki tena na kesi hiyo Zola” Zola akauliza tena

“Kwanini mafaili ya kesi bado yalikuwa hapa?”

“Kwasababu kesi ilianzia hapa lakini cha kushangaza baada ya kukamatwa tuliondolewa katika kesi hiyo”

“Nani alitoa oda ya Nyie kuacha hii kesi na ikaenda sehemu nyingine wakati nyie ndio mnakazi hiyo?”

“Aliyetoa oda ni Rais wa Nchi” Zola aliondoka baada ya kupata majibu yaliyochanganya akili yake kisha akawasiliana na Mzee Dawson wakapanga kukutana katika makazi ya siri ya Zola, Usiku Dawson alienda kuonana na Zola, kama kawaida yao waligida pombe ili maongezi yaanze

“Enhee umegundua nini Zola?” Aliuliza Dawson

“Mafaili yaliyobiwa katika kituo cha polisi yalikuwa ya kesi ya Mtu anayedaiwa kuwa alihusika kumuuwa Makam wa Rais” Alisema Zola

“Unasemaje? Ina maana polisi wanajuwa ni nani alihusika?”

“Sio polisi pekee hata Mkuu wako wa Nchi ambaye anakupa kazi ya kulisaka kundi la Mafia Gang anajuwa na kibaya zaidi ametoa amri ya jeshi la polisi kuiacha kazi hiyo” Mzee Dawson alionekana kushangaa sana

“Inawezekanaje Zola?”

“Hiyo ndio hali halisi ndio maana nimekuita hapa ili tuzungumze, nahisia mbaya juu ya Mkuu wa Nchi lakini sitaki kujiaminisha chochote”

“Unataka kusema Mkuu wa Nchi kuna kitu anakificha hapa?” Wote waliacha kunywa pombe wakazama katika maongezi yao
 
Ilipoishia “Inawezekanaje Zola?”

“Hiyo ndio hali halisi ndio maana nimekuita hapa ili tuzungumze, nahisia mbaya juu ya Mkuu wa Nchi lakini sitaki kujiaminisha chochote”

“Unataka kusema Mkuu wa Nchi kuna kitu anakificha hapa?” Wote waliacha kunywa pombe wakazama katika maongezi yao Endelea

SEHEMU YA SITA

“Kama hausiki kwanini atoe amri kwa jeshi la polisi? Kwanini Mtuhumiwa afungwe katika Gereza lililopo Ikulu?” Alihoji Zola huku Dawson akionesha kuanza kuvuta picha ya maelezo ya Zola.

“Mimi nafikiria kwasasa tujikite zaidi na upelelezi kuhusu Mafia Gang, hili jambo tuliweke kiporo Zola” Alisema Mzee Dawson, ni wazi kilichomfanya akae kimya kwa muda mrefu kilikuwa ni hicho.

“Wewe ni mwalimu mzuri sana Dawson, kuliacha hili jambo ni sawa na kumega Mkate alafu ukajiaminisha kuwa hakuna kilichotoka, umefundisha vijana wengi masuala ya upelelezi na Ujasusi, sidhani hata hicho unachokizungumza kinatoka katika akili yako, sitaki kuamini pia kuwa pombe imekuingia kiasi hicho. Ili tuukate huu mti ni lazima tukubali kung’oa mizizi ya Mti wenyewe ili usichipue tena”

“Zola tunaanzia wapi kumpeleleza Mkuu wa Nchi ambaye ndiye ametupa kazi hii, kama hili kundi lina maslahi kwake kwanini ameagiza tulifyeke? Nachelea kusema anaweza kuwa hausiki hapa” Alisema Dawson huku macho yake madogo kama ya paka yaking’aza huku na kule, pombe ilikuwa ikishuka kwenye koo lake lenye koromeo kubwa, kisha alibakua

“Ni bora kuachana na kazi hii Dawson kuliko kuruhusu dosali kwenye upelelezi huu, nimeweka Maisha yangu rehani, mwenyewe umeona nilitaka kuuawa kama sio wewe kuwahi kuniokoa, tukubaliane hapa kuwa Rais apelelezwe kuhusu Mfungwa aliyefungwa magereza ya Ikulu” Ulikuwa ndio msimamo wa Zola, Dawson alimuamini sana Zola akamwambia

“Kama ni hivyo basi uwanja ni wako Zola, siku ukithibitisha kuwa Rais anahusika na Mauwaji haya utanijulisha,” Ilikuwa ndio kauli ya mwisho ya Dawson, umri wake ulionesha ni jinsi gani alikuwa akipambana na akili za uzee alizonazo licha ya kuwa ni Mtu aliyeaminiwa sana na Idara ya Usalama wa Taifa, akamuaga Zola huku akimuachia ujumbe kuwa

“Wakati unawatafuta wao wapo macho wanakutafuta” Alisema kisha alijizoa na kuondoka pale kwa kutumia gari yake ya kifahari, licha ya uzee lakini alimudu kuliendesha mwenyewe. Muda huo mvua ilikuwa ikinyesha, Zola akawa anamtazama Dawson kupitia dirisha la kioo, Mzee Dawson alikuwa fundi wa kuendesha gari jambo lililomchekesha Zola akajikuta akisema

“Ng’ombe huyu amegoma kuzee Maini yake” Akarudi kuketi huku akizidi kutafakari, akamkubuka rafiki yake Mmoja aliyeitwa Sande Olise aliyekuwa uhamishoni Nchini Botswana, alipomkumbuka alijikuta akitabasamu kisha akaenda ukutani ambapo kulikuwa na picha waliyopiga pamoja.

Sande Olise alikuwa ni miongoni mwa Wanafunzi waliopelekwa Nchini Mexico kujifunza masuala ya upelelezi, Sande alipishana umri wa miaka saba na Zola, tabia zao za kupenda wanawake ndizo zilizowafanya wakafahamiana, akakumbuka Jinsi walivyopigana vita vya kukiokoa kisiwa kimoja kilichopo Nje kidogo ya Mji Mkuu, kisiwa hicho kilivamiwa na Waasi kutoka Nchi jirani na kukiweka chini ya Ulinzi kwa zaidi ya siku saba.

Zola alikaa chini akafikiria kumpigia simu Sande Olise, alipekuwa baadhi ya nyaraka fulani akakuta namba ya Sande kisha akampigia huku akitabasamu. Simu ilipokelewa huku sauti nzito ilisikika upande wa pili

“P045 Olise! Kuna mpango maalum?” Alichofanya Zola alipiga simu ya Sande kwa kutumia namba maalum za siri, Wapelelezi wote walikuwa na simu za siri hivyo Sande alipoona simu hiyo alijuwa kulikuwa na shida mahali, japo sauti yake ilionesha kuwa alikuwa ameamshwa na simu ya Zola lakini alikaza sauti yake

“P102 Zola! Over..” Alisema Zola

“Over!! Zola, za miaka mingi rafiki yangu” Alisema Sande Olise huku ile sauti ya ukakamavu ikiwa imetoweka baada ya kugundua aliyekuwa akimpigia alikuwa ni rafiki yake kipenzi, Mafunzo waliyoyapokea huko Mexico waliambiwa kitu pekee wanachotakiwa kukiepuka ni urafiki sababu usaliti wa Nchi huanza kirafiki hatimaye kuwa janga la Taifa, hivyo waliheshimu misingi hiyo, ndiyo sababu ya kukaa Miaka mingi bila kuwasiliana.

“Nzuri ndugu yangu Sande, upo wapi siku hizi?” Alihoji Zola “Nipo Botswana uhamishoni, nina kitengo cha siri huku”

“Pole kwa majukumu! Ulisikia juu ya kifo cha Makam wa Rais na Matukio yanayoendelea huku?”

