Jasusi damu zamwagika

Jasusi damu zamwagika

SEHEMU YA TISA

“Nina mashaka juu ya uhai wa Jesca, yeye ni mmoja wa walinzi wa hapa kanisani, sijasikia majibizano ya risasi, huwenda amekufa kifo Baridi” Alisema Mzee Dawson akionekana kushindwa kuzuia chozi lake

“Una maanisha nini kusema Kifo Baridi?” Alihoji Mtaalam Sande Olise huku akimtazama Dawson kwa jicho lililo kaza

“Kufa bila kujibu mapigo, Walengwa tunaotafutwa katika vita hii ni sisi. Sitaki makubwa yawakute wasio na hatia” Alinena Dawson

“Una maaana gani?”

“Ni bora nijitokeze kupambana nao ili kunusuru Maisha ya wengi yanayowekwa rehani, ikiwa kufa Mimi au kupona wao ninachotaka ni usawa” Aliongeza Dawson

“Kumbuka Polisi watakuangalia kama muarifu kuanzia hivi sasa, hautokuwa huru kufanya chochote kama Mkuu wa Kitengo, vita hii ni ngumu Mkuu! Vipi kama Rais ataamuwa kukupaka tope? Utakuwa salama?” Aliuliza Sande Olise, Mzee Dawson akameza funda zito la mate kisha akasema

“Tusipopambana sasa hivi tutakuja kupambana nje ya muda, tunapaswa kuwa macho zaidi”

“Unashauri tufanye Nini Mkuu tupo tayari kukusaidia katika vita hii” Alisema Kisko kwa utii Mkubwa, Dawson alikuwa kama Mzazi kwao, ndiye aliyewachukua kutoka katika kituo cha Watoto yatima na kuwaonesha Mwanga wa Maisha, Dawson akawageukia na kuwaambia

“Natamani hii vita msipigane sababu mna kila sababu ya kuwa hai ili mje mpigane hapo baadaye sisi tukiwa tumetundika daruga au tukiwa tumekufa. Niliwaandaa mje kuwa hazina muhimu baadaye” Alisema Dawson kwa sauti ya Baba kwa Watoto wake, nyuso za Kisko na Chande zilisinyaa huku macho yao yakitazama chini.

“Babaa!! ” Aliita Chande, Dawson akageuza macho yake kumtazama

“Tupo tayari kwa sasa kufa kwa ajili ya Taifa letu, turuhusu tukusaidie hii vita” Dawson alipomaliza kumsikiliza Chande akarudisha macho yake kwa Sande Olise, Wakajikuta wanatazamana huku sura zao zikizungumza Kijasusi

“Tuangalie tunatokaje hapa Shimoni, haribuni kila kitu ili kupoteza ushahidi wa kazi za hapa ndani, kila mmoja avae sura bandia haraka sana” Aliagiza Mzee Dawson kwa sauti iliyojaa mamlaka ya Kijeshi, kazi ikaanza rasmi.

MSAKO

“Shit!” Ilikuwa ni sauti ya John Brain baada ya kupokea taarifa usiku huo, hakutegemea kusikia kuwa Dawson na Sande Olise bado wanaendelea kupumua, aliona ni makosa makubwa ni sawa na kumjeruhi mnyama Mkali.

“Inawezekanaje wasiwepo kanisani wakati mtoa taarifa amehakikisha kuwa Sande aliingia hapo? Endapo Sande na Dawson wakapata muda wa kupanga mipango yao kazi hii itakuwa ngumu kwetu” Alisema tena John Brain huku akizitazama sura za Six na Malaika ambao walikuwa wamenywea.

“Nimefanya msako kanisa zima lakini sikupata kuhisi hata harufu zao, huenda walicheza mchezo wa sarafu baada ya kugundua kuwa tunawafuatilia” Alijibu Malaika

“Watakuwa wapi?” Aliuliza John Brain akionesha kutafakari jambo peke yake, kisha akawaambia

“Nendeni lakini Mjiandae kwa msako maalum” Malaika na Six wakaondoka, John Brain akampigia simu Rais na kumjulisha taarifa ile ambayo ilionekana kumchanganya sana Rais

“Hivi mnajua mnafanya masihara kwa Watu gani? Hao jamaa wana medali za ushindi kwenye kila jambo, Dawson ana fahamu siri yetu hivyo hapaswi kuendelea kuishi” Alisema Rais kama Mtu aliyeingia kwenye mshituko ni wazi kuwa alitarajia kusikia kuwa Dawson na Sande wameuawa

“Tunalijuwa hilo na vijana wangu wanalifanyia kazi jambo la muhimu ni kuhakikisha unatupatia Mtu wetu baada ya siku chache, tutakuwa tumeimaliza kazi hii na kuondoka hapa Nchini”

“Msifanye Makosa mengine John , mtajikuta mnawajibishwa! Ngoja nijisafishe haraka sana” Rais alikata simu, alionekana kuwa mwenye msongo wa mawazo huku akionekana kuwa na hofu juu ya mpango wake wa siri juu ya Mauwaji ya Makam wa Rais kujulikana na kuwekwa hadharani, akanyanyua simu na kumpigia Mkuu wa Idara ya polisi na kumueleza kuwa Dawson ni mharifu anapaswa kusakwa kwa kila njia ili apatikane, Rais aliamuwa kucheza karata mbili.

Moja ni kuwatumia Mafia Gang kumfyeka Dawson na nyingine ni kutumia Jeshi la polisi kumsaka popote alipo, agizo la Rais lilianza kutekelezwa, Polisi wakaagizwa kuelekea nyumbani kwa Dawson usiku huo huo.

Rais alikaa katika kiti chake huku akizidi kujiingiza mawazoni, Nchi ilikuwa imeingia katika Msako, Polisi walivunja nyumba ya Dawson na kufanya msako mkubwa bila mafanikio, wakati huo Dawson na timu yake wakiwa wanatoka katika shimo kule kanisani, Polisi wachache walikuwepo eneo la tukio kule kanisani usiku huo, Walifanikiwa kuchomoka pale kanisani kimya kimya kisha wakaruka ukuta wa kanisa na kutokomea.

Dawson alishajua kuwa polisi wataenda nyumbani kwake hivyo akawaambia wasiende huko badala yake waelekee kwenye makazi ya siri ambayo alikuwa akiishi Inspekta Zola, ilikuwa ni safari ya Kilomita kadhaa kutoka pale kanisani hadi kufika huko, walilazimika kutembea kwa mguu sababu polisi walikuwa wakikagua magari yanayoingia na kutoka kila kona ya jiji hilo, haikuwa salama kwao kutumia usafiri wa gari licha ya kuvaa sura bandia, mwendo wa masaa mawili Walifika kwenye makazi hayo, Dawson alifahamu namba za siri za kufungulia milango hiyo ikawa rahisi wao kuingia ndani.

Kumbukumbu ya Zola iliendelea kuwatesa baada ya kuingia humo, Sande aliiona picha aliyopiga na Zola wakiwa mafunzoni hadi chozi lilimbubujika aligundua kuwa Rafiki yake huyo alikuwa akimpenda na kumkumbuka sana, walikuwa na ndoto ya kuonana siku moja lakini ndiyo hivyo Sande alichelewa kurudi hadi Zola akauawa, Dawson aliifahamu nyumba hii vizuri sana sababu mpango wa nyumba hii aliusuka mwenyewe ili Zola aitumie nyumba hii kwa kazi zake maalum, akawaonesha chumba ambacho kilikuwa na silaha akawataka kujiandaa kwa ajili ya kazi hiyo kubwa iliyo mbele yao.

“Baada ya kupambazuka tutakuwa katika hekaheka nzito yenye maamuzi ya kuondoa uhai wetu au kuturuhusu kuendelea kupumua, kama tuna muda wa kufurahi basi huu Usiku uliobaki unaweza kuwa ndio muda pekee wa kufanya hivyo” Alisema Dawson akiwa ana mimina mvinyo kwenye glasi, kila mmoja akanyanyua na kuanza kunywa

“Kwa ajili ya Zola, tusherehekee Maisha yake sababu ameimaliza kazi aliyokula kiapo kuifanya ili kulinda Taifa lake” Yalikuwa ni maneno ya Sande Olise ambaye naye aliungana na Mzee Dawson wakanywa Glasi moja moja, Chande na Kisko wakaungana pale wote wakapata Mvinyo kama Ishara ya kuyaenzi Maisha ya Inspekta Zola ambaye ameuawa ndani ya Ikulu, hadi kufikia muda huo hakukuwa na taarifa iliyotolewa popote kuwa Inspekta Zola alikuwa amekufa, si akina Dawson wala upande wa Rais ambao ndio walitekeleza Mauwaji hayo.

Asubuhi ya siku iliyofuata iliwakuta Dawson na vijana wake wakiwa ndani ya jumba la siri hilo alilokuwa akiishi Mtaalam Zola, taarifa kuwa Dawson amelisaliti Taifa ilianza kuzagaa, akatajwa Dawson kama ndiye Mhusika namba moja wa Mauwaji ya Waumini kule kanisani, taarifa ikafika mbali na kusema ana viashiria kuwa alitaka kuipindua Nchi hiyo kwa kusababisha taharuki ikiwemo Mauwaji ya kutisha yaliyokuwa yakifanyika pia Mauwaji ya Makam wa Rais, gunzo lilikuwa limetanda, ni kama Bundi mweusi alikuwa ameyazunguka Maisha ya Dawson, ikatolewa taarifa kuwa Dawson anashirikiana na Askari mmoja wa Usalama wa Taifa aliyeitwa Sande Olise ambaye alikuwa akiishi Botswana.

“Huyu Mjinga anajaribu kuharibu taswira niliyoijenga Miaka mingi katika Taifa hili” Alisema Dawson kwa hasira huku akitafuta rimoti ya TV ili aizime, Sande alimzuia

“Huna haja ya kupaniki, anachokifanya Rais ni kujaribu kujisafisha na kuyatia doa Maisha yetu. Kwakuwa anajua una siri zake basi anaitumia hii nafasi kukudidimiza ili usiaminike na yeyote yule” Alisema Sande kisha Dawson akamuuliza

“Mimi ni mzalendo kwa Taifa hili, nimekuwa kwenye nafasi hii kwa Marais zaidi ya tano, iweje huyu aje kuharibu kila jema nililopanda kwenye Taifa hili, baada ya kuniulia Rafiki yangu anadiriki kuniita Msaliti wa Taifa hili” Dawson alionekana kuchukizwa sana na kitendo kile, akapapasa kiuno chake akatoa bastola

“Unaenda wapi?” Alihoji Sande

“Ikulu kuondoa uhai wa hayawani yule, hastahili kuishi pale, anastahili kuwa Kaburini au Jela kwa yote aliyoyafanya”

“Hebu tulia, kumbuka John Brain ni Mtu mwenye akili sana. Huu ni mtego na lengo ni kukufanya uchukie, Rais anakujua vizuri hupendi mchezo na uzushi, ukitoka hapa hata hufiki mbali wanakuuwa” Alisema Sande huku akimsistiza Dawson atulie, chozi lilikuwa likimbubujika Mzee Dawson, akajitupa kitini kama Mtu aliyekata tamaa.

“Huna haja ya kukurupuka, Tumetajwa kuwa Wauwaji na wasaliti, tukikamatwa huko nje hatutokaa kuonekana tena, tutaliacha Taifa hili katika giza kama ambavyo Zola ameliacha. Nimekuja hapa kwa ajili ya kazi hii, nitazame Mimi kwa sasa kama ambavyo ulikuwa ukimtazama Zola na kumuamini, hamisha kila kitu kutoka kwake kisha kiweke kwangu, Mimi ni Zola niliye katika Umbo la Sande, hakuna kitakacho haribika” Yalikuwa ni maneno ya Kikomandoo kutoka kwa Sande Olise, alisema akiwa amefanikiwa kumpokonya Bastola Dawson.

Akampatia ile Bastola Kisko akamwmbia

“Ukiitumia vibaya itakupeleka pabaya, tuliza akili ndipo uitume ifanye kazi yake” Alimkabidhi kisha Akasema

“Baada ya miaka mingi narudi kazini kupambana na John Brain, kivuli chake kitaendelea kuitesa hii Nchi, huyu Rais Mpumbavu siku zake za kuwa madarkani zinahesabika” Alisema kisha akaelekea kwenye moja ya vyumba vya siri vya jengo hilo ambavyo vilikuwa vimeshafunguliwa na Mzee Dawon.

Akakuta Ramani ya mpango wa Zola ikiwa ukutani, akaangalia namna Zola alivyopanga mambo yake pale akajikuta akitabasamu kwani kila jambo alikuwa ameliandika katika Ramani hiyo.

Nyuma ya Sande alikuja kusimama Mzee Dawson huku akimtazama Sande namna alivyokuwa makini kutazama Ramani ya Zola

“Ulikuwa na askari shujaa sana ambaye hasahau mbinu zako” Alisema Sande Olise kisha aligeuka na kumtazama Mzee Dawson aliyekuwa akifuta chozi lake, kifo cha Zola kilimuumiza sana.

“Nina uhakika kama utawatunza vijana hawa wawili wanaweza kuwa Sande na Zola wa baadaye, kwasasa Mzee Dawson pumzika. Afya yako haikuruhusu kuendelea na vita hii, nitapambana Mimi na hawa vijana, utabakia hapa” Aliongeza Sande, ni kweli afya ya Dawson haikuwa nzuri kutokana na pombe na sigara.

Wakapanga mipango ya kumuondoa Rais Madarakani kisha kuanika uchafu na madudu yake yote, Dawson alitakiwa kubakia pale kwenye jumba la siri wakati ambao Sande na vijana wawili wa Dawson watakapokuwa wanaondoka, wakapewa sura bandia ili watakapotoka nje wasijulikane.

Muda huo Magari mawili meusi yalikuwa yakiingia Ikulu, alikuwa ni John Brain, Six na Malaika, utatu ambao ulilisumbua Taifa kwa muda mrefu, waliitwa na Rais huyo Mshenzi. Waliingia wakiwa kama wageni wakiwa ndani ya sura bandia ili wasitambulike sababu Vyombo vingi vya habari hasa vya nje vilikuwa vikiripoti taarifa zao za Mauwaji na jinsi ambavyo walikuwa wakitafutwa, Waliongoza hadi ofisini kwa Rais huyo bila Ulinzi wowote kutokana na maagizo ya Rais.

Rais alipowaona alinyanyuka na kusogea karibu na John Brain kisha akamuuliza

“Mnataka niwape nini ili Dawson na Sande wauawe? Mnapaswa kujuwa kuwa Dawson ni nyati aliyejeruhiwa akitoka huko mafichoni hatutokuwa salama” Alisema huku akionekana kuchanganikiwa, jasho lilikuwa likimvuja

“Tatizo umechanganya vitu viwili kwa wakati mmoja, Polisi wanahangaika kuwatafuta na sisi tunahangaika kuwapata. Kila tunapopiga hatua polisi wanakuwa eneo la tukio, au unataka tusamabratishe na polisi wako?”

“Kama hilo ni tatizo nitawaingiza katika mfumo wa usalama wa Taifa mkiwa katika sura hizo, John utakaa pembeni sababu ya rangi yako ila Malaika na Six wataingia na kufanya kazi mara moja, watakuwa na amri kwa askari pindi wanapokutana katika jukumu la kuwawinda Sande na Dawson,watapewa vitambulisho maalum”

Rais akawaingiza Six na Malaika katika mfumo wa idara ya Usalama wa Taifa, wakapewa na Vitambulisho

vilivyowatambulisha kama Watu wa Usalama, ikawa rahisi kwao kuwa huru kufanya kazi ya kuwasaka Dawson na Sande Olise ambao walikuwa kizingiti kikubwa kwa Rais na John Brain kumpata kijana wake aliyekuwa akishikiliwa na Rais.

Polisi wakatawanywa kila kona ya Jiji kuhakikisha Dawson na Sande hawapigi hata hatua moja, kazi ya polisi ilikuwa kuwakamata lakini kazi ya Six na Malaika ni kuwauwa, wakiwa ndani ya Sura bandia walirudi pale Kanisani ambako walisababisha Mauwaji ya kutisha ya Waumini na Askari mmoja wa siri wa Mzee Dawson, walirudi kama Watu wa Usalama, wakahitaji kuchunguza eneo hilo huku akili zao zikiwaambia kuwa pengine Dawson na Sande bado wapp eneo hilo, walimjua vizuri Dawson jinsi alivyo na akili nyingi.

Walitumia vyema macho yao ya Kijasusi na mafunzo waliyoyapata kutoka kwa John Brain wakagundua kuwa kuna andaki eneo la maegesho ya Magari

Six na Malaika wakapeana ishara, haraka bastola zao zikawa zinatazmaa eneo hilo ili kama kuna Mtu atatokea basi wamdhibiti haraka sana.

Wakalisukuma gari na kuona mlango wa kuingia ndani, haraka wakiwa makini sana wakafungua na kuanza kuingia humo taratibu huku masikio yao yakiwa makini kusikiliza ndani ya andaki hilo lenye giza sana.

Walipofika chini wakawasha tochi ya simu kisha wakaona mahali ambapo wangewasha taa, walipowasha wakaona vitu vikiwa vimeharibiwa pale, wakakagua kila kona lakini hakukuwa na Watu, tayari Mzee Dawson na vijana wake walishaondoka pale muda mrefu sana kisha wakaharibu vitu ndani ya andaki hilo, elimu yao ya kijasusi haikuwafanya wao kukata tamaa ya kutaka kujuwa andaki hilo lilihusiana na nini

“Kwa vyovyote haya yalikuwa makazi ya siri ya Dawson! Huenda ameishi hapa kwa kitambo sana” Alisema Six

“Hata awe makini vipi ni lazima ataacha alama humu, tutajua kama ni yeye na ameenda wapi” Alisema Malaika, msako uliendelea ndani ya andaki hilo lililoonekana kuwa makazi ya kutulia sana, katika upekuzi wao waliona Makaburi manne ambayo yalikuwa ndani ya chumba kimoja.

Walipoangalia vizuri waliona namba za siri ambazo Mzee Dawson aliwapa vijana wake kama majina na alama zao, namba hizi zilikuwa za siri sana, ilikuwa ngumu kugundua chochote lakini alizitambua kisha akampigia simu John Brain na kumueleza kuhusu Makaburi hayo manne yenye namba za siri, John Brain alikuwa na mtandao mkubwa sana na alizijua siri nyingi za Mataifa mbalimbali

“Hayo ni majina ya Watu wa siri wa Mzee Dawson, Sande yupo hai, moja ya kaburi hapo linaweza kuwa kaburi la Zola, fukueni haraka sana.” Ilisikika sauti ya John Brain, aliamini Dawson ni Mtu mwenye akili sana kwenye mambo yake.

Mengine yalionekana kuwa ya zamani sana lakini moja lilikuwa bado jipya, wakalifukua hilo kwa kutumia chepe iliyo kwenye kona ya chumba hicho chenye makaburi. Kazi hii ilifanywa na Six aliyekuwa amebana rasta zake kwa nyuma. Jasho lilikuwa likimtoka, harufu kidogo ilianza kutapakaa pale, haikuwazuia kufanya kazi yao,
 
SEHEMU YA KUMI

“Oooh Shit!” Alisema Six huku akitema mate, Malaika ilimbidi asogee pale

“Duuh! Kweli huyu jamaa alipitia mafunzo makubwa sana” Alisema Malaika, mwili huo ulikuwa umeharibiwa kwa kemikali maalum ambayo iliwafanya akina Six washindwe kuitambuwa sura hiyo, wakati wanaendelea kushangaa tukio lile Malaika aliona kitu kama redio Call hivi kando ya aliposimama tena ikiwa imefukiwa kidogo, akaifuata na kuiokota akakuta redio hiyo ikiwa inafanya kazi.

Haraka Malaika akakimbilia alipoliacha begi lake, akatoa Laptop na baadhi ya vifaa fulani kisha akavaa Head Phone, akawasha kitu fulani kutoka katika Laptop yake akaona mawimbi ya redio hiyo yakiwa yanatoka kando ya Bahari ya Hindi.

“Umefanikiwa kugundua chochote?” Aliuliza Six akiwa ameshikilia chepe

“Eneo ulipo mtambo wa redio hii ni kando ya Bahari ya Hindi upande wa Mashariki”

“Inaweza kuwa mhusika wa andaki hili yupo huko, kama ni Dawson basi arobaini yake imefika” Alisema Six kisha kwa pamoja wakapanda juu kutoka katika lile andaki wakijiandaa kufuata mawimbi hayo. Walipotoka wakakutana na waumini waliokuwa wamesimama nje ya andaki hilo, walionekana kushangaa

“Nani amechimba andaki hili hapa?” Aliuliza Malaika huku akiwa ameshatoa kitambulisho feki walichopewa na Rais ili waonekane ni Watu wa Usalama wa Taifa. Macho ya watu hao yalionekana kujawa na woga wakawa wanasakiziana kujibu, mmoja akasikaka akisema

“Hatukuwahi kuona wala kuhisi uwepo wa shimo hilo, kwa miaka mingi nimeishi hapa lakini hili shimo sijawahi kuliona” Alisema huku akitikisa kichwa chake, alionekana kuwa Mzee sana mwenye mvi nyeupe zisizo na matunzo

“Kanisa hili limejengwa lini?” Aliuliza Six

“Miaka 15 iliyopita”

“Nani alihusika na ujenzi wake?” Six aliuliza tena, alichotaka kusikia ni jina la Mzee Dawson likitajwa ili wawe na uhakika wa wanachoenda kufanya

“Mfadhili alishafariki miaka mitatu baada ya kanisa hili kukamilika” Alijibu tena yule Mzee ambaye alijibebesha mzigo wa kujibu maswali ya Six

Walipoona hawawezi kupata walichokuwa wanakitaka waliondoka haraka eneo hilo ili kuanza safari ya kuelekea Kando ya Bahari ya Hindi upande wa Mashariki, upande huu ndiko ambako nyumba ya siri ya Marehemu Zola ilijengwa.

Kitendo cha Six na Malaika kuondoka kilimpa mwanya yule Mzee akawaacha wenzake wakiendelea kushangaa uwepo wa andaki kanisani, akaenda nyuma kabisa ya kanisa hilo, alihakikisha hakuna aliyemuona tena akionekana kuwa mwenye wasiwasi Mkubwa.

Akawa anatafuta kitu ardhini kwa kukita mguu wake, alifanya hivyo kwa dakika kadhaa hadi alipokita mahali aliposikia kama kuna sauti inamuitikia, ilikuwa ni sauti iliyoashiria uwepo wa kitu fulani sehemu hiyo, akafukua kwa kutumia mikono yake sababu eneo hilo lilikuwa limeloa kutokana na maji yaliyokuwa yakimwagika kutoka katika tanki, akafanikiwa kufukua na kutoa sanduku la rangi ya fedha, akapanda juu ya ukuta akiwa na sanduku hilo dogo kisha akatokomea zake pasipo kuonwa na yeyote yule.

Turudi kule kwenye Makazi ya siri ya Marehemu Zola, hali ya kutafakari ilikuwa imechukua nafasi kubwa sana. Dawson hali yake kiafya haikuwa nzuri hasa baada ya kupata mikiki ya hapa na pale kwa zaidi ya masaa nane bila kutuliza akili yake, kifua kilikuwa kikimbana mno huku Kisko akimsaidia baadhi ya dawa na huduma nyingine

“Asante Kisko! Natamani sana siku moja niwaone mkitoka katika Maisha haya ambayo nahisi yanawapa mateso makubwa sana, hamna uhuru wa kufanya mambo yenu. Nimewalea kwa muda mrefu sana” Alisema Dawson huku akiangalia saa yake mkononi, kisko akamuuliza

“Kwanini unaangalia saa hiyo kila wakati ilhali haioneshi chochote?” Mzee Dawson akajilazimisha kucheka kidogo

“Inaonekana kutokufanya kazi ndio lakini Je kama nikikwambia Hii saa ndiyo Mimi utaamini?” Kisko akacheka kisha akasema

“Hata Mtoto mdogo hawezi kuliamini hilo, Mtu anawezaje kuwa saa?”

“Bahati mbaya au nzuri, nyie mna majina yenu. Majina ambayo mlipewa huko mlipotoka, licha ya kupewa majina ya Kijeshi lakini hayakuweza kubadili uhalisia kuwa wewe ni Kisko, wenzako ni Jesca na Chande” Akasema kisha akakohoa na kutoa damu nzito sana, akapewa maji ya kusukutua

“Nawaza Jesca atakuwa wapi, ni masaa mengi yamepita bila kuwasiliana naye. Ulifanya kama nilivyo kwambia?” Alihoji Dawson

“Ndio redio Call niliiacha kwenye kile chumba chenye makaburi” Alijibu Kisko huku akionekana kuwa mwnye kiu ya kutaka kujuwa mengi

“Hata wewe pia ni mwenye Bahati kama ni hivyo, una jina lako halisi Kama Dawson” Dawson akacheka tena kisha akasema

“Sababu Mimi ni Afsa wa juu katika Nchi hii ni lazima nitumie jina halisi lakini kuna jambo lililo nyuma ya Pazia, utakuja kuelewa siku moja endapo Mungu atanijalia uhai mrefu wa kuishi” Yalikuwa ni maongezi yaliyojaa mafumbo ambayo hayakumshibisha Kisko, Muda huo Chande alikuwa kwenye chumba kimoja na Sande Olise wakiwa wanazungumza

“Tunasubiria nini?” Aliuliza Chande akiwa anamtazama Sande Olise aliyekuwa ameegesha nwili wake kwenye moja ya kioo na kujipa fursa ya kutazama chini ya jengo hilo la kifahari

“Hatuwezi kukurupuka! Tupo mawindoni Chande, kosa dogo unaadhibiwa kifo. Nchi inatutambua kama waasi kutoka masaa machache ya kujulikana kama Wazalendo wenye kulipigania Taifa, Dunia wakati mwingine inaweza isikupe maana halisi ya Binadamu”

“Ha!ha!ha!” Alicheka Chande, muda huo Kisko alikuja mbio na kuwaambia

“Mzee Dawson hali yake ni mbaya sana” Taarifa ikazua taharuki pale, wote wakaelekea chumbani kwa Dawson! Wakamkuta akiwa ana pumua kwa shida sana.

“Inabidi tumsaidie!” Alisema Chande akionekana kuwa na wenge la kutosha

“Tulia!! Hatuwezi kufanya hivyo kwa sasa, hatuwezi kuhatarisha Maisha yetu kirahisi hivyo!!” Alisema Sande kisha alimgeukia Dawson

“Yupo sahihi! Rais anajuwa Mimi naumwa kwa muda mrefu simalizagi wiki mbili kabla ya kupelekwa JNI Hospital kwa matibabu ya ugonjwa wangu sababu wao ndio speshelist wa tatizo hili, huu ni mtego mtakamatwa wote. Ni bora mniache nife nyie mbaki kuwa hai” Alisema Dawson kwa sauti iliyojaa maumivu mno

“Baba usiseme hivyo unayo nafasi ya kuendelea kuishi, sema unataka nifanye nini Baba” Chande alisema kwa uchungu huku macho yake yakibubujika chozi laini lililolowesha mashavu yake madogo, Mzee Dawson kwao alikuwa ndiye Baba yao sababu aliwatoa kwenye kituo cha kulea Watoto yatima miaka mingi, akawapeleka mafunzoni, wakapata mafunzo ya kijeshi na kijasusi

“Chande anayejuwa mwisho wangu atawapa tumaini endapo atanichukua” Alisema Dawson huku hali yake ikizidi kuwa mbaya!! Sande Olise akahisi jambo, haraka akaelekea kwenye kioo kutazama chini akaona gari nyeusi ikiwa imesimama nje ya uzio wa jumba hilo la siri, walikuwa ni Malaika na Six ambao walikuwa wakifuatilia mawimbi ya Redio Call kutoka kanisani hadi Ufukweni, kifaa chao kiliwaambia kuwa walikuwa wamefika eneo husika.

“Kuwa makini!” Alisema Six kisha akampatia Bastola Malaika. Sande akarudi kwenye kile chumba akawapa taarifa kuwa Kuna hali ya hatari wanapaswa kuokoa Maisha yao haraka iwezekanavyo, muda huo Mzee Dawson alikuwa katika hali mbaya ya kuumwa.

Ndani ya msitu mmoja ulio kando na Jiji hili, alionekana Mtu mmoja Mzee Akikimbia, mkononi alikuwa ameshikilia sanduku lenye kutu, alikuwa ni yule Mzee aliyefukua Sanduku kule kanisani. Alikuwa amechoka baada ya kukimbia kwa muda mrefu, mikono yake ilikuwa ikitetemeka. Akaingiza mkono mfunoni akatoa funguo kisha akasimma chini ya Mti mmoja mkubwa, akalifungua sanduku hilo.

Ndani ya sanduku kulikuwa na kifaa kimoja kilichoonekana kuwa cha zamani sana, akakiangalia kisha chozi likawa linamtoka. Akabonyeza kitufe cha kuwasha, kikawaka.

Kifaa kile kilikuwa kimeunganishwa na vifaa vinne ambavyo vilikuwa kwa Watu wanne, Mtu wa kwanza kupata ishara alikuwa ni John Brain, Mtu wa pili ni Mzee Dawson, wa tatu ni Malaika na Wanne ni Six ambaye alikuwa akitembea kuelekea kwenye jengo lingine kama kawaida yake kutafuta eneo zuri la kulenga shabaha, kitendo cha kuwashwa kile kifaa na yule Mzee kule msituni kilimfanya Six aanguke na kuhisi baridi kali sana, vivo hivyo kwa Malaika ambaye alikuwa ameshafika kwenye geti la kuingia katika jumba la siri ambalo Mzee Dawson na vijana wake walikuwemo, kwa Mzee Dawson iliwaka ile saa ambayo Kisko alimuuliza Dawson kwanini alikuwa akiiangalia mara kwa mara lakini wakati inawaka Mzee Dawson alikuwa ameshapoteza Fahamu zake, wote walishangaa kuona saa ya Dawson imewaka ghafla na kutoa mwanga wa kijani, katika saa hiyo kulikuwa na kitu kama ramani iliyokuwa ikizunguka ndani yake.

John Brain alishtuka sana baada kupata ishara kutoka katika moja ya saa yake ndogo ambayo mara nyingi alikuwa akitembea nayo, saa hiyo ilikuwa ikifanana sana na saa aliyokuwa akiivaa Mzee Dawson! Akasimama na kutabasamu kisha akajikuta mwenye furaha isiyo kifani.

“Baada ya miaka mingi hatimaye umeonekana, niliweka Maisha yangu rehani kwa muda mrefu kukutafuta” Alisema John Brain.

Muda huo yule Mzee ambaye hakujulikana ni nani na ametokea wapi, alichukua kifaa kingine ndani ya sanduku, kifaa ambacho kilikuwa kama simu hivi kisha akapiga mahali. Simu iliita ndani ya Ikulu, ilikuwa ni katika ofisi ya Rais

“Mimi ni P55 Mbaga” ilikuwa ni sauti komavu kutoka kwa Mzee huyo, Rais alishtuka sana kusikia jina hilo yaani P55 Mbaga, akakata simu haraka sana baada ya kusikia hivyo kisha akanyanyua simu kumpigia John Brain ambaye alikuwa katika hali ya furaha sana

“Mimi ni mfu John!!” Alisema Rais kwa sauti iliyoonesha alikuwa kwenye butwaaa

“Kivipi?” Alihoji Brain

“P55 Mbaga amejitokeza!!”

“Imarisha ulinzi haraka, Naingia kazini kupambana naye” Alisema John huku tabasamu likiwa limeimarika katika sura yake.

Muda huo yule Mzee ambaye ni P55 Mbaga alikuwa akitoka kule Msituni na kufunga safari ya kufuata uelekeo wa saa ya Mzee Dawson, alikuwa na kifaa chake alichokiamini sana, alionekana kuwa mtaalam wa kifaa hicho, Dakika tano baada ya vifaa vilivyofungwa katika miili ya Six na Malaika kuwaka, iliwafanya wabadili maamuzi yao. Mpango ulikuwa ni kuwauwa Sande na Mzee Dawson, haraka wakaingia kwenye gari na kuondoka eneo lile, huku maswali yakiwa mengi vichwani mwao.

Yule Mzee alifika hadi eneo la Mashariki ya Bahari ya Hindi, kifaa kikamwambia kuwa alikuwa amefika eneo ambalo saa hiyo ilikuwepo, muda huo Mzee Dawson alikuwa akirejea kwenye fahamu zake!! Alipoamka alishangaa kuona saa yake imewaka, akashtuka kisha akauliza

“Imeweka saa ngapi?” Aliwatumbulia macho vijana wake ambao walikuwa wamesimama mbele yake, alikuwepo Kisko na Chande

“Nusu saa iliyopita” alijibu Chande huku akimtazama Mzee Dawson aliyekuwa kitandani

“Na Sande yupo wapi?”

“Nafikiri yupo kwenye korido, unamuhitaji?”

“Hapana!! Nipe Maji ya kunywa” Alisema tena Mzee Dawson kisha alikohoa na kutoa damu.