“Nimesikia Zola, najua Mtaalam wa kazi utakuwa upo mzigoni, lakini hao mnaopambana nao sijui kama ni saizi yenu, walikuja huku Miaka mitatu iliyopita lakini balaa lake ni kubwa sana, wameuwa makomando 50, na taarifa nyingine zimefichwa” Yalikuwa ni maelezo ya Sande Olise

“Sande hali ni tete sana, hili jambo ni zito na hawa jamaa wana mtandao Mkubwa sana Duniani, kupambana nao ni sawa na kutupa jiwe gizani, wanauwa kama hawana akili nzuri”

“Ha!ha!ha!” Alicheka Sande

“Mbona unacheka Sande”

“Hao jamaa wanamafunzo maalum nasikia Mkuu wao anaitwa John Brain, huyo Brain ndiyo mwalimu wa Osama Bin Laden, anajihusisha pia na Alqaeda…Ni ngumu kumtambua kwa sura ila alama kubwa ni vidole viwili wanavyoviacha wakiwa wamefanya mauwaji, Mimi nipo Uhamishoni, majukumu yamepungua nakula bata tuu sababu Mimi huku ni Bosi” Alisema Sande, lengo kuu la Zola lilikuwa ni kumshawishi Sande arudi Nchini ili washirikiane kupambana na Mafia Gang sababu Sande ni Mtu pekee anayeweza kumuamini

“Sande lengo langu la kukupigia na kuhitaji msaada wako katika kazi hii ngumu niliyonayo, kuna uhusiano Mkubwa sana kati ya Rais wa Nchi na hawa Mafia Gang, ni hatari kwa sasa, siwezi kuinusa kwa pua zangu”

“Unataka nije kufa huko? CCP ina Wanafunzi wengi tulioenda Mexico kipindi kile, ni Mimi tu Zola?”

“Hadi nakupigia wewe nina uhakika kazi hii tutaiweza kabla mambo hayajaharibika zaidi, ujio wako utakuwa wa siri sana ili tupeleleze kwa kina ni jambo gani lipo nyuma ya kapeti”

“Ooh! Zola unajuwa siwezi kukukatalia, nitakujulisha nipe siku tatu”

“Over!”

“Over!” Simu ilikatika mara moja, Zola akawa na tumaini la Ujio wa Sande Olise ambaye waliwahi kumuita Duma wakimaanisha ni Mtu mwenye kufanya mambo kwa haraka sana.

Zola akaelekea kitandani na kujipumzisha huku picha ya Rais ikiwa katika macho na akili yake, alimuwazia Rais huyo. Akiwa bado hajapata Usingizi Zola alipokea ujumbe wa simu kuwa Askari aliyezungumza naye na kumpa taarifa juu ya Mfungwa aliyefungwa katika Gereza la Ikulu ameuawa kwa kupigwa Risasi akiwa ndani ya Kituo hicho, alishtuka kisha aliamka na kuwasha taa, muda huo huo simu kutoka kwa Dawson iliingia

“Zola umeisikia hiyo taarifa?” Aliuliza Dawson

“Ndio nimeipata muda huu” Alijibu Zola kisha simu ilikatika

“Uuups!” Zola alivuta pumzi zake, taswira mbili zilimjia kwa haraka haraka kuhusu mauwaji yale, upande mmoja ulimwambia kuwa Rais ndiye aliyekuwa akihusika na mauwaji yale lakini upande mwingine ulishindwa kumpa majibu ya kwanini Mafia Gang wanafanya matukio yale, Kichwa chake kiliwaka moto.

Asubuhi mapema aliamka na kueleka kituo cha polisi, akakuta hali ya huzunii ikiwa imetanda miongoni mwa polisi, Zola akauliza ni Nani aliyefanya Mauwaji yale, cha ajabu alikuwa ni mmoja wa polisi ndiye aliyemuuwa yule polisi, Zola akashika kiuno chake kwa mshangao, akapelekwa alipohifadhiwa Askari Muuwaji, hakutaka kuzungumza na Askari huyo akamwambia polisi mmoja amletee Mafaili ya kesi iliyowahusu Robert, Sandra na Bosco sababu ndio chanzo cha kuingizwa yeye katika majukumu yale mazito, akaondoka kituoni na kurudi katika Makazi yake ya siri, akayachoma moto mafaili hayo huku akiamini kuwa matukio yote yale yalifanywa kwa lengo la kupumbaza jeshi la polisi ili wasijikite zaidi, walifanikiwa kuwapoteza lakini Zola aliinusa hatari hiyo huku akijiuliza Mafia Gang wanataka nini katika Nchi yao.

Muda huo huo Hekeheka ndani ya Kichwa Cha Zola iliongezeka, alijikuta akiwa katika hali ambayo ilihitaji matumizi makubwa ya akili kuliko chochote kile. Kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka kwenye paji lake la uso, picha ya askari aliyeuawa ilizunguka katika akili yake huku akijiuliza ni nani alitoa maagizo ya Askari yule kuuawa, alijuwa fika kuwa askari aliyemuuwa Askari mwenzake alishinikizwa kufanya hivyo, bado aliamini Rais alikuwa mhusika namba moja wa mauwaji yale, akatoka nje huku akiwa anatazama taswira ya jua lilivyokuwa likichangamsha bustani yake ndogo katika Makazi yake, pembezoni kulikuwa na njiwa waliokuwa wakiruka na kulia kwa kupokezana.

Zola akaingia kwenye gari yake, akaelekea kituo cha polisi, safari hii alihitaji kumbana askari yule aliyemuuwa mwenzake, akaelekea chumba ambacho alihifadhiwa askari huyo kisha akaomba polisi wote waondoke, wakabakia wawili tuu.

Zola alimtazama askari aliyekuwa akimtazama Zola kwa sura kavu iliyojaa umakini, hakuonekana kujuta kwa kitendo kile hata kidogo, Zola akamshika kichwa Askari huyo akamuuliza

“Nani amekuagiza umuuwe Askari mwenzako?” Aliuliza Zola huku akizidi kuvuta nywele za Askari huyo aliyefungwa pingu mikononi kwa nyuma

“Nani yupo nyuma ya tukio hili? Sababu najuwa huwezi kufanya hivi pasipo agizo maalum, huyu Askari alinieleza siri aliyoijuwa….Nina imani hata wewe unaijuwa hiyo na ndiyo sababu ya kumuuwa Askari mwenzako!!” Aliuliza tena Zola baada ya kuona swali la kwanza halikujibiwa

“Fanya uliwezalo Zola, fanya tuu lakini siwezi kukwambia chochote zaidi tu ya kusema, nimemuuwa bila kuagizwa na Mtu yeyote” Zola akachukua rungu la polisi akawa anampiga polisi huyo sehemu za mbavu ili kuhakikisha anasema ni nani aliyemtuma kufanya mauwaji ndani ya kituo hicho cha polisi. Askari huyo alikuwa akipiga kelele za maumivu, Zola aliendelea kumpiga hadi akawa anatema damu mdomoni, Zola alionekana kujawa na jazba sana. Muda huo simu yake iliita, ikawa auheni kwa Askari huyo ambaye alikuwa akipunguza sauti ya kulalamika.

Zola akatupa lile rungu chini kisha akasogea ukutani akaipokea simu hiyo ambayo ilimfanya Zola kwanza awe mtii, mwenye kufuata maagizo, simu hiyo ilitoka ikulu, Zola alikuwa akizungumza na Rais aliyeitwa Jacob Zagamba.