“Baba kwanini hii saa ni muhimu sana kwako umeamka hujali afya yako unauliza kuhusu saa?” Alihoji Kisko

“Nilikwambia hii saa ndiyo Maisha yangu, Mimi ni hii saa, niliisibiria kwa miaka mingi na jambo hili lilibakia kuwa siri ambayo sina budi kuwaeleza mkiwa pamoja” Muda huo Chande alirejea akiwa na glasi yenye maji ya vuguvugu ambayo mara nyingi Mzee Dawson alikuwa akiyatumia. Ghafla, Sande aliingia chumbani bahati nzuri Dawson alikuwa ameshapata fahamu akasema

“Kuna Mtu anakuja upande huu, anaonekana kuwa anafuatilia jambo maana yupo bize na kitu mkononi, nafikiri ana GPS” Alisema Sande, Mzee Dawson akanyanyuka na kwenda kuangalia, alipofika dirishani alimuona Yule Mzee ambaye mara nyingi alikuwa akishinda kule kanisani akajiuliza alikuwa amefuata nini pale

“Unamfahamu?” Aliuliza Sande

“Ndio….huyu Ni Miongoni mwa Wazee wa kanisa letu, najiuliza amepajuaje hapa” Akajibu Mzee Dawson huku akionekana kujawa na mshangao

“Niachie Mimi” Sande alisema kisha akashusha ngazi kuelekea chini, akafungua mlango kisha akatoka. Akakutana yule Mzee

“Wewe ni nani?” Alihoji Sande lakini kwa tahadhari sababu Mzee huyo alikuwa makini kumtazama Sande na jinsi alivyomtazama Sande aligundua Mzee huyo alikuwa na macho makini kuliko maelezo.

Punde ikasikika sauti ya Dawson ikisema

“Mruhusu aje ndani” alipogeuka alikutana na macho ya Dawson, Mzee huyo akaruhusiwa kuingia ndani lakini tayari kila mmoja alikuwa na umakini mno. Tembea ya Mzee huyo bado ilikuwa makini sana, alionekana kutafuta kitu lakini alipoingia humo kifaa chake chenye GPS kilizimika sababu nyumba hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kazi za kipelelezi hivyo ilikuwa ni ngumu kwa baadhi ya vifaa kupenyeza.

Alipewa kiti akakaa kisha akaulizwa

“Umefikaje hapa?” Aliuliza Mzee Dawson, yule Mzee akawatazama kisha akasema bila kujibu swali la Dawson

“Nimekuja kwa ishara yako Dawson, nimetoka mbali, nimesubiri kwa miaka mingi kukuambia kuwa Dunia ilikuwa ikikutafuta kwa miaka hiyo, nilikuficha kwa muda mrefu sana” Alisema Mzee huyo

“Wewe ni nani hasa?”

“P55 Mbaga” Alijibu Mzee huyo na kusababisha mshangao kwa Mzee Dawson ambaye alionekana kulifahamu jambo hilo

“Haiwezekani, wewe ni Mzee wa kanisa umeijuaje siri hiyo niliyoificha kwa muda mrefu!”

“Hukuificha siri hiyo, siri hii inajulikana ila kuwaka kwa saa hiyo ni ishara kuwa mapambano yanaanza upya! Mapambano ya kung’oa mizizi ya utawala huu wa Mabavu”

“Una maana gani?”

Mzee huyo alisimama kisha akasema

“Naitwa Mbaga, nilikuwa rafiki mkubwa wa Baba yako japo alinizidi umri lakini alinipenda sana. Baba yako alikuwa ni miongoni mwa Askari wa ngazi ya juu, wakati huo, akatoroka na nyaraka za siri ambazo alianza kuzisambaza kuhusu Urais wa Nchii namna unavyo rithishwa, uozo na ufedhuli uliokuwa umejaa serikalini, aliishia kuuawa huku Taifa likiambiwa kuwa Baba yako alikuwa ni muasi” Alimeza mate kisha akaendelea Mzee Mbaga

“Kabla ya kuuawa kwake alinipa kifaa maalum, akaniambia unatakiwa kuvaa saa mkononi mwako na wakati wa ukombozi utakapofika mimi nitakuja kukusaidia. Teknolojia hii iligunduliwa huko Ujerumani, mmoja wa Watu wa siri wa Baba yako walimwambia Rais juu ya Mpango wetu Mimi na Baba yako, nilitafutwa kila kona bila mafanikio yoyote yale, ndipo Baba yako akapiga simu ukiwa masomoni ukabadilishwa Ubin wako ili usitambulike, akakuandaa ukawa Mwanajeshi lakini Alipouawa ulikuwa bado hujamaliza Mafunzo ya Kijeshi Nchini Cuba, Baada ya Teknolojia kugundulika wao wakatengeneza ya kwao ili kujuwa muda na mahala ambapo nitawasha kifaa nilichopewa na Baba yako kama ishara ya uhuru na ukombozi” Aliendelea kusema Mzee Mbaga na kuwaacha akina Dawson kinywa wazi

Machozi yalimtoka Dawson akakumbuka jinsi Mama yake alivyomwambia mpango huo, kuanzia kipindi hicho aliivaa saa hiyo katika Maisha yake yote hadi anafikia uzee wa Makamo, alimkumbatia Mzee Mbaga. Taarifa hii ilikuwa ni ajendaa kuu kwa kila Rais aliyetokea katika ukoo wa kurithi nafasi ya Urais, alitafutwa sana Mbaga bila mafanikio na Marais Kadhaa waliopita.
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA

John Brain alikipataje kifaa hicho wakati yeye ni mzungu? Kama ilivyo kwa Ukoo uliorithi Urais wa Nchi hii, ndivyo ambavyo mtandao wa kigaidi ulivyorithiwa kutoka kwa Babu yake John, kwenda kwa Baba yake John hadi kumfikia John mwenyewe. Hawa wote walikuwa na kazi hiyo ya kuhakikisha P55 hafanikishi mpango wa kuikomboa Nchi hiyo, ilikuwa ni moja ya kazi alizokuwa akizifanya katika Bara lote la Afrika.

Ulinzi ukaimarishwa Ikulu ili kumlinda Rais, walimjua vyena huyo P55 Mbaga jinsi alivyo na hatari, mbinu za kivita na akili nyingi ya kupambanua mambo.

Muda huo Mzee Mbaga alikuwa akimalizia kumsimulia, ndio muda ambao Six na Malaika walikuwa wakifika nyumbani kwa John Brain, walionekana kuwa wachovu sana

“Brain! Ile ishara imejitokeza katika miili yetu, tuambie nini hatari iliyo mbele ya macho yetu” Alihoji Six

“P55 amejitokeza, ni faraja kwetu sababu tunaenda kuvuna kiasi kikubwa cha pesa endapo tutamuangusha kabla hajaangusha utawala wa Rais wa Nchi hii, nitaongea na Rais amuachie Jamaal ili atusaidie katika hili” Alisema Mzungu John Brain huku akiwa anawatazama vijana wake waliokuwa wamefungwa vifaa maalum katika miili yao ndio maana kifaa cha Mzee Mbaga kilipowashwa ishara iliwaingia, John alifanya hivyo sababu Six na Malaika walikuwa ndio Watu waliomsaidia kazi za Ugaidi kote Duniani, aliwaamini Watu hao kuliko hata alivyojiamini yeye mwenyewe ndio maana aliwapa hiyo siri

“Ataiangusha vipi Nchi yenye jeshi kubwa kama hii, atawezaje Mtu mmoja?” Aliuliza Malaika

“Vizuri sana, P55 hatokuwa peke yake ipo hatari akaungana na Dawson na Sande Olise sababu wote wanatajwa kuwa Waasi, P55 ambaye jina lake halisi ni Mbaga alishawahi kutajwa kama muasi miaka mingi iliyopita baada ya kufanikisha kuijuwa siri ya Watawala, ipo siri ndani ya Ikulu ambayo Mbaga anaijuwa na siri hiyo ndiyo nguvu ya Utawala huu wa Kurithi” Alielezea John Brain huku akiwa anawatazama Six na Malaika alionekana kuwa anahitaji zaidi kueleweka kwa kauli yake.

“Inasemekana aliyempa siri Mbaga ambaye ni P55 ni Mtu mmoja anaitwa Aboubakari, huyu alikuwa Mmoja wa Askari wa ngazi ya juu wakati huo, wakatengeneza Teknolojia ambayo imewekwa kwenye miili yenu. Mmoja wa watu wa karibu wa Aboubakari aliiambia Serikali wakati huo, Aboubakari akawa anatafutwa ili auawe pamoja na rafiki yake ambaye ni huyu Mbaga. Haikuishia hapo, inasemekana Aboubakari aliagiza Mtoto wake aliye nje ya Nchi kubadilishwa jina na Ubini ili asitambulike huku Mtoto huyo akiwa anapata elimu, baadaye alipata mafunzo ya Kijeshi. Teknolojia hiyo ilifungwa katika saa ambayo hata Mimi ninayo baada ya serikali kugundua Teknolojia hiyo, Aboubakari aliuawa na Jeshi lakini Mbaga alitoweka, Ndipo Baba yangu alipopewa kazi ya kumtafuta Mbaga lakini hakufanikiwa hadi alipofariki kisha kazi hiyo nikairithi Mimi, nimefanya kazi na Rais aliyepita kabla ya kuwachukua ninyi,,,,Huyu Mbaga ni sumu kwa Uongozi huu, hivyo ni lazima nimfyeke ili nifanikishe ndoto za Baba yangu katika Taifa hili ambalo yeye alikuwa na urafiki na Rais wa zamani wa Nchi hii, nafikiria hapo mtakuwa mmepata picha halisi ni kwanini namuita Mbaga kama kirusi” Alieleza bila kupumzika kisha akameza mate na kuendelea

“Mpango wao ulikuwa ni kusubiria hadi pale Mbaga atakapokutana na Mtoto wa Rafiki yake, hatujafanikiwa kumjua huyo Mtoto, kuwashwa kwa Mashine ya Mbaga ni ishara kuwa wamekutana na kupanga mipango ya kuipindua Nchi hii, ni hatari kama Sande na Dawson watajumuishwa” Wakati anaendelea kuwaeleza mara simu yake ikaita, akaona mpigaji ni Rais, haraka akaipokea

“Umefikia wapi John?” Aliuliza Rais baada ya simu kupokelewa

“Tunapanga mipango ya jinsi ya Kupambana na P55 Mbaga, unapaswa kumuachia Jamaal ili tuifanye kazi hii pamoja!”

“Una uhakika na usemalo? Kama nitamuacha Jamaal mtaifanya kazi kwa pamoja bila kunigeuka?

“Hii kazi nimeirithi kama ambavyo wewe umerithi Urais, muache Jamaal awe huru. Baada ya kumsambaratisha P55 nitahitaji ujira mkubwa kuliko tulioahidiana sababu tunapambana vita viwili kwa wakati mmoja, Tunamtafuta P55 wakati huo tunawasaka Dawson na Sande Olise” Alisema John bila kupindisha maelezo

“Sawa! Mchana mje kumchukua Jamaal na kazi ianze mara moja, siwezi kuwa Rais niliyekaa madarakani kwa muda mfupi, sitaki kuuangusha ukoo wetu, mtasema mtachotaka zaidi hata kama ni mgodi wa Dhahabu nitawapa, piganeni vita vya siri huku mkijuwa kuwa mnaenda kuwa Mabilionea wa kutupwa” Ilikuwa ni kauli ya mwisho ya Rais huyo kijana kuliko wote waliopita kisha simu ilikatika, John akawatazama vijana wake akawaambia

“Maneno yangu pekee hayawezi kutosha kuwaeleza umuhimu wa hili, mmesikia maongezi mnatakiwa kujuwa kuwa tunaenda kuwa Mabilionea wa Kutupwa, kama mtahitaji nyongeza ya Askari nitapiga simu Al Qaeda, nitazungumza na Ibnu Abassi Mtoto wa Osama” Maneno ya John Brain yaliamsha tabasamu kwenye nyuso za Six na Malaika.

Mbele ya pesa ndefu vile, Six na Malaika waliona ni vema kuielekea kazi hiyo ngumu iliyo mbele yao huku wakijuwa wanaenda kupambana na Watu wagunu kiasi gani.

Jioni ya siku hiyo baada ya Mchana wa kumtoa Jamaal ndani ya ikulu kupita, ilikuwa ni ndani ya jengo la siri la Zola, watu watano walikuwa wameketi wakiwa wameizunguka meza ya duara, alikuwepo P55 Mbaga, Dawson, Chande, Kisko na Mtaalam Sande Olise. Mbaga alikuwa akipanga namna ya kuuangusha utawala huo ambao John Brain aliapa kuulinda kwa kutumia mbinu za Kigaidi kwa Maslahi yao Binafsi na vijana wake wawili waliounda kundi hatari Duniani kote la MAFIA GANG

“Ndani ya Ikulu kuna fimbo ya Almasi, fimbo hii ni siri ya utawala huu wa Kurithi ambao umekuwa ukiitawala hii Nchi kwa namna watakavyo wao bila kujali chochote, ukiwa nje unaweza ukahisi mambo yapo sawa lakini ukisogea ndani utagundua kuwa ni Nchi inayoendeshwa kwa utashi wa mtawala katili asiyejali utu” Alisema P55 Mbaga kisha akaendelea kusema

“Ndani ya Serikali hii ukionekana una viashiria vya kwenda kinyume na Mtawala utapewa kesi ya Uasi, utasakwa kila kona ili uuawe. Askari wengi wamepotea bila kujuwa walipoelekea baada tu ya kugundua siri ya Mtawala, Dawson!!” Alimgeukia Dawson aliyekuwa amezama katika fikra za kumsikiliza

“‘Muda mrefu nimekuwa nikikufuatilia baada tu ya kurejea Nchini ukitokea Cuba kwenye mafunzo ya Kijeshi, nilikufuatilia kila hatua hata ulipochimba andaki na kufadhili ujenzi wa kanisa, nilipoona Mauwaji ya kutisha ndani ya kanisa niligundua ndio muda muafaka wa kukupa taarifa juu ya nini ufanye, sikutaka uje kufa sababu Watawala hutumia mtandao mkubwa wa kigaidi kusaka Watu wanaoenda kinyume nao”

“Tunafanya nini kuuangusha utawala huu ili Nchi iwe huru?” Aliuliza Sande Olise, macho ya Mbaga yalitua ukutani ambapo kulikuwa na kalenda iliyoonesha Mwaka huo, ilikuwa ni Mwaka 1986, akasogea na kuchorea moja ya tarehe

“Mpango ulikuwa Novemba 1980 lakini ilishindikana sababu nilikuwa nakamilisha majukumu mengine ya siri, mpango mpya utaenda kufanyika Baada ya siku mbili, siku ya tatu kutakuwa na taarifa nyingine kabisa, umeuliza tutafanya nini? Nina imani sote hapa ni wanajeshi tumepishana vyeo tuu lakini haituzuii kuifanya hii kazi kwa pamoja” Mbaga alirudi kukaa huku mikono yake akiiegemeza kwenye meza akamgeukia Sande

“Nimesikia mengi kuhusu wewe, usiku wa siku ya Tukio utaenda Ikulu kwa ajili ya kuchukua fimbo ya Almasi ambayo ndiyo hazina ya utawala huu, Mimi, Dawson na Kijana mmoja tutakuwa na jukumu la kuhakikisha unaingia na kutoka Ikulu ukiwa salama!!” Macho ya Sande yakazama ndani kidogo kwa mshangao kisha akauliza swali

“Haitakuwa rahisi kama unavyofikiria, Ikulu inalindwa na Askari wengi tena kwa wakati huu ambao tumetajwa kuwa Waasi naamini ulinzi utaongezeka zaidi, hakuna mbadala wa hii njia?”

“Ha!ha!ha! Sijawahi kuwa na Plan B kwenye mipango yangu Olise, nina Plan A tu ambayo ni kuingia Ikulu, nitakupa Ramani ya kuingilia huko”

“Bado sielewi hili jambo linaenda kuwaje, nahisi hatari ya kupoteza Askari wengine ndani ya muda mchache sana!! Ilipo fimbo, kuna ulinzi wa Askari na Teknolojia ya Umeme, istoshe kuna nyaraka maalum zitakazo hitajika, ikiwa itachukuliwa fimbo bila nyaraka ni sawa na kutia mafuta katika gari bovu” Alisema Dawson ambaye alionekana kufahamu kidogo kuhusu Utawala huo.

“Ramani hii hapa” Mbaga alitoa ramani kutoka katika shati lake chakavu, ni wazi alikuwa amejipanga sana. Wote wakatupa macho yao kwenye ramani hiyo ambayo ilionekana kuwa ya kizamani sana. Dawson akanyanyua kichwa akamtazama Mbaga kisha akamwambia

“Hii ramani ni ya muda mrefu, mengi yamebadilika Kwa sasa. Inatupasa kuwa na ramani ya wakati huu”

“Hii ramani bado inaishi, hii ndiyo ramani ya kwanza ya jengo la Ikulu ambalo lilijengwa na Mtawala wa kwanza. Kilichobadikila hapa ni Teknolojia ya Ulinzi wa nyaraka na fimbo hiyo”

“Hebu niirudie” Alisema Dawson, akaichukua ramani na kuipitia tena ndipo akakubaliana na maneno ya Mbaga kuwa ramani ya jengo hilo ni ile ile. Akampatia ramani mhusika ambaye anatakiwa kwenda kuiba hiyo fimbo na nyaraka ndani ya Ikulu, alikuwa ni Sande Olise Mzee wa Operesheni Upepo.

“Utapitia hapo A ambapo kuna shimo la maji taka, kwa jinsi hali ilivyo ni wazi eneo hilo lina walinzi wa kutosha hivyo ni lazima upate mbinu ya kuwaondoa kabla hujazama hapo bila kuonwa, utaenda kutokea hapa B ambapo kuna shimo lenye hayo maji taka, kisha hapa C ndio kuna maungio yanayotoa maji kutoka katika vyumba vyote vya Ikulu zikiwemo bafu na vyoo” Pua za Sande olise zikavuta picha namna harufu ya vinyesi itakavyokuwa inammaliza

“Huu mshale mwekundu ndio uelekeo wa kilipo chumba cha Rais, utaenda kutokea kwenye Choo yake! Ni sehemu itakayokutaka kuvunja moja ya chemba za kuhifadhia Vifaa vya Hewa safi inayoingia humo. Ukicheza makida makida utajikuta unasababisha shoti sababu utakuwa na maji maji mwilini mwako na endapo shoti itatokea basi alamu maalum italia kuashiria uwepo wa hatari, utauawa” Maelezo haya yalimfanya Sande ajikunje kama Panya mwenye homa kali, alishahisi harufu ya kifo.

“Utapita katika chemba zote ukiwa na kitambaa ambacho kitakuwa kwenye nailoni, kitakusaidia kufuta maji yako kabla hujapita eneo husika, kisha utasogea kwa umakini sana ndipo utaona eneo lenye kizuizi chenye matundu, utapaswa kufungua kizuizi hicho kwa kutumia Star!! Utasukuma kizuizi utajikuta umetokea chooni kwa Rais ambapo ndio sehemu utakayoanzia mpango rasmi, eneo hilo halina kamera isipokuwa ukitoka na kufika chumbani kwa Rais kuna Kamera maalum ambazo huwashwa pindi Rais anapokuwa ametoka!! Hivyo unatakiwa kusubiria hadi Rais atakapoingia chumbani kwake!!” Wote walikuwa makini kumsikiliza Mzee Mbaga ambaye alionekana kuijuwa Ikulu vilivyo

“Utachagua mambo mawili, kuiba funguo za Ofisi ya Rais au kumteka Rais pindi atakapoingia Chumbani kwake ili akupeleke ofisini kwake ambako kuna hiyo chemba ambayo ukiingia unaenda kutokea kwenye chumba chenye nyaraka na fimbo, Hakuna anayeweza kuishika hiyo fimbo wala nyaraka sababu kufanya hivyo kutapelekea kufa mara moja kisha taarifa itawafikia walinzi”

“Kama siwezi kuishika nitakuwa nimeenda kufanya utalii na kutoka?” Aliuliza Sande Olise kisha wote wakacheka

“Nitakupa kifaa maalum kitakachokusaidia kunyonya mionzi hiyo lakini kwa muda wa sekunde 30 tu, ukishindwa kutoka ndani ya sekunde hizo basi utafia humo sababu kifaa hakitakuwa na uwezo wa kupambana na mionzi kwa zaidi ya sekunde hizo, hapo utakuwa umefanikiwa kunyakuwa nyaraka hizo na fimbo” Maelezo yalikuwa marefu lakini yalieleweka kichwani kwa Sande Olise.

Upande wa pili, Six na Malaika walitaka kufanya jaribio lingine la kufuata ishara ya redio Call wakiamini Watu wanaowatafuta watakuwa katika jumba hilo, ni kweli Dawson na Watu wengine walikuwa humo. Wakatoka kuelekea huko Kwenye jumba ambalo muda huu Mbaga alikuwa akipanga mipango ya jinsi gani watamuangusha Rais huyo.

Mwendo wa masaa mawili Six na Malaika walikuwa wakitafuta eneo lililojificha ili wapaki gari yao ndogo ambayo ilikuwa ikitumika kufanyia matukio hayo, kama kawaida yao Malaika ndiye aliyekuwa akifanya kazi ya kuelekea huko wakati Six akiwa kama mzimu wa kulenga shabaha ya mbali. Lakini safari hii walikuwa makini sana hasa baada ya kusikia kuwa P55 amejitokeza tena kukiwa na uwezekano kuwa anaweza akaungana na Mzee Dawson na Sande Olise, jengo hilo lilikuwa na kamera kila kona hivyo kitendo cha kulisogelea unakuwa umeshaonekana.

Basi Malaika akautumia uzio wa ukuta wa jumba hilo ambao ulikuwa mrefu, giza lilishaanza kuingia, alichofanya Malaika ni kuchumpa hadi ndani kwa kutumia upande wa nyuma, akapewa ishara na six aliyekuwa juu ya Ukuta kuwa hakuna ishara yoyote kuwa ameonekana, umakini wa Six uliongezeka akiwa anazidi kutupa macho yake kwenye jumba hilo ambalo lilikuwa likiwaka taa kupitia kwenye baadhi ya vioo vya madirisha.

Malaika akasogea hadi kwenye mlango wa Nyuma ambao ulikuwa ukionesha ndani ya jengo hilo,akafanikiwa kuiona meza nyeusi ya duara ikiwa na karatasi nyingi, akajaribu kuusukuma mlango huo akaona ni mwepesi ukafunguka bila kutumia nguvu, akampa ishara Six awe makini kumlinda. Akazama humo ndani kwa tahadhali akiwa anajuwa yupo karibu na hatari kiasi gani, bastola yake ikawa ya kwanza kukutana na mwanga wa taa kisha sura yake ikatokea.

Akaangaza huku na kule kisha kwa umakini akawa anaingia chumba kimoja badala ya kingine, jumba hilo lilionekana kuwa kimya sana wakati muda mchache uliopita Mbaga alikuwa akisuka mipango ya jinsi ya kuingia Ikulu, baada ya dakika kama tano Malaika alifanikiwa kujihakikishia kuwa hakukuwa na Mtu yeyote ndani ya jumba hilo.

Akaongeza umakini zaidi aliposogea karibu na meza ambayo ilikuwa na karatasi kadhaa juu yake huku sauti ya Six ikirindima kwenye masikio yake ikiwa inamuarifu hali ilivyo kwa upande wa nje, akafanikiwa kukuta ramani, akaikusanya na kuitia kwenye mfuko wake wa suruali kisha akaangaza huku na kule kisha akatoa simu na kupiga picha eneo hilo ambalo lilionekana kuwa na mvinyo na glasi kadhaa ambazo zilikuwa zina vinywaji vilivyo karibia kuisha.

“Walikuwepo hapa, nimekuta ramani” Alisema Malaika, hakupoteza muda akatoka ndani ya jengo hilo. Nje ya jengo hilo kulikuwa na gari moja iliyo haribika na kuchakaa, Mbaga na Vijana wake walikuwa wamejificha hapo kisha Mbaga akawaambia

“Tusogee mbele” wakasogea kidogo ili kuzidi kujificha ambapo Malaika alikuwa akikatiza eneo hilo, akasikia mchakacha kama wa kiatu cha Mtu, alikuwa ni Dawson ambaye hali yake ilibadilika ghafla akataka kuanguka lakini Kisko alifanikiwa kumzuia asiguse majani yaliyo kauka.

Malaika akachomoa Bastola yake huku akisikia sauti ya Six ikimuuliza

“Unahisi nini?” Malaika hakujibu, akazidi kuwa Makini huku macho yake akizidi kuyakaza kutafuta nuru eneo hilo ambalo lilikuwa kiza, ghafla akamuona Mbwa akikimbia, ndipo akashusha Bastola yake

“Ni mbwa!!” Akajibu Malaika akiwa anaweka Bastola yake kiunoni kisha akakimbia kuelekea mahali alipo Six

Mbaga akamshukuru yule Mbwa kwa jinsi alivyowaokoa kutoka mikono ya Malaika, wakahakikisha Six na Malaika wametoweka pale ndipo wao wakarudi ndani ya Jengo hilo la kifahari kisha wakafunga milango yote ambayo ilikuwa ikifungwa kwa Umeme

“Lengo lilikuwa nini?” Aliuliza Sande Olise ambaye alikuwa amesimama mbele ya Mzee Mbaga, sura yake ilionesha kukerwa na mbinu ile

“Wameshajuwa kuwa tulikuwa hapa umeridhika? Je kama tungelipatikana pale tukiwa tumejificha tena bila silaha yoyote?? Tungekufa kama Mizoga ya Mbwa kirahisi tuu” aliongeza Sande huku Mbaga akicheka

“Nyote ni Majasusi wa Kisasa, bado hamna mbinu za kumkwepa adui kwa vita baridi. Kibaya zaidi mmeaminishwa kuwa Bastola ni kiungo muhimu kufanikisha kazi zenu, walisahau kuwaambia kuwa unaweza kushinda vita bila kumwaga damu” Wote wakawa makini kumsikiliza Mbaga

“Ramani halisi ni hii hapa…( Mbaga akatoa Ramani )” “Na ile tuliyoiweka pale kwenye meza” Akauliza Kisko

“Nenda kakae na Dawson anahitaji Mtu wa kumuuliza mambo kule” Kisko akaondoka pale akawaacha Chande, Mbaga na Sande Olise

“Ile ni ramani feki, ikiwa na mpango feki wa siku halisi ya tukio letu. Tutawahadaa siku ya Tukio ili tufanikishe mipango yetu bila majibizano ya Risasi, Ramani ile inaonesha muda halisi wa tukio letu lakini tukio litafanyika katika Jumba la Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa, na tukio litakuwa ni kumuuwa!! Wataweka akili yao huko kufikiria watatunasa wakati huo sisi tunafanya mpango wa kuingia Ikulu kufanya tukio” Chande akajikuta anapiga makofi kwa kumsifia Mbaga ambaye kwa hakika mpango wake ulikuwa bora na salama zaidi.

“Bado naiona hatari mbele yetu ikiwa sasa wanajua muda na tarehe ya tukio letu hata kama tumewaingiza choo cha kike, ni bora tubadili siku ya tukio” Akasema Sande Olise, alionekana kutofurahishwa na Mbinu ya Mbaga japo Mzee huyo alikuwa na mbinu nyingi za kijeshi zilizoogopwa kuliko maelezo, Mbaga akamsogelea Sande akamwambia

“Najuwa hofu yako inatokana na nini, pengine ni sababu unafanya kazi na Mtu usiyemzoea tena kwenye mpango ambao unahisi utagharimu Maisha yako, niamini tuifanye kazi hii ngumu kwa ajili ya Wananchi Masikini huko nje ambao wana tegemeo kubwa na kuliombea Taifa hili” Mbaga akampa mkono Sande ambaye licha ya maneno yale hakufurahi, akampa pia mkono lakini kinyonge sana kisha akatabasamu ili kumfurahisha Mbaga.

Usiku huo, taarifa ilimfikia John Brain, akaikagua vizuri ramani hiyo waliyoichukua kwenye Jumba la siri la Zola. Ramani ilikuwa na maelezo mengi ya tukio la kuuawa kwa Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa, John Brain akatafakari kisha akawauliza Six na Malaika

“Ni rahisi kupata taarifa nyeti kama hii tena bila hata kumwaga damu? Yaani mpango mzito kiasi hiki unaswe kirahisi!” Alionesha tabasamu katika sura yake kisha akawauliza tena

“Inawezekana P55 anataka kuanza na Watu wa Usalama wa Taifa? Hapana, hata yeye alikuwa Mtu wa Usalama wa Taifa, hawezi kuuwa Familia yake, mna hakika hakukuwa na Mtu kabisa?”

“Ndio palikuwa kimya mithiri ya Bahari ituliavyo nyakati za Masika” Alijibu Malaika ambaye ndiye aliyeingia hapo ndani kuchukua ramani

“Six, jicho lako halikuona kitu cha ziada?” Six akatikisa kichwa kama ishara kuwa hakuona kitu chochote chenye kumtia mashaka.
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI

“Kama huu ni mpango wa kutuzuga, kama ni mtego wa kutaka kuwauwa, kama kweli ni nani anaweza kuuanika Mpango huu kirahisi rahisi? Jiandaeni kwa vita” Akasema John Brain kisha akawaruhusu waweze kuondoka, Muda huo John Brain aliutumia kumpigia simu Mtu wake wa Karibu zaidi ambaye alikuwa akishikiliwa na Rais, alikuwa ni Jamaal ambaye sasa yupo Uraiani.

“Jiandae kwa vita!” Akasema John Brain kisha akakata simu bila kusikiliza jibu la Jamaal.

Siku iliyofuata Usiku ambayo ndiyo siku ya maandalizi rasmi ili kesho yake wakatekeleze mpango ndani ya Ikulu, Mbaga alimfuata Dawson ambaye alikuwa kitandani akiwa anaumwa akwamwambia

“Ndoto yako inaenda kutimia, Baba yako atafurahi kusikia kuwa Waliomuuwa wameng’oka kwenye madaraka yao” Dawson alikuwa katika hali mbaya lakini alimudu kusema

“Nawaombea sana, sina shaka na uwezo wako sababu nilishausikia zaidi ya mara tano” Walikuwa katika Jumba lingine ambalo walidhamiria kumuacha hapo Dawson

“Kila jambo lina wakati wake, wakati wa wao kulipa kwa mabaya yao ndio huu Dawson” Alisema Mbaga kisha akamshika mkono Dawson kama ishara ya kumuunga mkono katika nyakati ngumu ya kuumwa, kila alipokooa Dawson alitema damu lakini haikumkatisha tamaa alionekana kutabasamu kila wakati japo alikuwa na maumivu makali, Usiku huo Mbaga alielekea katika makazi yake ya siri akarudi na Tranka lililo sheheni baadhi ya vifaa vya kazi na picha za ukumbusho za wakati huo akiwa askari, picha nyingine alipiga na Mama na Baba yake Dawson!!

Akawaonesha ni jinsi gani yeye na Baba yake Dawson walikuwa wanajeshi wenye vyeo vikubwa kabla ya sakata la kuiba siri na hatimaye kutafutwa kama waasi. Mbaga akapata muda wa kuzungumza na Sande Olise

“Sande hii ndio njia pekee endapo tutashindwa katika hili basi hakuna atakayekuwa hai, tupo mawindoni hatuna budi kuwa makini na kila hatua tupigayo” Alisema akiwa anampa kifaa chenye kunyonya mionzi ambayo atakutana nayo ndani ya chumba chenye fimbo na nyaraka.

“Hili ni jukumu zito sana kwangu, nimefanya operesheni ngumu zilizonipa sifa ndani na nje ya Serikali lakini hii inaweza kuwa ngumu kuliko hata ninavyoweza kuelezea” Alisema Sande akiwa anakitia kifaa hicho ndani ya Begi lake baada ya kukiangalia kwa makini, hakikuwa kifaa kigeni kwake

“Ni lazima tulikamilishe hili kama tuna hitaji kuliokoa Taifa, Wananchi wengi ni vipofu kuona yanayofanyika, itakuwa ni dhambi endapo tutakaa kimya ilhali Nchi yao inaendeshwa ndivyo sivyo” Akasema tena Mbaga akiwa anampa Sande Staa kwa ajili ya kufungulia baadhi ya nati atakapolifikia chemba maalum karibu na Choo cha Rais, akaiweka Staa hiyo ndani ya Begi lake jeusi la mgongoni.

“Tukifanikiwa hili una mpango gani?” Akauliza Sande akiwa analifunga begi lake

“Kwenda kuishi Maisha ya Shamba, sitafanya kazi ya kijeshi tena baada ya kuwa tumesafisha majina yetu, nyie mtaamuwa nini mnataka kufanya baada ya hapo, kila la kheri Sande” Akaongea kisha akamshika Bega, akatoka na kuelekea chumba kingine ambacho walikuwemo Kisko, Chande na Dawson.

“Nifuateni” Akasema Mbaga, Kisko na Chande wakamfuata Mbaga wakamuacha Dawson ambaye ni mgonjwa akiwa amelala Kitandani, wakati wao wanatoka Sande aliingia akiwa anatabasamu kidogo ili kumpa tumaini Dawson.

Mbaga akawaingiza vijana hao wawili katika chumba kingine ambacho kilikuwa kitupu kisha akafunga mlango, akawauliza

“Mko tayari kwa ajili ya kesho yenu na kesho ya Taifa zima?” Kisko na Chande wakatazamana kabla ya kuitikia kwa pamoja

“Ndio!!”

“Basi vizuri, nawapa majukumu ya Kesho. Kufanikiwa kwa mpango huu kutategemea zaidi na ukamilifu wenu kwenye mpango huu.