“Nakuja Mkuu” Alisema Zola kisha simu ilionekana kukatika, kijasho kilichokuwa kinamtoka Zola kilimwagika hadi kwenye singlendi yake nyeupe

“Shiti!!” Akasema kisha akamtazama yule Askari ambaye alikuwa akicheka kwa maumivu makali, Zola akachukua shati lake kisha akaondoka pale mara moja. Safari hii Zola alikuwa akielekea Ikulu kuitika wito wa Rais wa Nchi hiyo, akiwa kwenye gari akawasha Intaneti kisha akampigia simu ya Video Sande Olise aliyeko Botswana, bahati nzuri simu ilipokelewa haraka sana na Sande Olise

“Sande!! Mkuu wa Nchi ameniita, naelekea Ikulu sasa” Alisema Zola huku akiendelea kukanyaga mafuta kuelekea Ikulu.

“Nayaamini maneno yako, kuna mawili unaweza itiwa hapo, moja kuhamishwa kwenda Nchi nyingine au kuonywa”

“Kwa vyovyote Rais ni mhusika nambari moja wa Matukio yote, hajui kama ninafanya kazi na Dawson” Alieleza Zola

“Safi sana! Mchezo umeisha hapo, soma kauli yake kisha jiongeze Zola….Kifo chako kinaweza kutokea leo baada ya kukoswa sana Miaka mingi tulipokuwa tukifanya Operesheni Upepo, ulikuwa Simba usiyejulikana unayelipigania Taifa lako, Dawson anahitaji pongezi kwa kuwaficha Askari tunao tumika kwenye idara kwa siri sana vinginevyo tungekuwa tunakufa kama Kuku huku tukizungukwa na siasa Chafu” Ilikuwa ni sauti ya Sande Olise akizungumza kwa unakini mkubwa.

“Kama Maisha yangu yatakoma leo Ikulu, Sande uje kufanya hii kazi kuliokoa Taifa mara moja” Alisema Zola kisha chozi lilimtoka, akakata simu hiyo. Visa vya baadhi ya Askari kupotea vilikuwa vingi katika Taifa hilo, Zola baada ya Masaa mawili alikuwa akikaguliwa kwa ajili ya kuingia Ikulu, ilikuwa ni mara ya kwanza Zola kuitwa na Rais huyo, si Rais huyu Pekee bali Zola hakupata kujulikana na Rais yeyote aliyepita, hii ilimpa shaka sana Zola kwanini Rais ampigie simu wakati ambao alikuwa akimbana yule Askari amwambie ukweli kuwa Nani anafanya Mauwaji yale.
 
SEHEMU YA SABA

Upande wa Sande Olise, Chozi la Zola lilimkumbusha mbali sana wakati huo Zola alipokuwa akiogopa kwenda kufanya mafunzo hayo ya Ujasusi na Upelelezi Nchini Mexico, mafunzo hayo yaliambatana na Mafunzo ya Ukomando, Sande ndiye aliyemshawishi Zola kuingia huko laiti kama asingelimshawishi basi Zola angekuwa Askari wa kawaida kabisa, Mafunzo haya hufanywa siri sana, kitengo cha siri cha Mzee Dawson ndicho kilichokuwa kikifanya uchaguzi wa nani aende na Nani asiende hivyo Dawson alificha sana majina ya Askari wake wa siri ambao ndio alikuwa akiwatumia kwenye majukumu mazito ambayo Serikali ilimpa, haraka akafungua Kabati lake lililo chumbani kwake akaitoa simu ya Siri ambayo ilitumika kwa ajili ya Mawasiliano yao ya Kiaskari, akampigia Mzee Dawson.

Mzee Dawson ( Google ) aliposikia sauti ya Sande alijuwa kulikuwa na tatizo, akameza funda zito la Mate, sauti hiyo hakuisikia kwa miaka mingi sana. Licha ya kuwa ni Mmoja wa vijana wake wa Kitengo lakini Sande alikuwa Botswana kwa miaka mingi mno, alipojitambulisha ndio Mzee Dawson akapata kujihakikishia zaidi

“Sande! Bado unanikumbuka?” Alisema Dawson kwa sauti iliyojaa wasiwasi sana huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio, mara nyingi hakuwa akipokea simu za siri sababu yeye ndiye aliyekuwa akiratibu kazi za Kijasusi hivyo yeye ndiye aliyekuwa Mpigaji mara zote kutafuta vijana wake, leo alitafutwa yeye na Sande!!

“Naam! Mkuu wa Kitengo, Mimi ni P045! Simu ya dharura, narudi Nchini kwa kazi maalum, nahitaji Baraka zako!!” Ilikuwa ni sauti iliyojaa uzalendo na ujasiri wa hali ya juu uliombatana



na Utii sababu licha ya Mzee Dawson kuwa Mkubwa kiumri bado alikuwa ni Askari mwenye Cheo kikubwa sana! Alikuwa ni kama Baba yao mzazi kwenye kazi za Kijasusi.

“Zola amewasiliana na wewe?” Aliuliza Dawson

“Ndio, yupo hatarini. Maisha yake yapo mikononi mwa Rais Zagamba, narudi kumkomboa” Alisema Sande

“Uuuupss!!”

“Ndio Mkuu! Kwasasa Mkuu wa Nchi anawinda maisha ya Zola, ni ngumu kujuwa kama atatoka salama sababu yupo njiani anaenda Ikulu ameitwa na Rais” Kauli hii ilimpa mshituko Mkubwa sana Mzee Dawson,

“Tuongee baada ya dakika chache” Alisema Dawson, kisha alikata simu hiyo. Mara moja kanyanyua simu yake akampigia Zola ili kuthibitisha alichokisia, Simu ya Zola ilikuwa imezimwa.

“Shit!!” Akasema Dawson kisha akatoka nyumbani kwake akaelekea Ikulu, Sande alikaa kusubiria simu ya Mzee Dawson!!

Alipofika Ikulu, Dawson alikaguliwa kabla ya kuruhusiwa, moja kwa moja akaelekea ofisini kwa Rais, akamsimamia Rais na kumpigia Saluti kisha akaketi kwa heshima

“Dawson!! Kwanini umekuja kama Mkimbizi kutoka Somalia?” Alihoji kwa dhihaka huku akiwa anaandika kitu

Dawson alimtazama Rais Jacob Zagamba huku akili yake ikipingana na mawazo yake juu ya kuuliza kuhusu Inspekta Zola, hakutaka ijulikane kuwa Zola ni Askari wake wa siri wa Kitengo

“Nimekuja tuongee kuhusu Hii kesi”

“Umefikia wapi Dawson?”

“Bado uchunguzi unaendelea lakini nimefikia mahali pazuri sana na siku si nyingi nitakupa mrejesho kuhusu Kundi la Mafia Gang” Alisema Dawson huku macho yake yakionesha kuwa sicho kilichompeleka pale.

“Dawson nahitaji hili jambo ulimalize ndio maana nikalileta katika Meza yako, ninachotaka kusikia siku moja ni kuwa umeuwa Wahusika wote na kuileta miili hapa, hao Watu hawatakiwi kuishi kabisa” Alisema Rais na kumpa maswali Dawson, kwanini Rais atake Watu hao Wauawe?

“Nitawakamata kisha watahukumiwa kufungwa kifungo cha Maisha, hiyo ni ahadi yangu kwako Mkuu” Rais akamtazama Dawson kwa hasira kisha akagonga meza

“Nimesema nahitaji Miili yao, fyeka kundi hilo haramu na mazalia yake hapa Nchini, Dawson narudia tena nahitaji miili yao, hawana kesi ya kujibu….hili jambo linapaswa kufanywa siri, kinachotakiwa ni kuwa Watu hao wakifa basi vifo vitakoma, hakuna atakayeuliza wako wapi, haya ni maagizo yangu” Alisistiza Rais, muda huo akaingia Jamaa mmoja mweusi aliyepanda Hewani, alionekana kuwa ni Usalama wa Taifa, Rais akamuuliza Mtu huyo

“Safari inaanza?”

“Ndio Mkuu” Alijibu kwa Utii, kisha Rais akachukua funguo ya gari akampatia jamaa huyo, Dawson hakuelewa kilichoendelea pale japo hakujuwa Zola yupo wapi.

Baada ya jamaa huyo kuondoka Dawson akaaga ili aweze kuondoka

Alipofika karibu na Lango kuu la Ikulu alikutana na walinzi wawili ambao ni dhahiri walikuwa wakimsubiria yeye ili wamtoe nje, alipowafikia walimpa ishara kuwa wao walikuwa wanamsubiria, Dawson akatupa macho yake huku na kule, Milango mingi ilikuwa imefungwa, walinzi hao ambao walivalia suti nyeusi waliongozana na macho makali ya Dawson ili kujuwa alikuwa akiangalia nini, basi wakampa tena ishara kuwa aongozane nao, wakati anatoka pale mlangoni macho yake yalitupa uangavu kuelekea kwenye maegesho ya Magari ya Ikulu, ndipo alipomuona Jamaa aliyetoka kuzungumza na Rais akiwa amebeba begi kubwa lililomzidi uzito, Dawson alijikuta akiingiwa na shahuku ya kutaka Kujuwa jamaa huyo alikuwa akifanya safari gani. Akawageukia walinzi akawaambia

“Asanteni! Nitafika” Alikuwa na nia ya kuwatoroka ili afanye upelelezi wake sababu bado kichwa chake kilikuwa kinalia alamu kuwa Zola yupo matatizoni,

“Ni wajibu wetu kukufikisha lilipo gari lako” Alisema mmoja wa walinzi hao tena akiwa anatabasamu, walimjuwa vyema Dawson kuwa ni mmoja wa Askari waliotegemewa sana na Kila Rais aliyepita, alikuwa na cheo kikubwa mno, pale pale Zola akapata akili, akakohoa na kutoa damu kitu ambacho kiliwashtua wale Walinzi wakiamini anaumwa, ni kweli Dawson alikuwa anaumwa mapafu yake kutokana na uvutaji wa sigara ila hapa aliamuwa kucheza na akili za Walinzi hao ili awatoroke, taharuki ikazuka pale huku mmoja akijaribu kuita gari ya wagonjwa

“Msijali nahitaji Kitambaa” Alisema Zola kwa sauti yenye kikohozi, Walinzi hawakuwa na kitambaa, mmoja akatoka kwenda kuchukua tishu ili imsaidie Dawson, ulikuwa mtego. Haraka Dawson akajikunjua na kumpiga ngumi kali sehemu ya shingo na kufanikisha kumzimisha pale pale, akamburuza hadi maegesho ya magari yaliyo karibu, Wakati huo yule Jamaa akiwa analipakiza lile begi ndani ya buti.

Akamficha mlinzi yule kwenye maegesho, akaingia kwenye gari yake na taratibu akaanza kulifuata gari hilo ambalo lilikuwa likianza kutoka taratibu kuelekea getini, Naam!! Dawson aliliangalia gari hilo kwa taswira yenye mashaka sana huku akitilia mashaka lile begi, hakuacha hata hatua moja alikaa nyuma ya gari hilo lililokuwa likiingia barabara kuu iliyokuwa ikitoka Mjini, Gari hiyo ilibadilisha uelekeo na kuelekea eneo la Bahari ambako ni nadra sana kuona Magari yakiongoza huko, Dawson alisogea kwa spidi sawa na gari hilo kisha mbele aliona gari hilo likiwa limesimama kando ya Miti ya Mikoko, Dawson akalipita gari hilo makusudi ili kumuaminisha jamaa huyo kuwa yupo peke yake.

Alipofika mbele Dawson alisimama kisha akashuka ndani ya gari akawa anarudi Taratibu liliposimama gari lile alilokuwa akilifuatilia, walikuwa mbali zaidi ya Kilomita 15 kutoka Ikulu, eneo hilo gari chache sana zilikuwa zikipita. Yule jamaa akafungua buti na kulitoa begi kisha akalitelekeza eneo lile, Dawson alikuwa amejificha mahali, jamaa alipoondoka Dawson alisogea na kulifungua.

Alijikuta akianguka kwa Mshituko huku macho yake yakishindwa kuamini alichokiona ndani ya begi hilo, chozi lilianza kumbubujika Dawson, aliuwona mwili wa Inspketa Zola ukiwa ndani ya begi hilo, Dawson alijikuta akiwa amepoteza mmoja wa Maaskari wake wa siri ndani ya Kitengo hicho, alilia kwa uchungu sana! Maisha ya Inspekta Zola yalikuwa yametamatishwa ndani ya Ikulu, mwili wake ulikuwa na vidonda na matundu ya risasi, Dawson akalifunga begi hilo kisha akalivuta hadi kwenye gari yake akaliweka kwenye buti akaondoka na mwili huo.

Akiwa barabarani alionekana kuwa na hofu, nyuma yake kulikuwa na lile gari lililotoka Ikulu lilikuwa likimfuatilia kwa nyuma, Dawson aligundua hilo haraka akafanya ujanja ili kulipoteza lakini gari hilo lilikuwa bado nyuma ya Dawson kwa zaidi ya kilometa 35 kutoka usawa wa Bahari ambako aliuokota mwili huo ndani ya begi, Dawson alichofanya ni kutembea kwa mwendo wa kawaida ili apambane na Mtu aliye ndani ya gari hilo baada ya kuhisi kuwa hakukuwa na usalama wa Maisha yake, alisogea kwa umbali ndipo akaona kuna uzio wa Polisi waliokuwa wakifanya msako barabarani, Dawson akagundua kuwa kuna mchezo umechezwa ili yeye apotee, haraka akabadilisha uelekeo na kuingia Barabara ya pili ambayo ilikuwa ya vumbi kisha akaenda kutoka barabara nyingine, muda huo gari lile lilikuwa nyuma yake.

Dawson alikuwa na sifa kubwa juu ya ujuzi wa kuendesha magari, sifa ambayo Zola aliwahi kuishuhudia siku moja alipotembelewa na Dawson, Naam! Akaongeza spidi kwa haraka akachomoka kama ndege ya kivita, alifanya hivi makusudi ili kulipoteza gari lile lililotoka Ikulu, dakika chache alikuwa amesha lipoteza, akasogea hadi karibu na jengo moja chakavu sana, Dawson aliona sasa Maisha yake yanaweza kuingia dosari, aliona kuna kila dalili kuwa Rais alikuwa na lengo la kumpoteza baada ya kufanikisha kumfyeka Zola pale Ikulu, japo alikuwa Mzee lakini nyakati hizi mbaya alijitahidi kulibeba begi lenye mwili wa Zola akapanda nalo juu ya jengo hilo la ghorofa ambalo lilikuwa halijaisha.

Hadi anafika juu alikuwa hoi, akajikuta akianguka chini kisha akatoa simu yake yenye mkonga kutoka katika mfuko wake akapiga mahali.