Kisko na Chande nyie sura zenu ni ngeni sana kwenye macho ya Majasusi na wapelelezi, hata polisi sidhani kama walishawahi kuziona sura zenu. Kazi yenu itakuwa ni kuzuga Askari watakao kuwa wanalinda Ikulu, mkifanya kosa lolote mnauawa sababu Ulinzi umeimarishwa sana baada ya sisi kutajwa kama Waasi, wakati Sande anaingia kwenye chemba kazi yenu itakuwa ni kuzuga Askari hadi pale nitakapowaeleza kuwa Sande amekwisha zama ndani ya chemba, mna jukumu la kumlinda kwa hali na mali”

“Tunaweza vipi kuzuga Askari wenye silaha nzito tena Ikulu?” Akauliza Chande

“Hilo halitowezekana ni sawa na kuuza Maisha yetu” Kisko akadakia

“Nje ya jengo la Ikulu, Watu hupita japo sio kwa wingi huo, miongoni mwa wapitaji mtakuwa ninyi, chemba ambayo Sande anatakiwa kuingia iko nyuma ya geti dogo la kuingilia Ikulu kupitia nyuma ya jengo hilo, eneo hilo Watu hawapiti, na hulindwa sana. Mnachotakiwa kufanya ni kuhakikisha mnanunua muda wao na kuiba akili yao kwa muda wa sekunde 30, muda huo Sande atakuwa amefanikiwa kupenya” Alieleza Mbaga, huku mikono yake yenye misuli mingi ilitumika kuwapa picha halisi ya nini Mbaga alikuwa anataka., akafanikiwa kuteka akili zao kisha akawapa mpango wa kuhakikisha wanafanikisha zoezi hilo.

Akili zao zilishachoka, muda ulionesha kuwa ni saa Sita Usiku, Mbaga alipogundua akili za vijana hao haziwezi kuendelea kumsikiliza akawaruhusu kwenda kulala lakini Chande akauliza swali la mwisho ambalo lilionekana kumfikilisha sana.

“Wakati sisi tunatekeleza majukumu hayo wewe utakuwa wapi na unafanya nini? Tunajua Baba Dawson ni mgonjwa hawezi kushiriki mpango huu” Alipouliza alimtazama Kisko, ikaonesha ni wazi kuwa alichouliza kilikuwa kikizunguka hata kwenye kichwa cha Kisko.

“Vizuri sana, nilijuwa akili zenu zimechoka. Wakati mnatekeleza majukumu hayo Msisahau kuwa kuna Watu wana ramani feki, lengo lilikuwa kuwauza Watu wale sababu ni hatari kuliko hata hao Askari waliojazana Ikulu kumlinda Rais, Mimi nitaenda huko kupambana nao, nitahakikisha hawashtuki kuwa Ikulu imeshavamiwa” Kisko na Chande walijikuta wakipiga makofi kumsifu Mbaga kwa jinsi alivyousuka mpango huo.

“Nendeni mkapumzike” Alisema Mbaga, Kisko na Chande wakaenda kulala ili kupata muda mzuri wa kutuliza akili zao, Mbaga aliporejea chumbani kwa Dawson alimkuta Dawson akiwa anazungumza na Sande Olise.

Macho yao yalikuwa yakibubujikwa na machozi, kilichowaumiza zaidi kilikuwa ni kifo cha Inspekta Zola ambaye alikuwa ameuawa ndani ya Ikulu.

“Poleni, naona mmezama katika kumbukumbu fulani inayowaumiza, sitaki kujuwa mnafikiria nini lakini naamini mioyo yenu ipo tayari kuhakikisha Wabaya wanalipa kwa ubaya wao, Sande nenda kapumzike una jukumu zito sana masaa machache yajayo” Alisema Mbaga kisha macho yake akayatupa katika saa iliyopo mkononi mwake, akaona ni saa 6:30

Sande aliondoka pale na kuelekea chumbani kwake, Dawson akamtazama Mbaga ambaye alikuwa ni rafiki wa Baba yake akamwambia

“Nakutazama kama kioo kwangu na kwa vijana wangu, ushujaa na uzalendo ulionao unastahili kila kilicho bora kwako, hukuwa Askari uliyeishi kwa mkate bali ulisimama kulinda na kutetea maslahi ya Nchi hii”

“Dawson! Maneno yako ni kama ya Baba yako, umefanana naye sana karibia kwenye kila kitu, nikuonapo naona kama vile Aboubakari yupo hai alafu ninafanya naye mpango huu”

“Nawatakia kila la Kheri, nina imani mtarudi mkiwa hai”

“Usijali Dawson, utabakia hapa wakati tutakapokuwa tumeenda kwenye jukumu zito”

Usiku huo haukuwa usiku wa upande mmoja, kichwa chenye akili nyingi na gaidi anayetafutwa Duniani John Brain alikuwa akizungumza na vijana wake, John akawaambia wanatakiwa kuwa makini sababu kesho haitokuwa rahisi kwao.

“Jamaal utarudi Ikulu kuhakikisha usalama wa pale na Rais, Six na Malaika mtaenda kwenye huo mpango ili kama tutakuwa tumeuzwa basi nyie mtawasiliana mara moja ili wote muwe upande wa tukio halisi, muda walioupata umetosha wao kupanga kwa uhuru nini wanataka kufanya.” Alisema John Brain kisha akapiga pafu la sigara kidogo

“Hilo limeisha Mkuu, imani yako kwetu ni heshima tosha. Tutatekeleza jambo hili kwa jinsi itakavyowezekana” Alisema Jamaal, Six na Malaika wakatazamana, kila mmoja aliujuwa uwezo wa Jamaal kwenye suala la mapigano na matumizi mazuri ya akili ndio maana alifanikiwa kumuuwa Makam wa Rais akiwa nyumbani kwake tena akiwa na ulinzi wa kutisha.

“Six na Malaika nawasistizia kuwa ni lazima muwe makini kuliko wakati wowote ule, kazi yako Six ni kumlinda Malaika kama kawaida yako ili kuhakikisha anaifanya kazi na kutoka akiwa salama. Pesa tutakayovuna ndani ya Nchi hii ni nyingi kuliko hata tulizovuna kwenye mataifa mataifa ya Mwisho ya Chad, Benin na Angola, ni suala la kuchagua kati ya Kifo na Utajiri”

“Tumekuelewa Mkuu” wakaitikia kwa pamoja, kisha John Brain akampigia simu Rais na kumuahidi kuwa atahakikisha anakuwa salama na watammaliza Mbaga na washirika wake.

Chapter FINAL

VITA NDANI YA KIZA

Majira ya saa 12 Asubuhi, siku hiyo kulikuwa na hali fulani ya mawingu na kusababisha baridi kuanza mapema sana, wengi waling’ang’ania shuka zao lakini wazee wa kazi walikuwa macho tokea saa 10 Alfajiri, John Brain alipanga Watu wake sawa sawa huku Mbaga akiwapa maelekezo ya mwisho ya nini cha kufanya huku akiwasistizia kuwa yeye hana Plan B katika mipango yake.

Pumzi za Sande Olise ambaye alipewa mtihani mzito zilisikika na kumfanya Mbaga atambuwe kuwa alikuwa ni mwenye wasiwasi wa kuifanya kazi hiyo, akamfuata na kumtuliza

“Ondoa wasiwasi Sande, baada ya mpango huu kufanikiwa tutakuwa Watu wengine kabisa! Unaweza kufanya hivyo, kumbuka wewe ni Jasusi na lengo la Jasusi ni kukomboa Nchi yake” Sande aliitikia kwa kichwa akiwa anaingia ndani ya gari ndogo Nyeusi ambayo Mtaalam Mbaga aliingia humo pia.

Kisko na Chande kila mmoja alikuwa na pikipiki huku Mbaga akiwa amewajaza nini cha kufanya, manyunyu kidogo yalikuwa yameanza kudondoka. Wote walikuwa wameunganishwa na mtambo mmoja wa kunasa na kutoa sauti, yaani walikuwa wakisikilizana, Safari ilianza huku Dawson akiwachungulia akiwa dirishani, walipofika nje ya nyumba wakakutana na Barabara ya lami, jumba hilo lilikuwa nje ya Mji, Kisko na Chande wakashika upande wa Kusini, Sande na Mbaga wakashika upande wa kaskazini yaani kila mmoja alielekea upande wake.

Upande wa pili, Jamaal alikuwa akifanya safari ya kuelekea Ikulu ambako Sande na Mbaga walikuwa wakielekea, wakati huo John Brain akiwa ofisini kwake akiratibu mipango hiyo kwa pande zote mbili yaani Ikulu kwa Jamaal na kwa upande wa Malaika na Six ambao walikuwa wakielekea nyumbani kwa mkurugenzi wa idara ya Usalama wa Taifa.

Chande na Kisko walikuwa wa kwanza kufika eneo la Ikulu kwasababu walitumia Pikipiki, wakagawana kama

walivyoelekezwa, mmoja akasimama mbali ya eneo hilo ili wasije kushtukiwa na Askari ambao walikuwa wakifanya ulinzi, na mwingine pia alisimama mbali lakini wakiwa wanawasiliana. Walichoelekezwa ni kusubiria ishara ya Mbaga ili wafanye tukio, aliwapa mbinu ya kusababisha ajali eneo hilo ili kununua muda wa walinzi hao. Dakika 15 baadaye Sande na Mbaga walikuwa wamefika, nao wakapaki gari kwa mbali kidogo katika eneo ambalo isingelikuwa rahisi kwa Walinzi kuwaona.

“Una dakika tatu za kuufikia ukuta mrefu wa Ikulu, ni lazima uhakikishe hakuna anayekuona, ukishafika nijulishe haraka iwezekanavyo.” Alisema Mbaga, haraka Sande akashuka akiwa na kibegi mgongoni. Akakatiza chini ya miti yenye mauwa yanayonukia, muda huo mvua ilikuwa ikinyapia kwa karibu, walitakiwa kuwahi kabla ya mvua ili sauti ya ajali isikike. Kwa umakini wa Sande akafanikiwa kufika karibu na ukuta huo ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa umezungukwa na Kamera, akafungua begi na kutoa koti la Kijeshi lenye Nyasi bandia ili aendane na mazingira ya eneo lile ambalo lilikuwa kijani na nyasi fupi zilizofanya eneo hilo kuvutia zaidi.

Akaruhusu kinasa sauti kunasa sauti yake

“Nimeshafika” alisema Sande huku akiwa analala chini ili ajivute taratibu kusogea karibu na chemba hiyo ambayo ilikuwa ikilindwa na walinzi wawili warefu wenye Bunduki. Haraka Mbaga akapiga simu kwa Kisko na Chande kuwa wafanye tukio, vijana hao bila woga wakakanyaga mafuta ya pikipiki zao ili wagongane mbele ya jengo la Ikulu ambalo ilikuwa ni kawaida Watu kupita hapo wakiwa na Pikipiki au magari na wengine kwa miguu lakini upitaji ulikuwa wa kitaratibu mno, sauti ya kuvutwa kwa Pikipiki hizo zilisikika kwenye masikio ya Walinzi hao ambao waliweka umakini wa kuendelea kuzisikiliza.

Sande akafanikiwa kuwaona Askari waliokuwa wakilinda Chemba hiyo wakitazama barabarani kuona ni Nani anavuta moto kiasi hicho, akagundua itakuwa ngumu kwa walinzi hao kusogea, taratibu akavuta Kisu, sekunde sita baadaye ukasikika mlio wa ajali na sauti za kulalamika, ajali hiyo ilipangwa makusudi, Mlinzi mmoja wa chemba akamuacha mwenzake pale akaenda kuangalia ni nini kimetokea huku walinzi wengine wakikimbilia huko mara moja, Sande akaona ni bora autumie mwanya huo kufanya tukio, haraka akachomoka na kumkita kisu cha shingo.

Mlinzi huyo ambaye alionekana kutaka kuangukia kwenye Chemba hiyo, Sande akamdaka kisha haraka akalifungua chemba hilo lenye maji taka akamtia humo kisha mwenyewe akaingia humo, alafu akalifunika chemba hilo kisha akampa taarifa Mbaga kuwa amefanikiwa kuzama ndani ya Chemba.

Mbaga alipoona kila kitu kimeenda sawa akawasha gari lake, mara akaliona gari la wagonjwa likiwa linachukua miili ya Sande na Kisko, akaamini wapo salama. Akatimka na kuelekea nyumbani kwa Mkurugenzi wa idara ya Usalama wa Taifa ili kwenda kuwazuga Malaika na Six.

Ndani ya ofisi ya Rais, Jamaal alikuwa anazungumza na Rais huyo huku akimwambia kuwa amekuja kwa ajili ya kuhakikisha anakuwa salama, akawekwa Kama mlinzi binafsi wa Rais wakati Rais akiwa anaendelea na majukumu yake Jamaal akawa anacheza eneo hilo, hakuna aliyefahamu kilipo chumba kinachohifadhiwa nyaraka na fimbo zaidi ya Rais mwenyewe ndio Maana Sande alitakiwa kuhakikisha anamteka Rais huyo.

Basi, ndani ya chemba Sande Olise alizidi kusogea akiwa na ramani iliyochorwa na Mbaga, akawa anapita kama ramani inavyosema. Harufu ilikuwa kali sana lakini Sande hakujali zaidi alifanya haraka kuvuka ili harufu isimharibie mpango, ndani ya dakika 30 Mtaalam Mbaga alikuwa ameshafika eneo la tukio, akapaki gari yake mbali na eneo hilo huku akiwa na taarifa kuwa John Brain hupendelea sana walengaji, akajuwa tu eneo hilo haliwezi kukosa mlengaji. Alikuwa na begi lake, akasogea katika ghorofa moja ambalo lilikuwa likitumika kama Hoteli, akapandisha juu kabisa ya jengo hilo akiwa anaitazama nyumba ya Mkurugenzi huyo kwa usawa, maana ilikuwa ya ghorofa pia, akatafuta mahali akajibanza akafungua Begi lake, kumbe alikuwa na Bunduki ya masafa marefu, hakuwaambia akina Sande kuwa alikuwa na mpango wa kufanya Mauwaji ya kweli kwa Mkurugenzi huyo ambaye hadi kufikia muda huo alikuwa nyumbani kwake.

Akaweka vizuri Bunduki yake, alikuwa na kisasi kizito na Mkurugenzi huyo ambaye ndiye aliyeratibu mauwaji ya Aboubakari ambaye ni Baba yake na Dawson. Hakutaka kuwaambia ukweli sababu alijuwa angelimaliza jambo hilo bila wasiwasi wowote, jinsi alivyo huwezi kumzania kama ndio yule Mzee wa kanisa. Jambo la kwanza alilohitaji kulijuwa ni wapi alipo mlengaji shabaa!! Akajaribu kuangaza huku na kule bila mafanikio yoyote lakini akatumia ujanja mmoja, ndani ya begi lile kulikuwa na bunduki nyingine akaenda kuifunga eneo lingine ambalo lilikuwa mita kadhaa kutoka eneo ambalo atakaa, lengo likiwa endapo atakuwa analenga shabaa basi Mlengaji akisikia mlio wa risasi ataangalia umetokea wapi na akigundua ataanza kuiona ile bunduki ambayo haina Mtu kisha ataishambulia wakati anaishambulia Mbaga atakuwa amejuwa mlengaji yupo wapi na haraka atammaliza, huyo ndiyo Mbaga Askari wa zamani.

Basi akaweka kiwambo vizuri, macho yote yakawa nyumbani kwa Mkurugenzi ambaye alikuwa akijiandaa kuondoka nyumbani kwao, hakuwa na taarifa kuwa kuna vita ya chini chini ilikuwa ikiendelea eneo lile, Malaika hakuwa mbali na eneo lile lakini ilikuwa ngumu kumtambuwa sababu alikuwa akiangalia ni nani anaingia na nani anatoka, alikuwa nje ya jengo hilo la kifahari.

Basi, Mbaga akaweka tageti yake kwenye gari ambalo aliamini litatumiwa na Mkurugenzi huyo kutoka nyumbani kwake, haiku chukua hata dakika 10, alimuona Mkurugenzi akitoka akiwa na walinzi, akamuacha hadi alipoingia kwenye gari kisha akavuta triga na kufumua kioo cha gari alafu akamtandika risasi ya Kichwa Mkurugenzi huyo na kuanza kuzua taharuki, risasi mbili zilitosha kumuonesha Six ni wapi zilitoka lakini alikuwa ameshawekewa mtego wa akili sana, kitendo cha kuanza kufyetua risasi kuelekea pale ilipo bunduki bandi ambayo ilikuwa inaonekana eneo la mbele kilitosha kumuonesha Mbaga ni wapi alipo mlengaji, haraka akautumia uzoefu wake wa zamani, akamfumua risasi Six eneo la shingo, Majibizano haya yalimpa ishara Malaika kujuwa kuwa Six yupo kwenye wakati mgumu hakujuwa amsaidie nani kati ya Mkurugenzi ambaye tayari alishauawa au Six ambaye hakujua hali yake ipoje, akakimbilia kwenye ghorofa ambalo Six alikuwepo, wakati huo Mbaga alifanikiwa kumuona Malaika.