“Sande! Zola ameuawa Ikulu muda mchache uliopita” Alisema Dawson huku akijifuta jasho, jioni ilikuwa ikiingia

“Unasemaje?” Ilisikika sauti ya Sande upande wa pili

“Ndio hivyo, mwili wa Zola nipo nao hapa lakini hata Maisha yangu yapo hatarini, huyu Rais ni Mtu hatari kuliko inavyodhaniwa” Ilikuwa ni sauti iliyotoka kikomavu sana, Ghafla akasikia mchakacho, Dawson akakimbilia sehemu yenye uwazi kwa ajili ya kuchungulia chini, akaliona lile gari jeusi lililotoka Ikulu, ni wazi kuwa Rais alituma Mtu kwa ajili ya kumfuatilia Zola

“Mkuu mbona Kimya?” Aliuliza Sande Olise baada ya kuona ukimya umetawala

“Nacheza sarafu ya Kifo Sande!” Akakata simu mara moja baada ya kuwa ameshamuelekeza Sande, mara moja akatafuta sehemu ya kujificha, begi lile lilikuwa katikati ya chumba kimoja.

Hakuwa Mtu mmoja bali walikuwa wawili wakiwa ndani ya suti nyeusi, mmoja akiwa amevalia miwani nyeusi na mwingine akiwa na macho makavu sana, sura zao zilimtambulisha Dawson kuwa Watu hao walitoka Kitengo cha Usalama wa Taifa Ikulu, Dawson alishazoea Maisha ya kuwindana akavuta pumzi zake mara moja kisha akajikunja mithiri ya nyani Mzee huku Mgongo wake ukiwa umevunjika vilivyo, masikio ya Dawson yalikuwa makini sana kusikiliza hatua za Wataalam hao ambao wazi walikuwa na mafunzo maalum na walijuwa wanamtafuta Mtu wa namna gani, jinsi walivyokuwa wakipishana huku wakilindana ilimfanya Dawson afunge kiwambo cha kuzuia sauti ya Risasi kusikika.

Hata kabla Dawson hajafyatua Risasi, alisikia mlio wa gari ya polisi, kisha hatua za jamaa wale kukimbia zilisikika, Haraka Dawson akaenda kuchungulia akawaona jamaa hao jinsi walivyokuwa wakidanda kushuka chini kama nyani, akashusha pumzi zake kisha akili ya kujuwa afanye nini ili polisi wasiukute mwili wa Zola ilimjia, kando yake kulikuwa na dirisha lililokuwa na mabomba mawili yaliyoshuka hadi chini, akajivuta haraka akalibeba begi na kuteleza nalo hadi chini kisha akajificha nyuma ya kichaka kwa umakini zaidi sababu alijuwa maadui zake walikuwa eneo hilo, akanyata huku akiwa amelibeba begi akakatiza mtaro wa maji machafu akaenda kutokezea Barabarani akasimamisha Bajaji na kutokomea zake, Jamaa wale walipofika hawakujuwa Dawson aliondoka vipi pale, mmoja akavuta simu na kupiga mahali

“Mkuu!! Dawson ameyeyuka” Alisema kwa utii huku mkono wake uliobeba simu ukiwa na misuli na Glove!

“Mnamjuwa huyo Mtu vizuri, hakikisheni hachomoki” Ilikuwa ni sauti ya Rais Zagamba ikisikika katika sikio la Jamaa huyo

“Sawa Mkuu!” Aliitikia kisha alikata simu.

MSAKO GIZANI

Malaika, Six na John Brain baada ya kuona imekuwa ngumu kwao kumpata Mtu wao ambaye walihangaika Nchi nzima katika vituo vyote vya polisi bila mafanikio, waliuwa Maafisa wengi wa polisi ili kumtisha Rais aamuru kuachiwa kwa Mtu wao ilishindikana. John Brain akaja na Mpango wa kutaka kusambaza Ugonjwa hatari wa Ebola, Kabla ya kuanza kwa mpango huo John Brain alimpigia simu Rais ili kumtaka amuache Mtu wao haraka sana.

Kilichowafanya Mafia Gang kuendelea kuwepo Nchini ni Mtu wao ambaye alikamatwa, kesi iliyokuwa ikimkabili Mtu huyo ilikuwa ni kesi ya Mauwaji ya Makam wa Rais. Muda huo Rais alikuwa nyumbani kwake Ikulu akitafakari nini cha kufanya baada ya kumkosa Dawson ambaye sasa alikuwa ameshaupata mwili wa Zola na kwa vyovyote Dawson atakuwa ameifahamu siri ya Mauwaji yanayoendelea kutokea, mezani alikuwa na kikombe kidogo cha Kahawa ambacho kilikuwa kikitoka mvuke kuashiria kuwa Kahawa ilikuwa ya moto sana.

Simu ilipoita ilikuwa imemzindua kutoka Mawazoni, akaangalia ni nani aliyekuwa akipiga akaona ni John Brain. Akalamba midomo yake kabla ya kupokea huku akiwa anaelekea Chooni.

“Kazi yako imeshaisha, tumekutoa katika kesi ya wizi na ufisadi ambayo ushaidi alikuwa nao Makam wa Rais, kilichobakia kilikuwa ni kutupa Pesa zetu lakini cha ajabu unamshikilia Mtu wetu hadi hivi leo, tumekupa taarifa kupitia vifo vingi tulivyovisababisha lakini inaonekana hujataka kuelewa”

“Brain! Tukae mezani tulizungumze hilo”

“Michezo ya kitoto isiwepo tafadhali, kama utashindwa kukubaliana na sisi basi tutahakikisha unang’oka madarakani” Alisema John Brain

“Usijali Brain, hakuna kitakacho haribika” Rais alipotoka Chooni alisimama kando ya mlango, Mlinzi wake alisogea na kumuuliza kama yupo sawa!

“Hakikisheni Dawson anauawa haraka iwezekanavyo” Yalikuwa ndio maagizo pekee aliyoyatoa Rais kisha akarudi ofisini kwake.

Mzee Dawson, akiwa ndani ya Bajaji alitafakari mambo mengi aliyoyafanya na Rais huyo, jinsi alivyotumika kwa ajili ya Taifa, hakuwahi kufikiria kama Rais angelikuwa ndiye tatizo. Alijikuta chozi likimdondoka baada ya kulitazama begi hilo ambalo lilikuwa na mwili wa mmoja wa Askari wake wa siri sana, akapiga simu sehemu kisha akatoa maagizo fulani ya siri ambayo ni lazima uwe kwenye mfumo wake ili uweze kuelewa, hata dereva bajaji aliachwa njia panda, kisha akageuza na kumpigia simu Sande Olise.

“Sande ni lazima urejee Haraka sana” Alisema Dawson kisha alikata simu bila kusikiliza jibu la Sande Olise

“Hapo kunja kushoto! Ukiona kibao cha kanisa simama” Alielekeza Dawson, mara moja Bajaji lilifuata maagizo kisha likasimama.

“Pesa yako hii hapa” Dawson alitoa noti ya Elfu kumi na kumpatia dereva kisha akamwambia

“Chenji itakusaidia”

“Asante sana Kaka!!” Dereva alisema kisha akaondoka zake, Dawson alikuwa amesimama mbele ya geti la kanisa hilo. Wakaja Vijana wawili ambao walikuwa wamevalia nguo za kitawa wakalibeba begi hilo huku Dawson akiwa anatokwa na machozi, akawafuata huku vijana hao wakionekana kujuwa nini cha kufanya.

Walitembea na kuingia kanisani, wakasogea hadi kwenye maegesho ya magari, wakaweka begi chini kisha, mmoja akaingia kwenye gari moja iliyokuwa hapo maegesho, akalisogeza mbele kidogo alafu akashuka, Kijana aliyebakia akafunua kitambaa cheusi ambacho kilikuwa chakavu sana, pakaonekana kuwa na andaki fulani, akafungua mlango mdogo uliokuwa na hadhi ya mlango wa kisima cha maji, pakaonekana kuwa na ngazi ya kushuka chini, kisha mmoja akaingia na begi hilo huko chini, mwingine akafuatia kisha Dawson akamalizia, walipofanikiwa kuingia humo, akaja Mwanamke mmoja ambaye naye alikuwa amevalia nguo za Kitawa kisha akafunga ule mlango, akaweka kile kitambaa chakavu na kusali, alipomaliza akaingia kwenye gari na kulirudisha pale lilipokuwa mwanzo, huwezi kugundua kuwa kulikuwa na watu waliozama Ardhini.

Walipofika chini, waliwasha taa ndani ya andaki hilo ambalo Mzee Dawson alikuwa akilitumia kwa ajili ya kazi zake za siri, vijana hao walikuwa ni wanafunzi wake. Mmoja aliitwa Chande na mwingine Kisko, walikuwa ni vijana ambao alitumia gharama zake Binfsi kuwasomesha na kuwapeleka mafunzoni Nchini Korea, walijiingiza Katika kanisa hilo ili waweze kufanya kazi na Mzee Dawson.

Andaki hilo lilichimbwa muda mrefu kabla ya Mzee Dawson kufadhili ujenzi wa kanisa hilo. Ilikuwa ni siri kubwa sana na Watu wengi hawakujua kama kanisani kulikuwa na andaki lililotumika kufanyia kazi za Kijeshi, Mwanamke aliyekuja kuziba pale juu alikuwa ni miongoni mwa Watoto ambao walipoteza Wazazi wao kutokana na visa mbali mbali, aliwachukua na kuwafundisha kazi za Kijeshi, Mwanamke yule aliitwa Jesca. Huyo ndiyo Mzee Dawson.

Huzuni ilikuwa imetanda ndani ya andaki hilo, Chande na kisko walimpa pole Dwson kwa kumpoteza rafiki yake Kipenzi na Askari wake wa Siri aliyefanya naye kazi kwa muda mrefu, Zola alijulikana kama Polisi wa kawaida lakini nje alikuwa ni komando mwenye mafunzo ya Kijeshi na kijasusi.

Saa ya Dawson ilikuwa ikilia kushiria kuwa eneo hilo lilikuwa kimya sana, Chande akaenda kufungua mlango mmoja ambao ulionekana kufungwa muda mrefu sana, wakaingia huko wakiwa na begi, ndani ya chumba hicho kulikuwa na Makaburi matatu lakini kulikuwa na mashimo mengine mawili ambayo yalionekana kuchimbwa muda mrefu

Dawson akatoa amri ya kufunguliwa kwa begi hilo, hata akina Chande walijawa na maumivu ndani ya mioyo yao, Zola alikuwa amekufa, wakamzika kwemye moja ya mashimo yale lakini lilikuwa limebakia shimo moja, Kisko akauliza

“Mkuu Mashimo manne yamepokea Watu, bado moja. Kwanini ulichimba matano?” Dawson alicheka kwa maumivu kisha akamjibu Kisko

“Marafiki hukaa pamoja, hawa ni marafiki zangu pekee niliokuwa nawategemea katika Maisha yangu, wote wameniacha, hilo shimo moja ni kaburi langu mwenyewe” Chande na Kisko walimtazama Mzee Dawson kwa jicho lililojaa huzuni sana kisha akawaambia

“Muda wangu ukifika mtanifukia hapo kisha mtaharibu kila kitu hapa, hamtaishi tena kanisani, mtakuwa huru kuyatumikia Maisha yenu, mna muda mchache sana wa kuendelea kuwa pmoja na Mimi, nifuateni” Dawson alikaza sura yake kisha akaelekea mahali huku vijana wake wakimfuata huko.

Akafika mahali akasimama akawaambia

“Mwisho wa mtawala katili umefika, nawapa kazi ya kumfuta haraka sana”

“Mtawala gani huyo?” Dawson akafunua Shuka sehemu ambako kulikonekana kuwa na mitambo mingi sana, akawasha Projekta kisha akawaonesha picha ya Rais wa Nchi

Vijana wake wakashtuka sana sababu Kwa muda mrefu Dawson alikuwa pamoja na Rais huyo, Chande akauliza

“Tumfute Mkuu wa Nchi?”

“Hafai kupewa hicho cheo, yeye ndiye chanzo cha Mauwaji yanayoendeelea kutokea hapa Nchini, anapaswa kulipa kwa damu alizomwaga, anapaswa kulipa kwa Kifo cha Zola, kama sio Ujuzi wangu basi nami ningekufa kama Zola” Wakashusha Pumzi zao kisha mmoja akauliza

“Tutaweza vipi kumfuta Mtu mwenye Ulinzi mkali, Mtu ambaye anaishi Ikulu, Mtu mwenye jeshi?”

“Yupo atakayewasaidia”

“Nani huyo?”

“Anaitwa SANDE OLISE”

“Ndio Nani huyo?”

“Nalazimika kuvunja kanuni nilizowawekea, sikuruhusu Ma Ajenti kufahamiana lakini imenibidi, huyo ni P045 Olise”

“Familia inaungana” Alisema Kisko kisha wakampa saluti Dawson, aliwatengeneza vijana wake kujuwa kuwa Ajenti wake ni Familia yao.

Jioni ya siku hiyo, katika Ukumbi wa Maktaba maarufu ya vitabu iliyopo katikati ya Jiji, Rais alikutana na John Brain kwa ajili ya mazungumzo, walitazamana kwa sura mbili huku kila mmoja akiwa na silaha inayomlinda, John Brain alikuwa ameongozana na Malaika wakati huo Six akiwa kwenye moja ya majengo akiwa ameweka Ulinzi kwa kutumbia Bunduki, alikuwa na sifa nzuri sana ya Ulengaji wa shabaha kitu ambacho kilikuwa kikimpa sifa na Umaarufu Mkubwa kwa John Brain, taa nyekundu iliyoashiria kuwa Rais alikuwa akilengwa na Bunduki iligonga kwenye kifua, huku John Brain akiwa ana tabasamu, walinzi wa Rais walipogundua hilo wakataka kuingia kazini lakini Rais aliwazuia sababu alihitaji zaidi kuzungumza na John Brain.

Akaamuru Walinzi wake watoke nje kisha Kamwambia John Brain

“Haina haja ya kuwindana, sisi ni marafiki John, bado nahitaji kufanya kazi na nyie” Alisema Rais kisha akatoa picha kutoka katika mfuko wake wa koti jeusi lililomshika vizuri,

“Huyo anaitwa Dawson! Ni mmoja wa Askari wa kutumainiwa zaidi hapa Nchini, nahitaji mumpoteze sababu kuendelea kuishi ni sawa na Kuyaweka Maisha yangu rehani” Akasema Rais, John Brain akaivuta picha hiyo

“Namjuwa huyu nimewahi kumuona” Akasema Malaika kisha wote wakamtazama

“Kama siyo huyu basi Zola alikuwa anakufa kwa mikono yangu”

“Hata hivyo Zola ameshakufa, aliyebakia ni huyo Mtu, anahitajika kumfuata Zola alipo haraka iwezekanavyo” Aliongeza Rais kisha picha ya Dawson ikarejeshwa mikononi mwake

“Malipo kwanza kisha umuachie Mtu wangu ndipo kazi yako itafanyika, vinginevyo Nchi yako itatangaza Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola ndani ya wiki moja, Raia Watakufa kama Kuku, utakuwa ndio mwisho wa utawala wako” Akasema John Brain akiwa amemtumbulia macho Rais
 
SEHEMU YA NANE

Rais akamuita mmoja wa walinzi wake ambaye alikuja na Brifkesi yenye pesa

“Haya ni malipo ya kazi ya Kwanza ya kumuuwa Makam wa Rais na nyingine ni kwa ajili ya kazi mpya, nawaahidi kumuachia Mtu wenu endapo mtakamilisha kazi yangu sababu yupo hai” Alisema Rais kisha John akamtazama Rais kwa umakini sana

“Kumbuka kauli yako na utekeleze kwa vitendo, ukitugeuka tena hatutokuwa na muda wa mazungumzo, tutaacha simanzi ambayo itasababisha maandamano Nchi nzima, utaondolewa kinguvu madarakani kama mwenzako wa Moroco” Tayari, John na Malaika walikuwa wamesimama kwa ajili ya kuondoka

“Ndani ya masaa 48 nisikie habari njema John Brain, nakuamini” Ilikuwa ni sauti ya Rais kisha John na Malaika wakaondoka pale.