Hakutaka kupoteza tena muda, akakunja Bunduki zake na kuzirudisha kwenye begi kisha akashuka taratibu hadi chini, akalielekea gari lake akaweka lile begi akatoa Bastola kisha akaelekea kwenye ghorofa ambalo Malaika alikuwa ameenda, alishazisikia sifa za Malaika kuwa ni Mwanamke hatari sana linapokuja suala la mapigano hivyo akawa makini huku akimini Six hana uwezo wa kufanya lolote anachosubiria ni muda wa kukata roho kutokana na risasi aliyompiga.

“Umefikia wapi Sande!” Alihoji Mbaga baada ya kuwasha redio Call

“Nakaribia ila nimeumia eneo la mbavu nilitereza wakati napanda juu ya Bomba, sasa nakaribia ulipo umeme” ilisikika sauti ya Sande Olise ambaye alikuwa Ikulu

“Safi sana! Ongeza mwendo huku hali shwari” akasema kisha akazima redio akaongeza mwendo kuelekea kwenye ghorofa.
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU

Sande Upande wake alikuwa akitoka kwenye chemba na mwili ulikuwa ukivuja maji taka, akakumbuka alichoambiwa na Mbaga kuwa hapaswi kupita bila kujifuta maji, akafungua begi kisha akatoa kitambaa akajifuta yale maji ndipo akapita eneo lenye umeme, akapita kwa umakini ili asije sababisha shoti.

Alikuwa ameshachoka baada ya kutembea ndani ya chemba kwa zaidi ya nusu saa huku akiwa na maumivu makali kwenye mbavu zake, alipovuka umeme akajikuta akihitaji kupumzika kwanza kabla ya kuanza kufungua nati zilizo katika dirisha la juu ambalo akishaliondoa basi anakuwa amefika chooni kwa Rais huyo, punde akasikia sauti ya kufunguliwa kwa mlango akasimama na kuchungulia akamuona Mwanaume mmoja mwenye asili ya kiarabu akiwa anachunguza eneo hilo hapana shaka alisikia purukushani,

mwanaume huyo ndiye Jamaal ambaye amekuja pale Ikulu kumlinda Rais, Jamaal alionekana kuwa makini, akasogea hadi lilipo dirisha mahali ambapo Sande Olise alikuwa amesimama, dirisha hilo lilikuwa dogo na lenye Alminium na matundu madogo madogo.

Sande akabonyea kwa chini, Jamaal akaangaza bila kuona chochote kisha ikasikika sauti ya kufunga Mlango, hapana shaka Jamaal alikuwa ameondoka, Sande akajipa likizo fupi ili kutuliza maumivu ya mbavu zake, akaliondoa begi Mgongoni kisha akakaa kwenye bomba!!

Upande wa pili taarifa ya Kifo cha Mkurugenzi wa idara ya Usalama wa Taifa ilianza kuvuja kwa Askari wa juu wa Taifa, wakaitana ili kujadili. Wakati huo, Mwanaume Sande Olise alikuwa akipandisha ngazi kuelekea Ghorofa namba tano,

Ghorofa hilo lilikuwa halitumiki, hakuna aliyeshtuka kuwa eneo hilo liligeuzwa kuwa uwanja wa vita sababu Bunduki zilizotumika zilikuwa na vifaa maalum vya kuzuia sauti,

Malaika alikuwa ameshafika Ghorofa namba tano akamkuta Six akiwa amelala sakafuni damu ikiwa inamtoka, alikuwa hawezi kuzungumza. Muda huo huo Malaika akapiga simu kwa John Brain kumpa taarifa kuwa Six anakaribia kufa

“Nini?” Aliuliza kwa mshituko John Brain

“Hali yake sio nzuri, ameshambuliwa na mlengaji mwenzake ambaye yupo ghorofa lingine!! Hali sio shwari Boss” Alisema kwa sauti ya Chini huku akijuwa fika kuwa mlengaji anaweza kuja pale ili kuhakiki kama Six amekufa, ndicho ambacho Mzee Mbaga alikuwa akifanya.

Akakata simu kisha akaenda kuchungulia dirishani akapokelewa na ukimya uliopitiliza, akajuwa sasa

yupo mawindoni na Mtu asiyemfahamu.

Malaika na kamwili kake kadogo kama Miss Utalii, akachomoa Bastola yake akafunga kifaa maalum cha kuzuia Mlio wa risasi kisha akajiweka sawa!! Akatafuta mahali akajibanza, muda huo Mtaalam Mbaga alikuwa akizidi kusogea juu taratibu.

“SHIT” alisema John Brain akasimama kutoka kitini kisha akampigia simu Jamaal akamuuliza

“Kuna usalama ulipo? Six amepigwa risasi eneo baya sana huenda akafa, unatakiwa kuwahi haraka eneo la tukio” Alisema kwa sauti iliyojaa Kupagawa, kwa jinsi alivyokuwa akimuamini Six hakutegemea kama angelipigwa risasi kirahisi hivyo akajuwa kuwa mlengaji alikuwa Mtu hodari zaidi ya Six

“Natamaani kutoka hapa lakini nina hisia mbaya kuwa huenda ikulu imevamiwa pia, angalia nini cha kufanya Boss” Alisema Jamaal

“Okay!” Kisha simu ikakatika, akamrudia tena Malaika lakini simu ya Malaika haikupokelewa, wakati huo Malaika alikuwa akisikia namna Mtu alivyokuwa akipiga hatua kuelekea ndani ya chumba hicho.

Moja kwa moja akajuwa Mtu huyo alikuwa ndiye aliyempiga risasi Six, akabana Pumzi zake ili asimpe mwanya wa kujuwa yupo wapi kutokana na ukimya uliokuwa umetawala pale. Mbaga alizidi kusogea bila kujuwa kuwa anayemuwinda naye ameshakaa mkao wa kujibu mapigo, mara nyingi Mzee Mbaga hakupendelea sana kutumia Bastola lakini ilimlazimu kutokana na namna sifa za Mtu anayeenda kupambana naye zilivyo.

Fumba na kufumbua Mbaga na Malaika wakajikuta wakiwa ndani ya chumba kimoja kisicho na vitu ndani yake, Malaika alikuwa amejibanza nyuma ya moja ya kona za chumba hicho huku Mwili wa Six ukiwa bado sakafuni, hakukuwa tena na cha kusubiria kwa Malaika akafyatua risasi ili impate Mbaga eneo la Kichwa, lakini bahati mbaya Bastola yake haikutoa risasi, ilikuwa ni kama Bahati kwa Mbaga akafanikiwa kumuona Malaika, wakati Malaika anahangaika kufyatua risasi Mbaga alishamfikia na kuipiga teke Bastola ya Malaika.

Wakawa wanatazamana kwa macho yaliyojaa ufundi wa kusomana, Malaika alishasikia sifa za Mbaga na Mbaga alikuwa na sifa za Malaika, mviziano baina yao ukawa mkali huku kila Mtu akitafuta namna ya kumdhibiti mwenzake.

Upande wa Ikulu, mapumziko kwa Sande Olise hayakuchukua muda mrefu, akafungua begi akatoa Staa kwa ajili ya kufungua nati ili aweze kuingia kwenye Choo cha Rais bila kujuwa kuwa Jamaal alikuwa ameshtuka. Alizifungua haraka bila kupoteza muda kabisa, ndani ya dakika moja akawa amefanikiwa kisha akatoa dirisha hilo akaliweka pembeni kukawa na tundu ambalo angeliweza kupita na kwenda chooni kwa ajili ya kuanza mpango wake.

Muda huo Rais alikuwa akipewa taarifa ya kifo cha Mkurugenzi wa idara ya Usalama wa Taifa, na kushambuliwa kwa Six. Ilimfanya Rais akose amani akiwa ofisini kwake, akamuita Jamaal

“Usikae mbali na Mimi Jamaal, siwaamini hawa walinzi wengine, tegemeo langu lipo kwako tuu” Alisema huku akiwa anamtazama Jamaal aliyekuwa na ndevu nyingi.

“Nipo hapa Mkuu” akasema Jamaal wakati huo Sande akiwa anachumpa ili aingie chooni, akajikuta akinasa shati lake kwenye tundu hilo ambalo lilikuwa na baadhi ya misumali midogo baada ya kung’oa dirisha. Akajitahidi kujitoa lakini ikawa ngumu, katika purukushani akajikuta ameangukia chooni, mshindo ukamshtua Jamaal. Akamwambia Rais akae hapo pasipo kutoka kisha taratibu akaelekea chumbani kwa Rais.

Jamaal akawa anaelekea taratibu eneo ambalo alisikia mshindo huo, ilikuwa ni kule chooni ambako Sande Olise alikuwa ameangukia, Sande hakutaka sana kupoteza muda licha ya kuumia kidogo wakati alipoanguka, akajiokota haraka ili aanze mpango wa kumpata Rais bila kujuwa kuwa Jamaal alikuwa ameshakaribia mlango wa Choo hicho.

Upande wa pili, Mbaga alikuwa ameangushwa chini, Malaika akionekana kumdhibiti Mbaga kisawasawa, Mbaga akajiokotanisha kisha akamfuata Malaika na kutupa mapigo mawili takatifu, moja lilikuwa ni teke kali ambalo Malaika aliliona na kulikwepa lakini alikuwa ameunganisha na pigo jingine la teke la kushoto ambalo lilimpata Malaika akaanguka chini, bila kupoteza muda akajiokota pembezoni kukiwa na gongo, akalinyanyua ili kupambana na Mbaga, akatoka spidi na kujirusha mithiri ya ndege aina ya Mwewe anavyowinda

vifaranga vya kuku,

kisha akatua chini na kurusha gongo ambalo lilimpata Mbaga eneo la Bega hadi akapepesuka na

kujigonga ukutani, jinsi Mbaga alivyokuwa mwepesi ikawa ngumu kwa Malaika kuusoma umri sahihi wa Mbaga kama ni Mzee au Kijana kwa jinsi ambavyo alikuwa akipambana.

Mbaga akajiweka sawa kwa ajili ya kujibu mapigo kutoka kwa Malaika, akabonyea kidogo na kukaa staili ya nyani Mzee anayetaka kurukia Tawi la Mti, kisha akakunja miguu yake sawasawa huku akiwa anamtazama Malaika ambaye kwa kiasi kikubwa alikuwa mwepesi kutokana na umbo lake dogo na jembamba.

“Nitakuuwa kama nilivyomuuwa mwenzako” Akasema Mbaga ikiwa ni mbinu ya kumtuliza Malaika
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

“Risasi inaweza kwenda haraka zaidi kuliko hata mapigo yako, huwa sipigwi na Mtu mtaratibu kama Wewe” Pale pale Mbaga akamfuata Malaika kama Mtu anayekimbia kisha akabendi upande wa kushoto aliporudi kulia akatupa ngumi ambayo ilikwepwa kirahisi na Malaika kisha akapewa ngumi ya shingo alafu akamaliziwa na teke la kifua, Mbaga akaanguka chali, Malaika akajuwa kuwa hatakiwi kumpa Mbaga hata sekunde moja ya mapumziko, akampelekea mvua ya mateke ambayo yalikita zaidi eneo la kifua, Mbaga akarudi tena chini akiwa katika hali ya

uchovu sana hata moyo wake ukakiri kuwa amekutana na Mtu hatari kuliko alivyofikiria.

Malaika akajiweka sawa huku akikunja vidole vyake na kuwa mfano wa Uma, Mbaga akajuwa tu endapo atalegea basi anaweza kuuawa hapo na hilo pigo, akasimama ili apambane na Malaika, tayari mguu wa Mbaga ulikuwa na maumivu Makali mno, Malaika akaligundua hilo haraka akaufanyia kazi mguu huo kwa kuuchosha zaidi, akawa anapeleka mapigo ya Mateke kuelekea kwenye Mguu huo ambao ulikuwa mzito kusogea.

Kila pigo ambalo Malaika alilipeleka kwa Mbaga liliitikiwa na sauti ya kugugumia ya Mbaga na kumfanya Malaika ajuwe kuwa Mapigo yake yote yalikuwa yakifika sehemu husika, hali ya Mbaga ikaanza kuwa Mbaya hasa baada ya mguu wake kuonekana kukosa balansi ya kwenda mbele, dakika moja akajikuta akiwa sakafuni akiwa anatokwa na damu nyingi mdomoni, Mbaga hakuwa na uwezo hata wa kurusha ngumi kwa Malaika hata kunyanyuka.

“Nilikwambia huwezi kunidhibiti, nitakuuwa ili kulipa kisasi cha Kifo cha Six, nimefanya kazi na Six kwa miaka mingi na haikuwa kutokea hili lililotokea leo. Nitaandikwa katika historia ya vitabu vya Nchi hii kuwa nimemuondoa P55″ Alisema Malaika huku akiwa anacheka kwa maumivu, Six kwake alikuwa ni zaidi ya Mtu wa kufanya naye kazi.

Akamsogelea Six na kuthibitisha alichokiamini kuwa Six alikuwa ameshakufa kwa kupigwa rusasi moja tu ya Shingo.

Akamrudia Mbaga kisha akakunja mkono wake na kutengeneza umbo la Uma ambalo lilikuwa ni umbo hatari zaidi, lengo la Malaika lilikuwa ni kuondoa koromeo la Mbaga kwa hasira, wakati huo Mbaga hakuwa na nguvu hata ya kumzuia Malaika, Ghafla Malaika alihisi ubaridi kwenye mgongo wake, ubaridi ambao ulisababisha ahisi maumivu huku akizidi kuhisi giza machoni pake, akajaribu kugeuka nyuma akakutana na sura ya Dawon akiwa ameshikilia Bastola iliyokuwa ikitoa moshi.

Kabla hajasema chochote akapigwa risasi nyingine eneo lamoyo, akapigwa nyingine eneo la Kichwa, habari ya Malaika ikaishia hapo, akaanguka chini. Mbaga akahema kwa furaha,

Dawson akamfuata Mbaga

“Upo salama?” Aliuliza akiwa anamuinua

“Mungu anajuwa najisikiaje Dawson, sijui hata aliweza vipi kukuamsha kitandani na kukuleta hapa ukanisaidia, huyu Msichana alikuwa ananimaliza hapa” Alisema kisha alikohoa.

“Hatuna muda wa kupoteza hapa, mpigie Sande Olise tujuwe amefikia wapi, Kisko na Chande wapo Hospitali wanaendelea na matibabu” Alisema Dawson kisha mbaga akatoa redio Call akampigia Sande

Dakika tano zilizopita, Sande alikuwa ameshanyanyuka ili aangalie uwezekano wa kufika chumbani kwa Rais, akiwa anavuta kitasa akapokelewa na teke kali kutoka kwa Jamaal.

Akarudishwa nyuma akaangukia kwenye sinki la choo, akajitonesha yale maumivu ya Mbavu zake, akanyanyua macho ili amuone aliyempiga teke hilo akamuona Jamaal ambaye alikuwa na mwili wa mazoezi.

Kisha Jamaal akaufunga mlango wa choo kwa kutumia funguo alafu funguo akaitia kwenye Tundu la sink la choo

“Ukiweza kuniuwa utakuwa huru kutoka hapa lakini kama nitakuuwa nitakuzika kwenye chemba ya choo” Alisema Jamaal kisha akamfuata Sande ambaye bado alikuwa haelewi elewi ameweza vipi kushtukiwa.

Akamkamata Sande na kwenda kumgongesha ukutani, bahati nzuri Sande naye alikuwa Mtu wa

mazoezi akajiviringisha mikono akajitoa kwenye mwili wa Jamaal, akaona isiwe tabu ni bora apambane na Jamaal

Wakaanza kurushiana mapigo makali makali ambayo yalimpata kila mmoja wao, uzuri wa Jamaal alikuwa mrefu hivyo aliweza kumpelekea mapigo ya nguvu Sande kuliko Sande alivyopeleka kwa Jamaal, Sande akajikuta amepigwa teke akaangukia kwenye bomba la maji ambalo lilikatika kutokana na uzito wa Sande, maji yakaanza kumwagika chooni hapo huku mengine yakitafuta njia ya kutoka yakawa yanaelekea chumbani kwa Rais

Bado waliendelea kushambuliana kwa zamu, Jamaal hakutaka kufanya makosa kabisa sababu walishaahidiwa pesa ya kutosha, muda huo simu ya Jamaal iliita na alipoangalia akaona ni Rais ndiye anayepiga akaipokea na kuweka loud Spika

“Upo wapi mbona kuna kelele hivyo?” Aliuliza Rais

“Naoga Bosi muda mchache nitakuwa hapo”

“Haya sawa!” Simu ilikatika, Jamaal akaiweka mfukoni kisha akamfuata Sande Olise na kuanza kumsugua kichwa kwenye ukuta hadi mwisho wa ukuta akiwa amembana vizuri Sande kiasi kwamba hakuwa na uwezo wa kupurukuta. Akawa anampiga vifuti eneo la mgongo na kumfanya Sande azidi kukosa nguvu kisha akamtupia

kwenye Bwawa dogo lililopo pale chooni, akamfuata na kuanza kumkosesha pumzi kwa kumzamisha kwenye Bwawa hilo

Purukushani ikawa kubwa kwa jinsi Sande alivyokuwa ananyweshwa yale maji ilionesha ni wazi kuwa alikuwa na muda mchache wa kuendelea kuwa hai. Sande akakumbuka alikuwa na ile staa ya kufungulia dirisha akajitahidi kufungua zipu huku akiendelea kukosa pumzi, akafanikiwa kuitoa staa kisha akamchoma Jamaal eneo la mbavu, Jamaaal akamuacha Sande huku akigugumia kwa maumivu, Sande alikuwa hoi sana.