Siku iliyofuta Usiku wa saa nne, Ndani ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa, Sande Olise alikuwa akitua Nchini kwa maelekezo maalum ya Mzee Dawson, kifo cha rafiki yake kilimuuzunisha sana Sande, alijuwa kutua kwake ndani ya Nchi hii kunaweza kuweka Maisha yake katika hatari sababu aliwajuwa Vizuri Mafia Gang na kiongozi wao John Brain, akajuwa hatakiwi kumuamini Mtu kirahisi, siku hiyo Baridi kali lilikuwa limezingira Uwanja huo wa ndege, Sande akiwa ndani ya Koti akaona ni bora aanze safari ya kuelekea mahali ambapo alielekezwa na Dawson kuwa watakutana.

“Nipeleke Kanisa la Nabii Eira” Alisema Sande akiwa tayari ameingia ndani ya taksi hiyo yenye rangi nyeupe, mara moja safari ilianza. Sande alipata wasaa wa kuangalia uzuri wa taa za barabarani, alifarijika sana kurudi katika Ardhi ambayo aliitoroka kwa muda mrefu sana, hakuwa na ndugu na hakujuwa chochote kuhusu ndugu, ilikuwa ni kawaida kwa Askari wa siri wa Dawson kwani wengi wao walitokea kwenye vituo vya kulelea Watoto Yatima, sio yeye tu hata Zola hakuwahi kujuwa asili yake ilikuwa wapi

“Unaonekana hukuwepo hapa kwa muda mrefu hadi umesahau kuwa kipindi hiki ni kipindi cha Baridi” Alisema dereva Taksi, Sande alikuwa nyuma ya gari hilo lenye siti nne

“Ndio lakini haina maana kuwa nimesahau kila kitu, siwezi kusahau mnara wa wapigania uhuru wa Nchi hii” Walijikuta wakianza kuzunguma huku safari ikiwa inaendelea.

“Pengine kitambulisho chako ndio kitu kingine ambacho unaweza kukisahau” Alisema Dereva yule kisha alimpatia Sande kitambulisho kilichomtambulisha kuwa ni Askari maalum,

“Umekitoa wapi?” Akauliza Sande kwa sauti iliyojaa Mshangao mkubwa

“Wakati ulipokuja ulikidondosha nikakiokota” Sande akamshukuru yule dereva wa teksi, walipofika kanisani Sande alimshukuru tena yule dereva

“Usijali ndugu yangu” Alisema yule dereva kisha akaondoka zake, pale wakaja akina Chande na Kisko, wakampokea mabegi Sande na kumpeleka kwneye andaki. Wakati wao wanazama kwemye andaki yule dereva wa Teksi hakuondoka bali alishuhudia wakiingia kanisani akiwa amejificha mahali, akachukua simu yake kisha akamtumia Ujumbe mfupi John Brain, alikuwa ni miongoni mwa Watu wa siri wa John Brain ambao kazi yao ilikuwa ni kuchunguza Maafisa ambao wataingia Nchini.

Basi, Sande alipofika Chini ya andaki alifurahi sana kumuona Dawson ambaye hawakuonana kwa kipindi kirefu sana, ilikuwa ni faraja kwake lakini alipoliona kaburi la Zola alitokwa na machozi.

“Wote waliohusika na kifo chake hawastahili kuishi, wanastahili kilicho halali yao” Akasema Sande akiwa anapiga magoti kwenye kaburi hilo, wakati anapiga magoti akajikuta amedondosha kile kitambulisho alichopewa na dereva teksi kwa madai kuwa alikiangusha, alipokitazama vizuri akaja kugundua kuwa kilikuwa bandia, akaanza kujipapasa haraka pale bila mafanikio kisha akamwambia Dawson ambaye alikuwa amemkodolea macho kuwa

“Wanajuwa kuwa nipo hapa Nchini, wamebadilisha kitambulisho changu” Alisema Sande

“Shiti!! Nilitaka uwe Ajenti wa Siri ili tufanikishe mipango yetu”

“Na kama yule dereva ndiye alicheza huu mchezo basi amegundua mahala hapa na kwa vyovyote watakuja kututafuta” Ukimya ulitawala huku kila mmoja akiwa amezama kwenye tafakari, ilionesha ni jinsi gani John Brain alikuwa na mtandao mkubwa sana anapoingia Nchi yeyote ile ndio maana kazi zake zilikuwa zikifanikiwa mara zote.

Ndani ya dakika kumi na tano yule dereva alikuwa amewasiliana na John Brain na kumpa taarifa kuhusu ujio wa Sande Olise, moja kwa moja John aliona ndio wakati sahihi wa kuuwa ndege wawili kwa wakati mmoja, alikuwa akimfahamu vizuri Sande sababu alikuwa na data zote zilizohusu Usalama wa Nchi, aliwajuwa Maafisa wengi hasa huyu Sande ambaye alipata umaarufu katika Operesheni Upepo.

Taarifa ikawafikia Malaika na Six ambao walipewa kazi hiyo, walitakiwa kuwauwa wote wawili ili waweze kumkomboa jamaal ambaye alikuwa ndani ya Magereza Ikulu, Usiku huo Six na Malaika walijiandaa kupambana na Mzee Dawson na Sande Olise kwa maelekezo maalum yaliyotolewa na Rais.

Kibaridi kilichokuwa kikipiga kilifanya Watu wengi waingie majumbani mapema, ulikuwa ni wakati mzuri kwa Six na Malaika kulivamia kanisa la Nabii Eira, hawakuwa na siri ya andaki lililo katika maegesho ya Magari, humo ndimo Mzee Dawson, Sande na Vijana wake wawili walikuwa wakifikiria nini cha kufanya ili kuokoa uhai wao baada ya kugundua kuwa Sande Olise alikuwa akipelelezwa na dereva Taksi tokea Uwanja wa ndege akitokea Botswana.

Ndani ya nusu saa, gari nyeusi aina ya Toyota V8 ilikuwa ikisogea karibu na Kanisa hilo ambalo lilikuwa na ukuta wa mawe, pembezoni mwa Kanisa hilo kulikuwa na mawe makubwa ambayo yalifanya kanisa. Liwe na muonekano wa kuvutia sana. Gari lao walilisimamisha mbali kidogo ili kutoruhusu akili ya Kijasusi ya Mtu yeyote kugundua kuwa kuna damu iliyokuwa ikienda kumwagika mahali hapo, Six akapanda juu ya jiwe moja kubwa wakati huo Malaika akijipenyeza kuingia ndani.

Kazi ya Six ilikuwa ni kuhakikisha Malaika anaingia kanisani na kutoka akiwa salama, alikuwa mlenga shabaha mzuri sana ambaye John Brain alikuwa akiliimba jina lake kila mahali, Giza kwa upande wa nje lilikuwa limekithirika vya kutosha, haikuwa rahisi kutambua kuwa eneo hilo la kanisa lilikuwa limevamiwa na Manyambisi wawili waliokuwa kama mapacha vile. Baada ya kuwa Six amemaliza kujiweka sawa, akaweka jicho lake katika Kiwambo kish kampa ishara Malaika asogee akiwa na Bastola.