Akawa anataka kutoka pale kwenye lile bwawa dogo lakini Jamaal akamshika mguu na kumrudisha akawa anampiga eneo la uso kwa hasira sana. Hali ya Sande ikazidi kuwa mbaya, akaitumia tena ila Staa akamchoma eneo lilelile la mbavu kisha akamchoma tena eneo la mkono kwenye mishipa iliyokuwa na nguvu na kumfanya Jamaal ahisi mkono wake hauna nguvu.

Sande akaona ni bora amalizane na Jamaal pale pale, akampiga ngumi la uso, akampiga ngumi mfululizo hadi uso wa Jamaal ukaharibika na kusababisha damu nyingi kumwagika, akamchoma na ile staa eneo la shingo ikatokea upande mwingine, habari ya Jamaal ikaishia hapo.

Sande alikuwa hoi sana, ndipo akasikia simu ikiwa inaita, ilikuwa ndiyo ile simu ambayo Mbaga alikuwa akimpigia, akaipokea huku akiwa anahema juu juu

“Kulikoni Sande upo salama?” Aliuliza Mbaga

“Nilikiona kifo changu lakini kwa bahati nzuri nimefanikiwa kuokoka”

“Umefikia wapi?”

“Bado nipo Chooni, natoka sasa”

“Ok! Tunakuja huko sasa hivi kuja kukusaidia” ilisikika sauti ya Mbaga kisha simu ikakatika.

Ukimya alioupata Rais ulimtishia sana ukizingatia John Brain tayali alishampa taarifa kuwa Six amepigwa riasasi ameuawa, hakuwa na imani na walinzi wa Ikulu kwa namna ambavyo mara nyingi alikuwa akiwatumikisha kufanya mauwaji, moja ya Mauwaji hayo yalikuwa ni mauwaji ya Inspekta Zola, pia kutesa Watu wasio na hatia.

Akajaribu kumpigia simu Jamaal lakini simu iliita, Sande aliitazama bila kuipokea.

Rais akaona ni bora aelekee kwenye chumba cha siri ambacho kilikuwa kimehifadhi nyaraka za siri na ile fimbo ya alama ya Urais, akajisachi akakumbuka kuwa funguo aliiacha chumbani kwake kwenye moja ya koti lake, akakimbia haraka kuelekea chumbani, akashangaa kuona maji yakiwa yanatiririka kutokea

Chooni, akajaribu kuita kidogo

“Jamaal! Jamaal!” Akajibiwa na ukimya, akalazimika kuelekea mlango wa Choo, akausukuma lakini mlango huo ulikuwa umefungwa, angalau akawa na tumaini kuwa kuna usalama kumbe Sande alikuwa amejificha mahali, akaielekea ile funguo kwenye koti, chumba hicho ambacho Rais anataka kwenda ni chumba cha siri sana ambacho si rahisi ukakiona ( Utanielewa Mbeleni )

Akawa mbio akaipata funguo lakini akiwa anataka kutoka kuelekea huko wazo likamjia, kufungua choo ili azuie maji yaliyokuwa yakitiririka, Rais huyu alishaondoa ulinzi eneo la ndani kwa kumtegemea Jamaal alipoona hali ni mbaya akawa na mawazo mawili, kuita ulinzi kisha kuelekea chumba cha siri, haraka akachukua funguo ya Chooni ambayo alikuwa ameiunganisha kwenye funguo ya chumba cha siri, akafungua.

Sande hakutaka kumpa uwazi wa kutaka kukimbia baada ya kumuona Jamaal akiwa ametapakaa damu , akamkamata na kumzamisha Chooni.

“Sande ni wewe?” Aliuliza Rais

“Unataka nini sema unachotaka nitakupatia Sande” Alizidi kusema huku akiwa mwenye hofu,

“Leo unataka niendeleee kuishi wakati ulituma Watu waniuwe?

Kabla sijafa utatangulia wewe!!” Alisema kisha alimkunja kwa lengo la kumjaza hofu

“Sande tafadhali usifanye hivyo, kumbuka hapa ni Ikulu na ukifanya chochote kile utajiweka katika mazingira magumu ya kuwa hai, sema unataka nini nitakupa!!”

“Nautaka Urais wako! Mamlaka kisha nilipe kisasi kwa kifo cha Zola” Rais akawa ameelewa lengo la Sande kufika Ikulu lilikuwa ni nini

“Sande unajua fika nisingeliweza kumuuwa Huyo Zola, isipokuwa….” akakatizwa na ishara ya Sande

“Nahitaji unipeleke kwenye chumba cha siri cha Ikulu”

“Chumba cha siri? Nani amekuambia kuwa hapa kuna chumba cha siri! Hakuna hicho chumba ndani ya Hii Ikulu Sande, utakuwa umekosea” Alijitetea Rais akiwa anatabasamu kwa lengo la kumtoa mchezoni Sande huku macho ya Rais yakiwa yanatazama kipande cha bomba lililoanguka chini, akataka kumshambulia lakini Sande akashtuka akamvuta hadi ukutani akampa ngumi nne za uso ambazo ziliiweka akili ya Rais katika hali sawa!!

“Nipeleke chumba cha Siri” Rais hakuwa na jinsi ya kufanya akalazimika kuongozana na Sande, kwanza Sande akachomoa Bastola kisha akaiweka kwenye kichwa cha Rais huyo ili ije kuwa kama ngao ya kumlinda. Wakaongozana kuelekea huko huku Rais akijuwa fika kuwa Sande anaweza kumuuwa endapo hatofanya hivyo.

Mwendo wa taratibu eneo ambalo halikuwa na walinzi, wakafika mahali Rais akamuuliza Sande

“Unashirikiana na Muasi P55?”

“Twende sitaki maswali ya Kizandiki” Alisema Sande, wakafika hadi kwenye Ofisi ya Rais huyo, kitendo cha kufika tu Ofisini alamu maalum ikalia baada ya Kamera kuonesha kuwa Rais alikuwa ametekwa humo Ikulu, Askari wakamiminika kuelekea ndani ambako Rais alikuwepo.

“Funga mlango wako haraka sana” Alisema Sande huku akimtishia kumuuwa Rais, hakuwa na jinsi akafanya kama alivyoelekezwa sababu mlango huo ulikuwa wa umeme na ulikuwa na namba maalum za kuingilia ambazo alikuwa akizifahamu Rais pekee. Simu ya Rais ilikuwa ikiita, mpigaji alikuwa ni John Brain, baada ya kuwapigia vijana wake wote watatu simu haikuweza kupokelewa.

Sande akaichukua simu akaipokea

“Rais! kuna Usalama huko?” aliuliza punde simu ilipopokelewa

“Hakuna usalama sababu Ikulu ipo chini ya Uvamizi” Sauti ya Sande ilipofika kwa John ikampa ujumbe kuwa Rais alikuwa chini ya ulinzi.

“John! muda wa wewe kuendelea kutekeleza ugaidi Duniani umeisha, Dunia itaenda kuandika Historia Muda mchache ujao tutakapokufuta katika uso wa Dunia” John akawa amechanganikiwa, Sande akaendelea kumueleza

“Hakuna kijana wako hata mmoja anayepumua hadi kufikia wakati huu, umebaki mwenyewe katika Ardhi ambayo uliamrisha kila kitu kifanywe kwa matakwa yako” Kisha Sande akakata simu hiyo

“Waambie Askari wako wakae mbali na eneo hili vinginevyo nitakuuwa muda sio mrefu” Akasema Sande, pale pale Rais akabonyeza sehemu ambayo ilikuwa na Maiki akasema na Askari wote wakasikia.

“Nioneshe kilipo chumba cha siri”

“Sande hata ukienda huko utakufa sababu Kuna mfumo wa umeme ambao hauwezi kukuruhusu kupenya zaidi” Alieleza Rais, Sande akampiga teke la Mguu Rais kisha akamwambia

“hakuna muda wa kupoteza nipeleke huko” Rais akaelekea mahali ambapo kulikuwa na kabati kubwa la vitabu akabonyeza sehemu kisha mlango ukafunguka.

Kila ambacho Mbaga alimueleza Sande kilionekana, ni kweli ndani ya chumba hicho kulikuwa na mionzi iliyokuwa ikipishana “Unaona? ule ni mfumo wa Umeme Sande, unachotaka kipo mbele zaidi ya pale ambapo kuna mionzi utafia huko” Sande akaona Rais huyo anamtia kelele, akamfunga kamba mikononi na miguuni kisha akamuweka chini ya Meza, akatoa kifaa cha kunyonya mionzi ambacho alipewa na Mbaga akakiwasha kikaanza kuhesabu sekunde ambapo baada ya sekunde 30 kupita kitazima hivyo

Sande alipaswa kutumia muda mfupi kuchukua vitu viwili, Fimbo na nyaraka za siri ambazo alielezwa kuwa zilikuwa zipo pamoja ndani ya chumba hicho.

Sande akaingia ndani ya chumba hichi kisha akaweka kifaa sehemu ambapo mionzi yote ya umemeikaunganika na kukielekea kifaa hicho, Sande akapata nafasi ya kuzama zaidi ndani ya chumba hicho, akawa anahaingaika jinsi ya kuviona vitu alivyokuwa akivitaka, akajikuta akitumia sekunde 10 bila Mafanikio, kumbe Rais alikuwa na kisu kidogo alichokuwa amekificha kwenye kiatu chake, akawa amejitahidi na kukata kamba hizo. Akaangalia kwenye Kioo ambacho kilikuwa kikitumika kuonesha Video za CCTV, akaona kuna Askari waliokuwa mlangoni, haraka akakimbilia kuwafungulia.

Sekunde zilikuwa zimeshaisha, Sande alikuwa ameshapata nyaraka na hiyo fimbo kisha haraka akawahi kutoka, mlango ukajifunga. Akakutana Uso kwa uso na Askari wawili waliofunguliwa Mlango na Rais, Aksari hao wakachomoa Bastola zao huku wakiwa wamefunika nyuso zao, Sande akajikuta yupo chini ya Ulinzi wa Askari hao.

Rais akampokonya Sande vile Vitu kisha akawa anapiga hatua kuelekea kufungua lango la chumba cha Siri, ghafla akashangaa Askari hao wawili wakimnyooshea Bastola, wakavua walichovaa kwenye nyuso zao,

Rais hakuamini kuwaona Dawson na Mbaga wakiwa ndani ya Mavazi ya kijeshi, akataka kufanya ujanja kufungua mlango ili aingie huko, akapigwa risasi ya mguu.

Wakavichukua vitu hivyo alafu wakamwambia Rais atangaze katika TV ya Taifa kutokea Ikulu kuwa Nchi ipo chini ya Jeshi. Muda huo John Brain alikuwa akikusanya kila kilicho chake ili aondoke Nchini, akiwa anataka kutoka akasikia Sauti ya Rais kutokea kwnye TV ikiitangazia Nchi kuwa Nchi hiyo ipo chini ya Jeshi, wakaonekana akina Dawson na Mbaga ambao walitajwa kuwa Waasi kwa nyakati tofauti tofauti, wakamlazimisha Rais alekeze kila kitu, akasema kila kitu hata mauwaji ya Makamu wa Rais ni yeye ndiye aliyehusika nayo, vifo vilivyokuwa vikitokea vilitokana na yeye.

Kisha picha ya John Brain ikaanikwa kwenye TV, Watu ndio wakapata kumjua John Brain ambaye Taifa la Marekani lilikuwa likimsaka. Taarifa hii ilienda mbali zaidi hadi vituo vya Runinga vya Aljazeera vikaitoa.

John Brain akaondoka Nchini kwa kutumia Helkopta, akatua Uganda ili apande ndege akiwa amevalia sura Bandia. Tayari Marekani walikuwa wameshaipata Taarifa hiyo wakatuma FBI Dunia nzima wakiwa na sampo ya DNA ya John Brain baada ya kumfahamu. John akakamatwa kwenye mpaka wa Somalia akiwa anajiandaa kuonana na Kundi la Alqaeda na Baada ya kupimwa akagundulika kuwa ni yeye, FBI wakarudi Marekani wakiwa na

John Brain ili awaoneshe Makundi mengine ya Kigaidi.

Taifa hilo likawataja Mbaga, Sande Olise na Dawson kama Mashujaa wa Dunia kwa kumfichua John Brain ambaye Mataifa mengi yalihangaika kwa muda mrefu, Kama ilivyo ahadi ya Mbaga aliondoka kwenda kuishi Shamba katika Nchi ya Eritrea, akajiwekeza na kilimo huku akiwa ameiacha Nchi hiyo ikiwa inaingia kwenye Uchaguzi wa kuunda Serikali itakayoongozwa kikatiba tofauti na Mwanzo ambavyo Watu walikuwa wakirithi nafasi ya Urais.

Baada ya miezi mwili Dawson alifariki kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu, Kisko na Chande walichukuliwa na Taifa la Marekani kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi, wakati huo Sande akistaafu kazi ya Kijeshi akapanda ndege kwenda Eritrea kuishi pamoja na Mzee Mbaga

MWISHO
 
1737206654840.png
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

“Risasi inaweza kwenda haraka zaidi kuliko hata mapigo yako, huwa sipigwi na Mtu mtaratibu kama Wewe” Pale pale Mbaga akamfuata Malaika kama Mtu anayekimbia kisha akabendi upande wa kushoto aliporudi kulia akatupa ngumi ambayo ilikwepwa kirahisi na Malaika kisha akapewa ngumi ya shingo alafu akamaliziwa na teke la kifua, Mbaga akaanguka chali, Malaika akajuwa kuwa hatakiwi kumpa Mbaga hata sekunde moja ya mapumziko, akampelekea mvua ya mateke ambayo yalikita zaidi eneo la kifua, Mbaga akarudi tena chini akiwa katika hali ya

uchovu sana hata moyo wake ukakiri kuwa amekutana na Mtu hatari kuliko alivyofikiria.

Malaika akajiweka sawa huku akikunja vidole vyake na kuwa mfano wa Uma, Mbaga akajuwa tu endapo atalegea basi anaweza kuuawa hapo na hilo pigo, akasimama ili apambane na Malaika, tayari mguu wa Mbaga ulikuwa na maumivu Makali mno, Malaika akaligundua hilo haraka akaufanyia kazi mguu huo kwa kuuchosha zaidi, akawa anapeleka mapigo ya Mateke kuelekea kwenye Mguu huo ambao ulikuwa mzito kusogea.

Kila pigo ambalo Malaika alilipeleka kwa Mbaga liliitikiwa na sauti ya kugugumia ya Mbaga na kumfanya Malaika ajuwe kuwa Mapigo yake yote yalikuwa yakifika sehemu husika, hali ya Mbaga ikaanza kuwa Mbaya hasa baada ya mguu wake kuonekana kukosa balansi ya kwenda mbele, dakika moja akajikuta akiwa sakafuni akiwa anatokwa na damu nyingi mdomoni, Mbaga hakuwa na uwezo hata wa kurusha ngumi kwa Malaika hata kunyanyuka.

“Nilikwambia huwezi kunidhibiti, nitakuuwa ili kulipa kisasi cha Kifo cha Six, nimefanya kazi na Six kwa miaka mingi na haikuwa kutokea hili lililotokea leo. Nitaandikwa katika historia ya vitabu vya Nchi hii kuwa nimemuondoa P55″ Alisema Malaika huku akiwa anacheka kwa maumivu, Six kwake alikuwa ni zaidi ya Mtu wa kufanya naye kazi.

Akamsogelea Six na kuthibitisha alichokiamini kuwa Six alikuwa ameshakufa kwa kupigwa rusasi moja tu ya Shingo.

Akamrudia Mbaga kisha akakunja mkono wake na kutengeneza umbo la Uma ambalo lilikuwa ni umbo hatari zaidi, lengo la Malaika lilikuwa ni kuondoa koromeo la Mbaga kwa hasira, wakati huo Mbaga hakuwa na nguvu hata ya kumzuia Malaika, Ghafla Malaika alihisi ubaridi kwenye mgongo wake, ubaridi ambao ulisababisha ahisi maumivu huku akizidi kuhisi giza machoni pake, akajaribu kugeuka nyuma akakutana na sura ya Dawon akiwa ameshikilia Bastola iliyokuwa ikitoa moshi.

Kabla hajasema chochote akapigwa risasi nyingine eneo lamoyo, akapigwa nyingine eneo la Kichwa, habari ya Malaika ikaishia hapo, akaanguka chini. Mbaga akahema kwa furaha,

Dawson akamfuata Mbaga

“Upo salama?” Aliuliza akiwa anamuinua

“Mungu anajuwa najisikiaje Dawson, sijui hata aliweza vipi kukuamsha kitandani na kukuleta hapa ukanisaidia, huyu Msichana alikuwa ananimaliza hapa” Alisema kisha alikohoa.

“Hatuna muda wa kupoteza hapa, mpigie Sande Olise tujuwe amefikia wapi, Kisko na Chande wapo Hospitali wanaendelea na matibabu” Alisema Dawson kisha mbaga akatoa redio Call akampigia Sande

Dakika tano zilizopita, Sande alikuwa ameshanyanyuka ili aangalie uwezekano wa kufika chumbani kwa Rais, akiwa anavuta kitasa akapokelewa na teke kali kutoka kwa Jamaal.

Akarudishwa nyuma akaangukia kwenye sinki la choo, akajitonesha yale maumivu ya Mbavu zake, akanyanyua macho ili amuone aliyempiga teke hilo akamuona Jamaal ambaye alikuwa na mwili wa mazoezi.

Kisha Jamaal akaufunga mlango wa choo kwa kutumia funguo alafu funguo akaitia kwenye Tundu la sink la choo

“Ukiweza kuniuwa utakuwa huru kutoka hapa lakini kama nitakuuwa nitakuzika kwenye chemba ya choo” Alisema Jamaal kisha akamfuata Sande ambaye bado alikuwa haelewi elewi ameweza vipi kushtukiwa.

Akamkamata Sande na kwenda kumgongesha ukutani, bahati nzuri Sande naye alikuwa Mtu wa

mazoezi akajiviringisha mikono akajitoa kwenye mwili wa Jamaal, akaona isiwe tabu ni bora apambane na Jamaal

Wakaanza kurushiana mapigo makali makali ambayo yalimpata kila mmoja wao, uzuri wa Jamaal alikuwa mrefu hivyo aliweza kumpelekea mapigo ya nguvu Sande kuliko Sande alivyopeleka kwa Jamaal, Sande akajikuta amepigwa teke akaangukia kwenye bomba la maji ambalo lilikatika kutokana na uzito wa Sande, maji yakaanza kumwagika chooni hapo huku mengine yakitafuta njia ya kutoka yakawa yanaelekea chumbani kwa Rais

Bado waliendelea kushambuliana kwa zamu, Jamaal hakutaka kufanya makosa kabisa sababu walishaahidiwa pesa ya kutosha, muda huo simu ya Jamaal iliita na alipoangalia akaona ni Rais ndiye anayepiga akaipokea na kuweka loud Spika

“Upo wapi mbona kuna kelele hivyo?” Aliuliza Rais

“Naoga Bosi muda mchache nitakuwa hapo”

“Haya sawa!” Simu ilikatika, Jamaal akaiweka mfukoni kisha akamfuata Sande Olise na kuanza kumsugua kichwa kwenye ukuta hadi mwisho wa ukuta akiwa amembana vizuri Sande kiasi kwamba hakuwa na uwezo wa kupurukuta. Akawa anampiga vifuti eneo la mgongo na kumfanya Sande azidi kukosa nguvu kisha akamtupia

kwenye Bwawa dogo lililopo pale chooni, akamfuata na kuanza kumkosesha pumzi kwa kumzamisha kwenye Bwawa hilo

Purukushani ikawa kubwa kwa jinsi Sande alivyokuwa ananyweshwa yale maji ilionesha ni wazi kuwa alikuwa na muda mchache wa kuendelea kuwa hai. Sande akakumbuka alikuwa na ile staa ya kufungulia dirisha akajitahidi kufungua zipu huku akiendelea kukosa pumzi, akafanikiwa kuitoa staa kisha akamchoma Jamaal eneo la mbavu, Jamaaal akamuacha Sande huku akigugumia kwa maumivu, Sande alikuwa hoi sana.

Akawa anataka kutoka pale kwenye lile bwawa dogo lakini Jamaal akamshika mguu na kumrudisha akawa anampiga eneo la uso kwa hasira sana. Hali ya Sande ikazidi kuwa mbaya, akaitumia tena ila Staa akamchoma eneo lilelile la mbavu kisha akamchoma tena eneo la mkono kwenye mishipa iliyokuwa na nguvu na kumfanya Jamaal ahisi mkono wake hauna nguvu.

Sande akaona ni bora amalizane na Jamaal pale pale, akampiga ngumi la uso, akampiga ngumi mfululizo hadi uso wa Jamaal ukaharibika na kusababisha damu nyingi kumwagika, akamchoma na ile staa eneo la shingo ikatokea upande mwingine, habari ya Jamaal ikaishia hapo.

Sande alikuwa hoi sana, ndipo akasikia simu ikiwa inaita, ilikuwa ndiyo ile simu ambayo Mbaga alikuwa akimpigia, akaipokea huku akiwa anahema juu juu

“Kulikoni Sande upo salama?” Aliuliza Mbaga

“Nilikiona kifo changu lakini kwa bahati nzuri nimefanikiwa kuokoka”

“Umefikia wapi?”

“Bado nipo Chooni, natoka sasa”

“Ok! Tunakuja huko sasa hivi kuja kukusaidia” ilisikika sauti ya Mbaga kisha simu ikakatika.

Ukimya alioupata Rais ulimtishia sana ukizingatia John Brain tayali alishampa taarifa kuwa Six amepigwa riasasi ameuawa, hakuwa na imani na walinzi wa Ikulu kwa namna ambavyo mara nyingi alikuwa akiwatumikisha kufanya mauwaji, moja ya Mauwaji hayo yalikuwa ni mauwaji ya Inspekta Zola, pia kutesa Watu wasio na hatia.

Akajaribu kumpigia simu Jamaal lakini simu iliita, Sande aliitazama bila kuipokea.

Rais akaona ni bora aelekee kwenye chumba cha siri ambacho kilikuwa kimehifadhi nyaraka za siri na ile fimbo ya alama ya Urais, akajisachi akakumbuka kuwa funguo aliiacha chumbani kwake kwenye moja ya koti lake, akakimbia haraka kuelekea chumbani, akashangaa kuona maji yakiwa yanatiririka kutokea

Chooni, akajaribu kuita kidogo

“Jamaal! Jamaal!” Akajibiwa na ukimya, akalazimika kuelekea mlango wa Choo, akausukuma lakini mlango huo ulikuwa umefungwa, angalau akawa na tumaini kuwa kuna usalama kumbe Sande alikuwa amejificha mahali, akaielekea ile funguo kwenye koti, chumba hicho ambacho Rais anataka kwenda ni chumba cha siri sana ambacho si rahisi ukakiona ( Utanielewa Mbeleni )

Akawa mbio akaipata funguo lakini akiwa anataka kutoka kuelekea huko wazo likamjia, kufungua choo ili azuie maji yaliyokuwa yakitiririka, Rais huyu alishaondoa ulinzi eneo la ndani kwa kumtegemea Jamaal alipoona hali ni mbaya akawa na mawazo mawili, kuita ulinzi kisha kuelekea chumba cha siri, haraka akachukua funguo ya Chooni ambayo alikuwa ameiunganisha kwenye funguo ya chumba cha siri, akafungua.

Sande hakutaka kumpa uwazi wa kutaka kukimbia baada ya kumuona Jamaal akiwa ametapakaa damu , akamkamata na kumzamisha Chooni.

“Sande ni wewe?” Aliuliza Rais

“Unataka nini sema unachotaka nitakupatia Sande” Alizidi kusema huku akiwa mwenye hofu,

“Leo unataka niendeleee kuishi wakati ulituma Watu waniuwe?

Kabla sijafa utatangulia wewe!!” Alisema kisha alimkunja kwa lengo la kumjaza hofu

“Sande tafadhali usifanye hivyo, kumbuka hapa ni Ikulu na ukifanya chochote kile utajiweka katika mazingira magumu ya kuwa hai, sema unataka nini nitakupa!!”

“Nautaka Urais wako! Mamlaka kisha nilipe kisasi kwa kifo cha Zola” Rais akawa ameelewa lengo la Sande kufika Ikulu lilikuwa ni nini

“Sande unajua fika nisingeliweza kumuuwa Huyo Zola, isipokuwa….” akakatizwa na ishara ya Sande

“Nahitaji unipeleke kwenye chumba cha siri cha Ikulu”

“Chumba cha siri? Nani amekuambia kuwa hapa kuna chumba cha siri! Hakuna hicho chumba ndani ya Hii Ikulu Sande, utakuwa umekosea” Alijitetea Rais akiwa anatabasamu kwa lengo la kumtoa mchezoni Sande huku macho ya Rais yakiwa yanatazama kipande cha bomba lililoanguka chini, akataka kumshambulia lakini Sande akashtuka akamvuta hadi ukutani akampa ngumi nne za uso ambazo ziliiweka akili ya Rais katika hali sawa!!

“Nipeleke chumba cha Siri” Rais hakuwa na jinsi ya kufanya akalazimika kuongozana na Sande, kwanza Sande akachomoa Bastola kisha akaiweka kwenye kichwa cha Rais huyo ili ije kuwa kama ngao ya kumlinda. Wakaongozana kuelekea huko huku Rais akijuwa fika kuwa Sande anaweza kumuuwa endapo hatofanya hivyo.

Mwendo wa taratibu eneo ambalo halikuwa na walinzi, wakafika mahali Rais akamuuliza Sande

“Unashirikiana na Muasi P55?”

“Twende sitaki maswali ya Kizandiki” Alisema Sande, wakafika hadi kwenye Ofisi ya Rais huyo, kitendo cha kufika tu Ofisini alamu maalum ikalia baada ya Kamera kuonesha kuwa Rais alikuwa ametekwa humo Ikulu, Askari wakamiminika kuelekea ndani ambako Rais alikuwepo.

“Funga mlango wako haraka sana” Alisema Sande huku akimtishia kumuuwa Rais, hakuwa na jinsi akafanya kama alivyoelekezwa sababu mlango huo ulikuwa wa umeme na ulikuwa na namba maalum za kuingilia ambazo alikuwa akizifahamu Rais pekee. Simu ya Rais ilikuwa ikiita, mpigaji alikuwa ni John Brain, baada ya kuwapigia vijana wake wote watatu simu haikuweza kupokelewa.

Sande akaichukua simu akaipokea

“Rais! kuna Usalama huko?” aliuliza punde simu ilipopokelewa

“Hakuna usalama sababu Ikulu ipo chini ya Uvamizi” Sauti ya Sande ilipofika kwa John ikampa ujumbe kuwa Rais alikuwa chini ya ulinzi.

“John! muda wa wewe kuendelea kutekeleza ugaidi Duniani umeisha, Dunia itaenda kuandika Historia Muda mchache ujao tutakapokufuta katika uso wa Dunia” John akawa amechanganikiwa, Sande akaendelea kumueleza

“Hakuna kijana wako hata mmoja anayepumua hadi kufikia wakati huu, umebaki mwenyewe katika Ardhi ambayo uliamrisha kila kitu kifanywe kwa matakwa yako” Kisha Sande akakata simu hiyo

“Waambie Askari wako wakae mbali na eneo hili vinginevyo nitakuuwa muda sio mrefu” Akasema Sande, pale pale Rais akabonyeza sehemu ambayo ilikuwa na Maiki akasema na Askari wote wakasikia.

“Nioneshe kilipo chumba cha siri”

“Sande hata ukienda huko utakufa sababu Kuna mfumo wa umeme ambao hauwezi kukuruhusu kupenya zaidi” Alieleza Rais, Sande akampiga teke la Mguu Rais kisha akamwambia

“hakuna muda wa kupoteza nipeleke huko” Rais akaelekea mahali ambapo kulikuwa na kabati kubwa la vitabu akabonyeza sehemu kisha mlango ukafunguka.

Kila ambacho Mbaga alimueleza Sande kilionekana, ni kweli ndani ya chumba hicho kulikuwa na mionzi iliyokuwa ikipishana “Unaona? ule ni mfumo wa Umeme Sande, unachotaka kipo mbele zaidi ya pale ambapo kuna mionzi utafia huko” Sande akaona Rais huyo anamtia kelele, akamfunga kamba mikononi na miguuni kisha akamuweka chini ya Meza, akatoa kifaa cha kunyonya mionzi ambacho alipewa na Mbaga akakiwasha kikaanza kuhesabu sekunde ambapo baada ya sekunde 30 kupita kitazima hivyo

Sande alipaswa kutumia muda mfupi kuchukua vitu viwili, Fimbo na nyaraka za siri ambazo alielezwa kuwa zilikuwa zipo pamoja ndani ya chumba hicho.

Sande akaingia ndani ya chumba hichi kisha akaweka kifaa sehemu ambapo mionzi yote ya umemeikaunganika na kukielekea kifaa hicho, Sande akapata nafasi ya kuzama zaidi ndani ya chumba hicho, akawa anahaingaika jinsi ya kuviona vitu alivyokuwa akivitaka, akajikuta akitumia sekunde 10 bila Mafanikio, kumbe Rais alikuwa na kisu kidogo alichokuwa amekificha kwenye kiatu chake, akawa amejitahidi na kukata kamba hizo. Akaangalia kwenye Kioo ambacho kilikuwa kikitumika kuonesha Video za CCTV, akaona kuna Askari waliokuwa mlangoni, haraka akakimbilia kuwafungulia.

Sekunde zilikuwa zimeshaisha, Sande alikuwa ameshapata nyaraka na hiyo fimbo kisha haraka akawahi kutoka, mlango ukajifunga. Akakutana Uso kwa uso na Askari wawili waliofunguliwa Mlango na Rais, Aksari hao wakachomoa Bastola zao huku wakiwa wamefunika nyuso zao, Sande akajikuta yupo chini ya Ulinzi wa Askari hao.

Rais akampokonya Sande vile Vitu kisha akawa anapiga hatua kuelekea kufungua lango la chumba cha Siri, ghafla akashangaa Askari hao wawili wakimnyooshea Bastola, wakavua walichovaa kwenye nyuso zao,

Rais hakuamini kuwaona Dawson na Mbaga wakiwa ndani ya Mavazi ya kijeshi, akataka kufanya ujanja kufungua mlango ili aingie huko, akapigwa risasi ya mguu.

Wakavichukua vitu hivyo alafu wakamwambia Rais atangaze katika TV ya Taifa kutokea Ikulu kuwa Nchi ipo chini ya Jeshi. Muda huo John Brain alikuwa akikusanya kila kilicho chake ili aondoke Nchini, akiwa anataka kutoka akasikia Sauti ya Rais kutokea kwnye TV ikiitangazia Nchi kuwa Nchi hiyo ipo chini ya Jeshi, wakaonekana akina Dawson na Mbaga ambao walitajwa kuwa Waasi kwa nyakati tofauti tofauti, wakamlazimisha Rais alekeze kila kitu, akasema kila kitu hata mauwaji ya Makamu wa Rais ni yeye ndiye aliyehusika nayo, vifo vilivyokuwa vikitokea vilitokana na yeye.

Kisha picha ya John Brain ikaanikwa kwenye TV, Watu ndio wakapata kumjua John Brain ambaye Taifa la Marekani lilikuwa likimsaka. Taarifa hii ilienda mbali zaidi hadi vituo vya Runinga vya Aljazeera vikaitoa.

John Brain akaondoka Nchini kwa kutumia Helkopta, akatua Uganda ili apande ndege akiwa amevalia sura Bandia. Tayari Marekani walikuwa wameshaipata Taarifa hiyo wakatuma FBI Dunia nzima wakiwa na sampo ya DNA ya John Brain baada ya kumfahamu. John akakamatwa kwenye mpaka wa Somalia akiwa anajiandaa kuonana na Kundi la Alqaeda na Baada ya kupimwa akagundulika kuwa ni yeye, FBI wakarudi Marekani wakiwa na

John Brain ili awaoneshe Makundi mengine ya Kigaidi.

Taifa hilo likawataja Mbaga, Sande Olise na Dawson kama Mashujaa wa Dunia kwa kumfichua John Brain ambaye Mataifa mengi yalihangaika kwa muda mrefu, Kama ilivyo ahadi ya Mbaga aliondoka kwenda kuishi Shamba katika Nchi ya Eritrea, akajiwekeza na kilimo huku akiwa ameiacha Nchi hiyo ikiwa inaingia kwenye Uchaguzi wa kuunda Serikali itakayoongozwa kikatiba tofauti na Mwanzo ambavyo Watu walikuwa wakirithi nafasi ya Urais.

Baada ya miezi mwili Dawson alifariki kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu, Kisko na Chande walichukuliwa na Taifa la Marekani kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi, wakati huo Sande akistaafu kazi ya Kijeshi akapanda ndege kwenda Eritrea kuishi pamoja na Mzee Mbaga

MWISHO
Shukrani kwako mtunzi huna mbambamba kweny kuleta kazi hongera Sana.
 
We jamaa vp mbona huleti story ilikuwaje mzee Dowson baada ya malaika kuvamia pale na six embu Lete muendelezo basi nipo tu nimetulia nasubir story
 
Back
Top Bottom