Wakati Malaika alipokuwa akisogea, Jesca yule Kijana wa Dawson ambaye alipandikizwa pale kanisani ili kulinda andaki, alihisi jambo lisilo la kawaida akiwa anamtazama Malaika aliyekuwa akitembea kwa maringo sana akiwa ndani ya suruali nyeusi na Tisheti jeupe, Jesca akiwa anaendelea kumshangaa Malaika…..Kule kwenye andaki….

Mzee Dawson na Vijana wake walikuwa wakipandisha ngazi, harufu ya hatari ilikuwa imenuswa vyema sana.

“Wewe ni nani?” Aliuliza Jesca akiwa ndani ya mavazi ya Kitawa, aliuliza akiwa anamsogelea Malaika aliyekuwa amesimama getini kwa nje

“Mimi ni Malaika” Alijibu

“Malaika?” Akauliza kwa mshangao Jesca, alishawahi kulisikia jina hilo, akajipa muda wa kutaka kumsikiliza Malaika bila kujuwa kuwa alikuwa kwenye shabaha ya Six aliyekuwa juu ya jiwe kubwa.

“Ha!ha! Ndio, Mimi ni Malaika mbona umeshangaa?” Alihoji tena Malaika akionekana kutafuna Bigijii

“Una shida gani?” Aliuliza tena Jesca huku mwili wake ukiwa unajiandaa kufanya tukio pale, alihisi hali isiyo ya kawaida kila alipozidi kutazamana na Malaika

“Nani huyo Jesca?” Ilikuwa ni sauti ya Mlinzi ambaye alikuwa kwenye kijumba kidogo ambacho Jesca alitokea, mara nyingi Jesca alikuwa akiutumia muda wa Usiku kulinda mazingira ya kanisa kitu ambacho Watu wengi walikuwa wakimsifu.

Mlinzi alikuwa akisogea karibu na Jesca, kisha akaona ishara ya mkono wa Jesca kwa chini ukimwambia asisogee pale, Mlinzi akaelewa kisha akasimama pasipo kuendelea kuuliza.

“Nimekuuliza una shida gani?” Alihoji tena Jesca, laiti kama angelijuwa basi angelikaa mbali na Mwanamke huyo kwani kama Zola na ufundi wake wote alishindwa kumdhibiti yeye ataweza?

“Nimekuja kuchukua roho za Watu wawili, ukiwa mdadisi sana nitachukua roho za wengi, fungua geti” alisema Malaika huku ile sura ya kicheko ikipotea, sasa Jesca akajuwa kuwa Malaika aliyekuwa akimsikia kupitia kwa Mzee Dawson alikuwa mbele yake, alijuwa ni jinsi gani Malaika alikuwa hatari, akakumbuka visa vyote alivyovisikia. Kuhusu Malaika. Akapelekea mkono wake ndani ya sketi yake ili kuchomoa bastola, kitendo kile kilimfanya Six afyatue risasi kutoka juu ya lile jiwe, Risasi ikatua kwenye mkono wa Jesca na nyingine ikatua katika shingo ya Jesca, Milio ya Risasi iliwafanya Mzee Dawson na Vijana wake kusitisha zoezi la kutoka kwenye andaki, wakawa wamesimama kwenye ngazi ndani ya andaki hilo la siri.

Risasi mbili zilitosha kugeuza jina la Jesca kutoka Mtu hadi Marehemu, Jesca alikufa pale pale bila hata kumeza mate. Mlinzi akakimbilia kwenye kibanda chake na kuanza kupuliza filimbi, akasikia tu mlio wa Risasi, akaona kioo cha dirisha kikiwa kimepasuka alafu akahisi ubaridi kwenye koo lake, Risasi ya Six ilikuwa ikipita katika shingo ya Mlinzi huyo, naye alikufa pale pale.

Haraka Malaika akapanda juu ya geti na kuingia ndani, kisha akatoa bastola yake akawa anazama kanisani humo, akafungua lango kuu la kanisa akakuta Waumini wakiwa katika hali ya hofu sana.

Bastola ya Malaika ilikuwa mbele, mkono mwingine akiwa ameshikilia sprei Maalum ambayo ilikuwa imejazwa sumu kali, akawasogelea kwa tahadhali kubwa sana kisha akawauliza

“Dawson yupo wapi?” Sauti za vilio ziliendelea kusikika kisha akazinyamazisha kwa kuwatisha kuwauwa, akapekuwa huku na kule bila mafanikio ndani ya jengo la Kanisa, alipowakosa akapuliza ile Sprei kisha akatoka nje haraka na kufunga mlango, akaendelea na Msako mkali katika nyumba za watawa, akapuliza ile sumu kila chumba kisha akampigia simu Six na kumwambia kuwa hakufanikiwa kuwaona Ila amepuliza sumu kila chumba

“Hatuna muda wa kuendelea kuwa hapa, tumia sekunde 30 zilizobakia kutoka humo kanisani” Alisema Six, Malaika akafanya kama alivyoambiwa lakini akiwa anatoka alihisi kama kuna sehemu ilikuwa ikicheza hivi, akasimama karibu na maegesho ya Magari, akasogea chini ya uvungu wa gari akafunua lile shuka akaona kuna mlango mdogo, kwa namna eneo lile lilivyo, hakutaka kujiaminisha kuwa kilikuwa ni kisima sababu kilikuwa kimefunikwa kwa shuka alafu kipo chini ya gari, akataka kufungua ili kutazama ndani ya shimo hilo wakati huo Mzee Dawson akiwa anachomoa Bastola yake na kujiweka sawa kwa Majibizano, Malaika akapeleka Mkono ili afungue kusudi aone kulikuwa na nini mle, Ghafla akasikia king’ora cha polisi, akachomoka uvunguni kisha akaelekea getini na kuruka, akakimbilia gari lao liliposimama, wakaingia kwenye gari na kuondoka, Polisi wakalizingira eneo la kanisa mara moja baada ya kupigiwa simu kuwa kuna risasi zimesikika kanisani hapo.

Wakaingia kwa tahadhali ndipo wakakutana na miili miwili ya Jesca na Mlinzi wa kanisa lile, miili yao ilikuwa na joto kwa mbali kuonesha kuwa Mauwaji hayo yalitokea muda mchache uliopita.

“Hizi ni risasi zilezile, chukueni maiti hizi na wengine fanyeni msako hapa haraka sana” Ilikuwa ni sauti ya mmoja wa Askari waliokuja pale kanisani, bado Mtaalam Sande, Mzee Dawson na vijana wake wakiwa ndani ya Andaki bila kuwa na taarifa kuwa Jesca alikuwa ameuawa na Six, lilipofunguliwa lango kuu la Kanisa ndipo mshituko na Mshangao mkubwa ulipowashika polisi hao, walikuta Miili ya watu ikiwa inatokwa na mvuke kama vile nyama inayochomwa, harufu ya nyama ilitapakaa kanisa zima wakaagiza zima moto kumwaga Maji katika kanisa hilo, muda mchache polisi walifanikiwa kuingia ndani ya kanisa na kukuta Miili mingi ikiwa imeharibika vibaya sana.

Taarifa ilizagaa kwa haraka sana juu ya shambulio hilo la kutisha ambalo lilitumia silaha ya sumu na risasi, Sande akawashauri akina Mzee Dawson kuwa hawapaswi kutoka kwa wakati huo hadi polisi watakapo maliza msako wao.
 
Back
Top Bottom